ZANZIBAR KUIMARISHA KANUNI ZA KUKATAZA MATUMIZI YA TUMBAKU KATIKA KULINDA AFYA ZA WANANCHI

September 13, 2017
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt Ghirmay Andemichael akitoa maelezo ya Shirika hilo kwenye warsha ya siku tatu ya kuimarisha kanuni za kupambana na matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akifungua warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Dkt. William Maina kutoka WHOAFRO akitoa maelezo ya Azimio la WHO na sheria za kimataifa dhidi ya mapambano ya matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku katika warsha ya kuimarisha kanuni za mapambano hayo katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya kumiarisha mikakati ya kanuni za kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya GoldenTulip Malindi Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya kuimarisha mikakati ya kupiga vita matumizi ya tumbaku inayofanyika Hoteli ya Goden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

PIKIPIKI 356 ZAMATAWA TANGA KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI YA USALAMA BARABARANI

September 13, 2017

ZAIDI ya Pikipiki  350 alimaarufu bodaboda zimekamatwa na Jeshi laPolisi Mkoani Tanga kutokana na makosa  mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo madereva wake kutokuvaa kofia ngumu pindi watumiaji vyombo hivyo.



Pikipiki hizo zilikamatwa wakati wa operesheni ya Jeshi hiloinayoendelea katika maeneo mbalimbali Jijini Tanga  ikiwa ni mkakati wa kupambana uvunjifu wa sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali
ambavyo vimekuwa zikigharimu maisha ya wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Benedict Wakulyamba (Pichani Juu} aliwaambia waandishi wa habari kuwa zoezi la ukamati wa pikipiki hizo limetokana na ukaidi wa madereva na abiria wa kutokutii sheria za barabarani ikiwa pamoja kutokuwa na leseni .

Alisema katika ukamataji huo pikipiki 206 ambazo zilikamatwa na madereva wake wakikabiliwa na makosa ya kutokuwa na kofia ngumu, madereva 87 hawakuwa na leseni,pikipiki 33 hazikuwa na bima 25 mbovu na 5 kuzidisha abiria(mshikaki).

Aidha alisema kufuatia hali hiyo jeshi hilo baada ya kujiridhisha na hatua za kisheria pikipiki 244 zilitozwa tozo za papo kwa pao,32 dereva na abiria wake walifikishwa mahakamani,32 walionywa kutokana na
utaratibu wa kisheria na 48 bado zipo kituo cha polisi cha mabawa kwa hatua zaidi za kisheria.

“Niseme tu kutii sheria bila shuruti limeonekana kama jambo geni hasa hapa Jijini kwetu na watu walifikiri ni kitu hakiwezekani lakini tumeliamua kweli na tutashughulika nao wanaokaidi sheria za barabarani”Alisema Kamanda Wakulyamba.

Alisema kumekuwepo na malalamiko dhidi ya jeshi hilo kuwa ukamataji wa pikipiki hizo hauzingatii utaratibu wa kisheria kutokana na namna ya ukamataji wake unavyofanyika ikiwa pamoja na askari kuvaa kiraia na
hata kuwavizia katika baadhi ya maeneo.

“Hatuwezi kupangiwa jinsi ya kumkamata mtu tunayemuhisi anamakosa,kinachofanywa na askari wangu ni kumsimamisha mwendesha boadaboda au chombo chochote cha moto lakini kama hataki kutii tunalazimika kumkamata kwa njia yoyote”Alisema Wakulyamba.

Hata hivyo amewatahadharisha wananchi Mkoani hapa kuwa zoezi hilo si nguvu ya soda na litaendelea ikiwa sehemu ya kukomesha virendo vya kutokutii sheria za barabarani na hakutakuwa na simile kwa atakae
kamatwa awe derva au abiria wote wataingia kwenye makosa.
USAILI WA WAIMBAJI NA WAPIGAJI KWENYE IBADA YA KITAIFA YA KUABUDU KUFANYIKA JUMAMOSI HII

USAILI WA WAIMBAJI NA WAPIGAJI KWENYE IBADA YA KITAIFA YA KUABUDU KUFANYIKA JUMAMOSI HII

September 13, 2017
THE WORSHIPPERS TANZANIA ni umoja wa makanisa yote wanaopenda kumwabudu Mungu wameandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya kumwabudu Mungu katika jiji la Dar es salaam kwa Wana Dar es Salaam wote wapendao kuabudu utakaofanyika 1.12.2017 siku ya Ijumaa kuanzia saa 3 usiku Upanga CCC.
  1. Je wewe ni muimbaji ama una kipaji cha kuimba ama wapiga vyombo kanisani?
  2. Uko tayari kumwabudu Mungu?
Ikiwa umejibu ndiyo basi wewe ni kati ya wale 200 tunaowahitaji kujisajili kushiriki mkesha huu. Jisajili kwa kupiga simu ziziopo hapa chini, Usaili utafanyika tarehe 16.9.2017 Jumamosi saa 2 hadi saa 8 mchana. JISAJILI SASA +255657266777 au +255768570703  

POLISI WAKANUSHA ASKARI WAKE KUMFUATILIA MBUNGE LISSU KENYA

September 13, 2017
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA



Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”
Ofisi ya Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 21355
S.L.P. 9141,

DAR ES SALAAM.





12/09/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika siku za karibuni kumejitokeza vitendo vya baadhi ya watu kutumia majina ama picha za watu na kuwahusisha na matukio ya kihalifu au matukio yanayohusiana na uhalifu kwa lengo la kujipatia umaarufu, kuwachafua watu hao au kuwakosanisha na jamii inayowazunguka.

Mnamo tarehe 11.09.2017 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa picha ya askari wa Jeshi la Polisi akihusishwa na muendelezo wa tukio la kujeruhiwa kwa risasi kwa Mhe. Tundu Lissu (MB) ambapo taarifa hiyo ilimtambulisha askari huyo kuwa ni kachero wa Kitengo cha Interpol na kwamba yupo jijini Nairobi nchini Kenya akifuatilia taarifa za Mhe. Lissu.

Jeshi la Polisi linapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni za uongo zenye lengo la kumchafua askari huyo na Jeshi la Polisi kwa ujumla. Askari huyo hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.

Kuhusiana na safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya kimafunzo kuanzia tarehe 04.09.2017 na kurejea tarehe 08.09.2017, huku Mhe. Lissu akipatwa na mkasa wa kujeruhiwa kwa risasi Tarehe 07.09.2017 na kusafirishwa kwenda Nairobi usiku wa kuamkia tarehe 08.09.2017.

Jeshi la Polisi linakemea vikali kitendo hiki chenye lengo la kumharibia maisha yake askari wetu, na linawataka wale wote waliohusika kusambaza au kutajwa katika taarifa hizo kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya mahojiano. Vilevile tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua upande wa serikali.

Suala hili la Mhe. Lissu lipo chini ya uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hili na hatimaye kuwafikisha mahakamani. Ni vema wananchi na wanasiasa wakaliacha Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza kupata ukweli wa jambo hili.

Jamii itambue kuwa Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Nchi na kamwe halifanyi kazi kwa kuvizia. Endapo mtu yeyote anahitaji taarifa, tunayo mifumo yetu rasmi inayotuwezesha kupata taarifa tuzitakazo kupitia uhusiano tulionao ndani na nje ya nchi.

Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha upelelezi wa makosi ya mitandao (Cyber Crime Investigation Unit) linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na kusambaa kwa taarifa hizi za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na kuihabarisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.


Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi.


www.policeforce.go.tz         www.twitter.com/tanpol            www.facebook.com/tanpol    www.usalama2.blogspot.com