MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA MAJIPU

April 20, 2016
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kwa kufanyakazi chini ya kiwango pamoja na wasaidiziwake wawili.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo, Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango . Kulia ni Msaidizi wa Meya, Semmy Mbegha.
Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi, Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi unaoendelea.

Kuyeko alisema  kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.

Alisema baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta kero ndani ya manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina malalamiko mengi kutoka kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya kusimamia ujenzi wa barabara chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa na maofisa hao.

Alisema madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa akikaidi wito wao wa kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi zinapobainika jambo ambalo limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara nyingi mbovu.

Jitihada za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia kusimamishwa kwake kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na wakati wote kuwa imefungwa.


TANAPA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI MLIMA KILIMANJARO

TANAPA KUZINDUA KAMPENI YA USAFI MLIMA KILIMANJARO

April 20, 2016

PAS
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (kati) akiongea na wanahabari jijini Arusha jana kuhusiana na Kampeni ya siku Kumi ya Usafi wa Mlima Kilimanjaro inayotarajiwa kuanza leo. Wengine pichani ni Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Utalii  Tanzania Bw. Cyril Ako (kulia) na Mwakilishi kutoka Hoteli ya Kibo Palace BI. Jenipher Swai.
…………………………………………………………………………………………………..
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kesho tarehe 21.04.2016 litazindua Kampeni Maalum ya siku 10 ya usafi wa Mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo Utafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Mecky Sadik.
Kazi hii ya kusafisha Mlima Kilimanjaro itafanywa na watumishi wa hifadhi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii zaidi ya 200, wakiwemo mawakala wa utalii  (tour operators), waongoza wageni (guides), wapagazi (porters) na wapishi (cooks) wanaowahudumia watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.
Usafi huu utahusisha maeneo mbalimbali ya hifadhi kama vile njia za kupandia mlimani, maeneo ya kupiga kambi, maeneo ya mabanda, na maeneo ya kupumzikia wageni (picnic sites).
Kampeni hii ni muendelezo wa utaratibu wa kawaida wa hifadhi unaofanyika kila wakati kuhakikisha maeneo ya hifadhi hasa yanayotumika na wageni yanakuwa katika viwango vya kimataifa vya utoaji huduma kwa wageni. Huu ni utaratibu wenye lengo la kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wanauweka Mlima Kilimanjaro katika hali ya usafi muda wote.
Mlima Kilimanjaro unachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 60 ambazo ni sawa na asilimia 34 kwa mwaka katika mapato ya TANAPA. Aidha, Mlima Kilimanjaro hutoa ajira zaidi ya laki tatu(300,000) kwa mwaka kwa Watanzania wanaofanya shughuli za utalii mlimani.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
20.04.2016
RAIS DK SHEIN ATEMBELEA KAMBI YA KIPINDUPINDU

RAIS DK SHEIN ATEMBELEA KAMBI YA KIPINDUPINDU

April 20, 2016

KIP1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana wa Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu Ramadhan Mikidadi Suleiman leo asubuhi alipotembelea kituoni hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja,wengine ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo(wa pili kushoto) na naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Said Suleiman na Katibu Mkuu Dkt.Juma Malik Akili (katikati).[Picha na Ikulu.]
KIP2
Baadahi ya watoa huduma na wananchi wakisubiri huduma katika Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu kama wanavyoonekwanwa wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotembelea kituoni hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
KIP3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka Mkurugenzi kinga Wizara ya Afya Dk.Mohamed Dahoma (katikati) wakati alipotembelea  Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo asubuhi,wengine ni Daktari dhamana wa Kituo cha Maradhi ya KipindupinduRamadhan Mikidadi Suleiman (kushoto)Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Jama Adam Taib(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.]
KIP4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maelezo kwa Uongozi wa Wizara ya Afya wakati alipotembelea  Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo asubuhi,(wa pili kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo, [Picha na Ikulu.]
KIP5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la LIONS CLUBS Kanda ya Tanzania na Uganda Bw.Hyderall Gangji wakati alipotembelea  Kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni karakana Wilaya ya Magharibi Unguja leo asubuhi,wengine (kushoto) Mustafa kudrati  LIONS CLUBS Tanzania na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo,[Picha na Ikulu.]
KIP6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akimsikiliza Mwanamama Siti Akida Makame  mkaazi wa Ziwa Maboga aliyeruhusiwa kurudi nyumbani katika kituo cha Maradhi ya Kipindupindu hapo Chumbuni Karakana Wilaya ya Magharibi Unguja,baada ya kuugua maradhi hayo wakati Rais  alipotembelea  Kituo hicho leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]