MTOTO WA MAREHEMU MBARAKA MWINSHEHE AWACHOMA VISU WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA

MTOTO WA MAREHEMU MBARAKA MWINSHEHE AWACHOMA VISU WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA

December 18, 2013

Imewekwa leo Desemba 19 2013 saa 10:54 Asubuhi.Na Makongoro Oging’

MASIKU Mbaraka Mwishehe ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kinondoni, Dar es Salaam kwa madai ya kuwashambulia kwa kisu watu wawili wa familia moja.
Tukio hili lilitokea hivi karibuni Mwananyamala Kisiwani, Dar ambapo kwa mujibu wa taarifa ya kipolisi, mtuhumiwa huyo alikutwa ndani ya nyumba ya Nelson Ainea Shoo, saa kumi na moja alfajiri.
Akizungumza na Amani, mke wa Nelson aliyejitambulisha kwa jina la Neema Hamis Zame (32), alikuwa na haya ya kusema:
“Siku ya tukio, ilikuwa alfajiri kabla hatujaamka, ghafla nilimsikia shemeji yangu aitwaye Goodluck (Ainea Shoo) akipiga kelele na kusema: ‘Kaka kuna mwizi.’ Mume wangu aliamka akatoka kuelekea sebuleni na mimi nilikuwa nyuma yake.


NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE YASHINDWA KUTUA KIA,YALAZIMIKA KUTUA NA KUSIMAMA NJE YA UWANJA WA ARUSHA

December 18, 2013
imewekwa leo desemba 18 saa 7:48 usiku.
Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka jijini Arusha, zinasema kuwa abiria zaidi ya 200 waliokuwa ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) wamenusurika mchana wa leo baada ya ndege hiyo kushindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyojitokeza kwa dharula Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha.

MASHABIKI YANGA WASHINDA AIRPORT WAKIMSUBIRI OKWI BADALA YAKE WAJIKUTA WAKIMPOKEA BEKI WA SIMBA GILBERT KAZE

December 18, 2013
IMEWEKWA LEO DESEMBA 18 SAA 7.35 USIKU
 

TANZANIA NI NCHI YA KWANZA BARANI AFRIKA KWA SAFARI ZA UTALII , SERENGETI NA RUAHA IRINGA ZAONGOZA

December 18, 2013

 Kaimu mkurugenzi  mkuu  wa hifadhi  za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe ( kulia) akimakabidhi  Bi Jane Mwakinyuke kutoka Hifadhi ya Taifa Mikumi , cheti  cha  kuhitimu mafunzo  ya mwezi mmoja ya kuongoza  watalii katika hifadhi  za Taif
Kaim mkurugenzi mkuu wa TANAPA DR Ezekiel Dembe wa pili kulia waliokaa akiwa na  kaim mhifadhi wa Ruaha Bw John Nyamhanga kulia ,Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST kushoto wa  pili na kaimu RAS Iringa pamoja na  walimu wa mafunzo  hayo na askari  waliohitimu mafunzo  waliosimama

MTEJA KWETU NI MFALME:TANGA BEACH RESORT YAMFANYIA SHEREHE MAALUMU MTEJA WAO.

December 18, 2013


MENEJA MKUU WA HOTELI YA TANGA BEACH RESORT ,MR.JOSEPH ALIYESHIKA MIKONO KATIKATI AKIWA NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA HOTEL HIYO KATIKA SHEREHE HIZO AMBAZO ZILIFANYIKA LACASACHIKA CLUB.






MENEJA MKUU WA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT,MR.JOSEPH AKIWAASA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA BIDII KATIKA TAFRIJA HIYO


BAADA YA KUMFANYIA PARTY MGENI WAO WAKAMPATIA CHETI MAALUMU CHA KUMTHAMINI .

MILIONI 20 KUTUMIKA UKARABATI UWANJA WA CCM MKWAKWANI

December 18, 2013
IMEWEKWA 06;49 Desemba 18,2013.
 Na Oscar Assenga,Tanga.

UONGOZI wa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga umetenga kiasi cha  sh.milioni 20 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo ambapo fedha hizo zitatumika kwa awamu mbili tofauti.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM),Gustav Mubba akiwa eneo la uwanja huo leo wakati harakati za kuukarabati zikiendelea

sehemu ya uwanja wa Mkwakwani ikiwa imetifuliwa kwa ajili ya ukarabati leo


Akizungumza na TANGA RAHA BLOG leo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(CCM) Gustav Mubba(pichani Juu)alisema awamu ya kwanza ya ukarabati huo ilianza tokea Novemba Mosi kwa kukarabati vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji pamoja na kuuweka imara mfumo wa maji taka na safi.

 

Mubba alisema matengenezo mengine ni ufumuaji wa mfumo wa kumwagilia maji uwanjani badala ya kuweka mpira uwanjani wanaweka mfumo wa kumwagilia kupitia mashine ya paipu.


Aidha alisema awamu ya kwanza inatarajiwa kutumia sh.milioni 7 mpaka kumalika kwakea na kiasi kilichobakia kitatumika kwa awamu inayofuatia lengo ni kuhakikisha uwanja huo unakuwa wa kisasa zaidi.

 

Alisema matengenezo mengine yatakayofanyika ni kuweka mageti ndani ya uwanja ili kuweza kuzuia mashabiki wa soka kuingia uwanjani mara baada ya mechi kumaliza ambapo suala hilo linasababisha vurugu kutokea au timu pinzani kuletewa fujo.


Katibu huyo alisema pia ukarabati huo utaendana sambamba na uwekaji upya wa mabenchi ya ufundi uwanjani ambayo hutumiwa na timu shiriki wakati wa michezo mbalimbali ikiwa inaendelea.

Release No. 210 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Desemba 18, 2013

December 18, 2013
Imewekwa saa 12:30 mchana Desemba 18.
KIINGILIO MECHI YA MTANI JEMBE 5,000/- Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Desemba 21 mwaka huu) ni sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648. 

 Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 40,000. Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja katika vituo mbalimbali, mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

 Vituo ambavyo tiketi hizo zitauzwa keshokutwa (Ijumaa) ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani. 

Mechi hiyo itachezeshwa na Ramadhan Ibada (Kibo) kutoka Zanzibar, ambapo atasaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba, na Simon Charles kutoka Dodoma. Mwamuzi wa akiba ni Israel Nkongo wa Dar es Salaam wakati mtathimini wa waamuzi ni Soud Abdi wa Arusha. 

TANZANITE YAWASILI JOHANNESBURG KUIVAA BATSESANA Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi tisa cha timu ya Tanzania ya wasichana chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili leo jijini Johannesburg tayari kwa mechi dhidi ya wenyeji Afrika Kusini (Batsesana). 

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Canada. 

Tanzanite imefikia Millpark Garden Court Hotel tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini. 

Wachezaji wa Tanzanite walioko katika kikosi hicho ni Amina Bilali, Amina Hemed, Amisa Hussein, Anastaz Katunzi, Anna Mwaisula, Belina Nyamwihula, Donisia Minja, Fatuma Maonyo, Happiness Mwaipaja, Latifa Salum, Maimuna Kaimu, Najiat Idrisa, Neema Kiniga, Rehema Rhamia, Sada Hussein, Shelda Mafuru, Stumai Athuman, Tatu Salum, Theresa Kashilim na Vumilia Maarifa. 

Boniface Wambura Mgoyo Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)