COASTAL UNION YAIPIGIA HESABU MWADUI

September 23, 2015
KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union, Jackson Mayanja ameanza kikiandaa kikamili kikosi chake kwa ajili ya kuhakikisha kinaubuka na ushindi dhidi ya Mwadui FC kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.

Akizungumza , Mayanja alisema kuwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye kikosi hicho kwenye michezo yao miwili tayari walikwisha kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa hivyo wapo vizuri kupambana kwa mafanikio.

Alisema kuwa tatizo ambalo linaisumbua timu hiyo la umaliziaji alikwisha kulifanyia kazi pamoja na lile la wachezaji kutokuwa makini hali inayomfanya kuanza kupata matumaini mapya ya kikosi hicho kurejesha makali yake.

Aidha alisema kuwa makosa madogo madogo yaliyoanza kuonekana kwenye mechi yao dhidi ya Toto African alikwisha kuyarekebisha baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu pacha ya kutokufunga.
 
“Nimekwisha kurekebisha baadhi ya mapungufu na sasa bado tunaendelea kujiandaa na michezo yetu inayokuwa ikiwemo ule wa Mwadui FC lengo kubwa likiwa kuhakikisha tunarudisha makali ya kikosi hiki “Alisema Kocha Mayanja.

Hata hivyo alisema kuwa dhamira yao bado ipo pale pale kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa afrika.


Coastal Union mpaka sasa imekwisha kucheza michezo mitatu ikipoteza miwili kwa kufungwa na Yanga na Ndanda ikiwemo kutoa sare ya bila kufungana ikiwa na pointi moja kwa michezo hiyo iliyokwisha kuchezwa.


















KIKWETE AWAPA ZAWADI YA IDD MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA

September 23, 2015

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda(wa pili kulia)kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi za Idd el Hajj Meneja wa Mahabusu ya Watoto mkoa wa Arusha,Mussa Mapua leo kwaajili ya kusherekea siku kuu hiyo kesho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ametoa zawadi mbalimbali katika Mahabusu ya watoto walikinzana na sheria iliyopo jijini Arusha.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kikwete,Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda amesema pamoja na kuwa watoto hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujibu lakini mheshimiwa Rais anatambua haki zao za kushiriki na jamii kufurahia siku kuu hiyo ya kidini.

"Kama mnavyofahamu Rais Kikwete amekua na utamaduni wa kuwakumbuka katika siku kama hizi ili nanyi mfurahie siku kuu hii,"alisema Mapunda

Akipokea zawadi hizo Meneja wa Mahabusu hiyo,Mussa Mapua amesema imekua ni faraja kwa kiongozi wa nchi kuwakumbuka na kuomba taasisi nyingine na watu binafsi kuiga mfano huo na kumtakia Rais Kikwete mapumziko mema anapojiandaa kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake.
KARSAN AWASHUKIA VIONGOZI WA DINI, WANAHABARI

KARSAN AWASHUKIA VIONGOZI WA DINI, WANAHABARI

September 23, 2015
IMG_0481
Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza kushiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na wa pili kulia ni Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Modewjiblog team
WAKATI viongozi wa dini wametakiwa kuacha kufanya siasa na badala yake wahubiri upendo na si upinde, waandishi wa habari wameelezwa kununuliwa na wanasiasa kulainisha maneno yao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho Siku ya Amani Duniani iliyofanyika Mwanza.
Alisema katika mazungumzo yake hayo kukengeuka kwa wanahabari na viongozi wa dini ambao ni wadau muhimu wa amani hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi ni kasoro inayotakiwa kufutwa mara moja.
Akikazia kwa viongozi wa kidini alisema kwamba amani ya nchi inahitaji kulindwa na wote lakini viongozi wa dini wana wajibu mkubwa katika hilo.
Alisema kutokana na wadhifa wake amekuwa akipata habari nyingi ambazo zinakengeuka na zenye mwelekeo hatarishi na nyingi zinakuwa ni za viongozi wa dini.
“Habari zinapoandikwa Tanzania, inapofika saa saba, saa nane ya usiku, mimi huletewa habari nyingi sana, kuziangalia na miongoni mwa habari tulizozizuia ni mbaya kweli kweli zinatoka kwa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini.” alisema Karsan
IMG_1136
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho Siku ya Amani Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
“Sasa nawaomba sana kwa unyenyekevu mkubwa kwa viongozi wa dini nchini, nawaomba muhubiri upendo na msihubiri upinde!..” alisisitiza Karsan.
Kiongozi huyo wa UTPC yenye wanachama zaidi ya elfu nne alisema kwamba anashangaa viongozi hao wa dini kugeuka wanasiasa kwani anaamini kwamba Kwa Msajili wa Vyama hakuna chama cha dini kilichosajiliwa.
Alisema pamoja na kwamba hakuna chama cha siasa cha kidini kusajiliwa anashuhudia anashuhudia baadhi ya viongozi wa dini wakihubiri siasa.
Pamoja na kuhimiza viongozi wa dini wasitoke katika mstari wao wa kuhubiri amani, alisema kuna kasoro kubwa miongoni mwa wanahabari kwa kuwa wengi wao tayari wamenunuliwa.
“Wanahabari wengi baadhi yao wameshanunuliwa hasa kwa habari zao wanazoandika nyingi wanawachagulia wananchi kwa habari zao za kununuliwa. Andikeni habari na sio kuandika hatari.” alisema Karsan.
Na kuongeza kuwa: “Magazeti yanapiga kura, radio inapiga kura, Televisheni inapiga kura, tena inapiga kura sasa wakati siku ya kura ni Oktoba 25. Acheni kabisa michezo hiyo kwani tunawaomba muwe waandishi wa habari na sio waandishi wa hatari…Andikeni habari na sio hatari!!” alisisitiza Karsan.
Kwa kuzingatia miiko ya taaluma ya habari nchini, alipigilia msumari kwa wamiliki wa vyombo vya habari, wanasiasa kuacha kuwahonga waandishi hasa kwa kutumia fedha ili kulainisha habari huku wakionekana kuunadi Uhuru wakati mioyoni mwao hawana utu.
“Nawaomba wananchi wa Tanzania, msiwachague viongozi wa nchi hii kupitia magazeti, radio na Televisheni. Puuzeni habari zote nendeni kwenye mkutano wa wanasiasa na msikilize kila mgombea anasema nini na kila chama kinasema nini hao wanaoandika kwenye magazeti yao ni yao wenyewe na mengi hayana ukweli.” Alisema.
IMG_1161
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akisisitiza jambo kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani duniani jijini Mwanza.
UTPC ina zaidi ya waandishi wa habari 4600 nchini kote ambapo makao yake makuu yapo Mkoani Mwanza.
Pia aliwawaomba wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuhakikisha wanawalipa mishahara waandishi wao kwani hadi sasa baadhi yao wanahabari wanadai mishahara zaidi ya miezi mitatu.
“Nawaomba wamiliki wa vyombo vya habari, ili waandishi waweze kufanya vizuri, basi walipeni mishahara yao. Wapo ambao hadi leo baadhi yao wanawadai mishahara zaidi ya miezi mitatu” alifafanua Karsan.
Karsan aliwataka wamiliki hao kuacha kusimama majukwaani na kujinadi mambo mazuri wakati wanashindwa hata kuwalipa wafanyakazi wao mishahara mizuri na hapo hapo wanataka waandike habari za haki.
Aidha alikemea tabia ya wamiliki wa vyombo vya habari ya kuwachagulia habari wahariri.
Naye mwakilishi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafa hiyo aliwataka watanzania katika umoja wao kuhakikisha kwamba amani inaendelea kuwapo nchini ikizingatiwa kwamba taifa hili lilipata uhuru kwa njia ya amani.
Alisema Tanzania tangu zamani imeweka mbele mazungumzo katika kutatua mambo mbalimbali na kusema hatua hiyo ya mazungumzo ni hatua kubwa ya kidekrasia ambayo imefanikisha amani na kusema ni tumaini lake kwamba itaendelea kuwapo.
Naye Naibu kamishina wa Polisi Charles Mkumbo ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza akizungumza katika hafla hiyo aliwataka wananchi kutii sheria bila shuruti na kwamba jeshi la polisi limejipanga kuzuia uhalifu na vitendo vinavyotia hofu kuelekea na siku ya uchaguzi.
Alisema jeshi lake limejipanga vyema pamoja na kutumia weledi na busara kuelekea uchaguzi, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Aliwatahadharisha wananchi umuhimu wa kulinda amani kwani gharama ya kuipoteza na kutaka kuirudisha ni kubwa.
IMG_1421
Pichani ni viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini nchini waliohudhuria maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.

LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA KUANZA MWAKANI

September 23, 2015

KATIKA harakati za kuinua kiwango cha soka ya wanawake nchini, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepanga kuendesha Ligi Kuu ya wanawake nchini kuanzia mwakani.
 
Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema kwamba TFF imeviagiza vyama vya mikoa kuendesha mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa kwa wanawake haraka iwezekanavyo kabla ya Desemba 31, mwaka huu ili kupata timu za kushiriki Ligi Kuu.
 
"Kila chama cha mkoa cha mpira wa miguu nchini kinapaswa kuwasilisha jina la bingwa wa mkoa mwishoni wa mwezi Disemba mwaka huu, kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kufanyika mwakani,"amesema Kizuguto.
 
Ligi ya Taifa ya Wanawake inatarajiwa kuanza mapema mwakani baada ya kupatikana mabingwa wa mikoa 27 nchini ikijumuisha mkoa wa Dar es salaam utakaokuwa na timu tatu za Ilala, Kinondoni na Temeke.
 
Jumla ya timu 10 zinatarajiwa kupanda Ligi Kuu ya Wanawake Taifa baada ya timu za mikoa 27 kucheza ligi ya mabingwa na kupata timu 10 zitakazoanza kwenye ligi hiyo ya wanawake mwakani.

MAMA SAMIA AWANADI PROFESA MAJI MAREFU NA MARY CHATANDA, TANGA

September 23, 2015


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi, kufanya mkutano wa kampeni jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga leo.
 Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa  Shule ya Msingi Mazoezi wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika katika  leo katika jimbo la Korogwe mjini leo.
 Mgombea Ubunge jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mama Samia katika jimbo hilo leo.
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia katika mkutano wa kampeni uliofayika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Mazoezi katika jimbo la Korogwe mjini leo
 Wasanii wa bendi ya Hapa Kazi tu wakitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Uwanja wa shule ya msingiMazoezi katika jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanga leo
 Wasanii waliopo katika kundi la Mama Sema na mwanao, Kamarade Ally Choky na Snura wakiburudisha wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanga
 Sunura akiimba wimbo wa kuifagilia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Korogwe mjini leo
 Mgombea Ubunge jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani, maarufu kwa jina la Maji Marefu akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanga leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwanadi Mgombea Ubunge jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda na Mgombea Ubunge jimbo la Korogwe Vijijini Stecen Ngonyaji maarufu wa jina la Maji Marefu katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanaga leo
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Mazoezi katika jimbo la Korogwe mjini akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanga. Kushoto ni Mama Samia na kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Korogwe Vijijini Steven Ngonyani.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa meza kuu na Mgombea ubunge jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda wakati wa mkutano wa kampeni uliofayika leo katika jimbo hilo mkoani Tanga
Wananchi wakimsikiliza kwa makini mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanga
 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama samia suluhu Hassan katika eneo la Mombo, wakati akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Lushoto katika jimbo la Korogwe Jijijini, mkoani Tanga leo.
 Wananchi wakaiwa wamezuia msafara wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan wakati akienda Kijiji cha Mwangoi, kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Korogwe Vijijini mkoani Tanga leo
 Wananchi wakiwa na bango la kumfagilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Kijiji cha Mwangoi jimbo la Korogwe Vijijini leo.
 Mbunge wa Bumbuli mkoa wa Tanga, Januari Makamba akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Kijiji cha Mwangoi jimbo la Mlalo mkoani Tanga leo
 Vijana wa kazi waliopo katika msafara wa kampeni za mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia wakionyeshana kameara ya kisasa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo jimbola Mlalo mkoani Tanga
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mlalo, Brigedia Mstaafu, Hassan Ngwlizi, akimnadi Mgombea mpya wa jimbo hilo, Rashid Shangazi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Tanga leo.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
KUZIONA SIMBA, YANGA 7000/

KUZIONA SIMBA, YANGA 7000/

September 23, 2015
Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba (7,000).
Katika mchezo huo kiingilio cha juu kitakua ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000) kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.
Tiketi za mchezo ho zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vifuatavyo: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni – Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry – Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya daladala.
TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchin kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia tiketi ili kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA, Israel Nkongo (Dsm) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza) mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku hiyo ya Jumamosi itakua ni kati ya Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Prisons) watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Stand United katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Majimjaji ya Songea katika uwanja wa Manungu wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo miwili ambapo waoka mikate wa Azam FC watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa Chamazi Complex, huku African Sports wakiwa wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
AFISA MTENDAJI MKUU WA SHEAR ILLUSIONS AFRICA AWATAKA WANAWAKE KUDHUBUTU

AFISA MTENDAJI MKUU WA SHEAR ILLUSIONS AFRICA AWATAKA WANAWAKE KUDHUBUTU

September 23, 2015

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser (Kushoto )Akimkabidhi Cheti Mshiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali Hafla iliyofanyika Katika Ukumbi wa Parokia ya Yombo Dovya, Temeke Yalio chini ya Taasisi “Sauti ya Mama na Mtoto.”.Mama Shekha Nasser ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Shuguli hiyo Kutokana na Juhudi zake za Kupambana Kama mwanamke Mzalendo wa Kiafrika na Mtanzania Pekee anayemiliki Bidhaa yake ya Vipodozi Ijulukanayo Luv Touch Manjano.Pia anahangaika usiku na Mchana kuwasaidia Wanawake wengine wa Kitanzania Kuondokana na tatizo la Ajira na kuwawezesha wanawake Kudhubutu na Kujikita kwenye biashara hasa kwa Kutumia Vipodozi Ambapo Ameweza kusidia zaidi ya wanawake 30 Kwa kuanzisha Taasisi ya Manjanio Foundation.
     Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser Akiwa kwenye Picha pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya “Sauti ya Mama na Mtoto.”Ndugu  David Mwandele wa Pili kutoka Kushoto,Pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi Hiyo..Shughuli ilikuwa ni kutoa vyeti kwa kina mama 50 waliopewa mafunzo ya ujasiriamali na taasisi hiyo  ili kuwejengea uwezo wanawake hao wanaoishi katika mazingira magumu ili kuona kwamba wanapata elimu ya kuwawezesha kujikimu na mahitaji yao msingi, yaani waweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa watoto wao, kwa kupitia elimu ya ujasiriamali waliopata.
 Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali wakimpokea kwa Furaha  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser kwenye Halfa hiyo. Easter Lukindo ni mwanamke aliye Dhubutu na kuanza Biashara kwa Kupitia Vipodozi vya Luv Touch Manjano chini ya Taasisi ya Manjano Foundation akizungumza Machache kwenye halfa hiyo ambapo aliwaasa washiriki wa Mafunzo hayo Kuacha woga na kujiamini kwamba nao wanaweza,Pia aliwataka Washiriki hao nkuanza Kuchangamkia Fursa zilizopo haraka mara baada ya Kupata elimu ya Ujasiriamali.Alitumia Muda huo Pia Kumshukuru Mama Shekha Nasse Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambayo imempa nafasi ya Yeye Kuongeza Kipato kwa  kujikita kwenye Biashara,
   
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali.