SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU .

April 28, 2018

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Festo Kiswaga .
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa( TANAPA) Allan Kjazi akikabidhi Hundi ya Kiasi cha Sh Mil 50 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa huo ,wengine kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi ,Bw Festo Kiswaga .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za TAifa (TANAPA) Pascal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa wa Simiyu.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi , Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana .

Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.

Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za wasichana na wavulana.

Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa makubwa kwao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.

Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.

RMO,DMO TENGENI SIKU ZA UCHUNGUZI WA SARATANI-WAZIRI UMMY

April 28, 2018

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza leo Jijini Tanga wakati alipozindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Clemence Marcell akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema kuwa takribani wanawake 38,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi mkoani Tanga.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi akizungumza katika uzinduzi huo

Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon akizungumza wakati wa uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO)Jairy Khanga mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha Afya cha Ngamiani alipokwenda kuzindua chanjo hiyo


WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga wakiangalia ngoma ya Msanja wakati wa uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo kabla ya kufanya uzinduzi huo kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Monica Kinala

Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati wa uzinduzi huo ksuhoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapa Selebosi katikati ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifurahia jambo mara baada ya kuzindua kampeni hiyo ya chanjo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimpongeza mwanafunzi wa shule ya Sekondari mara baada ya kuchanjwa chanjo hiyo kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Thobias Mwilapwa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga na katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitazama namna mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Masiwani Hanifa Juma anavyopatiwa chanjo wakati wa uzinduzi wake leo kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Thobias Mwilapwa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akifurahia jambo mara baada ya kumaliza uzinduzi huo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia kadi walizopatiwa wanafunzi hao baada ya kupitiwa chanjo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Tanga na wanafunzi mbele waliopatiwa chanjo wakati wa uzinduzi huo
Wanafunzi waliopatiwa chanjo wakionyesha kadi zao
Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Tanga Dkt Ben Nahayo Simon kulia akiteta jambo na Dkt Hamisi mara baada ya kufanyika uzinduzi huo

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wote wa mikoa na wilaya nchi nzima kutenga siku moja kwa mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake na tezi dume.

Waziri huyo ametoa agizo hilo mkoani Tanga leo wakati akizindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Amesema kuwa hali ya saratani kwa nchi zinazoendelea haswa zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania wagonjwa wa saratani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka.

Amesema kuwa Tanzania kunakuwa na wagonjwa 50,000 waliogunduliwa na tatizo la saratani.

Amesema kuwa katika wagonjwa hao asilimia 33 wanakutwa na saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 12 wanagundulika na saratani ya matiti.

Amebainisha kuwa kila katika wagonjwa 100,wagonjwa 80 wanakuwa katika hatua za mwisho za ugonjwa na kufanya matibabu kuwa magumu.

" Narudia kutoa agizo kuwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutenga siku moja kila mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani kwa wanawake na wanaume" alisema.


Kuhusu chanjo amesema kuwa mwaka huu wamelenga kutoa kwa wanawake laki sita na elfu kumi sita kwa mabinti wenye umri wa miaka 14 kutokana na uchache wa chanjo.

" Kwa kuanzia mwaka huu tutatoa chanjo laki sita na elfu kumi na sita kutokana dozi ya chanjo tuliyoipata ni laki sita na elfu ishirini" alisema.

Aidha alitoa wito chanjo itolewe kwa mabinti hali ya kuwa wazazi au walezi wao wameridhia.

" Ninatoa wito kwa watoa huduma za afya hii chanjo mnapoitoa hakikisheni wazazi au walezi wameridhia" alisema

Awali kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Clemence Marcell alisema kuwa takribani wanawake 38,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi mkoani Tanga.

Kati ya hao 30,000 ni wanafunzi wa shule mbalimbali na 8,000 kutokana nyumbani watapatiwa katika hospitali na vituo vya Afya 18 vilivyoteuliwa.

MAKALA: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII INAVYOIMARISHA SEKTA YA UHIFADHI NA UTALII NCHINI

April 28, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaongoza Maafisa wa Wanyamapori 87 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania– TAWA, Shirika la Hifadhi za Taifa – TANAPA na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kupiga gwaride la ukakamavu muda mfupi baada ya kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu hivi karibuni katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.


Na Hamza Temba-WMU


........................................................


Wakati huu tunapoadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni takriban miaka miwili sasa na miezi kadhaa tangu Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mhe. Rais, Dk. John Pombe Joseph Magufuli iingie madarakani.

Itakumbukwa kuwa katika hotuba yake ya kwanza ya kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa mjini Dodoma, Mhe. Rais Magufuli alitoa vipaombele kadhaa vya kutekelezwa na wizara zake huku Wizara ya Maliasili na Utalii akiipa vipaombele vikuu vitatu ambavyo ni kukabiliana na ujangili, kutatua migogoro ya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Wizara ya Maliasili imeendelea kutekeleza vipaombele hivyo pamoja na jukumu lake la msingi la kuhifadhi na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za maliasili na malikale, na kuendeleza Utalii kwa faida ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Ujangili
Wizara imefanikiwa kuanzisha mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori ambayo imeanza kuzaa matunda.

Mikakati hiyo ni pamoja na kuanzishwa kwa Kikosi Kazi Maalum cha Kudhibiti Uhalifu wa Misitu na Wanyamapori nchini ambacho kilianzishwa mwezi Julai, 2016 sambamba na kuimarishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambayo ilianza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai, 2016.

Mikakati mingine ni mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia kwenda wa Jeshi Usu, matumizi ya teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani (drones) kwa ajili ya doria, ushirikishwaji wa wananchi kwenye uhifadhi na matumizi ya mbwa maalum wa kunusa ili kutambua nyara katika viwanja vya ndege na bandari.

Kupitia mikakati hiyo, mwaka 2016/2017 Wizara kupitia taasisi zake iliendesha doria mbalimbali ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 7,085 kwa makosa mbalimbali. Aidha, meno ya tembo 129 na vipande 95 vyenye uzito wa jumla ya kilo 810.03 vilikamatwa.

Vielelezo kadhaa pia vilikamatwa ikiwemo silaha za kivita 48, silaha za kiraia 150, risasi 1,058, magobore 406, silaha za jadi 22,307 na roda 120,538.

Jumla ya kesi 2,097 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali na kesi 802 zilimalizika. Watuhumiwa 472 katika kesi 262 walifungwa jela jumla ya miezi 42,153 na watuhumiwa 79 katika kesi 43 waliachiwa huru huku watuhumiwa wengine 469 katika kesi 276 wakilipa faini ya jumla ya shilingi milioni 452.1.

Katika kuelekea kwenye Mfumo wa Jeshi Usu, Wizara imeendesha mafunzo kwa watumishi 661 kuhusu ukakamavu, uongozi na ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia kuhusu Ujangili. Watumishi walioshiriki mafunzo hayo ni 139 kutoka TAWA, 388 kutoka TANAPA, 117 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na 17 kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

Kutokana na jitihada hizi hali ya ujangili imepungua kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, katika Pori la Akiba Selous idadi ya Tembo waliouwawa imepungua kutoka tembo 17 mwaka 2015/16 hadi tembo 7 mwaka 2016/17.

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, wanyamapori hasa tembo wameanza kuonekana katika maeneo mbalimbali ambayo kwa kipindi kirefu hawakuwa wakionekana, mfano hivi karibuni tembo kadhaa walionekana katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Aprili 18 mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma, alinukuliwa akisema kuwa ujangili hapa nchini umepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita hadi kufikia mwezi huu wa Aprili hakuna mauaji mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa kuhusiana na ujangili na kwamba nyara zinazokamatwa hivi sasa ni masalia ya zamani ambayo yanatafutiwa masoko.

Alisema mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama sambamba na kuwashirikisha wananchi kwa kuimarisha ulinzi na doria za mara kwa mara za kiitelijensia katika maeneo ya hifadhi.

Utalii

Katika kuongeza idadi ya watalii nchini, Wizara imeendelea kutekeleza shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye maeneo ya hifadhi, kuboresha miundo mbinu kwenye maeneo ya vivutio, kuanzisha huduma mpya za utalii pamoja na utangazaji.

Juhudi hizo zimewezesha ongezeko la watalii wa kimataifa kutoka 1,284,279 mwaka 2016 hadi kufikia 1,327,143 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 3.2.

Aidha, mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 2.1 mwaka 2016 hadi Dola za Marekani bilioni 2.2 mwaka 2017.

Sekta hii ya utalii imetoa ajira takriban 500,000 za moja kwa moja na ajira nyingine milioni moja zisizo za moja kwa moja kwa mwaka.

Sekta hii pia inachangia takriban asilimia 17.5 ya Pato la Taifa na wastani wa asilimia 25 ya fedha zote za kigeni.

Aidha, Wizara imedhamiria kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini kwa kufungua utalii wa Kanda ya Kusini ili kuongeza idadi ya watalii na mapato ya Serikali.

Kupitia dhamira hiyo Serikali imesaini mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Marekani milioni 150, sawa na takriban shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Kusimamia Maliasili na Kuendeleza Utalii wa Ukanda wa Kusini –REGROW.

Mradi huu ambao maandalizi yake yalianza mwezi Novemba 2014 ulizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 12 Februari, 2018 katika viwanja vya Kihesa Kilolo Mjini Iringa huku Kauli Mbiu yake ikiwa “Utalii kwa Maendeleo Endelevu- Karibu Kusini”.

Mama Samia alisema lengo la mradi huo ni kuongeza mchango wa sekta ya maliasili na utalii katika uchumi wa taifa kwa kuboresha vivutio vya utalii, miundombinu, usimamizi wa vivutio na kuongeza faida za kiuchumi kwa jamii zinazoishi jirani na maeneo ya hifadhi katika ukanda huo wa kusini.

Katika kuongeza jitihada za kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, Wizara imeendelea kuongeza bajeti ya utangazaji ambapo Bodi ya Utalii Tanzania kwa mwaka wa fedha 2017/18 imeongezewa bajeti kufikia shilingi bilioni 6.6 ikilinganishwa na shilingi bilioni 4.1 mwaka 2016/2017 na bilioni 4.3 mwaka 2015/16.

Aidha, katika kufungua masoko mapya ya utalii nje ya nchi, Wizara inaangazia masoko mapya katika nchi za China, Israel, Urusi, Australia na nchi nyingine za Skandinavia.

Wananchi wanavyonufaika na uhifadhi

Wizara ya Maliasili inaendelea na juhudi za kuhakikisha wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi wananufaika na rasilimali zilizopo. Kupitia Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori, jamii zinanufaika kwa kupata ajira, kitoweo, elimu, miradi ya kijamii na kuongeza kipato.

Hadi hivi sasa jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori 38 zimeanzishwa. Aidha, wananchi wanaoishi jirani na misitu wananufaika kupitia miradi ya ufugaji nyuki ambapo kupitia uwezeshaji wa Mfuko wa Misitu Tanzania miradi 254 ya kuboresha kipato cha jamii zinazoishi pembezoni mwa misitu imetekelezwa.

Miradi hiyo ni ya ufugaji nyuki ambapo vikundi vya ufugaji nyuki 399 na watu binafsi 27 wamewezeshwa kupata mizinga ipatayo 11,730.

Udhibiti wa migogoro baina ya wananchi na hifadhi

Katika kudhibiti migogoro ya mipaka kati ya wananchi na maeneo jirani na hifadhi, Wizara kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali na Wadau imeendelea kuhakiki mipaka yote ya maeneo ya hifadhi na kuweka alama za kudumu na mabango ya tahadhari.

Hadi kufikia mwezi Mei, 2017 vigingi 14,755 vimesimikwa sawa na asilimia 62.4 ya vigingi 23,638 vinavyohitajika katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Taifa na Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro.

Aidha, kupitia program ya Panda Miti Kibiashara, Wizara imewezesha vijiji 48 kuandaa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi katika Wilaya za Ludewa, Madaba, Makete, Mufindi, Njombe Mjini, Njombe Vijijini, Kilolo na Nyasa.

Mikakati mipya chini ya Waziri wa Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla

Aidha chini ya Uongozi Mpya wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ipo baadhi ya mikakati yake mipya inayolenga kutoa uelekeo mpya wa kuimarisha sekta Maliasili na Utalii nchini.

Dk. Kigwangalla anaeleza mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuanzisha kwa mwezi maalum wa Urithi wa Mtanzania (Tanzania Heritage Month) ambao utaadhimishwa mwezi Septemba kila mwaka, kuanzishwa kwa Makumbusho ya Marais Wastaafu waliotawala Tanzania mjini Dodoma na Kuboresha na kuendeleza utalii wa fukwe kwa kuanzisha Mamlaka ya Fukwe.
Mikakati mingine ni pamoja na kujenga makumbusho ya meno ya tembo katika miji ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Iringa pamoja na kutambua barabara iliyokuwa ikitumika katika biashara ya utumwa wakati wa ukoloni ili iweze kutumika kiutalii.

Akizungumzia migogoro ya mipaka iliyopo baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi, Dk. Kigwangalla amesema Serikali itatatua migogoro hiyo kwa kushirikisha wananchi sambamba na kuwasaidia kutatua changamoto za msingi ambazo ni kuimarisha maeneo ya malisho ya mifugo, upatikanaji wa maji kwa ajili ya wananchi na mifugo, mpango bora wa matumizi ya ardhi na uendelezaji wa kilimo na ufugaji.

Kwa upande wa vitalu vya uwindaji wa kitalii, Dk. Kigwangalla amesema Serikali itafanya mabadiliko katika mfumo wa ugawaji vitalu vya uwindaji wa kitalii kutoka mfumo unaotumika hivi sasa wa Kamati “Administrative Allocation” na kutumia mfumo wa mnada “Auction”.engo ikiwa ni kuongeza uwazi na kuruhusu nguvu ya soko kuamua bei ambapo mapato ya Serikali nayo yatatarajiwa kuongezeka maradufu. Ili kutekeleza hilo, sheria na kanuni zinafanyiwa marekebisho.

#MWISHO#

KATIKA MAHAFALI YA 24 YA KIDATO CHA SITA SHULE YA SEKONDARI YA JITEGEMEE JKT MGULANI WAZAZI WAAMBIWA URITHI WA WATOTO WAO NI ELIMU

April 28, 2018

Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba (katikati), akihutubia kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Felix Lyaviva ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee Mgulani JKT yaliyofanyika leo hii jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu Laurance Magere.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu Laurance Magere akihutubia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu, Utamaduni na Michezo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makao Makuu Luteni Kanali Meidimi.

Mkuu wa Shule hiyo, Kanali Robert Kessy , akihutubia.

Makamu Mkuu wa Shule, Kapteni Benitho Lubida akiwakaribisha wageni waalikwa.

Wahitimu wakipiga makofi.

Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.




Baadhi ya walimu wa shule hiyo.

Burudani zikitolewa.

Wasoma risala wakisalimia meza kuu.


Na Dotto Mwaibale

IMEELEZWA kwamba elimu ndio urithi pekee utakao wafaa watoto wetu katika ndoto za maisha yao.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Felix Lyaviva ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akihutubia katika mahafali ya 24 ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee Mgulani JKT yaliyofanyika leo hii jijini Dar es Salaam.

"Napenda kuwaeleza wazazi kuwa urithi pekee wa watoto wetu hawa ni elimu na si vinginevyo kwani elimu ndio kila kitu na kwenye elimu hakuna kisichowezekana' alisema Komba.

Komba alisema elimu ndio njia pekee isiyoweza kumdanganya mtu na kama mtu aliteseka wakati akiitafuta akimaliza kuitafuta na kuipata elimu hiyo itamuhudumia mtu huyo.

Katika hatua nyingine Komba aliwataka wanafunzi hao kutojiingiza katika vitendo vichafu kupitia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii badala yake watumie mitandao hiyo kwa manufaa hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inaingia kwenye uchumi wa viwanda kama Rais wetu Dk.John Magufuli anavyohimiza.

"Vijana wengi wamejikuta wakiharibikiwa maisha yao kwa kujiingiza katika vitendo viovu kama kuvuta bangi, kupata ukimwi na vingine vingi kutokana na matumizi mabaya ya tehama" alisema Komba.

Mkuu wa shule hiyo Kanali Robert Kessy akizungumza katika mahafali hayo alisema wahitimu wote 551 wameandaliwa vizuri na wanauhakika watafanya vizuri katika mtihani wao wanaotarajia kufanya hivi karibuni.

"Ndugu mgeni rasmi wahitimu hawa unaowaona tumewanoa vizuri na kipimo kizuri ni kushika nafasi ya sita baada ya kufanya mitihani mitatu mikubwa ya kujipima hivyo hatuna wasiwasi nao kabisa" alisema Kessy.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu Laurance Magere aliwapongeza wanafunzi hao kwa kufikia hatua hiyo pamoja na kuwa na moyo wa fadhila kwa wadau wa maendeleo walioisaidia shule hiyo kwenye maeneo tofauti ikiwemo ya kukarabati majengo.

Wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi wanafunzi hao walisema kwamba karibu changamoto nyingi zilizokuwepo zimetatuliwa isipo kuwa ni ile ya uchakavu wa sakafu ambapo inawalazimu kutumia muda mrefu wa kufanya usafi mda ambao wangeweza kuhutumia kuwa darasani.

Komba katika mahafali hayo ametoa ahadi ya kuwalipia ada wanafunzi wawili ambao wanadaiwa ambapo mkuu wa wilaya hiyo, Felix Lyaviva ametoa mifuko 2000 ya saruji pamoja na shilingi milioni 1.5 ili kusaidia kukabiliana na changamoto zilizopo shuleni hapo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

MUENDESHA BODABODA KUTOKA KIBITI AJINYAKULIA MILIONI 140 ZA TATU MZUKA

April 28, 2018


Pichani kulia ni Muendesha boda boda Magembe Daniel akiwa na Mama yake Mzazi Mama Magembe,wakiwa wameshika mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 140 baada ya kuibuka mshindi wa mchezo wa kubahatisha TatuMzuka hivi karibuni

Magembe ambaye ni Mkazi wa Kibiti-Rufiji anamshukuru Mama yake Mzazi kwa kumlea vizuri,kama vile haitoshi anamshukuru zaidi kwa kumnunulia Piki piki na kuifanyia biashara,anasema na ndi maana mara baada ya kupata taarifa kuwa nimeshinda mchezo wa TatuMzuka,Mtu kwanza kabisa kumtaarifu alikuwa ni mama yake mzazi, kuwa ameshinda mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,anasema mama yake hakuamini lakini alimtia moyo yakuwa na subira zaidi ili kubaini kama ni kweli ama la.

"Vijana wenzangu ninaofanya nao kazi wamenisihi nitulie,kwa sababu mara nyingi baada ya kuipata fedha nyingi, vijana hukengeuka,nilijiwekea nadhiri kuwa nikipata fedha nyingi ntafanya biashara zangu,lakini ndoto yangu kubwa ni kujenga nyumba kubwa ambayo ntaishi na familia yangu,ingawaje bado sijaoa",aliongeza kusema Magembe.




Pichani kulia ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha kijana mwendesha boda boda,Mageme Daniel aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar

Maganga alisema kuwa mpaka sasa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umevunja historia kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 20 za Kitanzania,ambazo zimekwenda kwa Washindi mbalimbali wa Mzuka Jackpot,Washindi wa Mzuka Daily na washindi mbalimbali,ambapo washindi milioni 58 wamejitokeza kujishindia mamilioni ya TatuMzuka.

"Tatumzuka imeendelea kuwa fahari ya wachezaji wa mchezo wa kubahatisha kwa sababu ina uwezo wa kutoa washindi wengi,hivyo nawaomba Watanzania waendelee kucheza mchezo huu,na kwamba hamasa kubwa ni kuendelea kuwafikia washiriki wengi zaidi kila kona ya nchi yetu,kuhakikisha mchezo huu unakuwa fahari ya Watanzania,wenye kuwaletea tija ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali",alisema Maganga.



Pichani kushoto ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akiwa pamoja na kijana mwendesha boda boda,Magembe Daniel aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar.

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.