Mhe. Samia asema : Ofisi yangu imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, Ni baada ya kuhamia Dodoma rasmi

December 15, 2017
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.

Akizungumza wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.

“Siku ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza Mhe. Samia.Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji miti .

“Tarehe 21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza azma hii” ameongeza Mhe. Samia.Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.

“Tunaendelea kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi 2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali na kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine” amefafanua Waziri Mkuu.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.

“Sikuwaza kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.

Kwa upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.

Mbali na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima, hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha kuandaa mashamba.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa na na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa Rais Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2017.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

SERIKALI YAIAGIZA MAKUMBUSHO YA TAIFA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO

December 15, 2017


  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto)  akizungumza leo na Watumishi wa Makumbusho ya Taifa makao makuu jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara jana ya siku moja ya kutembelea makumbusho hiyo  pamoja na kijiji cha  makumbusho. Kulia na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Fortunatus Mabula pamoja na Katibu wa Naibu Waziri, Zulu ngondya ( wa kwanza kushoto)  (Picha na Lusungu Helela-MNRT)




  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga  akipata maelezo kutoka kwa  Afisa Elimu, Anamery Bagenyi ( wa kwanza kulia)  kuhusiana na  baadhi ya  magari yaliyokuwa yakitumika Ikulu  na Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa uongozi wake.  Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Fortunatus Maabula pamoja na Katibu wa Naibu Waziri, Zulu ngondya ( wa nne kulia) (Picha na Lusungu Helela-MNRT



  1. Baadhi ya Watumishi wa Makumbusho ya Taifa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipofanya leo    kwenye Makumbusho ya hayo  makao makuu jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu Helela-MNRT




  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, ( wa pili kushoto)  Japhet Hasunga akiwa ameongoza na Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa wakati alipofanya leo  ziara ya siku moja   kwenye Makumbusho ya Taifa makao makuu jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu Helela-MNRT



Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameipa Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa muda usiozidi miezi miwili iwe ishabuni vyanzo vipya vya mapato ili iweze kutatua changamoto mbalimbali  zinazoikabili baadala ya kutegemea ruzuku pekee kutoka serikalini.
Amesema Makumbusho ya Taifa ina mali nyingi lakini imekuwa hajui namna ya kuzitumia ‘’Mkae chini mnambie namna gani mnaweza kuongeza mapato katika rasilimali mlizo nazo  halafu mniletee andiko  ofisini kwangu ndani ya muda usiozidi miezi miwili ’’ Aliagiza
Amesema kazi kubwa ya Makumbusho ya taifa ni kuhifadhi lakini wakati ikihifadhi inahitaji kupata mapato kidogo hapo hapo ili iweze kuendelea kuwepo.
Aliyasema hayo  leo  alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Makumbusho ya Taifa makao Makuu jijini Dares Salaam wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujionea namna Taasisi hiyo inavyofanya kazi
,Aliwataka Watumishi hao wasitumie muda mwingi  kulalamika baadala yake wasaidie katika kubuni vyanzo vipya vya mapato ili viwasaidie katika kujikwamua kimapato.
Naibu Waziri Hasunga aliongeza kuwa, licha ya Serikali  ya kutambua umuhimu wa Makumbusho hayo lakini hata hivyo Serikali imekuwa na masuala mengi yakufanya na yanayohitaji pesa katika kuyashughulikia.
Wakati huo huo, Ameiagiza taasisi hiyo ijitangaze kwa vile imekuwa haijulikani licha ya  kuwa na umuhimu mkubwa katika kuihudumia jamii.
‘’Mmekuwa mnafanya mambo makubwa  kisiri kisiri kwa ajili ya wananchi lakini wananchi mnaowahudumia hawajui mnayoyafanya kwa ajili yao hivyo jitangazeni’’  alisisitiza.
Pia, Aliwaagiza watumishi kuendelea kufanya tafiti ili waweze kuvumbua mambo mengi zaidi yatakayoisadia Taasisi hiyo kuweza kupiga hatua katika kuihudumia jamii.
‘’Sisi kama serikali hatujaweza kufanya vizuri katika eneo la utafiti tumekuwa  tukitenga bajeti ndogo lakini kwa kulitambua hilo nataka mpate pesa ya kutosha ili mfanye tafiti nyingi zaidi’’ alisisitiza
Aidha, Ameiagiza Menejimenti hiyo iimarishe mfumo wa ndani katika masuala ya Tehama, alisema haiwezekani taasisi hiyo hadi hivi sasa isiwe na kanzidata licha ya changamoto kubwa ya udukuzi unafanywa na mataifa makubwa katika masuala ya uhifadhi.
 Awali, Mkurugenzi Mkuu, Prof. Fortunatus Mabula amemuhakikishia Naibu Waziri Hasunga   ushirikiano mkubwa katika kazi.
Aidha, Prof. Mabula alimwambia  Naibu Waziri kuwa tayari wameshapata eneo la kujenga makumbusho ya Marais katika eneo la Iyombe  mjini Dodoma ikiwa ni kutekeleza agizo alilolitoa Waziri  wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla alipozungumza na wadau wa Wizara mwezi uliopita mjini Dodoma