Maafisa wa Afya na Mazingira wapewa MAFUNZO KWA VITENDO BANDARI

Maafisa wa Afya na Mazingira wapewa MAFUNZO KWA VITENDO BANDARI

November 13, 2015

2
Baadhi ya Maafisa wa Afya na Mazingira kutoka, Bandari, Viwanja vya Ndege na Mipakani  wakiwa katika   ziara ya mafunzo kwa vitendo  kuhusu masuala ya ukaguzi ya vyombo vya usafari iliyofanyika leo kwenye eneo la Bandari ya Dares Salaam.
4
5
Baadhi ya Maafisa wa Afya na Mazingira kutoka, Bandari, Viwanja vya Ndege na Mipakani  wakipanda moja ya meli ikiwa   ziara ya mafunzo kwa vitendo  kuhusu masuala ya ukaguzi ya vyombo vya usafari iliyofanyika leo kwenye eneo la Bandari ya Dares Salaam.
6
picha ya pamoja  ya baadhi ya Maafisa wa Afya na Mazingira kutoka, Bandari, Viwanja vya Ndege na Mipakani  mara baada ya kufanya   ziara ya mafunzo kwa vitendo  kuhusu masuala ya ukaguzi ya vyombo vya usafari iliyofanyika leo kwenye eneo la Bandari ya Dares Salaam.
Picha zote na Magreth Kinabo- MAELEZO

ZOEZI LA USAJILI WA WABUNGE LAANZA LEO MJINI DODOMA.

November 13, 2015

Maafisa wa Bunge wakipokea nyaraka toka kwa wabunge wateule katika zoezi lililoanza leo Mjini Dodoma
Wabunge wateule wakipiga picha kwa ajili ya vitambulisho vitakavyotumika kwa ajili ya matumizi ya Bunge Leo Mjini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Mwanga Mkoani Kilimanjaro Mh. Jumanne Maghembe akikabidhi nyaraka zake wakati wa zoezi la usajili linaloendelea leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Willium Ngeleja akisajili kwa Afisa wa bunge
Maafisa wa benki wakiwapa maelezo wabunge wakati wa zoezi la usajili linaloendelea Mjini Dodoma
Maafisa wa Bunge wakimkabidhi nyaraka Moja ya Mbunge wakati wa Zoezi la Usajili leo Mjini Dodoma

Tigo yadhamini tamasha kubwa la muziki mikoa ya kusini

November 13, 2015

 Iringa, 13th Novemba 2015- Kampuni ya Tigo Tanzania imedhamini tamasha la muziki
kwa wanamuziki chipukizi katika mikoa ya Kanda ya kusini ikiwa ni fursa ya wasanii
hao  kuonesha vipaji vyao kwa wapenzi wa muziki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo
Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, udhamini wa tamasha hilo liitwalo ‘Mtikisiko’ ni sehemu ya sera ya
kampuni hiyo ya kusaidia makundi mbalimbali katka kijamii wakiwemo vijana na
wasanii kufikia ndoto zao za kimaisha.
Akifafanua zaidi tamasha hilo Kiswaga,
alisema bonanza la Mtikisiko litakuwa
nyenzo ya kuwasaidia wanamuziki wapya kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe,
Ruvuma na Rukwa kwa kuwatambulisha mbele ya mashabiki na wapenzi hivyo kuwaweka
katika nafasi ya kujipatia kipato kutokana na kazi zao zao.
 “Udhamini huu umeonesha ni jinsi gani Tigo imedhamiria
kusaidia kuendeleza mikakati na shughuli mbalimbali za ubunifu zinayofanywa na
vijana katika harakati zao za kujiinua kiuchumi,” alisema Kiswaga.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema mapema
mwaka huu kampuni ya Tigo ilizindua huduma iitwayo Tigo Music ambayo inawapa
wanamuziki nchini fursa ya kupakia nyimbo zao kwenye mtandao wao Internet na hivyo
kuweza kusikilizwa na hadhira ya kitaifa na kimataifa jambo ambalo linawapa wasanii
kipato cha ziada na fursa ya kujulikana kimataifa.
“Jukwaa la Tigo Music limetoa
mchango  muhimu katika kuwanyanyua
wasanii wanaoibukia  na kuchangia kuibuka
kwa nyota wa ndani hadi kufikia viwango vya kimataifa. Ni matarajio yetu kwamba
Bonanza hili la Mtikisiko ambalo litakalofanyika
kwa kipindi cha wiki mbili litaibua majina na vipaji vipya katika Sanaa ya
muziki nchini,” alisema Kiswaga
 

WATANZANIA WAPEWA SOMO KUHUSU DIPLOMASIA YA uCHUM (ECONOMIC DIPLOMACY)

November 13, 2015

Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Ahmed Kiwanuka,Nduwayo Mzonya,Hussein Melele,na Rashid Njenga wakiwasikiliza wachangaji mbalimbali katka kongamano hilo lijulikanalo Epowerment of Economic Diplomacy in Tanzania .

Balozi mstafu wa Tanzania Nchini India ambaye pia ni mwalimu katika chuo cha diplomasia Balozi Ahmed Kiwanuka akitoa mhuadhara elo kuhusu namna Tanzania inavyoweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kupitia ekta mbalimbali na kwa kutumia makundi mbalimbali

Allan Kasamala(mwenye shati ya bluu) akiwa na Baadhi ya washiriki walioshiriki kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Wanafunzi,wahitimu na marafiki wa chuo cha diplomasia leo katka ukumbi wa chuo hicho  kilichopo kurasini jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hilo limeandaliwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi wakishirikiana na wahitimu wa Kozi mbalimbali za mwaka wa masomo 2014/2015 wakiongozwa na Simalenga Simon amaye amemaliza PGD MFR 2014/2015.
Washiriki wa kongamano hilo.

KICHUPA KIPYA; JOH MAKINI FT AKA - DON'T BOTHER

November 13, 2015
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

UZINDUZI WA USHIRIKA WA MAMA NA BABA LISHE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA 15, 2015

November 13, 2015
Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Jumuiya Ya Mama na Baba Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Said Said (wa pili toka kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam. Lengo la jumuiya hiyo kuunganisha kwa pamoja wadau mbalimbali, kutoa fursa kulinda haki za ajira na kuzitafutia ufumbuzi na kuondoa tatizo la ajira kupitia tasnia hii ikiwa ni kumtambua mama na baba lishe kama sehemu ya maisha ya kila mmoja wetu, kwani kila mtanzania anaufahamu umuhimu wa mama na baba lishe na takwimu zinaonyesha asilimia 50% ya wanzania waishio mijini hupata huduma ya chakula. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Mhonzu akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Mama Lishe wakiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Waaandishi wa habari wakufuatia mkutano huo.

JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA AANZA KUPIGA MZIGO FASTA

November 13, 2015

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi,Ofisi Ndogo Lumumba.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti Ndugu Anamringi Macha mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Lumumba.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wapenzi na wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye ofisi yake,waliosimama ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib (kulia) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi.

Ulinzi wa Tembo kwa kutumia Satelaiti waanza Ruaha

November 13, 2015

Shirika la Hifadhi za Taifa limezindua program maalum ambapo tembo 30 wanaoongoza makundi 30 katika mfumo wa Ikolojia wa Ruaha Rungwa watavalishwa kola malum shingoni zenye vifaa vinavyorekodi mienendo yao kwa kutumia satelaiti. Program hii inafadhiliwa kwa pamoja na taasisi za Global Environment Facility pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi alisema kuwa “ Lengo kuu la program hii ni kupata taarifa za kina juu ya mienendo ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwa zitakazosaidia kubainisha maeneo ya shoroba na mitawanyiko kwa ajili ya ulinzi wa tembo”

UNDP kupitia ushirika wake na TANAPA/SPANEST wametoa kandarasi ya kazi hii kwa taasisi ya World Elephant Centre ya nchini Tanzania inayotarajiwa kuongeza hali ya usalama wa tembo hifadhini.

Teknolojia hiii inawezesha kujua mwenendo wa tembo ndani na nje ya hifadhi, kujua walipo, wanapopita, kasi yao ya kutembea, sehemu wanazojificha, wanazokunywa maji, wanazopumzika, maeneo wanayokaa kwa muda mrefu, kama wamekufa, wamejeruhiwa,wamehama hifadhi moja hadi nyingie na taarifa nyingine nyingi hivyo itakuwa rahisi kwa askari wa wanyamapori kufuatilia usalama wao.

Kola hizo zenye uwezo wa kufanya kazi kwa miaka mitatu bila kubadili betri zake zinafungwa kwa Tembo 30 wanaoongoza makundi 30.
Wataalam wa Uhifadhi wakiongozwa na Dk. Alfred Kikoti (wa kwanza kulia) wakiendelea na zoezi la uwekaji kola maalum kwa tembo zinazosaidia kudhibiti mienendo ya tembo ndani na nje ya hifadhi ya Mfumo wa Ikolojia wa Ruaha Rungwa.
Zoezi la uvalishaji wa kola maalum kwa tembo katika hifadhi ya Ruaha likiendelea.
Helikopta maalum inayotumiwa na madaktari kwa ajili ya kutambua na kupiga dawa ya usingizi kwa tembo kabla ya uvalishaji wa kola maalum.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (mwenye kofia) akishuhudia zoezi la uvalishaji kola maalum kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Daktari wa Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) akijiandaa kumdunga sindano ya kumzindua tembo baada ya kukamilika kwa zoezi la kumvalisha kola maalum.
Picha ya pamoja ya wahifadhi walioshiriki zoezi la uzinduzi wa program maalum ya uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Iringa wakati wa zoezi la uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
S.L.P 3134
ARUSHA
Baruapepe: dg@tanzaniapaks.com
Wavuti: www.tanzaniaparks.com

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASHIRIKI MSIBA WA MJUKUU WA RAIS MAGUFULI

November 13, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mjukuu wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Maryfaustna Mlyambina, aliyefariki Nov 11, 2015. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu zilifanyika leo Nov 13, 2015 Kimara jijini Dar es Salaam, na baadaye msiba huo kusafirishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Maryfaustna Mlyambina zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo. Marehemu ni mjukuu wa Mhe Rais. 
Wazazi wa marehemu wakiwa na baadhi ya wanafamilia, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu.
Rais Dkt. John Magufuli (wa tatu kuli) Makamu wake (wa Nne kulia) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli (kulia) na Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete (kushoto) wakishiriki ibada maalum ya kumuombea marehemu wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Kimara jijini Dar es Salaam, leo Nov 13, 2015.

Sehemu ya wanafamilia ya wafiwa katika ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Mjukuu wa Mhe Rais John Magufuli, marehemu Maryfaustna Mlyambina, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika Kimara jijini Dar es Dalaam,leo Nov 13, 2015.
Baadhi ya kinamama wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mjukuu wa Rais Dkt. John Magufuli, baada ya shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Kimara, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mama mzazi wa marehemu na baadhi ya wanafamilia wafiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati aliposindikiza msiba wa mjukuu wa Mhe. Rais, marehemu Maryfaustna Mlyambina, leo Nov 13, 2015. 
Picha na OMR

WADAU WA AFYA MKOANI MBEYA WAKUTANA NA KUJADILIANA KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA UKIMWI DUNIANI

November 13, 2015
Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stellah Kategile akiwasilisha maada kwa wadau wa Sekta ya Afya Mkoani Mbeya katika kikao cha kujadili juu ya kuelekea katika siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani Tarehe 1 Desemba mwaka huu.

Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoani Mbeya (RACC-Regional AIDS Control Coodinator ) Dkt Francis Philly akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya mkoani  katika ukumbi wa Cofee Garden jijini Mbeya

Mrakibu wa Polisi Mkuu  dawati la jinsi na watoto Mkoa wa mbeya Ndugu Debora Mrema akielezea masuala mbaliimbali  yanayolikumba Dawati hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsi Mkoani humo huku akisisitiza juu ya wadau kujitokeza na kutoa michango yao ya kifedha sanjali na rasilimali nyingine ili kuweza kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali mkoani humo hususani maeneo ya vijijini..

Wadau wakiendelea na majadiliano katika mkutano huo.


Mwakilishi wa Kampuni ya Mbeya Cement jijini Mbeya ambaye ni Mratibu wa Masulaa ya Afya na Jamii Grace Nyatori akichangia katika mkutano hiuo ambao unalenga kujadili na kupitisha bajeti kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani .

Mhariri wa habari kutoka Radio Ushindi jijini Mbeya Edom Mwasamya akizungumza namna ambavyo vituo vya radio vitakavyo weza kuchangia kufanikisha zoezi hilo la siku ya Ukimwi Duniani.

Festo Sikagonamo  kushoto Mkuu wa shirika la Elimisha  pamoja na Neema Stanton Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Maji safi na maji taka jijini hapa wakishirika katika mkutano huo.

Wadau wakiendelea na majadiliano.
Na Emanuel Madafa, JamiimojablogMbeya