MAADHIMISHO YA NANENANE 2017 KITAIFA KUFANYIKA LINDI KUANZIA KESHO

July 31, 2017
Na Mathias Canal, Lindi
   
Maonesho ya Kilimo (NaneNane) yanataraji kuanza kesho Agosti 1, 2017 kote nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda huku Maonesho hayo Kitaifa yakifanyika Mkoani Lindi huku Maandalizi na maonesho ya  Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa  mikoa husika.


Maandalizi ya Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yatafanyika kwa siku 8 ambapo Kitaifa yatafika ukomo jioni ya Agosti 8, 2017 katika Viwanja vya Ngongo na Maeneo mengine yatakapoadhimishwa kikanda  katika  viwanja vya maonesho ni John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni -  Dodoma; Nyahongolo – Mwanza; na Fatuma Mwassa - Tabora. 


Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini. 


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg Mathew Mtigumwe wakati akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com  kueleza muktadha wa Maonesho hayo ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi na kubebwa na kauli mbiu mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo "Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati" 


Mtigumwe ameuambia Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com kuwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo wataendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa.

Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi.

Teknolojia/Bidhaa zitakazooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa.

Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta.

Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yohusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalifunguliwa tarehe 03 Agosti 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.


Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo.

Miaka ya 1990 sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.Ambapo Lengo la serikali likawa kuitumia Saba Saba kama siku ya maonyesho ya biashara ya kimataifa, ambapo wafanyabiashara wengi walijitokeza ama hujitokeza kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha na siyo kuwafundisha Watanzania mbinu za kuzalisha biadhaa hizo.

Picha zaidi zinaonyesha maandalizi ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi

UNAITUMIAJE TEKNOLOJIA KURAHISISHA SHUGHULI ZAKO ZA KILA SIKU?

July 31, 2017


Na Jumia Travel Tanzania

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia binadamu waliyonayo kwa sasa si jambo la kushangaza kumuwezesha mtu akafanya shughuli zako zote akiwa yupo sehemu moja ndanin ya muda mfupi.

Kwa mfano, kwa kutumia simu yako ya mkononi unaweza kutatua changamoto kadhaa hapo nyumbani kwako kama vile kufanya miamala ya fedha kutoka benki na kisha kutoa kwa mawakala huduma za fedha, kulipia umeme, kulipia maji, kulipia king’amuzi, kuagiza chakula, kuagiza usafiri, kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali.

Lakini swali ni kwamba, je ni watanzania wangapi wanaiona fursa hiyo iliyoletwa na teknolojia kama suluhu za changamoto tofauti zinazowazunguka?

NMB YAZINDUWA SIKU YA WALIMU MKOANI DODOMA

July 31, 2017

Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (wa kwanza kulia) akifurahi pamoja na maofisa wa Benki ya NMB mara baada ya uzinduzi rasmi wa hafla ya siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu ilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hazini jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya Mwalimu katika mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.

BENKI ya NMB imezindua rasmi siku ya walimu katika Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo wa siku ya walimu Mkoa wa Dodoma ulizinduliwa rasmi na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana.
Hafla hii adhimu ilifanyika katika ukumbi wa Hazina na kuhudhuliwa na zaidi ya walimu 200 wa mkoa huo mwishoni mwa wiki. Uzinduzi wa hafla hii ni miongoni mwa mikakati ya NMB ya kuwafikia walimu nchini kote. Kusudi kubwa la hafla hiyo ya NMB na Walimu ni kuwaongezea uelewa walimu juu ya huduma za benki.
Hii ni kutokana na umuhimu wa kundi hili kubwa katika jamii inayotuzunguka. NMB wanaimani kwamba mwalimu akielimika jamii nzima itakua imepata elimu ya huduma za kifedha. Lakini pia kwa kuzingatia ukubwa wa kundi hili NMB imekua ikitumia fursa hii kupokea mrejesho ya jinsi huduma za kibenki zinavyopokelewa na wateja wake.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo mjini Dodoma, Meneja mwandamizi wa wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga alisema NMB inazo huduma mbalimbali ambazo kusudi lake kubwa ni kumsaidia mteja aweze kujikwamua kiuchumi. Aliongeza kuwa zipo huduma za mikopo ya aina mbalimbali ambapo walimu wanaweza kunufaika nayo.
Mikopo ambayo inatolewa na Benki ya NMB sio kwa ajili ya wafanyabiashara tu bali ni kwa ajili ya kila mtu mwenye vigezo vya kukopeshwa ambapo walimu ni miongoni mwa walengwa wa mikopo hii. Msichukue mkopo benki kama hamna mipango thabiti ya matumizi ya mkopo huo, Ni vyema kuchukua mkopo benki ukiwa na mipango endelevu," alisema Bw. Omari Mtiga.
"...Tukiwa kwenye mikakati ya serikali ya Viwanda ni vyema mkatumia vizuri maonyesho ya Nane nane yanayotarajiwa kuanza kutembelea mabanda ambayo mtajifunza namna ya uwekezaji kwenye sekta viwanda ili kujikwamua kiuchumi kwa kutumia uwepo wa benki ya NMB kwenye jamii yetu bila kuathiri mwenendo wa jaira zetu. Alisema kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge katika hafla hiyo.

Sehemu ya walimu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya walimu mkoa wa Dodoma.

Picha za kumbukumbu na Sehemu ya walimu pamoja na Afisa Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rehema Madenge.
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

MAMA NAMAINGO ‘AWAFUNDA’ AKINAMAMA WA GREEN VOICES KILIMOBIASHARA NA UJASIRIAMALI

July 31, 2017
Mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahim
Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia Cedaba, akiwapa majukumu washiriki wa warsha hiyo.

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim, amewataka akinamama wanatekeleza mradi wa Green Voices Tanzania kuwa wabunifu na kutokata tamaa katika shughuli wanazozifanya.
July 31, 2017
Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA. Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo. Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu. Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo. Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo.[/caption] Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, ambao ni wafadhili wakubwa wa mtandao huo Bw. Christophe Legay kwa niaba ya Mkuu wa ofisi Bi. Zulmira Rodrigues amepongeza hatua iliyofikiwa na Radio wanachama ya kuunda mtandao mpya. Alieleza kuwa UNESCO itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na shirika hilo jipya la TADIO ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma sahihi za kihabari zitakazosaidia kuboresha maisha yao na kuchochea maendeleo ya upashanaji wa habari nchini. Bw. Christophe amehimiza kwamba vyombo vya jamii vinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha sauti za watu wanaowahudumia hasa wanaoishi vijijini.
UNCDF YAWEZESHA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA BWAWA LA KALEMAWE

UNCDF YAWEZESHA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA BWAWA LA KALEMAWE

July 31, 2017
SERIKALI ya Tanzania, imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) kwa kuwezesha watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi wanayoidhamini au kuitafutia fedha. Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa kupeleka madaraka kwa umma na shughuli za maendeleo ya kiuchumi . Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa kongamano la siku 2 la Wadau wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la Kalemawe lililoko wilaya ya Same mwishoni mwa wiki. “Tunafurahishwa kwa namna ya pekee na UNCDF kwa jitihada zake zinazoendeshwa kupitia katika Mpango wa Ufadhili Miradi ya kiuchumi (LFI),” alisema Iyombe na kuongeza: “Tunapokutana hapa tunapewa fursa na kufunuliwa uzoefu wa ushiriki wa UNCDF katika miradi mbalimbali, safari hii tukishuhudia hatua yake ya kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro.” [caption id="attachment_2552" align="aligncenter" width="1404"] Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo kuhusu mradi wa ufugaji samaki katika shamba hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mh. Naghenjwa Kaboyoka na Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (wa pili kulia).[/caption] Pamoja na kushukuru kwa hatua mbalimbali zilizofikiwa na taasisi hiyo katika kusaidia watanzania, aliwataka wakazi wa Same kuhakikisha kwamba mradi huo ulioundiwa kampuni ili kwenda kibiashara unafanikiwa na kuwa mfano kwa wengine. Halmashauri ya wilaya ya Same, na jamii inayozunguka bwawa la Kalemawe wanashirikiana na UNCDF kuboresha miundo mbinu ya bwawa hilo na kuwezesha uwapo wa uwekezaji kwa kuanzisha kampuni. Kampuni hiyo iliyosajiliwa ya Kalemawe Dam Investment Limited katika mpango maalum (SPV) inamilikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Same, halmashauri ya vijiji sita, wakala wa serikali, watu binafsi pamoja na makundi ya kijamii. Kuwapo kwa kampuni hiyo ni juhudi zinazofanywa za kuwezesha uhusiano mahsusi wa kibiashara unaohusisha ubia wa Serikali, Binafsi na jamii (PPCP) kwa kutoa umiliki linganifu mpaka katika ngazi za chini za mamlaka za kijiji, ambazo kimsingi ndizo wamiliki wa maliasili muhimu ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1999.