HAPA KAZI TU

October 15, 2015
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

MAGUFULI AHUTUBIA KISIWANI PEMBA LEO,AAHIDI KUULINDA MUUNGANO KWA NGUVU ZOTE.

October 15, 2015
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.

Katika mkutano huo wa Kampeni,Dkt Magufuli ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano,atadumisha na kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulioanzishwa na Waasisi wetu akiwemo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Abeid Amani Karume.Dkt Magufuli kesho atahutubia kwenye mkutano mkubwa wa kampeni mjini Unguja.
Wananchi wa Kisiwani Pemba wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale ,wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao. 
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.Dkt Shein amewataka wakazi wa Kisiwani Pemba kuilinda amani iliyopo ndani ya kisiwa hicho na kuwa Wananchi wakajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu Mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana Mama Shadia Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Gombani ya Kale kwa ajili ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo kisiwani Pemba.
Umati wa wakazi wa kisiwani Pemba kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa kiswani Pemba wakifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,kwenye uwanja wa Gombani ya kale kisiwani humo.
Wananchi wa kiswani Pemba wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein walitumia jukwaa na mkutano huo kuwaomba kura za kutosha ili wakaiongoze Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.

PICHA NA MICHUZI JR-PEMBA


-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA TANZANIA.ZANZIBAR

October 15, 2015

Viongozi wa Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wa kuomba Dua Mkutano huo wa Baraza la Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania uliovikutanisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tamzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.wa kwanza Jaji Lubuva Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Mzirai na Msajili Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzani Mhe Ibrahim Mkwawa.
Mmoja wa Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania akiuombea Mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. ukizungumzia maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania .
 Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiitikia dua kabla ya kuaza kwa mkutano huo kuutakia baraka 

 Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Peter Mzirai kuaza kwa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tanzania.
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakimsikiliza Mtoa Mada Msaidizi Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Ibrahim Mkwawa, akiwasilisha mada ya Maadili iliotiwa saini na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Msajili Msaini wa Vyama vya Siasa Tanzania Mhe Ibrahim Mkwawa akiwasilisha Mada ya Maadili ya Vyama vya Siasa kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wote wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu mwezi huu. 
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakifuatilia Mkutano Huo. katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiwa makini wakifuatilia mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania ukizungumzia Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanxzania unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Viongozi wa Chama cha TADEA wakifuatila mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania. 
Viongozi wa Chama cha AFP wakifuatilia mkutano huo kwa makini unaozungumzia Maadilidi ya Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot Zanzinews.com.
Mobeli No 0777 424152 or 0715424152
Email, othmanmaulid@gmail.com.

RAIS JAKAYA KIKWETE KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO

October 15, 2015

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza na waandi wa habari wapo picha juu ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.kikao hichi kimefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza juu ya ujenzi huo na  Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na  Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbarimbari na Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba kwenye maeneo ya mji huo.
Akizungumza na wandishi wa habari badaa ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Merchants Group itakayosimamia ujenzi huo, Dk Hu Jianhao, Membe alisema katika ujenzi huo utakaochukua hekta 2400, wananchi wote watakaohuswa hawataachwa bure.
“Mradi huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group, wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi,” alisema.
Mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.
Mazungumzo hayo ni sehemu ya awali ya maandalizi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo, katika sherehe inayotarajiwa kuongozwana Rais Jakaya Kikwete leo.
Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka jana, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi huo.
Eneo hilo  litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).
Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.
Dk Turuka alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano.
Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.
Kwa mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.
mwaka 2008, Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.
Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.
Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo, Shehe Abdullah Al Saadi.

DK. MAGUFULI APOKELEWA KWA NDEREMO NA VIFIJO KISARAWE NA UKONGA WAKATI WA MKUTANO WA KUOMBA KURA

October 15, 2015
 Wananchi wa Jimbo la Kisarawe, mkoani Pwani wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kisarawe leo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kisarawe, Seleman Javo wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kisarawe leo.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiwanadi wagombea wa viti maalum wa Kisarawe.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akionyesha picha aliyochorwa.mm
 Wakazi wa Mombasa, Ukonga, Dar es Salaam wakiuzuia msafara wa Dk Magufuli ulipokuwa ukitoka Kisarawe kwenda eneo Moshi Bar kuendelea na kampeni.
 Shamra shamra za kumpokea Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli mapema leo, wakati akielekea Ukonga katika barabara ya Moshi - Bar.
 Msafara wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli ukipokelewa kwa nderemo na vifijo.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akiingia Ukonga katika mkutano wake wa kuomba kura.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Ramadhan Madabida  akimnadi Dk. Magufuli kwa wakazi wa Ukonga.
 Akina mama wakiwa na nyuso za furaha.
 Umati wa watu waliohudhuria mkutano huo.
Kila mmoja akitaka kumuona mgombea.
Dk. Magufuli akitoa ahadi ya ujenzi wa Barabara ya Mombasa hadi Moshi Baa kwa kiwango cha Lami.
 Mmoja ya wafuasi wa CCM akisiliza sera za mgombea Urais wa Tanzania, Dk. John Magufuli huku akiwa amebeba mboga mboga zake.
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akinyooshewa vidole gumba na wakazi wa Jimbo la Ukonga ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura ya ndiyo , wakati wa mkutano wa kampeni eneo la Moshi Bar, Ukonga Dar es Salaam.
Dk. Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo. Dk. Magufuli akiwanadi wagombea wa viti maalum wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo. -- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''