RIPOTI: IDADI YA WATALII WALIOINGIA NCHINI YAONGEZEKA

RIPOTI: IDADI YA WATALII WALIOINGIA NCHINI YAONGEZEKA

May 03, 2018

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu za watalii nchini kwa mwaka 2017 inayoonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa mwaka 2017. Kulia ni Kamishina wa Idara ya Uhamiaji, Hannelore Manyanga na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) Dkt. Albina Chuwa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsius Mdamu akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kukua kwa kasi kwa utalii wa fukwe na jinsi Idara ilivyojipanga kuimarisha fukwe zilizopo nchini wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu za watalii nchini kwa mwaka 2017, inayoonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa 2017.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru (katika) akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya kutathimini twakimu za watalii wakati wa uzinduzi wa taarifa ya takwimu ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka 2017, uliofanyika leo jijini Dar es Salam
Baadhi ya wadau wa sekta ya Utalii wakiwa kwenye kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam cha uzinduzi wa taarifa ya takwimu ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka 2017 huku ikionesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa 2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na wadau wa sekta ya utalii wakifuatilia uzinduzi wa taarifa ya takwimu ya watalii waliokuja nchini kwa mwaka 2017,Taarifa hiyo inaonesha watalii wameongezeka kutoka 1.2 milioni kwa 2016 hadi kufikia 1.3 kwa 2017.

Picha na Lusungu Helela- MNRT

…………………

NA LUSUNGU HELELA-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetaja idadi ya watalii walioingia nchini kuwa imeongezeka kutoka Milioni 1.2 Mwaka 2016 hadi kufikia watalii Milioni 1.3 mwaka 2017 huku watalii kutoka nchini Marekani wakiwa vinara.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni kukua kwa kasi ya uchumi huku ikisaidiwa na ujenzi wa miundombinu ya barabara katika hifadhi za Taifa.

Mbali na idadi hiyo, Serikali imetaja mapato yaliyopatikana kutokana na watalii hao kuwa yameongezeka kutoka wastani wa Dola za Kimarekani Milioni 2.1 Mwaka 2016 hadi kufikia Dola Milioni 2.2 Mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudance Milanzi amesema taarifa ya utafiti huo unaonesha kuwa Tanzania inazidi kufanya vizuri katika sekta ya utalii kwa vile kila mwaka idadi ya watalii na mapato yamekuwa yakiongezeka.

Awali, Milanzi alisema ripoti hiyo ya pamoja iliandaliwa kwa ushirikiano wa Benki Kuu Tanzania(BOT), Tume ya Taifa ya Takwimu(NBS), Idara ya Uhamiaji Zanzibar,

Kwa mujibu wa Milanzi, ripoti hiyo iliyopatikana kutokana na ‘survey’ iliyofanywa katika njia kuu za watalii, ikiwemo viwanja vya ndege pamoja na maeneo ya njia za mipaka ya kuingia nchini, pia imebaini idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini wanatoka katika nchi za Marekani, Uingereza, India, Uholanzi pamoja na Uswiswi.

Katika uzinduzi wa taarifa hiyo Milanzi amesema taarifa hizo zilikusanywa kupitia viwanja vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro(KIA), Abeid Aman Karume(Zanzibar) pamoja na mipaka ya Namanga, Tunduma, Mtukula na kwingineko, kwa kiasi kikubwa imechangiwa na idadi ya watalii walioingia nchini na kutembelea fukwe pamoja wanyamapori

Alisema kimsingi ongezeko la watalii waliongia nchini, pia limetokana na kasi ya kuvitangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini inayofanywa na Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) kupitia mamlaka iliyopewa ya kuvitangaza vivutio hivyo, zikiwemo mbuga za wanyama, fukwe, mlima Kilimanjaro na vinginevyo.

Aidha alisema mbali na vivutio hivyo pia siku za hivi karibuni Tanzania imekuwa ikipata wageni wanaofika nchini kwa ajili ya kupata matibabu katika hospitali zetu mbalimbali, ambao pamoja na huitaji wao katika masuala ya tiba, wanapata fursa ya kufanya utalii na hivyo kuchangia ongezeko katika eneo hilo.

Alisema ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Hifadhi za Taifa pia kwa kiasi kikubwa kumechangia kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini, hatua aliyosema kuwa itazidi kuutangaza utalii wetu.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Deograsius Mdamu amesema kwa sasa idara imeanza kuwekeza nguvu katika utalii wa fukwe kwa vile ni aina ya utalii ambao unaonekana kupendwa na watalii wengi wanaongiana nchini.

Wakati huo huo , amesema wanataraji kushirikiana na mamlaka mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Uendelezaji Uchumi(EPZA) katika kutangaza utalii.

Aidha alitaja changamoto mbalimbali zilizokuwa zinazowakabili watalii, ikiwemo masuala ya viza pamoja na huduma za kifedha kupitia utaratibu kadi maalumu, ni maoneo yanayoendelea kufanyiwa kazi na Wizara hiyo ili kuzidi kuutangaza utali hapa nchini.

UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE

May 03, 2018



Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (wa pili kulia) pamoja na Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem (kushoto).

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa kwanza kushoto), Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege ( wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung Tanzania, Andreas (wa pili kulia) pamoja na Meneja Programu wa Tanzania Media Fund (TMF), Razia Mwawanga (kulia)

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Programu wa Tanzania Media Fund (TMF), Razia Mwawanga mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo (katikati) kuhusu ripoti ya uvamizi wa kituo cha habari cha CLOUDS wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Tehama na Programu za Vyombo vya Habari wa TMF, Baraka Kiranga (kushoto) kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mwandishi wa kujitegemea Adelina Johnbosco (katikati) pamoja na Mtayarishaji bora wa makala na vipindi vya TV kuhusu utalii na uhifadhi, Anwary Msechu (kulia).

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimpongeza Mtayarishaji bora wa makala na vipindi vya TV kuhusu Utalii na Uhifadhi, Anwary Msechu ambaye alishinda tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) katika kipengele cha mwandaaji bora wa makala na makala bora iliyohusu malipo duni ya kwa wapagazi Mlima Kilimanjaro wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mratibu wa Miradi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, Amon Petro akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuhusu malengo ya taasisi hiyo ambayo ni Kukuza Demokrasia, Utawala Bora na Haki Jamii ambapo alieleza ili kufikia malengo hayo wanafanyakazi na asasi mbalimbali za kiraia, vyama vya siasa na vyama vya wafanyakazi pamoja na waandishi wa habari wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, Mwandishi wa kujitegemea Adelina Johnbosco, Mdau wa tasnia ya Habari na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Innocent Mungy pamoja na Mtayarishaji bora wa makala na vipindi vya TV kuhusu Utalii na Uhifadhi, Anwary Msechu ambaye alishinda tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) katika kipengele cha mwandaaji bora wa makala na makala bora iliyohusu malipo duni ya kwa wapagazi Mlima Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja banda la maonyesho la TMF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mshehereshaji wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Neville Meena akitambulisha meza kuu katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari akitoa salamu za MISA-TAN wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit, akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Audrey Azoulay wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa salamu za Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Fausta Musokwa akitoa salamu za TMF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, Andreas Quasten akizungumza wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akitoa salamu za TEF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akitoa salamu za UTPC wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mwakilishi waandishi wa habari wakongwe (Veterans), Kiondo Mshana akitoa salamu za Ma-Veterans ambapo alisema amani tuliyonayo inadumu kutokana na weledi wa uandishi wa habari nchini wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akitoa salamu za taasisi hiyo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart akitoa salamu za Umoja huo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akichambua ripoti inayohusu uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari kabla ya kuikabidhi kwa Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akimkabidhi Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe nakala ya ripoti inayohusu uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizundua Ripoti ya tathimini ya Hali ya Habari Tanzania 2017 - So This is Democracy? Iliyoandaliwa na MISA-TAN wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Gasirigwa Sengiyumva (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Mawasiliano Msaidizi wa MISA-TAN, Fredy Njeje (kushoto aliyeketi).

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa Kujitegemea, Rose Haji Mwalimu wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mkuu wa wilaya ya Kongwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Deogratius Ndejembi akizungumza na washiriki wakati akifunga kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakongwe (Veterans) mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri, Mameneja wa Redio za Jamii na Waandishi wa habari mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki, wadau wa habari na wanafunzi wa Dodoma College of Jorunalism mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.


Na Mwandishi wetu


VYOMBO vya habari nchini vimekumbushwa kwamba uhuru wa habari sio kuiangalia tu serikali, bali kujiangalia wenyewe na pia vyombo vyao vya habari.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akihutubia hadhira ya waandishi wa habari katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, sherehe zilizofanyika kitaifa katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.

Katika hotuba yake baada ya kusikiliza hoja kadha kutoka taasisi mbalimbali kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari nchini na hisia kwamba vinaminywa Waziri huyo alisema kwamba ipo haja ya tasnia kujiangalia yenyewe kama inatenda haki na weledi kwa taifa hili.


“Kalamu ya ...

DK. KIGWANGALLA ASEMA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE, AAHIDI KUSHUGHULIKIA KERO ZAO

May 03, 2018


Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi wa kata ya Nkimiziwa jimboni humo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi. Akiwa jimboni humo alitembelea pia kata ya Ndala ambapo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi na viongozi wa chama na Serikali wa kata ya Nkimiziwa jimboni humo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi ambapo aliwataka viongozi wa chama na Serikali ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi mkoa kuwasilisha kwake kero za wananchi wa jimbo lake ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi na viongozi wa chama na Serikali wa kata ya Nkimiziwa jimboni humo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi ambapo aliwataka viongozi wa chama na Serikali ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi mkoa kuwasilisha kwake kero za wananchi wa jimbo lake ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.


Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi na viongozi wa chama na Serikali wa kata ya Nkimiziwa jimboni humo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi ambapo aliwataka viongozi wa chama na Serikali ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi mkoa kuwasilisha kwake kero za wananchi wa jimbo lake ili aweze kuzitafutia ufumbuzi.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wananchi wa kata ya Nkimiziwa jimboni humo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi. Akiwa jimboni humo alitembelea pia kata ya Ndala ambapo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye, Dk. Hamisi Kigwangalla akishiriki kwenye maandamano na wananchi, viongozi wa chama na Serikali wa kata ya Nkimiziwa jimboni humo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi.

MKONGWE NDIMARA ATAKA SERIKALI KUTOPEWA SABABU YA ‘KUBANA’ WAANDISHI WA HABARI

May 03, 2018





Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung Tanzania, Andreas Quasten (kushoto) pamoja na Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem (kulia) wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi akisalimiana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari zinazofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem




Mshehereshaji wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Innocent Mungy (katikati), Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Gasirigwa Sengiyumva wakipitia ratiba ya maadhimisho hayo yanayofanyika katika hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akisalimiana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa tatu kushoto), Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem (wa pili kulia) pamoja na Mshehereshaji wa kongamano hilo, Innocent Mungy (kulia).




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai (wa tatu kulia) akiongozana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia), Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndenjembi (kushoto) kuelekea kwenye mabanda ya maonyesho mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipitia nakala ya gazeti la Majira huku akipata maelezo kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira, Imma Mbuguni (wa pili kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kulia ni Meneja Usambaza wa Gazeti la Majira, Sophia Mshangama.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mjenga Uwezo wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Deogratius Bwire kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari zinazofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Deo Ndenjembi (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa tatu kushoto)




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipokea nakala ya gazeti la Mwananchi kutoka kwa wafanyakazi wa Mwananchi Communications wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Wakurugenzi na Mmiliki wa Gazeti la Jamhuri Deodatus Balile wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akipokea majarida na machapisho mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kutoka Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakati alipotembelea banda la UN kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena mjini Dodoma.




Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kuhusiana na kitabu cha Maadili ya Uandishi wa Habari wakati alipokuwa akitembelea banda la Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Logistic wa Baraza hilo, Athuman Mbegu.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano tayari kuanza kwa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mshehereshaji wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Innocent Mungy akiwakaribishwa meza kuu, wanahabari na wadau wa habari kwenye kongamano la maadhimisho hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Meza kuu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji.




Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akitoa salamu za Unesco wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kufungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumzia malengo ya maendeleo endelevu na jukumu la waandishi wa habari kutumia nafasi zao kutoa taarifa kuhusu malengo hayo kwa jamii ili yatekelezeke kwa urahisi, katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa kujitegemea, Rose Haji Mwalimu akiongoza mjadala kuhusu mada: Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mwandishi wa Habari Nguli, Ndimara Tegambwage na mwezeshaji wa mada inayohusu; Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka: wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.



Wakili na Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, James Marenga akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Nashera jijini Dodoma.




Mdau wa Habari Ernest Sungura akishiriki kuchangia maoni katika mjadala uliowasilishwa na mwandishi nguli Ndimara Tegambwage (hayupo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.




Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege (kulia) na Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

























Pichani juu na chini Sehemu ya washiriki ambao ni wahariri, waandishi wa habari, wadau wa tasnia ya habari na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.


Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakiwemo wahariri, wadau wa habari na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma


Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Ubalozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari vya kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma

Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja waandishi wa habari wakonge (Veterans) waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.