WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA LINDI, MTWARA

February 18, 2015

Na Veronica Simba

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi mbalimbali.

Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.

“Kutokana na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri. Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

“Tunaendelea na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema.

Ziara hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka huu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia) akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud (Kulia kwa Waziri.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Matanki ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi wanaoishi maeneo jirani.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Mhandisi Kapuulya Musomba (wa pili kushoto) akimwonyesha kitu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakati alipotembelea Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, mwanzoni mwa wiki.
Baadhi ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi huo mwanzoni mwa wiki.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki Yusuf (Kulia) akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa umeme kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara yake kukagua Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara. Kulia kwa Waziri ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Mhandisi Kapuulya Musomba na kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kushoto), akisalimiana na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Msimbati, Joha Matwili, alipowasili MnaziBay kujionea athari za mmonyoko wa ardhi uliotishia hali ya usalama wa mazingira ya Kampuni ya Tawel & Prom inayozalisha umeme unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hawa Dendegu (aliyenyoosha mkono), akimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, jinsi maji ya bahari yalivyoathiri eneola MnaziBay, karibu na kampuni ya kuzalisha umeme ya Maurel & Prom.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (aliyenyoosha mkono) akimwonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (wa pili kulia) wakati Waziri alipotembelea eneo hilo kujionea athari za mmomonyoko wa ardhi uliotishia usalama wa mazingira ya Kampuni ya kufua umeme ya Maurel & Prom iliyo jirani na eneo hilo.
Athari ya mmomonyoko wa ardhi katika eneo la MnaziBay inavyoonekana pichani. Mmomonyoko huo umetishia usalama wa Kiwanda cha kufua umeme unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara cha Maurel & Prom.
Meneja Uzalishaji na Uendeshaji wa Kampuni ya Maurel & Prom, David Chajdronnier (katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hawa Dendegu (Kulia) kuhusu mmomonyoko wa ardhi eneo la MnaziBay, Mtwara. Kampuni hiyo ndiyo inazalisha umeme unaotumiwa na wakazi wa Mtwara na Lindi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki Yusuf (Kulia) akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa umeme kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu.
Kisima cha gesi namba 3 kilichopo Msimbati, Mtwara. Kisima hiki hupokea gesi asilia kutoka Kisima namba 1 na Kisima namba 2, kisha kupelekwa Madimba kwenye mtambo wa kuchakata gesi hiyo.
Sehemu ya mtambo wa kisima cha gesi namba 3 kilichopo Msimbati, Mtwara ambacho hupokea gesi kutoka Visima namba 1 na 2, kisha kupelekwa Madimba katika mtambo wa kuchakata gesi.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akicheza mchezo wa ‘Pool Table’ katika ukumbi uliopo kwenye nyumba za wafanyakazi wa mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara baada ya kuhitimisha ziara yake mwanzoni mwa wiki. Mahali hapo pa michezo ni maalum kwa wafanyakazi kwa ajili ya kujichangamsha baada ya kazi. Anayefuatilia mchezo huo ni Msaidizi wa Waziri, Mhandisi Joseph Kumburu.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akikagua moja ya Valvu ya gesi, eneo la Somanga Fungu akiwa katika ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini na mwenye kofia nyeupe ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba.

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF MJINI DODOMA

February 18, 2015

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (Kushoto) akizindua huduma mpya itolewayo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ya Fao la Uzazi, mwanzoni mwa mkutano mkuu wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia, ni naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo, GHeorge Yambesi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ,Adam Mayingu kihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.
Waziri mkuu Mizengo Pinda (Kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, huku Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo, George Yambesi, (Kulia), na Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa wakishuhudia, wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 4 wa wanachama na wadau wa Mfuko huo mjini Dodoma, Jumatano Feb 18, 2015.
Waziri mkuu Mizengo Pinda, akimpongeza Zainab Khalid, mmoja kati ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, aliyefaidika na mkopo wa elimu ambapo sasa anasoma chuo kikuu Huria jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilikuwa sehemu ya ufunghuzi wa mkutano mkuu wan ne wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma Jumatano Februari 18, 2015.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, waliopita na wa sasa, wakipiga makofi wakati waziri mkuu Mizengo Pinda, wakati akifungua mkutano mkuu wa Nne wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma, Jumatano Februari 18, 2015.
Baadhi wa washiriki wa mkutano mkuu wan ne wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mjini Dodoma Jumatano Feb 18, 2015.
WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI WA MFUKO KUWAENZI WAASISI WA TAIFA

WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI WA MFUKO KUWAENZI WAASISI WA TAIFA

February 18, 2015

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiongoza Ujumbe wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa leo.
Picha na Ikulu.
3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani (aliyesimama) akisoma taarifa ya wajumbe wa   Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa wakati wajumbe walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi (wengine) Mwenyekiti Vikabenga Nsa Kaisi (wa pili kushoto) na Aisha Ali Karume Mjumbe (kushoto),
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27

February 18, 2015

images 
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).
……………………………
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA. FEBRUARI 18, 2015.
 mkutano wa Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wafanyika

mkutano wa Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wafanyika

February 18, 2015
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika mkutano wa siku moja uliozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,
Picha na Ikulu.
3
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Amali   wakimsikiliza Waziri  wa Wizara hiyo Ali Juma Shamuhuna  alipokuwa akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika mkutano uliofanyika leo asubuhi ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar mbele ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka Malawi,Kuwait.Afrika ya Kusini na Kenya

Rais Kikwete apokea hati za utambulisho kutoka Malawi,Kuwait.Afrika ya Kusini na Kenya

February 18, 2015
1
Baliozi mpya wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndilowe akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za Utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam Februari 18, 2015.Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
2
Balozi Ndilowe akiwa katika picha na Rais Kikwete na kufanya naye mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Baliozi mpya wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa Ndilowemara mara baada ya kuwakilisha hati za Utambulisho.
4
Balozi mpya wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam Februari 18, 2015.
5
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akiwa katika picha na Rais Dkt.Jakaya Kikwete.
6
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania na Rais Dkt.Jakaya Kikwete.wakiwa katika mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
7
Balozi Mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Mhe.Thamsanqa Dennis Mseleku akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
8
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na balozi mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Thamsanqa Dennis Mseleku baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho na kufanya naye mazungumzo.
910
Balozi Mpya wa Kenya nchini Tanzania Mhe.Chirau Ali Mwakwere akiwasilisha Kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam leo. . Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
.1111
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere wakikumbatiana na kwa furaha muda mfupi baada ya balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam leo.
(picha zote na Freddy Maro)