TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA TFF LEO
Release No. 206
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 6, 2013
TUMEJIANDAA VIZURI KWA MECHI- TANZANITE
Tanzanite
imesema iko vizuri kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa
wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Afrika Kusini
(Basetsana) inayochezwa kesho Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Kocha
Mkuu wa Tanzanite, Rogasian Kaijage amesema wamejiandaa vizuri kwa
mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa kuanzia saa 10
kamili jioni.
KWAHERI MADIBA [1918-2013
Leo hii dunia nzima inaomboleza kifo cha Nelson Mandela
“Madiba”.Mandela ambaye alizaliwa tarehe 18 Julai mwaka 1918 huko
Mvezo, Afrika Kusini amefariki akiwa na miaka 95.
Tangazo la kifo cha Mandela lilitolewa rasmi jana usiku [kwa saa za Afrika Kusini] na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma akisema;
Tangazo la kifo cha Mandela lilitolewa rasmi jana usiku [kwa saa za Afrika Kusini] na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma akisema;
“Our nation has lost its greatest son. Our people have lost a father. Although we knew that this day would come, nothing can diminish our sense of a profound and enduring loss, His tireless struggle for freedom earned him the respect of the world. His humility, his compassion and his humanity earned him their love”
TANGA RAHA inaungana na watu wote duniani katika kuomboleza msiba huu mkubwa.
Mandela alikuwa na atabia kuwa ishara au alama ya ushujaa,
amani,demokrasia na utumishi wa umma uliotukuka.Mungu ailaze roho yake
mahali pema peponi.
*KIDUMU ATUA NCHINI KUWASHA MOTO CLUB E LEO
Msanii
kutoka nchini Burundi, Jean Pierre “Kidum” akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julias Nyerere jana usiku kuja kutumbuiza katika Shererhe ya
Kampuni ya Sigara Tanzania(TCC) “CLUB E” inayotarajiwa kufanyika leo katika
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Msanii
kutoka nchini Burundi, Jean Pierre “Kidum”(kulia) akiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jana usiku kuja kutumbuiza katika Shererhe
ya Kampuni ya Sigara Tanzania(TCC) “CLUB E” inayotarajiwa kufanyika leo katika
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwenyeji wake, Ather.
Msanii
kutoka nchini Burundi, Jean Pierre “Kidum” (katikati) akiwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jana usiku na waimbaji
wake kuja kutumbuiza katika Shererhe ya Kampuni ya Sigara Tanzania(TCC)
“CLUB E” inayotarajiwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es Salaam.
KIGOMBE BINGWA WA KOMBE LA MKONGE CUP 2013
TIMU ya Shamba la Mkonge la Kigombe mkoani Tanga leo
wameibuka na ubingwa wa Kombe la Mkonge Cup mara baada ya kuibamiza China Farm ya
Morogoro mabao 4-3 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la soka
Mkwakwani.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa
ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyoweza kuona lango
la mwenzie,kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya mashambulizi kwa timu zote.
Wakionekana kujipanga na kujiimarisha vilivyo,Kigombe
waliweza kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa China Farm na
kufanikiwa kuandika bao lao la kwanza dakika ya 56 kupitia Said Yasin kwa njia
ya penati iliyotokana na mshambuliaji wa China Farm kumchezea faulu eneo la
hatari Abdallah Maduba.
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MZEE MANDERA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais wa zamani wa Afrika ya
Kusini, Nelson Mandera, aliyefariki usiku wa kuamkia leo wakati
alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika ya Kusini zilizopo
Masaki jijini Dar es salaam leo. Mzee Nelson Mandela (95) alifariki
Dunia jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg. Kushoto ni
Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini, Henry Thanduyise Chilize.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya picha ya marehemu Nelson Mandera
baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania, Henry Thanduyise Chiliza (kulia) na baadhi ya Viongozi wa
Ubalozi huo kwenye ofisi za Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini
Dar es salaam leo, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
Subscribe to:
Posts (Atom)