KIWANDA CHA RHINO CEMENT CHA TANGA CHAFUNGIWA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

KIWANDA CHA RHINO CEMENT CHA TANGA CHAFUNGIWA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

March 17, 2016

 3 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akitolea ufafanuzi namna ambayo fukwe ya Pangani imeathirika na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
4 
kushoto meneja mkuu wa kiwanda cha maziwa cha tanga fresh Bw. Michael Kalata, akimuonyesha mh Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, moja nya bidhaa ya maziwa inayozaliswa katika kiwanda hicho. mh Mpina alitembelea baadhi ya viwanda jijini tanga kujionea namna ambavyo vinatekeleza sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake.
5 
Mh Luhaga Mpina Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira mwenye  nguo nyeusi akipata maelezo toka kwa mtaalam katika kiwanda cha Twiga cement alipokitembelea leo jijini tanga kuona namna ambavyo kiwanda hicho kinatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
12 
Pichani Namna ambavyo fukwe ya Pangani Jijini Tanga ilivyoliwa na maji ya bahari, kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari ikiwa ni athari zitokanano na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. na baaadhi ya visiwa nchini viko hatarini kumezwa na bahari.
Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi
…………………………………………………………………………………………….
NA EVELYN MKOKOI TANGA Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (MB) amekifungia kiwanda cha kuzalisha cement na chokaa kilichopo jijini Tanga cha Rhino Cement, leo jioni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni uharibu na uchafuzi wa mazingira na kuvunja sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake. Mh. Mpina amechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya maweni kupitia diwani wa kata hiyo Bw. Joseph Colvas na kujionea mwenyewe namna ambavyo kiwanda hicho kinavyo achilia moshi mzito kwenda angani, pamoja na vumbi lisilovumilika kusambaa katika maeneo ya makazi ya wanachi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaa katika maeneo ya shule ya sekondari ya Don Bosco ambapo, Mh. Mpina ameelezwa kuwa athari zitokanazo na uachiachi wa hewa hiyo chafu angani si tu kwa watoto wa shule zinazozunguka kata hiyo bali pia ni kwa viumbe hai na mazingira. “Hawa jamaa wamekuwa wakiachilia vumbi jingi na moshi mzito kutoka katika kiwanda hiki mara kwa mara, hivi tangu jana wamezima mitambo yao wakijua kabisa kuwa kuna ugeni wa Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Alisisitiza Bw. Joseph.” Kwa upande wake Afisa Afya wa jiji la tanga aliyejulikana kwa jina moja la bwana Kizito alimuelezea Naibu Waziri Mpina kuwa ni kweli kiwanda hicho kimekuwa kikifanya uchafuzi huo wa mazingira, na Afisa uendeshaji kutoka Baraza la Taifa na HIfadhi ya Mazingira NEMC Bw. Novatus Mushi ameeleza kuwa kiwanda hicho kimeshawahi kutozwa faini ya shilingi milioni kumi na saba (17) kwa kosa la kuchelewa kulipa ada ya mwaka ya mazingira pamoja na uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa na kiwanda hicho kwa upande wa kuzalisha chokaa. Mh. Mpina ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kukifunga kiwanda hicho kisiendelee na uzalishaji kwa muda usiopungua miezi mitatu, na kulitaka baraza hilo lijiridhishe na kufuatilia namna kiwanda hicho kinavyotakiwa kutekeleza sheria ya mazingira kwa kujenga mfumo wa kisasa wa kutoa taka zitokanazo na uzalishaji kiwandani hapo pamoja, na kupima vumbi na moshi utokao kiwandani hapo kama hautakuwa na madhara na athari kwa mazingira na viumbe hai. Kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa moja kwa moja. Aidha, akitolea mfano wa kiwanda cha bonite bottles cha mjini moshi kwa kuwa kinara katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira, mh Mpina alivitaka viwanda vingine viige mfano wa kiwanda hicho cha coke cola. Ziara ya Mh. Mpina Jijini Tanga ilihusisha pia kuangalia namna ukuta wa fukwe ya Pangani uliojengwa enzi za mkoloni, ulivyo athirika na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kusema kuwa, ukuta huo huko kwenye mchakato wa kujengwa na kuboreshwa upya, ifikapo mwezi wa nne mwaka huu mradi wa ujenzi wa ukuta huo utaanza kutekelezeka kwa kuwa tenda imeshatangazwa na jumla ya kiasi cha fedha za kimarekani dola milioni 1,400 zimepatikana kupitia mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCf). Mh. Mpina aliwaasa wakazi wa mji wa Tanga na viunga vyake kutunza mazingira kwa kupanda miti na kufanya usafi kama ilivyoagizwa na serikali, ili kuhepukana na nchi kuwa janga na magonjwa yatokanayo na uchafu. Waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh na kiwanda cha Tanga Cement na kuridhirishwa na namna ambayo wanatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

MAKALA ATAKA SUALA LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU LIWE HISTORIA MKOANI MBEYA

March 17, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abasi Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akizungumza na watumishi  waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu .
KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

March 17, 2016

01
 Mbunge wa Busega na Kaimu  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za kurekebisha  zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia jamii katika suala zima la afya  , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
1
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika ofisi za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
2
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
3
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.
5
Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mh. Azzan Zungu,  Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe, Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni, Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndugulile, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF Bw. Michael Muhando na  Mkurugenzi wa huduma za utabibu na ufundi Dk.Frank Lekey wakielekea kwenye mkutano.
6
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.
7
Wajumbe wa kamati hiyo wakisikiliza wakati Kaimu Mkurugenzi wa NHIF alipokuwa akiwasilisha ripoti ya shirika hilo kwa kamati hiyo leo.
8
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
9
Mjumbe wa kamati Mbunge wa Buchosa Mh. Dk Charles Tizema akitoa mchango wake katika mkutano huo. 
11
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati na Mbunge wa jimbo la Buseka Dk. Raphael Chegeni.
12
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
13
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
15
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
16
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa  NHIF Bw. Michael Muhando wakati akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko huo.