Mama Salma Kikwete ajiunga na waombolezaji kwenye msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja Banza Stone aliyezikwa leo jijini Dar es salaam

July 18, 2015

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilakiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrer Mngereza alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015. Marehemu Banza Stone, aliyefariki jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu,  amezikwa jioni hii katika makaburi ya Sinza. Marehemu Banza Stone atakumbukwa kwa umahiri wake wa utunzi na uimbaji alipokuwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta, Tot na Extra Bongo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika  alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa Katibu wa bendi ya TOT, Gasper Tumaini, ambako marehemu Banza Stone aliwahi kufanya kazi enzi za uhai wake
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole kaka wa marehemu alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa wana familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji mama mzazi wa marehemu  katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na kiongozi wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta Asha Baraka  katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu   katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na  Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu   katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu  Ramadhani Masanja "Banza Stone" likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Waombolezaji wakilia kwa uchungu wakati mwili wa Banza Stone ukipelekwa mazikoni
 Mama Salma Kikwete, Asha Barka na mama wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni wakati  mwili wa merehemu Banza Stone ukipelekwa mazikoni
 Mama Salma Kikwete akiagana na kiongozi na mwimbaji wa African Stars wana Twanga Pepeta ambaye alifanya kazi kwa karibu na Banza Stone tokea kuanza kwa bendi hiyo
Mama Salma Kikwete akiaga waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015. 
PICHA NA IKULU

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAJITOKEZA KUMLAKI KWA SHANGWE DKT MAGUFULI JIJINI MWANZA LEO.

July 18, 2015
 Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo.
Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili leo jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.
 Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwasili jijini Mwanza jioni ya leo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Magufuli yuko jijini Mwanza kujitambulisha kwa Wananchi.
 Mke wa Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt.John Pombe Magufuli,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake waliojiotokeza kwa wingi kuwapokea,Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.
 Baadhi ya Wananchi wakilikimbiza gari la  Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa shangwe kama waonekanavyo pichani ,wakati Magufuli lipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.
 Baadhi ya Wananchi wa jiji la Mwanza wakiwa wamefunga barabara kwa muda wakishangilia ujio wa  Mgombea Uraisi wa CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.
 kuna wengine waliacha kazi kwa muda kama hizi na kuja kwenda kushangilia ujio wa Mh.Dkt John Magufuli
  Wananchi wa Passians wakimpokea na kumshangila Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.
 Baadhi ya Wanahabari wakiwa kazini.
  Wananchi wa eneo la kona ya Bwiru wakiwa wamezuia  msafara wa Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.
 Wananchi wa eneo la kona ya Bwiru wakiwa wamezuia  msafara wa Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla.
    Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jiji hilo mapema leo mchana,kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu.
    Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh John Monela mara baada ya katika uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza mapema leo mchana.
   Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alisalimiana na wafuasi wa chama hicho wakiwemo viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza,alipowasili katika uwanja wa ndege wa jiji hilo mapema leo mchana.PICHA NI MICHUZI JR-MWANZA