HIVI NDIVYO MWENYEKITI WA COASTAL UNION HEMED AURORA ALIVYOFUNGUA TAWI LA WAPENZI WA COASTAL UNION MAKORORA.

June 10, 2014
MWENYEKTI WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA,HEMED AURORA "MPIGANAJI" AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UFUNGUZI WA TAWI LA WAPENZI LA MAKOKORA MWISHONI MWA WIKI

HAPA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,HEMED MORROCO AKIPANDISHA BENDERA

Mwenyekiti wa tawi la Coastal Union Makorora,Nassoro Athumani kushoto akikabidhiwa hati ya usajili wa tawi hilo na Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora mara baada ya kulifungua jana

STARS KUMENYANA NA UGANDA KABLA YA VITA YA KUUA MAMBA

June 10, 2014

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

TANZANIA itacheza na Uganda mchezo maalum wa kirafiki kujipima nguvu kabla ya kucheza na Msumbiji kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015.
BIN ZUBEIRY inafahamu Mashirikisho ya Soka Uganda (FUFA) na Tanzania (TFF) tayari yamefikia makubaliano juu ya mchezo huo ambao utachezwa Dar es Salaam katika tarehe ambayo itatajwa hivi karibuni.
Wakati Tanzania itacheza na Msumbiji mwezi ujao, Uganda itamenyana na Equatorial Guinea kusaka nafasi ya kuingia kwenye makundi baada ya kuitoa Madagascar.
Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars

Taifa Stars itacheza mechi yake kwanza na Mambas Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Stars ambayo iiliitupa Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ kwa jumla ya mabao 3-2, ikitoa sare ya 2-2 baada ya kushinda 1-0, inatarajiwa kuingia kambini Juni 11, kuanza maandalizi.
Mechi nyingine za hatua hiyo ya mwisho ya mchujo zitakuwa kati ya Lesotho na Kenya, Kongo na Rwanda, Botswana na Guinea Bissau, Sierra Leone na Shelisheli na Benin na Malawi.

BREAKING NEWS; KOCHA MPYA BARCELONA AKIMBIZWA HOSPITALI, KUFANYIWA UPASUAJI LEO

June 10, 2014
KOCHA wa Barcelona, Luis Enrique leo anatarajiwa kufanyiwa operesheni ya ugonjwa wa kidoletumbo.
Kwa mujibu wa gazeti Mundo Deportivo la Hispania, mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 44 alikimbizwa chumba cha dharula cha wagonjwa, kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo kuthibitisha tatizo lake.
Enrique, ambaye aliwachezea vigogo hao wa Hispania kuanzia mwaka 1996 hadi 2004, aliteuliwa kuwa kocha Mkuu wa Barcelona mwezi uliopita kwa Mkataba wa miaka miwili.

Chini ya kisu: Kocha wa Barcelona, Luis Enrique leo atafanyiwa upasuaji wa kidoletumbo 

Baada ya upasuaji huo, kocha huyo Mspanyola atahitaji kukaa nje muda mrefu kwa maumziko bila kuanya kazi.
Enrique anaweza kuondoka hospital baada ya saa 24 iwapo mambo yatakwenda vizuri bila matatizo yoyote. 
Kocha huyo wa zamani wa Celta Vigo atakuwa tayari kurejea kazini kwa ajili ya msimu mpya, iwapo mambo yatakwenda vizuri.
Gerard Pique na Javier Mascherano waliosaini mikataba mipya hive karibuni kubaki katika klabu hiyo, wakati kiungo wa Sevilla, Ivan Rakitic yupo mbioni kutua Nou Camp.
Enrique anatarajiwa kumpoteza Cesc Fabregas msimu ujao ambaye anatakiwa na Chelsea walio tayari kutoa Pauni  Milioni 30 kumchukua nyota huyo azibe pengo la Frank Lampard aliyeondoka baada ya kumaliza Mkataba.

KURA SILAHA YA MWISHO KUMRUDISHA WAMBURA KUGOMBEA SIMBA

June 10, 2014


Mgombea wa urais wa Simba aliyekuwa ameondolewa na kamati ya usajili, huenda akarudi.
Taarifa zinaeleza wajumbe wa kamati ya rufaa ya TFF, ngoma imekuwa ngumu kuhusiana na Michael Wambura.
Habari kutoka ndani zinaeleza kutokana na mvutano kuwa mgumu, wajumbe wameona uamuzi wa kupiga kura.
Uamuzi wa kupiga kura unaonekana kumpa Wambura nafasi ya kurudi kwa kuwa wajumbe watatu wako tayari arudi na wawili wanapinga.
Hata hivyo hakujawa na uthibitisho wa kutosha kuhusiana na hilo.
Lakini mtu mmoja wa karibu na Wambura, amezungumza Tanga Raha blog na kusema: “Mambo mazuri, subiri kidogo.”
Basi ndiyo hivyo, tunaendelea kusubiri wakati kikao hicho kinaendelea.
Washauri kuundwa sheria kusimamia utekelezaji wa bajeti

Washauri kuundwa sheria kusimamia utekelezaji wa bajeti

June 10, 2014

Mmoja wa washiriki wa mjadala wa wazi akichangia mada.
Mmoja wa washiriki wa mjadala wa wazi akichangia mada.
Mmoja wa washiriki akichangia mada kwenye mjadala wa wazi.
Mmoja wa washiriki akichangia mada kwenye mjadala wa wazi.
Baadhi ya washiriki wa mjadala kutoka asasi anuai wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa mjadala kutoka asasi anuai wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa mjadala kutoka asasi anuai wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa mjadala kutoka asasi anuai wakifuatilia mada.
Washiriki wa mjadala.
Washiriki wa mjadala.
Mwakilishi wa asasi ya Network for Vulnerables Rescue Foundation (NVRF), Ezekiel William akichangia hoja.
Mwakilishi wa asasi ya Network for Vulnerables Rescue Foundation (NVRF), Ezekiel William akichangia hoja.
BAADHI ya wanaharakati wamevitaka vyombo vinavyotunga sheria nchini kwa pamoja kwa kushirikiana na wanaharakati kuhakikisha wanashinikiza kutungwa kwa sheria itakayo simamia bajeti za kila mwaka na pale ambapo Serikali na idara fulani zinaonekana kukwamisha utekelezaji sheria ichukue mkondo wake.

RAIS KIKWETE AZINDUA CHAPISHO LA TATU LA TAARIFA ZA SENSA.

June 10, 2014



 Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake  kabla ya kuzindua Chapisho la Tatu la taarifa za msingi za Kidemografia,Kijamii na Kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na Matumizi ya tovuti katika kupata  taarifa mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dares Saalam leo.
 Rais Jakaya Kikwete(wa tatu kulia) akizindua Chapisho la Tatu la taarifa za msingi za Kidemografia,Kijamii na Kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na Matumizi ya tovuti katika kupata  taarifa mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dares Saalam leo.Wengine kwa kwanza kulia ni Kamishna wa Sensa Hajjat Amina  Mrisho   Saidi, wa pili Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya na kushoto wa kwanza ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seid Ali Iddi wa   pili ni Mwakilishi wa UNFPA Mariam Khan na watatu ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akizindua  tovuti kwa ajili ya kupata  taarifa mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dares Saalam leo.
Picha zote na Magreth Kinabo na Maelezo

*MAMA SALMA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA WATOTO,ZINGA-BAGAMOYO.

June 10, 2014

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Shirika la International Health Partiners (IHP)-JEMA Tanzania, Mama Mary Ellen Kitundu mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo, mkoani Pwani. Mama Salma alikwenda kijijini hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la hospitali ya watoto inayojengwa na Shirika la IHP-JEMA Tanzania,Katikati ni Mkurugenzi wa Mradi huo Dkt. Jesse Kitundu.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi wakitembelea eneo linalojengwa hospitali ya watoto itakayo kuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 500 katika kijiji cha Zinga huko Bagamoyo 
 Baadhi ya wananchi kutoka katika kijiji cha Zinga na wageni waalikwa kwenye sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto wakifurahia jambo wakati mgeni rasmi Mama Salma Kikwete alipokuwa akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo.

*KAMPUNI YA NEW HABARI YACHEZESHA DROO YA TWENZETU BRAZIL.

June 10, 2014

 Mhariri Mwandamizi wa gazeti la The African Balinagwe mwambungu akichagua kuponi ya mshindi wa promosheni ya mshindi wa promosheni ya Twenzetu Brazili( Picha zote na Humphrey Shao)
 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd Absolom Kibanda akizungumza na waandishi wa habari an wadau waliofika kushuhudia promosheni hiyo 

 Ikupa Mwakiteleko akichanganya na kuchagua karatasi ya kumtafuta mshindi wa twenzetu Brazili 
Mfanyakzi wa Kampuni ya New Habari lati Mbonea akichanga kuponi na kuchagua kuponi kwa ajili ya kumtangaza mshindi wa promosheni wa twenzetu Brazili,Pembeni GME wa New Habari(2006) Ltd , Absolom Kibanda na Meneja Mauzo Michael Budigila akishuhudia tukio  hilo