Waziri Mwakyembe ashuhudia uwekaji saini wa Shillingi Bilioni 2.1 baina ya TFF na SBL kusaidia Taifa Stars

Waziri Mwakyembe ashuhudia uwekaji saini wa Shillingi Bilioni 2.1 baina ya TFF na SBL kusaidia Taifa Stars

May 12, 2017
unnamed
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na wadau wa michezo wakati wa uwekaji saini wa msaada wa fedha wa Shillingi Bilioni 2.1 baina ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kulia ni Rais wa TFF Jamal Malinzi na Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  wa SBL Bibi. Helene Weesie.
A
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Jamal Malinzi (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa kuweka saina msaada wa fedha kiasi cha Shillingi Bilioni 2.1 zilizotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kuisadia timu ya Taifa Stars,katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  wa SBL Bibi. Helene Weesie.
A 1
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimshuhudia Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Jamal malinzi (kulia) akiweka  saini hati ya makabidhiano ya ya  pesa Shillingi Bilion 2.1 zilizotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa ajili ya kuisaidia timu ya Taifa Stars leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Bibi. Helene Weesie.
A 2
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akishudia Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Jamal Malinzi (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bibi. Helen Weesie (kushoto) wakibadilishana hati baada ya kuweka saini leo Jijini Dar es Salaam.
A 3
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Jamal Malinzi(wa pili kushoto) na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bibi. Helen (wa kwanza kulia) Weesie wakipeana mkono baada ya kukabidhi hundi ya Shillingi Bilioni 2.1 kusaidia timu ya Taifa Stars ,wa pili kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw.Yussuph Singo.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.
RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA ALIVYOSHIRIKI KATIKA DHIFA YA KITAIFA ALIYOANDALIWA JANA USIKU NA RAIS DKT. MAGUFULI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA ALIVYOSHIRIKI KATIKA DHIFA YA KITAIFA ALIYOANDALIWA JANA USIKU NA RAIS DKT. MAGUFULI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

May 12, 2017
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali (hawaonekani pichani) waliohudhuria katika Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
A
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Mama Janeth Magufuli (Mke wa Rais), Mama Sizakele Zuma wakwanza kulia (Mke wa Rais wa Afrika Kusini) wakati nyimbo ya Taifa ikipigwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 3
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 4
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiwa amemshika mkono Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim wakati akizungumza jambo na Rais Msaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa mara baada ya kumalizika kwa Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati Bendi ya Kilimanjaro “Wana njenje” ilipokuwa ikitumbuiza katika Ukumbi wa Ikulu katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais Zuma.
A 6
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati Bendi ya Kilimanjaro “Wana njenje” ilipokuwa ikitumbuiza katika Ukumbi wa Ikulu katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais Zuma.
A 7
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni ni Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
A 8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais huyo wa Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 9
Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na Serikali wakiwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

VIWANJA VINAUZWA BEI POA VIPO KISEMVULE MKURANGA MKOANI PWANI

May 12, 2017

 Sehemu ya viwanja hivyo vinavyoonekana nyuma ya Kiwanda cha Saruji cha Rhino kilichopo eneo hilo la Kisemvule.
 Kijana anayesimamia viwanja hivyo akionesha mipaka.
 Viwanja hivyo vikiwa vimepimwa na kuwekewa bicon
Mmoja wa wafanyabiashara alikiangalia viwanja hivyo kwa ajili ya kuvinunua.

VIWANJA VINAUZWA VIMEKWISHA PIMWA  UKUBWA WAKE NI 15X15 BEI NI SHILINGI MILIONI 2 NA NUSU NA VYENYE UKUBWA WA 30X30 NI SH. MILIONI 5 VIPO KIJIJI CHA KISEMVULE KATA YA VIKINDU WILAYA YA MKURANGA MKOANI PWANI JIRANI NA KIWANDA CHA SARUJI CHA RHINO BARABARA KUU YA KWENDA MIKOA YA KUSINI NA VIPO KATIKA MIUNDOMBINU YA BARABARA, MAJI NA UMEME, ANAYEVIHITAJI ANAWEZA KUWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MUHUSIKA KWA NAMBA 0756430981.