ZIDANE KOCHA BORA WA DUNIA, ASHINDA TUZO YA FIFA LONDON

October 23, 2017
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametangazwa kuwa kocha bora katika tuzo za Fifa mjini London.
Tuzo hizo zinaendelea jijini London na Zidane amefanikiwa kubeba tuzo hiyo kutokana na mafanikio makubwa msimu uliopita akibeba La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo.
Sherehe za tuzo hizo zinaendelea jijini London, England.
Tuzo za Mawaziri na Wabunge watakaofanya vizuri zazinduliwa

Tuzo za Mawaziri na Wabunge watakaofanya vizuri zazinduliwa

October 23, 2017
Kamati ya utawala ya shindano la tuzo za utekelezaji maendeleo kwa kasi ya juu kwa Wabunge na Mawaziri (THSDA) imezindua shindano la kutoa tuzo kwa Wabunge na Mawaziri watakaofanya vizuri katika kutekeleza majukumu ya kuwaletea Wananchi maendeleo.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Kamati hiyo Bw. Wilson Maage alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, juu ya uzinduzi wa shindano hilo ambalo litafanyika kwa muda wa miezi miwili.
“Tuzo hizo zimetokana na kuwepo wazo bunifu (intellectual property) ambalo azma yake ni kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za huduma na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania na kupima kasi ya utekelezaji wa shughuli hizo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika sekta na taasisi za kiserikali hapa nchini,” alifafanua Maage.
Aliendelea kusema kuwa, vigezo vitakavyotumiwa katika kuteua viongozi hao ambao ni wabunge pamoja na Mawaziri ni pamoja na kuwa mtetezi wa Wananchi wake bila uoga akiwa ndani au nje ya Bunge, mtendaji bora wa maendeleo yenye kuonekana, sifa ya kutoa hoja zenye tija kwa kutumia lugha ya staha bila matusi, sifa ya utekelezaji wa haraka apatapo matatizo ya Wananchi wake pamoja na sifa ya kutetea demokrasia, uhuru na kutetea wanyonge.
“Faida za shindano la tuzo hizi ni kwamba zinaweka Wananchi karibu na viongozi, kuchochea utekelezaji huduma na maendeleo kwa kasi ya juu, utawla bora na uwajibikaji wa viongozi kwa Wananchi, uhusiano mzuri kati ya serikali na Wananchi na kuimarisha furaha, utulivu na amani,” alieleza Maage.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Kamati hiyo, Herman Mnenuka alisema kuwa Wananchi ndiyo nguzo kuu ya kupata kiongozi atakayepata tuzo hiyo kwani wao ndio watakaopendekeza majina ya wabunge pamoja na wamaziri wanaofaa kuwania tuzo hiyo.
Katika tuzo hiyo, hatua ya kwanza, wananchi wanapaswa kupendekeza wabumge 15 kwa kila kigezo shindanishi, pia Wananchi watawateua Mawaziri 5 kwa kila kipengele shindanishi kwaajili ya kuingia kwenye ushindani wa tuzo hiyo na wabunge watano na Mawaziri watatu watakaopata kura nyingi kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kwa wananchi wataingia katika fainali ya king’anyiro kuwania tuzo hiyo.
Aidha aliongeza kuwa, katika hatua nyingine, wananchi kupitia simu watawachuja washiriki waliofika hatua ya fainali kwa kutuma SMS na mbunge pamoja na waziri atakayepata kura nyingi ndiye atakaye kuwa mshindi katika kilele cha tuzo hiyo kitakachofanyika tarehe 23 Desemba Mwaka huu.
“Niwaombe wananchi washiriki kikamilifu ili kuweza kupata kiongozi anayejishughulisha na anayechapa kazi kupitia tuzo hii na mwisho wa kilele tutapata mshindi wa kila kipengele kilichowekwa ambacho kina tija muhimu katika taifa kupitia waheshimiwa wabunge na mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alieleza Mnenuka.
Aidha aliongeza kuwa, Wananchi watapendekeza majina kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kupitia namba 15555 kwa mitandao ya Tigo, Airtel, Vodacom, Halotel Smart na Zantel na kila SMS itatozwa gharama ya shilingi 500 vilevile kutakuwa na vipindi vya radio runinga na magazeti ili kuwakumbusha mwenendo na hatua za shindano la tuzo za THSDA hadi siku ya kilele.
Hizi ni tuzo za kwanza kuandaliwa hapa nchini na kamati hiyo ambazo zitafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha.
RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA AfYA

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA AfYA

October 23, 2017
DSC_2320
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya  katika  kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,(kushoto) Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,
DSC_2328
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika   Wizara ya Afya   wakiwa katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
DSC_2331
Baadhi ya Maafisa  wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Afya wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akifungua  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,
DSC_2341
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika  kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,
DSC_2434
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dk.Jamala Adam Taib (wa pili kulia) alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
Picha na Ikulu.

WALIMU WANAWAKE MANISPAA YA IRINGA WALALAMA KUTOPEWA NAFASI ZA KUONGOZA

October 23, 2017
Mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.
 Baadhi ya walimu wanawake waliohudhuria mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Walimu wanawake manispaa ya Iringa walalamikia kutokuwepo kwa uwiano wa viongozi wanawake na wanaume katika sekta nyeti kama vile wakuu wa shule,maafisa elimu kata na wilaya wakati walimu wa wanawake ndio wengi hivyo inafifisha ndoto za kuwa viongozi kwa kuwa wanauwezo wa kuongoza na kusimamia mambo mengi yakaenda kama yalivyopangwa.

Hayo yamesemwa na walimu wanawake katika mkutano mkuu wa chama cha walimu wanawake kilichokuwa kinaongozwa na katibu wa wilaya mwl. Fortunata Njalale katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

Akisoma risala iliyoandaliwa na kamati ya kitengo cha walimu wanawake MWL. Evon Mhewa alisema kuwa walimu wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi katika kukamilisha majukumu yao.

“Mwalimu wa kike anacheleweshewa kulipwa madeni mbalimbali anayokuwa anaidai serikali maana bila kulipwa madeni yetu walimu hawawezi kufundisha kwa moyo kwa kuwa maisha yanakuwa magumu na kuwapelekea kubuni njia mbadala za kujiingizia kipato” alisema Mhewa

Mhewa alizitaja changamoto nyingine ni kutopata nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kusimama kwa mwaka wa pili sasa,walimu kutopandishwa madaraja na wengine kupandishwa na kupokwa mshahara pamoja na walimu wanawake kutokuwa na uwiano wa vyote katika sekta nyeti.

“Sisi walimu wa kike kwa sasa tumesoma sana na tunaweza kuwa viongozi sehemu yoyote kwa kuwa tayari tumethibisha hilo kwa wanawake waliopewa kazi hiyo kwani wameifanya ipavyo na kuleta matokeo chanya kwa serikali hivyo tunaomba walimu wanawake tupewa nafasi katika ngazi ambazo tunastahili” alisema Mhewa.

Akijibu risala hiyo mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga alisema kuwa ni kweli walimu wanamadi mengi serikalini lakini akasema kuwa hiyo yote imetokana na swala la uhakiki wa watumishi hivyo mchakato wa uhakiki ukimalizika kila kitu kitakuwa sawa ninauhakika na hilo.

“Unajua serikali imechelewesha maswala mbalimbali ambayo ni kero kwa walimu kutokana na uhakiki hivyo nawaomba walimu wawe na uvumilivu kwa kuwa kila kitu kitakuja kutengemaa kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Kayinga

Kayinga aliwataka walimu wanawake kuendelea kusoma ili kuwa na elimu ndio itakayowapa nafasi mbalimbali ambazo zinashikiriwa na walimu wanaume hivyo bila kuwa na elimu walimu wanawake wataendelea kuongozwa na walimu wanaume kila sekta.

“Najua kuwa walimu wanawake wanakipawa cha kuwa viongozi lakini mitaala mingi inataka walimu kuwa na elimu ili kupata kuongoza sekta mbalimbali sasa inatubidi walimu kujiendeleza kimasomo ili kukidhivigezo ambavyo mara nyingi imekuwa ni elimu ya walimu anayepaswa kupewa kitendo husika” alisema Kayinga

Aidha Kainga aliwataka walimu wanawake kugombea nafasi mbalimbali zinazojitokeza ili kupata nafasi za kuongoza na sio kila wakati kuwaacha walimu wanaume wakigombea pekee yao.

“Tumieni fursa za kugombea nafasi zinazojitokeza msiogope wanawake mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuogmbea kwa kuwa katika kada ya ualimu walimu wanawake tupo wengi hivyo kuanzia saizi walimu wanawake amkeni mjitume kuhakikisha mnagombea” alisema Kayinga

Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa mkutano huo ni wa kikatiba kwa mjibu wa katiba ya chama cha walimu taifa hivyo katiba imewaagiza kukaa na viongozi wa walimu wanawake kuzijadili changamoto za wanawake ili kuzipeleka katika mkutano mkuu wa wilaya.

RC KAGERA AONGOZA UZINDUZI WA MASHAMBA DARASA WILAYANI MISSENYI

October 23, 2017

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu  (wa tatu kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi  rasmi wa mashamba darasa ya kilimo bora cha mihogo na migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa (tissue culture), kwa ufadhili  wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) katika vijiji vya  Bunazi na Kashaba wilayani Missenyi mkoani humo leo. Shamba hilo litasimamiwa na Kikundi cha Ushirika cha Batekaka. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Belington Kyokwete, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho.

 Miche ya migomba ikiwa tayari kupandwa.
 Ofisa Ugani wa Kata ya Kasambya, Hakika Ibrahim, akizungumza kataika uzinduzi huo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice  Lyimo akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku akielezea mbegu hiyo mpya ya migomba. 

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa tatu kulia),  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mkuu wa  Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila (kulia), pamoja na Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika cha Batekaka, Belington Kyokwete, wakiwa wameshika mmoja wa mche wa mgomba katika uzinduzi huo. 

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akipanda mche wa mgomba kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Bunazi.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akipanda mgomba kwenye shamba darasa hilo.



   Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kashaba kabla ya kuzindua shamba darasa la zao la mhogo.

LULU AIAMBIA MAHAMAKA KUWA KANUMBA ALIMSHIKIA PANGA, ALITAKA KUMUUA

October 23, 2017
 Msaanii wa Bongo Muvi,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akiwa na wazazi waki wakiteta jambo na Wakili Peter Kibatala kabla ya shahidi amaye ni Daktari wa Hospitali ya Muhimbili kutoa ushahidiwake mbele ya mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MSANII maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, ameileza Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam  kuwa hakusababisha kifo cha marehemu Kanumba bali yeye ndiye aliyeshambuliwa.

Ameeleza kuwa kama siyo Kanumba kudondoka na panga kumtoka mkononi, basi yeye ndie angekuwa marehemu sasa hivi. Kwani kwa mwili wake mkubwa sikuweza kumfanya kitu chochote.

Lulu amedai hayo mbele ya Jaji Sam Rumanyika wakati akitoa utetezi wake katika kesi inayomkabili ya mauaji ya bila kukisudia dhidi ya msanii mwenzake, Marehemu Steven Kanumba, yanayodaiwa kutokea April 6, mwaka 2012 huko Sinza Vatkan.

Akiongozwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala, Lulu amedai, mbali ya kuwa wanafanya kazi pamoja kama wasanii, pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba kwa takribani miezi minne kabla ya tukio kitokea.
Msaanii wa Bongo Muvi,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akipitia maelezo aliyochukuliwa na Polisi kipindi alipokamatwa ambayo aliyatoa kwaajili ya ushahidi kwa kuhusishwa na kifo cha Msanii Mwenzake Steven Kanumba. Maelezo hayo ameyapitia leo katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam. 
Akisimulia jinsi tukio zima lilivyotokea amedai, April 6 2012,  saa mbili usiku alienda nyumbani kwa rafiki zake mikocheni, akiwa huko Kanumba alikuwa akimpigia simu mara kwa mara kumuuliza mahali alipo. " sikimwambia nipo mikocheni maana mara nyingi alikuwa hapendi niwe mtu wa kutoka toka hasa kwenda sehemu za starehe bila yeye kiwepo". Amedai lulu.

Amedai baada ya kuona Kanumba anazidi kumpigia simu kumuuliza yuko wapi, aliamua kumwambia kuwa anataka kutoka ndipo akamwambia aende Sinza kumuaga.

Akadai alipita kumuaga na alipokaribia alimpigia simu kumwambia kuwa amekaribia kufika ndipo Kanumba alimwambia kuwa akifika aingie ndani moja kwa moja hadi ndani amemuachia mlango wazi.
"Niliingia ndani, nilimkuta anapaka Mafuta nywele zake akiwa kwenye dressing table na kwa kuwa chumbani hakukuwa na kiti nilipofika nilikaa kitandani tukasalimiana ambapo muda mfupi simu yake ikaita, alipokea na kuongea, " namalizia nakuja", nikajua anaongea na Chazi baba ndipo nami nikamwambia nataka kutoka"amedai lulu.

Ameendelea kudai, alipofika pale aligindua Kanumba ameishakunywa, akaniambia kama anatoka waende wote sehemu moja, akaongeza mara nyingi walipokuwa wakitoka wote sehemu moja kunatokea ugomvi, kwani ilipokuwa mtu akimsalimia akimkumbatia alikuwa akimpiga na pia walikuwa wanakwepa kwenda sehemu pamoja kwa ajili ya kukwepa vyombo vya habari.

Nilimwambia kuwa nataka nitoke na rafiki zangu twende Disco mimi sipendi muziki wa Dansi kwani ni kama wakizee, lakini yeye alikuwa hataki badala yake anataka twende wote kwenye dansi,".
Lulu amedai,  wakati akiendelea kuongea na Kanumba, simu yake iliita ambapo aliogopa kupokea mbele ya Kanumba kwa sababu alihisi rafiki zake wanampigia na alishamwambia Kanumba kuwa hatoki tena hivyo endapo wangemuuliza kuhusu suala la kutoka basi Kanumba angesikia.
Akadai kuwa, baada ya kuona hivyo, alimwambia Kanumba kwamba anaenda jikoni kuchukua  maji, alipokea ile simu na kuwaambia rafiki zake kuwa naenda baada ya muda mfupi
"Nikiwa naelekea kuchukua Maji nilipokea simu, ambapo nikaanza kuongea na rafiki zangu kwamba wasubiri nitatoka, lakini wakati nakata simu Kanumba alikuwa ananifatilia kwa nyuma na kuanza kuniuliza naongea na nani,
" Nilikuwa naongea na rafiki yangu, akaanza kunifuata taratibu, nikaanza kumtania kwa kumwambia unanifata hadi jikoni kujua naongea na nani,"
TUNATEKELEZA- MERERANI WAPATIWA FEDHA ZA UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA

TUNATEKELEZA- MERERANI WAPATIWA FEDHA ZA UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA

October 23, 2017

1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta Mhagama akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo wakati wa uzinduzi wa namba maalum ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti ukimwi.

2

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta Mhagama akimkabidhi Hundi ya Tsh. Mil 200 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mererani wakati wa uzinduzi wa namba maalum ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.

3

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo akikabidhi hundi ya Tsh mil 200 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Mererani; Fedha hizo ni kutoka kwenye Mfuko wa udhamini wa kudhibiti ukimwi. 4

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo(aliyesimama) akitoa  neno la Shukrani baada ya kukabdhiwa Tsh Mil 200 za Ujenzi wa Kituo cha Afya Mererani kutoka katika Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.

5

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta Mhagama(katikati) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(tatu kulia), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(tatu kushoto) pamoja na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa namba maalumu ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.
……..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Genesta Mhagama amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jaffo Tsh mil 200,000 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya Mererani ikiwa ni ahadi ya Rais Dr.John Magufuli aliyoitoa wakati wa ziara yake Mkoani hapo mwezi uliopita.
Ujenzi wa Kituo hicho ambao utaboresha huduma za mama na mtoto pia ni maalumu kwa ajili ya kusaidiazaidi katika kutoa huduma kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi katika Wilaya ya Simanjiro.
Ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zilizoathirika zaidi na virus vya Ukimwi haswa katika eneo la mererani imeonekana inahitaji msaada wa haraka ili kudhibiti au kupunguza kabisa tatizo hilo katika jamii ya eneo hilo.
Fedha hizo zimetoka katika mfuko wa udhamini wa udhibiti wa Ukimwi ambao ulizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na kuanza kazi rasmi ya kukusanya fedha kutoka katika vyanzo vya ndani kusaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Akipokea Hundi hiyo Waziri wa Tamisemi Mhe. Selemani Jaffo kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Joel Bendera amesema umefika wakati ambapo jamii ya watanzania wanapaswa kuunga mkono jitihada hizi ili kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Wakati huo huo Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imezindua rasmi namba maalum ya kuchangia Mfuko huo wa udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.
Katika uzinduzi huo ambapo mgeni Rasmi alikua Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe. Genesta Mhagama alitaja namba ya uchangiaji wa mfuko huo kuwa 0684909090 na kwamba kila mwananchi anahimizwa kuchangia Fedha ili fedha itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
Katika hatua Nyingine Waziri Mhagama alimkabidhi hundi ya Tsh. Milioni 660 kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kwa ajili ya kununua dawa aina ya Contrimaxozole za watu wanaoishi na VVU.
Fedha zote hizi zimetoka katika Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.
TAMISEMI YA WANANCHI

UKUTA MKUBWA WA BEIJING (THE GREAT WALL) UNAVYOINEMEESHA NCHI YA CHINA KATIKA SEKTA YA UTALII

October 23, 2017
Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,ambapo Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni hufurika kutembelea ukuta huo wenye historia kubwa nchini humo.Kuusoma zaidi BOFYA HAPA,Ukuta huo umekuwa kivutio kikubwa kwa wenyeji na wageni mbalimbali ambao wamekuwa wakifurika kila kukicha na kujionea historia kubwa ya ukuta huo nchini China,inaelezwa kuwa ukuta huo ni mojawapo ya chanzo kikubwa cha mapato katika nchi hiyo hasa kwa upande wa sekta ya Utalii.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wapita maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wao kabla ya kupanda Ukuta wa The Great Wall mapema leo mchana,ikiwa ni sehemu ya kujifunza,kuona na kutazama fursa mbalimbali za Kiutalii mjini humo na namna wenyeji wa mji wa Beijing wanavyofanya shughuli zao kiutalii.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies na baadhi ya wenyeji wakielekea kwenye geti kuu la kuingilia Ukuta huo wa The Great wall,mapema leo mchana.
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa na Mwenyeji wao,wa tatu kulia wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya The Great Wall,mjini Beijing nchini China.Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa (mwenye njano),akipata maelezo mafupi kutoka kwa mmoja wa wadau wake aliombatana nao Risasi Mwaulanga,huku baaadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakisikiliza kwa makini,kulia ni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Philomena Kasanga, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha,Mansoury Kisebebo pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (pichani kati)Zuberi Mhinana na nyuma yake ni Katibu Tawala Msaidizi – Uchumi na Uzalishaji -Mkoa wa Pwani,Shangwe Twamala pamoja 
Sehemu ye Ukuta Mkubwa ndani ya Mji wa Beijing nchini China (The Great Wall),kama uonekanavyo pichani mapema leo mchana,huku ukiwa mesheheni Maelfu ya watu wakiwemo Wenyeji na wageni (watalii) wakipanda ukuta huo ikiwa kama sehemu ya utalii na kujua historia ya ukuta huo uliopo nje kidogo ya mji wa Beijing nchini China.
The Great Wall ndani ya mji wa Beijing kama uonekanavyo mapema leo.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani na Uongozi wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies wakiwa katika  picha ya pamoja mapema leo mara baada ya kupanda Ukuta wa kihistoria ndani ya mji wa Beijing,nchini China
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kilua Industrial Group of Companies Mohamed Said Kiluwa akiwa na Wenyeji wake,ambao kwa pamoja wanatarajia kuandaa kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda kwa kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani (ambao tayari wamekwishawasili mjini humu),wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali,litakalofanyika jijini Beijing,nchini China Oktoba 25,2017 ,litakalojumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
LIGI YA WANAWAKE KUANZIA NOVEMBA 26

LIGI YA WANAWAKE KUANZIA NOVEMBA 26

October 23, 2017


Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, imefahamika.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema Kundi A litakuwa Dar es Salaam na timu za Simba Queens ya jijini Dar Es Salaam iliyopanda daraja msimu huu.
Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen zote za Dar es Salaam pamoja na timu za Fair Play ya Tanga na mabingwa watetezi – Mlandizi Queens.
Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka kituo cha Dodoma. Timu nyingine ni Marsh Academy pia ya Mwanza; Panama ya Iringa; Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens ya Singida.
Time hizo zitapambana katika vituo hadi Desemba 9, mwaka huu kabla ya kutoa jumla ya timu nane kwa maana ya nne kutoka kila kundi. Timu hizo nane zitapambana katika hatua ya Nane Bora ya Ligi hiyo kuelekea ubingwa. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.
Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, TFF imetoa kalenda ya mashindano hayo ambako usajili utakuwa kati ya Oktoba 25 na Novemba 10, mwaka huu.
Novemba 12 hadi 17, mwaka huu ni kipindi cha pingamizi  wakati Novemba 18, mwaka huu kutakuwa na kikao cha  Kamati ya Sheria kabla ya Novemba 20, mwaka huu kutoa leseni za wachezaji.
Novemba 24, mwaka huu kutakuwa na Semina ya Viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika hatua ya makundi Desemba 9, mwaka huu Ligi Kuu hatua ya Nane Bora ‘Super 8’ itaanza Desemba 20, mwaka huu.
Benki ya Standard Chartered yadhamini Kongamano la Wanawake na Fedha kimataifa

Benki ya Standard Chartered yadhamini Kongamano la Wanawake na Fedha kimataifa

October 23, 2017
Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani (Kushoto) akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam juu ya benki hiyo kudhamini Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha linalotarajia kufanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, nchini Tanzania. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Women's World Banking, Tom Jones pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya Mabenki, Bi. Heidi Toribio (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Women's World Banking, Tom Jones akizungumza katika mkutano na wanahabari kuzungumzia udhamini Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha uliotolewa na Benki ya Standard Chartered. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya Mabenki, Bi. Heidi Toribio akishuhudia.
BENKI ya Standard Chartered imetangaza kudhamini Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha linalotarajia kufanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, nchini Tanzania. Kongamano hilo la siku mbili linatarajia kukutanisha pamoja wanawake viongozi katika fani mbalimbali, zikiwemo mabenki, teknolojia, wafanyabiashara, mashirika ya umma na binafsi. Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani alisema kongamano hilo linatarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. Akizungumzia udhamini huo Bw. Rughani alisema Benki ya Standard Chartered imekubali kudhamini mkutano huo ikiwa ni jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi. "Alisema wanawake wana mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao, tumejidhatiti kikamilifu kuwawezesha wanawake kuwa na uhuru wa uchumi na fedha, kupata mitaji na kuwa na elimu ya mambo ya fedha na uchumi. Sisi kama benki tutaendelea kumuwezesha mwanamke wa Kitanzania kuchangia maendeleo ya nchi yetu," alisema Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Rughani. Aidha aliongeza kuwa, Benki ya Standard Chartered inaamini kongamano hilo litaleta mageuzi ya kiuchumi na kuwawezesha wanawake kuwa wadau wakuu katika kuleta maendeleo ya nchi ya Tanzania na nchi anuai zitakazo shiriki kwenye kongamano. Aidha kongamano hilo linalotarajia kushirikisha wanawake zaidi ya 300 kutoka nchi mbalimbali duniani na wakiwemo wanachama wa shirika la Women's World Banking kutoka mataifa 32. "Siku mbili zijazo zitasaidia kuleta mageuzi hasa katika kuwawezesha wanawake kuwa wadau wakuu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania na katika nchi zingine....," alisisitiza Bw. Rughani. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Women's World Banking, Tom Jones alisema uwepo wa washiriki wanawake kutoka katika sekta mbalimbali watakaoshiriki Kongamano hilo ni ushaidi tosha kuona namna wanawake walivyo na kiu ya kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao. Benki ya Standard Chartered Tanzania inaadhimisha miaka 100 tangu ifungue biashara zake nchini Tanzania na katika kuadhimisha sherehe hizo Mwezi Machi mwaka huu iliwaalika viongozi 40 kutoka mabara ya Afrika na Asia na kuzungumza nao kwa kina namna ya kukuza uchumi wa nchi zao kupitia fursa anuai zilizopo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya Mabenki, Bi. Heidi Toribio (kulia) akizungumza katika mkutano na wanahabari kuzungumzia udhamini huo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akifuatilia. Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano kuzungumzia udhamini Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha uliotolewa na Benki ya Standard Chartered. Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano kuzungumzia udhamini Kongamano la kimataifa la Wanawake na Fedha uliotolewa na Benki ya Standard Chartered. ___________________________________________________________________________________ Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com. Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com

KIKAO CHA TPLB KUFANYIKA OKT. 26, 2017

October 23, 2017
Kamati mpya ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) inafanya kikao chake cha kwanza Alhamisi, Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Moja ya ajenda katika kikao hicho ni kuteua Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, na kamati nyingine mbalimbali.
TPLB ilifanya uchaguzi Jumapili, Oktoba 15 mwaka huu na kupata uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Clement Sanga.
Viongozi wengine waliochaguliwa ni Shani Mligo (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe Hamisi Madaki, Ramadhani Mahano, Almasi Kasongo na Edgar Chibura.
KOCHA SWEDEN AKUTANA NA RC MOROGORO, RAIS KARIA

KOCHA SWEDEN AKUTANA NA RC MOROGORO, RAIS KARIA

October 23, 2017
Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Sweden,Mariane Sundhage leo Oktoba 23, 2017 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe katika Ofisi ya Mkoa na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuboresha soka la wanawake nchini.
Kadhalika, Kocha Mariane Sundhage amefanya mazungumzo yanayofanana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia ambaye baadaye aliongozana naye kwenda kuangalia Kliniki kwenye Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa.
Katika Kliniki hiyo, mbali ya Rais Karia wengine waliokuwako kushuhudia kliniki hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA), Amina Karuma na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka la Wanawake, Mia Mjengwa.
Kocha Mariane Sundhage yuko nchini Tanzania na kesho Jumanne Oktoba 24, 2017 anatarajiwa kuwa na kliniki maalumu kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo mahiri ambaye mbali ya Sweden ambako anafundisha sasa, tayari alikwisha kuzinoa timu za taifa za  Marekani na China.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi, kliniki hiyo itaanza saa 3.30 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana baada ya hapo kocha huyo atakuwa na nafasi ya kuzungumza na wanahabari.
“Karibu sana wanahabari kesho kushuhudia ufundi wa Kocha Pia Sundhage akizinoa baadhi ya timu ambazo TFF imezialika wakiwamo wachezaji wa timu ya taifa,” amesema Madadi alipokuwa anatambulisha ziara ya kocha huyo.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU VYETI VYA SHUKRANI NA PONGEZI KWA KAMATI MAALUMU ZA UCHUNGUZI NA MAJADILIANO KUHUSU RASILIMALI ZA MADINI NCHINI

October 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Profesa Nehemiah Eliakim Osoro  cheti cha pongezi na shukrani katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku  Mwenyekiti wa Kamati ya Kwanza ya Makinikia Profesa Abdulkarim Mruma     cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Mama Fatuma Ndugai ambaye ni Mke wa Spika Mhe. Job Ndugai cheti cha pongezi na shukrani mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uchunguzi wa Makinikia Profesa Osolo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Katibu wa Bunge Mhe. Stephen Kagaigai baada ya kumtunuku Spika Job Ndugai (kupitia kwa mkewe Mama Fatuma Ndugai) cheti cha pongezi na shukrani mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uchunguzi wa Makinikia Profesa Osolo katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi  cheti cha pongezi na shukrani  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtunuku Profesa Florens Luoga cheti cha pongezi na shukrani katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kutunuku vyeti vya pongezi na shukrani kwa wajumbe wa Kamati Maalumu za Uchunguzi na Majadiliano kuhusu Rasilimali za madini nchini  katika hafla iliyofanyika Ikulu jijjini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2017