HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA YAZIDUA UPIMAJI USIKIVU WA WATOTO WACHANGA
Waziri
wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango
wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto)
mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Daktari
Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika
uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika
Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Waziri
wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa
kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Mjumbe
wa Bodi ya ZOP Yahya Mohammed Slim akitoa maelezo kuhusu Jumuiya hiyo
inavyotoa huduma za kijamii vijijini katika usinduzi wa kuwapima usikivu
watoto wachanga.
Wafanyakazi
wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga
wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
baadhi
ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto
wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mvuvi katika kisiwa cha Yozu wilaya ya Sengerema Aibuka na Toyota IST
Kaimu
Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru akimkabithi
gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa
wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni
ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel,Bi. Jane
Matinde.
Mshindi
wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso
akifungua gari mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya
kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema
Mwanza. akishuhudia ni Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel David
Wankuru.
Mshindi
wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso
akiwa ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara
baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya
Sengerema Mwanza.
Kaimu
Katibu wa Wilaya ya Sengerema Bwana Aaron L Laizer ( wa pili kushoto)
akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi
na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa
promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa
Airtel Bi Jane Matinde na Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel
Bwana David Wankuru.
Mkazi
wa wilaya ya sengerma na mvuvi katika kisiwa cha Yozu bwana Kijiji Gweso
Jana amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel yatosha
zaidi.
Akiongea
wakati wa halfa ya kukabithiwa gari lake Bwana kijiji Gweso alisema”
nilipopigiwa simu na Airtel nilipuuzia sikuamini kabisa kama nimeshinda
gari mpaka ndugu zangu waliponipigia na kunihakikishia kuwa mimi
nimetangazwa mshindi ndipo nilipoenda ofisi za Airtel na kukuta kweli
nimejishindia. Mimi ni mvuvi na mke na watoto wawili na nilinunua
kifurushi cha Airtel yatosha cha mia tano tu na furahi sana kushinda
gari hili kupitia promosheni hii”.
“Sijawahi
kumiliki gari hivyo usafiri huu utanisaidia katika shughuli zangu za
uvuvi, za kifamilia na kiuchumi kwa ujumla, nachukua fulsa hii kuwaambia
watanzania wenzangu waamini kuwa Airtel inatoa magari na kwamba wao pia
wanaweza kuwaibuka washindi. Nawashukuru sana Airtel kwa kuboresha
maisha yangu na yawatanzania wengine walioshinda kama mimi”aliongeza
Gweso.
Akiongea
wakati wa kukabithi gari kaimu katibu wa wilaya ya sengerema bwana
Aaron L Laizer alisema” nampongeza sana bwana Kijiji Gweso kwa kuibuka
mshindi, ushindi huu umetuthihirishia wakazi wa sengerema kuwa
promosheni hii ya ya ukweli na zawadi zinatolewa. Tunawashukuru sana
Airtel kwa kutoa huduma bora za mawasiliano nchini ambazo zimerahisisha
shughuli za kiuchumi, kijamii na kiusalama lakini pia kuanzisha
promosheni inayowazawadia wateja wake, na kwa wananchi wa sengerema na
wa mwanza kwa jumla hii nifulsa kwetu tuendelee kutumia huduma za Airtel
na kupata nafasi ya kushinda”.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa kanda ya Airtel Bwana David Wankuru alisema “
promosheni hii bado inaendelea mpaka sasa ni washindi 24
tumeshapatikana , magari bado yapo hivyo natoa wito kwa wakazi wa kanda
yangu na watanzania kwa ujumla kuweza kushiriki. Tunafurahi kuwa na
washindi wane mpaka sasa kutoka katika kanda ya ziwa washindi hawa ni
pamoja na Bi Ester Mathias Mashauri muuguzi bugando, Bi kajala kokutima
said mkulima na mkazi wa bukoba, Seleman Daudi Onesmo mkazi wa nyakato
Mwanza na leo tunamkabithi gari bwana Kijiji Gweso mkazi wa Sengerema’.
Wankuru
aliongeza kwa kusema “kujishindia unatakiwa kujinga na kifurushi
chochote cha Airtel yatosha cha siku, wiki au mwenzi kwa kupiga *149*99#
au kununua vocha ya Airtel yatosha au kwa kununua kupiita huduma ya
Airtel Money, baada ya kununua kifurushi chako namba yako moja kwa moja
itaingizwa kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya
Toyota IST kila siku”.
Promosheni
ya Airtel yatosha Zaidi ilizinduliwa na kampuni simu za mkononi ya
Airtel Mwanzoni mwa mwenzi wa Februari, watanzania wengi kutoka katika
mikoa mbalimbali wameweza kujishindia magari na kubadili maisha ya
kupitia promosheni hii. Magari 24 yameshapata washindi toka promosheni
hii ianze hadi sasa.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME YA REA MKOANI DODOMA
Mtaalam kutoka kampuni ya
kitanzania ya Derm Electric inayojenga miundombinu ya umeme katika mkoa
wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Azizi Msuya
(kushoto) akiielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika mkoa wa
Dodoma katika eneo iliyopo bohari ya kuhifadhi vifaa vya ujenzi vya
kampuni hiyo, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kamati hiyo inafanya ziara
kwenye miradi ya umeme mkoani Dodoma lengo likiwa ni kujionea
utekelezwaji wake pamoja na kuzungumza na wawakilishi wa wananchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa (kushoto) akitoa maelekezo
kwa wataalamu wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara kamati hiyo
ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya umeme katika kijiji cha Msanga
kilichopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mtaalam kutoka kampuni ya
kitanzania ya Derm Electric inayojenga miundombinu ya umeme katika mkoa
wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Azizi Msuya (wa pili
kutoka kushoto) akielezea Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini, wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na wataalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa katika usambazaji
wa miundombinu ya umeme katika eneo la Kibaigwa wilayani Kongwa mkoani
Dodoma. Kamati hiyo iliiagiza kampuni hiyo kuweka miundombinu ya umeme
katika vijiji vilivyosahaulika.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chambani- Pemba,
Yusuph Salim (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalamu kutoka Shirika
la Umeme Nchini (Tanesco) na Wizara ya Nishati na Madini (hawapo
pichani)
Meneja wa Shirika la Umeme Nchini
(Tanesco) Dodoma, Zakayo Temu ( wa pili kutoka kulia) akielezea mikakati
ya shirika hilo katika usimamizi wa miradi inayofadhiliwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini, wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)
na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Geita,
Josephine Chagula ( wa tatu kutoka kulia) akitoa ushauri kwa kampuni ya
kitanzania ya Derm Electric inayojenga miundombinu ya umeme katika mkoa
wa Dodoma chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wa namna ya
kuboresha kasi ya usambazaji wa miundombinu ya umeme katika mkoa wa
Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa, Murtaza
Mangungu (katikati) akilishauri Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) namna
bora ya kuwawezesha wananchi kuunganishiwa na huduma ya umeme mara baada
ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya umeme inayotekelezwa na
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili.
KWAMBA SASA KUMEKUCHA,HIVI NDIVYO OFISI MPYA YA BAYPORT FINANCIAL INAVYOONEKANA
Hivi ndivyo ofisi mpya ya tawi la 79 la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services wilayani Kwimba, mkoani Mwanza inavyoonekana kwa mbele siku lilipozinduliwa rasmi mapema wiki hii, huku mgeni rasmi akiwa ni Vicent Emmanuel, Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba, hayupo pichani.
Katibu Tawala wa wilaya Mwanza, Vicent Emmanuel wa pili kutoka kulia, akiangalia matukio tofauti katika uzinduzi wa tawi la Bayport Financial Services, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia kwa Katibu Tawala ni OCS Adam Amir, akiafutiwa na Meneja wa Bayport Mwanza, August Tesha. Bayport wamezindua tawi la 79 nchi nzima kwa ajili ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
MAN UNITED SAMBAMBA NA IlKAY GUNDOGAN
Baada
ya klabu ya Manchester United kupwaya katika nafasi ya kiungo siku za
hivi karibuni, klabu hiyo chini ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal yenye
maskani yake katika dimba la Old Trafford, ipo mbioni kumfukuzia kiungo
wa klabu ya Borrusia Dortmund Ilkay Gundogan.
Gundogan
ambaye amekuwa akifanya vizuri katika mechi za karibuni akiwa na klabu
yake ya Dortmund sasa ameonekana Lulu kwa Manchester United huku klabu
hiyo ikifanya jitihada za kumpeleka Old Trafford.
MAGEREZA WAJIFUA TAYARI KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Sehemu
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi makali
katika mitaa ya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima
Kilimanjaro ifikapo Machi 6,2015. Katikati (mwenye vazi jeupe) ni
Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy kutoka Makao Makuu ya
Magereza, wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Mbezi
Ramadhani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga na wa kwanza
kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Jamhuri Yassin kutoka Makao Makuu ya
Magereza, Dar es salaam.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya
kutembea katika viunga vya Manispaa ya Moshi ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6, 2015. Kutoka kushoto ni Mkaguzi
wa Magereza Vicent Magessa kutoka Gereza Bagamoyo Mkoa wa Pwani,
Mkaguzi wa Magereza Tumaini Kihampa na Mkaguzi wa Magereza Jamhuri
Yassin wote kutoka Makao Makuu ya Magereza.
Maafisa
na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa
katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015. Wa sita kutoka mbele
ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomiah Hamis na wa mwisho ni
Mkaguzi wa Magereza Abas Mikidadi.
Maafisa
na Askari na baadhi wa watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa
katika mazoezi makali ya kupita katika njia ngumu ikiwa ni maandalizi ya
kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Machi 6, 2015.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika mazoezi ya
viungo baada ya kutembea na kukimbia katika viunga vya Manispaa ya
Moshi ikiwa ni maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro mnamo Machi 6,
2015.
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipata kifungua kinywa
baada ya mazoezi mazito ya maandalizi ya kupanda mlima Kilimanjaro
ifikapo Machi 6,2015. Maafisa hao wako kambini eneo la Gereza Karanga
mjini Moshi.
Baadhi
wa washiriki wa Kilimanjaro Marathon Machi 1, 2015 mbio ambazo baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walishiriki ikiwa ni
maandalizi ya kupanda Mlima Kilimanjaro mnao Machi 6, 2015. Picha zote
na Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja
Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini
Balozi Lu Youqing akizungumza na Mhe. Membe |
Maafisa walioambatana na Balozi Lu wakinukuu mazungumzo akiwemo Kaimu Mkuu wa masuala ya Siasa katika Ubalozi huo, Bw. Li Xhuhang (kulia). |
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya (kulia) na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba nao wakisikiliza mazungumzo hayo. |
Mazungumzo yakiendelea |
WaziriMembe akiagana na Balozi Lu Youqing mara baada ya mazungumzo yao.
Picha na Reginald Philip.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)