Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi alihutubia Bunge Dodoma

Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi alihutubia Bunge Dodoma

May 19, 2015


C2
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Anna Makinda akimkaribisha Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge hilo.
C3 C5
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
C6
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia.
C7
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
C9 C10
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge lao mjini Dodoma(Picha na Freddy Maro)
MANISPAA YA KINONDONI YAENDELEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUONDOA MAJI KWENYE MAKAZI YA WATU TEGETA, BUNJU NA KUNDUCHI NA KUJENGA MFEREJI WA KUDUMU KUPITISHA MAJI KUELEKEA BAHARINI.

MANISPAA YA KINONDONI YAENDELEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA KUONDOA MAJI KWENYE MAKAZI YA WATU TEGETA, BUNJU NA KUNDUCHI NA KUJENGA MFEREJI WA KUDUMU KUPITISHA MAJI KUELEKEA BAHARINI.

May 19, 2015

AT1
Mkuu wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi.
AT2
Kazi ya ujenzi wa mfereji huo mkubwa wenye urefu wa kilometa 2.1 ikiendelea katika eneo la Kunduchi Ununio.
AT3
Maji yaliyotuama yakiwa bado yamezingira nyumba na makazi ya watu eneo la Boko jijini Dar es salaam ambayo harakati za kuyaoondoa zinaendelea kufanywa na manispaa ya Kinondoni.
AT4
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo la Basihayo Tegeta.
………………………………………………………………….
Na.Aron Msigwa- MAELEZO .Dar es Salaam.
Manispaa ya Kinondoni inaendelelea kujenga mfereji wa kudumu wenye urefu wa Kilometa 2.1 ili kuondoa maji yaliyojaa kwenye makazi ya watu, eneo la Basihayo -Tegeta,Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa hivi karibuni mara baada ya kuwatembelea wananchi katika maeneo hayo walioathiriwa na mafuriko.
Akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo kujionea utekelezaji wa agizo hilo leo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki amesema kazi ya ujenzi wa mfereji huo utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 900 inafanyika kwa kasi inayoridhisha licha ya ugumu uliopo wa kutafuta uelekeo wa maji hayo kutoakana na uwepo wa makazi ya watu.
Amesema ujenzi wa mfereji huo mkubwa unakwenda sambamba na kazi ya uondoaji wa maji ya mvua yaliyojaa katika makazi ya watu katika eneo la Basihaya inayofanywa na Shirika la maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam huku Manispaa ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Muhandisi wake Baraka Mkuya ikiendelea na uchimbaji wa mfereji wa juu na ule utakaopita chini ardhi kuelekea baharini.
Amesema kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi mkubwa bila kuathiri makazi ya watu na kulazimika kulipa fidia kwa wananchi Manispaa hiyo inaendelea kuzungumza na baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yatatumika kupitisha mfereji huo waruhusu kazi hiyo iendelee huku taratibu nyingine zikiendelea kufanyika.
Aidha amesema kwa baadhi ya wananchi waliojenga kuta na nyumba kwenye mkondo wa maji hususani eneo la Kunduchi Ununio na kuzuia maji kuelekea baharini maeneo yao yatabomolewa na baadhi ya hati za viwanja kufutwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Nati akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo kushuhudia zoezi la uondoaji wa maji na ujenzi wa mfereji huo amesema kuwa fedha zinazotumika katika kazi hiyo zinatolewa na manispaa ya Kinondoni, na kazi hiyo itafanywa na wataalam wa Manispaa hiyo na kufafanua kuwa kukamilika kwake kutaondoa adha ya muda mrefu ya mafuriko waliyokuwa wanaipata wakazi hao kipindi cha mvua.
“Manispaa ya Kinondoni tumetenga kiasi cha shilingi 900 kwa ajili ya kufungua maji na kujenga mifereji ya kudumu inayoelekea baharini katika ili wananchi waweze kuishi bila usumbufu wowote,na kazi hii tutaimaliza ndani ya mwezi mmoja” Amesisitiza.
Naye Muhandisi wa Manispaa hiyo Baraka Mkuya amesema kuwa kazi ya uondoaji wa maji na ujenzi wa mifereji ya wazi na ile inayopita chini ya ardhi kutokea eneo la Basihayo Tegeta na kukatisha barabara ya Bagamoyo kuelekea bahari ya Hindi urefu wa kilometa 2.1 itakamilika ndani ya mwezi mmoja.
Kwa upande wao madiwani wa eneo hilo Bw.Majisafi Sharifu,Diwani wa Kata ya Bunju (CHADEMA) na Bi.Janet Lite kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa mfereji huo inakwenda na kueleza kuwa itakuwa faraja kwa wakazi wa kata hizo kutokana na adha kubwa ya mafuriko ya maji waliyokua wanaipata wakati wa msimu wa mvua.
MATUKIO BUNGENI LEO

MATUKIO BUNGENI LEO

May 19, 2015

pin1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 18, 20154, Victor Mwambalaswa wa Lupa, Sylvester Mabumba  wa  Dole na Dkt. Hamisi Kigwangalla wa Nzega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pin2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 18, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jamii yatakiwa kuwa na nidhamu katika shughuli za kujiletea maendeleo

Jamii yatakiwa kuwa na nidhamu katika shughuli za kujiletea maendeleo

May 19, 2015

so1
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa mbele akionyesha Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 wakati wa mafunzo ya elimu ya Ujasiriamali, Mfuko wa Vijana, Stadi za Maisha na Uongozi bora kwa Vijana wa Halmashauri ya Tunduru.
so2
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga aliyeshoosha mkono akiwa katika ukaguzi wa mradi wa kikundi cha Hatubanani kilichopo Halmashauri ya mji wa Tunduru kinachojishughulisha na duka la uuzaji wa vinywaji baridi, mradi wa kikundi hicho umepata mkopo wa shilingi milioni nne kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana.wa kwanza kushoto ni katibu wa kikundi hichi Bi Hawa Mayanga na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mkoani Mbeya Bw. Laurian Masele.
so3
Maafisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika ukaguzi wa mradi wa ufugaji samaki kilichopo Halmashauri ya mji wa Tunduru wakati wa mafunzo kwa vijana ya kuwakwamua kiuchumi.Katikati ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Vijana Sasanda kilichopo Mkoani Mbeya Bw. Laurian Masele.
so4
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga aliyeshoosha mkono akitoa mada ya jinsi ya utendaji kazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa mafunzo ya kuwakwamua vijana wa Halmashauri ya Tunduru kiuchumi.
…………………………………………………………………………..
Jamii imetakiwa kuwa na nidhamu ikiwa ni pamoja na kuwa na usimamizi mzuri katika shughuli za kujiletea maendelo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Manfred Hyera amesema chanzo cha mafanikio katika ujasiriamali nikuwa na nidhamu kwa jamii inayowazunguka kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kuwaongezea kipato.
Bw.Hyera amesema kitendo cha baadhi ya wajasiriamali kutumia lugha chafu kwa wateja ndio chanzo kinachowarudisha nyuma na kufilisika kibiashara.
“Baadhi ya wajasirimali mnatumia lugha chafu kwa wateja wenu hiki ni chanzo kikubwa cha kufilisika kibiashara na kubaki kuilalamikia serikali”.Alisema.
Alisema serikali kupitia WizarayaHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaniayadhati yakushirikiana na wanachi wote hususani Vijana ilikukabiliana na tatizo la ajira nchini.
Katika hatua nyingine AfisaVijana Bi. Amina Sanga amewashauri vijana kuwa wabunifu ili kuendana naushindani wa soko la biashara unaoendelea nchini na duniani kwa ujumla.
Akitolea mfano wa ujenzi unaoendelea wa barabara kwa kiwango cha lami Bi. Sanga alisema ni fursa mojawapo kwa vijana wa Halmashauri hiyo kubuni biashara ambayo itawaingizia kipato kiurahisi kwani kwa kukamilika kwabarabara hiyo kutakuza uchumi wa maeneo ya Wilaya ya Tunduru.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa amewashauri vijana hao kuweka itikadi za siasa pembeni kwani serikali yao hushirikiana vijana wote bila ubaguzi wa dini au kabila.

MAANDAMANO YAKIWA YANAENDELEA RAIS NKURUNZIZA AWAFUTA KAZI MAWAZIRI WA 3

May 19, 2015


Nkurunziza
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita.

Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara.
Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.

JK KUFUNGUA MKUTANO WA MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI

May 19, 2015
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa  Shughuli za Serikali kwa uwazi (OGP).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21, 2015 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Aidha, imeeleza kuwa dhumuni la  mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.

“Kupata uzoefu wa utekelezaji wa OGP kutoka nchi wanachama katika bara la Afrika nan je ya Afrika kama vile taarifa za uwazi zinazoimarisha uwajibikaji” iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema  kuwa mkutano huo ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania na ni wa pili kwa Kanda ya Afrika ambapo kwa mara ya kwanza  ulifanyika nchini Mombasa nchini Kenya mwaka 2013.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki 200 kutoka Serikalini, Asasi za kirai, Washirika wa Maendeleo wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya nchi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali, wawakilishi kutoka Nchi wanachana wa OGP kutoka bara la Afrika.

Washiriki wengine ni kutoka nchi za Botswana, Zambia, Uganda, Marekani, Zimbabwe pamoja na washirika wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, UNDP, UNICEF, UNESCO, MCC, USAID, DFID na JICA.
MIRINDA NYEUSI AREJEA TENA MASHUJAA BAND ...sasa bendi ina marapa watatu A+ A- Print Email Rapa Mirinda Nyeusi amerejea tena Mashujaa Band baada ya kuzitumikia Twanga Pepeta na Malaika Band kwa vipindi tofauti. Kwa mujibu wa matangazo ya vipeperushi vya Mashujaa Band, Mirinda anaungana na Rogart Hegga na Daddy Diperon katika safu ya waimbaji wapya waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni. Vipeperushi vya Mashujaa vya kunadi onyesho lao la kila Ijumaa ndani ya Mashujaa Grill & Lounge, ambavyo Saluti5 inayo nakala yake, vinasema: “Njoo ucheze Kibega na pamoja na wanamuziki wapya Rogart Hegga, Daddy Diperon na Mirinda Nyeusi." Lakini hata Mirinda Nyeusi mwenyewe pia ameithibitishia Saluti5 kuwa amerejea rasmi bendi yake za zamani. Mirinda Nyeusi amerejea tena Mashujaa Band Kimuziki kwa hapa nchini, safari ya Mirinda Nyeusi ambaye jina lake halisi ni Abraham Mpoyo, ilianzia Vibration Sound mwishoni mwa miaka ya 2000 kabla haijanunuliwa na kuwa Mashujaa Musica (Mashujaa Band) aliyoitumikia hadi mwaka 2012 na kupunguzwa kazi kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa kati yake na viongozi wa bendi. Baada ya hapo akajiunga Mirinda ambaye ni mmoja wa marapa wenye uwezo wa hali ya juu, Twanga na kudumu nayo hadi Mei 2014 na kukumbwa tena na balaa la kupunguzwa kazi kwa staili ile ile ya mizengwe, lakini Malaika Band wakahitaji huduma yake na kumuongeza kwenye kikosi chao. Kabla hajabahatika kurekodi wimbo wowote na Malaika Band akapata dili la kwenda Uarabuni huku Malaika wakiweka wazi kuwa nafasi yake haitakuwepo tena pindi atakaporejea Bongo. Kurejea kwa Mirinda Nyeusi Mashujaa Band, kunafanya idadi ya marapa kuwa watatu hiyo ikiwa ni pamoja na Ferguson na Sauti ya Radi.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/mirinda-nyeusi-arejea-tena-mashujaa.html#more
Copyright © saluti 5
MIRINDA NYEUSI AREJEA TENA MASHUJAA BAND ...sasa bendi ina marapa watatu A+ A- Print Email Rapa Mirinda Nyeusi amerejea tena Mashujaa Band baada ya kuzitumikia Twanga Pepeta na Malaika Band kwa vipindi tofauti. Kwa mujibu wa matangazo ya vipeperushi vya Mashujaa Band, Mirinda anaungana na Rogart Hegga na Daddy Diperon katika safu ya waimbaji wapya waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni. Vipeperushi vya Mashujaa vya kunadi onyesho lao la kila Ijumaa ndani ya Mashujaa Grill & Lounge, ambavyo Saluti5 inayo nakala yake, vinasema: “Njoo ucheze Kibega na pamoja na wanamuziki wapya Rogart Hegga, Daddy Diperon na Mirinda Nyeusi." Lakini hata Mirinda Nyeusi mwenyewe pia ameithibitishia Saluti5 kuwa amerejea rasmi bendi yake za zamani. Mirinda Nyeusi amerejea tena Mashujaa Band Kimuziki kwa hapa nchini, safari ya Mirinda Nyeusi ambaye jina lake halisi ni Abraham Mpoyo, ilianzia Vibration Sound mwishoni mwa miaka ya 2000 kabla haijanunuliwa na kuwa Mashujaa Musica (Mashujaa Band) aliyoitumikia hadi mwaka 2012 na kupunguzwa kazi kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa kati yake na viongozi wa bendi. Baada ya hapo akajiunga Mirinda ambaye ni mmoja wa marapa wenye uwezo wa hali ya juu, Twanga na kudumu nayo hadi Mei 2014 na kukumbwa tena na balaa la kupunguzwa kazi kwa staili ile ile ya mizengwe, lakini Malaika Band wakahitaji huduma yake na kumuongeza kwenye kikosi chao. Kabla hajabahatika kurekodi wimbo wowote na Malaika Band akapata dili la kwenda Uarabuni huku Malaika wakiweka wazi kuwa nafasi yake haitakuwepo tena pindi atakaporejea Bongo. Kurejea kwa Mirinda Nyeusi Mashujaa Band, kunafanya idadi ya marapa kuwa watatu hiyo ikiwa ni pamoja na Ferguson na Sauti ya Radi.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/mirinda-nyeusi-arejea-tena-mashujaa.html#more
Copyright © saluti 5
MIRINDA NYEUSI AREJEA TENA MASHUJAA BAND ...sasa bendi ina marapa watatu A+ A- Print Email Rapa Mirinda Nyeusi amerejea tena Mashujaa Band baada ya kuzitumikia Twanga Pepeta na Malaika Band kwa vipindi tofauti. Kwa mujibu wa matangazo ya vipeperushi vya Mashujaa Band, Mirinda anaungana na Rogart Hegga na Daddy Diperon katika safu ya waimbaji wapya waliojiunga na bendi hiyo hivi karibuni. Vipeperushi vya Mashujaa vya kunadi onyesho lao la kila Ijumaa ndani ya Mashujaa Grill & Lounge, ambavyo Saluti5 inayo nakala yake, vinasema: “Njoo ucheze Kibega na pamoja na wanamuziki wapya Rogart Hegga, Daddy Diperon na Mirinda Nyeusi." Lakini hata Mirinda Nyeusi mwenyewe pia ameithibitishia Saluti5 kuwa amerejea rasmi bendi yake za zamani. Mirinda Nyeusi amerejea tena Mashujaa Band Kimuziki kwa hapa nchini, safari ya Mirinda Nyeusi ambaye jina lake halisi ni Abraham Mpoyo, ilianzia Vibration Sound mwishoni mwa miaka ya 2000 kabla haijanunuliwa na kuwa Mashujaa Musica (Mashujaa Band) aliyoitumikia hadi mwaka 2012 na kupunguzwa kazi kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa kati yake na viongozi wa bendi. Baada ya hapo akajiunga Mirinda ambaye ni mmoja wa marapa wenye uwezo wa hali ya juu, Twanga na kudumu nayo hadi Mei 2014 na kukumbwa tena na balaa la kupunguzwa kazi kwa staili ile ile ya mizengwe, lakini Malaika Band wakahitaji huduma yake na kumuongeza kwenye kikosi chao. Kabla hajabahatika kurekodi wimbo wowote na Malaika Band akapata dili la kwenda Uarabuni huku Malaika wakiweka wazi kuwa nafasi yake haitakuwepo tena pindi atakaporejea Bongo. Kurejea kwa Mirinda Nyeusi Mashujaa Band, kunafanya idadi ya marapa kuwa watatu hiyo ikiwa ni pamoja na Ferguson na Sauti ya Radi.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/mirinda-nyeusi-arejea-tena-mashujaa.html#more
Copyright © saluti 5

NOOIJ AKALIA KUTI KAVU TAIFA STARS, MECHI 14 TIMU IMESHINDA TATU TU TANGU ATUE APRILI

May 19, 2015

Mart Nooij amekalia kuti kavu Taifa Stars
Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij anaweza kufukuzwa wakati wowote kuanzia sasa, kufuatia idadi kubwa ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutomkubali.
Nooij ameiongoza Stars katika mechi ya 14 jana tangu awasili mwishoni mwa Aprili kuchukua mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen na timu hiyo imefungwa bao 1-0 na Swaziland katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Kombe la COSAFA Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini hapa.
Matokeo hayo yanaiweka Stars katika mazingira magumu ya kwenda Robo Fainali- baada ya Madagascar kuifunga 2-1 Lesotho katika mchezo wa kwanza.
Stars sasa lazima ishinde mechi zake mbili zijazo dhidi ya Lesotho na Madagascar ili kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali.
Swaziland ambayo bao lake pekee lilifungwa na  Sifiso Mabila kwa shuti kali dakika ya 42 baada ya kutanguliziwa pasi kwenye njia na Xolani Sibandze aliyemtoka Oscar Joshua upande wa kushoto, waliizidi ufundi uwanjani Stars jana.
Stars ilicheza ovyo jana, mpango pekee wa kutafuta mabao ni kwa mipira ya kutokea pembeni, wakati huo huo timu ilitumia mshambuliaji mmoja tu, John Bocco ambaye muda mwingi alikuwa anakwenda kutafuta mipira pembeni.
Ilikuwa vigumu kuelewa Stars wanacheza mfumo gani jana, kwani pamoja na kuwa na viungo watatu uwanjani, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla, lakini bado timu ilikuwa haikai na mpira.
Mipira yote ilikuwa inapelekwa pembeni kwa mawinga akina Mrisho Ngassa na Simon Msuva wakampigie krosi Bocco aliyedhibitiwa vizuri na mabeki wa Swaziland.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kipindi cha pili, kwani Stars haikurudi na mpango mbadala- matokeo yake Swaziland wakang’ara zaidi uwanjani.
Mabadiliko yaliyofanywa na Nooij kipindi cha pili, yalikuwa kichekesho pia- kwani baada ya dakika 10 kipindi cha pili, Stars ilionekana kabisa ilihitaji kiungo mbadala wa Mwinyi Kazimoto, lakini Mholanzi huyo alimtoa Said Ndemla na kumuingiza Juma Luizio dakika ya 65.  
Maana yake alipunguza kiungo akaongeza mshambuliaji, lakini dakika 10 baadaye akapunguza tena mshambuliaji, Mrisho Ngassa na aliyeonekana kuwa muhimu zaidi uwanjani jana na kuingiza kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Kikosi cha Taifa Stars kilichofungwa 1-0 na Swaziland jana 

Mtu ambaye alitakiwa kumbadili mapema tu, pengine tangu mwanzoni mwa kipindi cha pili, Simon Msuva akamtoa mwishioni mwa mchezo dakika ya 82 akimuingiza Ibrahim Hajibu.
Pamoja na mapungufu ya wachezaji kutokana na nyota kadhaa wa timu hiyo kubaki Dar es Salaam kwa sababu mbalimbali, ikiwemo majeruhi, lakini hata upangaji wa timu Nooij pia ulikuwa ni tatizo.
Bado kutoka wachezaji aliokuja nao hapa, angeweza kupanga timu tofauti na aliyopanga jana na ikacheza kwa uelewano mzuri na kupata matokeo mazuri.
Wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji wa TFF wanaamini Stars haipo katika mikono salama kwa Nooij na wanataka mabadiliko mapema kabla ya kuanza kwa kampeni za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Juni.
Kuna wasiwasi hata juu ya mbinu za ufundishaji wa Nooij na ndiyo maana amekuwa hataki hata Waandishi wa Habari wa Tanzania wahudhurie mazoezi yake wala kupiga picha.
Mfumo pekee wa kushambulia anaofundisha mazoezini na kiungo kupeleka pasi pembeni, imkute winga apige krosi watu ‘wagombee goli’ na ndivyo hata Stars inavyoonekana kucheza sasa.
Utamu wa soka ya Taifa Stars umepungua kwa kiasi kikubwa kutoka ulivyokuwa chini ya kocha aliyetangulia, Kim Poulsen hadi Nooij na mchezo wa kesho wa COSAFA dhidi ya Madagascar unaweza kuamua hatima ya Mholanzi huyo.
Ingawa kuna imani kwamba, Nooij anapotoshwa na mtu wake wa karibu katika uteuzi wa wachezaji, lakini hata yeye mwenyewe kama kocha ni tatizo.
Katika mechi 14 ambazo Nooij ameiongoza Stars, imeshinda tatu tu, ikifungwa tano na kutoa sare mara sita, tena mechi nyingi ikicheza nyumbani.
TFF ilihadaika na wasifu mzuri wa Nooij aliyetua Tanzania akitokea klabu ya St George ya Ethiopia Aprili mwaka jana na kumpa Mkataba mnono.
Wasifu wa Nooij unasema amewahi kuwa mwalimu maalum katika programu za maendeleo ya soka katika Chama cha Soka Uholanzi (DFA) na pia amewahi kufundisha timu ya EVC 1913 ya Marekani na baadaye Kazakhstan.
Alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Burkina Faso katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2003 na mwaka 2004 alikuwa kocha wa muda wa klabu ya FC Volendam ya Uholanzi.
Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa Msumbiji na akaiwezesha kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza Mambas wanashiriki AFCON baada ya msoto wa miaka 12.
Hata hivyo, katika fainali hizo, Msumbiji ilishika mkia katika kundi lake baada ya kuambulia sare moja na kufungwa mechi mbili. Baada ya kukosa tiketi ya AFCON 2012, Nooij akajiuzulu Septemba mwaka 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani, Gert Engels.
Aprili 19 mwaka 2012, aliajiriwa na klabu ya Santos ya Afrika Kusini, ambako hata hivyo alifukuzwa Desemba 18, mwaka 2012 na kuhamia St George ya Ethiopia kabla ya kuja Tanzania Aprili mwaka jana. 
John Bocco pamoja na kuwa mshambuliaji pekee jana, lakini alilazimika kwenda pembeni kutafuta mipira jana

REKODI YA MART NOOIJ TAIFA STARS
Tanzania 0-0 Malawi (Kirafiki Mbeya)
Tanzania 1-0 Zimbabwe (kufuzu AFCON Dar es Salaam)
Tanzania 1-0 Malawi (kirafiki Taifa)
Tanzania 2-2 Zimbabwe (Kufuzu AFCON Harare)
Tanzania 2-4 Botswana (kirafiki Harare)
Tanzania 2-2 Msumbiji (Kufuzu AFCON Dar es Salaam)
Tanzania 1-2 Msumbiji (Kufuzu AFCON Maputo)
Tanzania 0-2 Burundi (Kirafiki, Bujumbura)
Tanzania 4-1 Benin (Kirafiki, Dar es Salaam)
Tanzania 1-1 Swaziland (Kirafiki, Mbabane)
Tanzania 1-2 Burundi (Kirafiki, Taifa. Stars Maboresho)
Tanzania 1-1 Rwanda (kirafiki Mwanza, Maboresho)
Tanzania 1-1 Malawi  (Kirafiki Mwanza, Stars kubwa)
Tanzania 0-1 Swaziland (COSAFA Rustenburg)

STARS YAPOTEZA MCHEZO DHIDI YA SWAZIAND

May 19, 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya COSAFA Castel Cup dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland, baada ya kufungwa bao 1- 0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.

Stars ilipoteza nafasi zaidi ya tano kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake Saimon Msuva na nahodha John Bocco ambao walishindwa kukwamisha mpira wavuni katika kipindi cha kwanza, ambacho Taifa Stars ilicheza vizuri.

Swaziland walipata bao lao la kwanza na la ushindi dakika ya 42 ya mchezo, kupitia kwa mlinzi wa kulia Sifiso Mabila aliyepanda kuongeza nguvu ya mashambulizi na kuachia shuti lililouacha mlinda mlango wa Stars akikosa cha kufanya kuokoa mchomo huo.

Kipindi cha pili Stars walizidiwa kwani mashambulizi yao hayakua na madhara langoni mwa Swaziland na kumuacha mlinda mlango Mphikeleli Dlamnini akiwa likizo kwa muda mrefu.

Mara baada ya mchezo kocha wa Stars Mart Nooij alisema, amepoteza mchezo wa kwanza ambao alitegemea kupata ushindi, vijana walicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini bao la mapema lilionekana kuwapoteza mchezoni.

“Presha ya mchezo ilikua kubwa hasa kipindi cha pili, kutokana na vijana wangu kucheza kwa kusaka bao, huku Swaziland wakimiliki zaidi mpira na kukuta mipango yetu  kutokua na madhara” alisema Nooi.

Akiongelea michuano ya COSAFA amesema anashukuru kwa kupata mwaliko huu, kwani kwake anatumia michuano hii kama sehemu ya maandalizi ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika (AFCON, CHAN) mwezi juni, huku akisema anaamini wachezaji aliowacha majeruhi nyumbani pamoja na wachezaji wa kimataifa wanaochezea klabu ya TP Mazembe, wataongeza nguvu katika kikosi chake watakaporejea Tanzania.

Baadhi ya watanzania waishio nchini Afrika Kusini walijitokeza uwanja wa Royal Bafokeng kuishangilia timu ya Taifa ya tanznaia Taifa Stars wakiwa sambamba na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili siku ya jumatano saa 11 za jioni kwa saa za Afrika kusini, sawa na saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki dhidi ya Madagascar katika uwanja wa Royal Bafokeng., ambao katika mchezo wa awali wamibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho.

Wakati huo huo kiungo wa Taifa Sars Said Juma “Makapu” ambaye anasumbuliwa na majeruhi, anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania leo kwa ajili ya kupata vipimo zaidi na matibabu.


TFF YATUMA RAMBIRAMBI RUREFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kufuatia kifo cha katibu mkuu msataafu wa chama hicho Adolph Choma aliyefariki jumamosi na kuzikwa jana.

Katika salamu hizo, TFF imesema inawapa pole familia ya marehemu Adolph Choma, ndugu jamaa na marafiki, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu nchini na kusema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

NB:Picha za mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Swaziland zimeambatanishwa.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania