WAZIRI MAKYEMBE AWATANGAZIA VITA WAHUJUMU MIUNDO MBINU YA RELI NCHINI.

September 19, 2013
Sussan Uhinga na Oscar Assenga,Tanga.
WAZIRI wa Uchukuzi,Dr.Harrison Mwakyembe amesema wizara yake haitasita kuwachukulia hatua  wahujumu wa miundo mbinu ya reli ikiwemo kuhakikisha wana kamatwa na  kuwachukulia hatua kali zidi yao ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza katika kikao kilichokuwa kikuhusu mpango wa serikali kwenye sekta ya uchukuzi ambacho kiliwajumuisha wadau kutoka kila wilaya ,wizarani pamoja na wazawa waliopo nje ya mkoa wa Tanga.

Alisema wananchi wa Tanga waelewe kuwa miundo mbinu ya reli ni muhimu sana katika kufanikisha maendeleo yao hivyo watakikishe wanaitunza kwa sababu ni gharama kubwa kuitengeneza na kuiomba mikoa iwasaidia katika suala hilo ili iweze kuwa salama.

   "Reli yetu imeonekana kuny'ofolewa kuanzia eneo la Mombo,Mkomazi kuelekea Taveta hakuna kitu sasa nasema mtu atakaye igusa reli akimkamata atamnyoa nywele kwa chupa....hakuna sababu kwani uhujumu wake unaipa hasara kubwa serikali hasa katika harakati zake za kuwaletea maendeleo wananchi "alisema Mwakyembe akisisitiza hatakuwa na msamaha kwa watu wa aina hiyo.

Akizungumzia huduma za usafiri wa ndege mkoani hapa,Dr.Mwakyembe alisema mkoa wa Tanga umeonyesha mabadiliko makubwa sana katika kipindi cha kuanzia mwaka 2007 hadi 2013 kwa watumiaji wa huduma za ndege kutoka watu 7700 mpaka 20200 wanaotumia huduma hiyo.

Alisema serikali mpango wa kuwekeza kwenye kiwanja hicho kwa kukiimarisha ikiwemo kukiongea urefu ili ndege kubwa zenye uwezo wa  kubeba abiria 70 ziweze kutua mkoani hapa na kuwataka wawekezaji wenye nia  kuwekeza kwenye kiwanja hicho wajitokeze.

Aidha aliwaomba wawekezaji waelewe nguvu kubwa ya usafiri wa anga  kuja Tanga kwa sababu wanapoendeleza miundo mbinu ya ndege wakati huo huo kuna ukarabati na zote zinafanyika na hivyo  kutatoa nafasi ya kuzikaribisha sekta nyengine binafsi.

Kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini,Yusuph Nassir alimuomba waziri mwakyembe kuangalia uwezekano wa uimarishaji wa kiwanja hicho uendane sambamba na uwanja wa ndege wa Tanga uwe wa kushusha mizigo ili watu wakinunua mizigo kutoka nchi za dubai na sehemu nyengine ili kutumia uwanja huo hasa wafanyabishara wa kanda ya kaskazini na mikoa ya jirani.

Akitolea ufafanuzi suala hilo,Waziri Mwakyembe alisema suala hilo ni zuri na kuiagiza mamlaka ya uwanja wa ndege hapa nchini (TAA)kulifanyia kazi hilo ikiwemo kuangalia upana wa eneo husika baadae amuwasilishie katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Octoba mosi.

MWENYEKITI UVCCM TANGA AWAFUNDA VIJANA PANGANI.

September 19, 2013
Na Oscar Assenga,Pangani.
VIJANA wametakiwa kupenda michezo na kuithamini ili iweze kuwa mkombozi wao kwenye maisha yao ikiwemo kuacha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufikria kutumia madawa ya kulevya.

Kauli hiyo alitolewa juzi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga(UVCCM),Abdi Makange wakati akifungua ligi ya wilaya hiyo ambayo inashirikisha timu kumi na mbili kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo.

Makange alisema michezo ni ajira ya pakee ambayo wakijipanga na kucheza kwa kujituma mafanikio yake ni makubwa sana kuliko wanavofikiria hivyo wahakikishe wanatumia vema mashindano hayo katika kukuza na kuendeleza vipaji vyao.

Aidha aliwataka vijana hao kucheza soka kwa umakini mkubwa ikiwemo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika kila mchezo ili baadae waweze kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa hapa nchini na nje ya nchini.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi huo,Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Pangani(PDFA)Mussa Lyimo alisema ligi hiyo inashirikisha timu kumi na mbili kati ya hizo timu tatu zinamilikiwa na makampuni na nyengine zinajiendesha zenyewe.

Alizitaja timu hiyo kuwa ni Magic Power,Mapo Fc,Madanga Rangers,TMK Fc,Mwera City,Barcelona,Mshongo Fc,Beach Boy na Nondo Fc na kuwataka wadau wa soka wilayani humo kuvisapoti vilabu ambavyo havina wafadhili ili viweze kujiendesha.

Lyimo alisema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha bingwa wa mkoa wa Tanga anapatikana kutoka wilayani humo kutokana na uwepo wa timu zenye uwezo wa kushindana kikamilifu ikiwemo kuleta upinzani.

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE KUSHOTO MWENYE KOFIA YA KIJANI AKIONGOZWA NA KATIBU WA CHAMA CHA SOKA WILAYA YA PANGANI,MUSSA LYIMO WAKATI WA UFUNGUZI WA MASHINDAO YA LIGI YA WILAYA HIYO.

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,(UVCCM) ABDI MAKANGE AKISALIANA NA MWAMUZI WA WILAYA YA PANGANI KABLA YA KUANZA LIGI YA WILAYA HIYO HIVI KARIBUNI.

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE ALIYEVAA TISHETI NYEKUNDU NA MISTARI MEUPE AKIWALIMIANA NA WACHEZAJI WA TIMU ZILIZOFUNGUA PAZIA LA MASHINDANO YA LIGI YA WILAYA YA PANGANI

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE WA KWANZA KUSHOTO WALIOSIMAMA AKIWA NA MOJA KATI YA TIMU ZA WILAYA YA PANGANI.

MIL 58/- ZAPATIKANA MECHI YA SIMBA, MGAMBO

September 19, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 58,365,000.

Watazamaji 10,241 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 23 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 13,839,327.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,903,135.59.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,036,946.16, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 4,222,167.70, Kamati ya Ligi sh. 4,222,167.70, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,641,954.10.

MIKATABA YA MAKOCHA VPL, FDL YATAKIWA TFF

September 19, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka huu.

Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.

MGOGORO WA WAKULIMA WA CHAI WAINGIA SURA MPYA, WAZIRI CHIZZA APENDEKEZA KUUNDWA MENEJIMENTI YA MUDA KIWANDANI

September 19, 2013

Na  Raisa  Said, Bumbuli

WAZIRI  wa  Chakula, Kilimo  na  Ushirika, Injinia Christopher  Chizza amependekeza kuundwa kwa menejimenti ya muda katika kiwanda cha chai cha Mponde kama njia ya kusuluhisha mgogoro uliopo katia ya wakuilima wa chai na mwekezaji wa kiwanda hicho, Kampuni ya Chai Lushoto. 
Akizungumza katika mkutano wa  hadhara  uliofanyika  katika  uwanja  wa  mazoezi katika kata ya Mponde, Chiza  ambaye aliahidi kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wakulima wa chai na mwekezaji wa kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Bumbuli, Tanga, ili kiendelee kutoa huduma bora.

 
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atashauriana  na  Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda kuhusu sala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo..

"Nitaishauri  serikali  kuchukua  kiwanda  hicho  na  baadaye   kuwakabidhi  wananchi  ambao  ndio  wamiliki  wa  kiwanda  hicho," alisema..
Mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji unatokana na madai ya wakulima hao kuelezea kuwepo kwa upotevu wa fedha kiwandani na viongozi wa Chama cha Utega kupoteza imani kwa wakulima kwa madai kuwa wako upande wa mwekezaji ambaye walidai anaendelea kuwanyonya wakulima wa chai.
Waziri huyo pia alisema  watapeleka  wakaguzi  kutoka  serikalini  kuchunguza  kama  kun a ubadhirifu  wowote  kiwandani  hapo  ili  kuwasaidia  wakulima  wa chai  kupata   haki  yao na kulisaidia  zao  hilo ambalo  ndio  kitega  uchumi   cha  wakazi  wa Bumbuli lisife  .

Waziri  Chiza  alisema  kuwa   ana imani  uchunguzi  utakaofanywa  na  wakaguzi kutoka  serikalini utaleta  majibu  mazuri  kwa kuwa  utaonyesha   kama  kuna ubadhirifu  na  upotevu  wa  rasilimali  zingine ndani  na  nje ya  kiwanda hicho .

Alisema  wao  kama  Serikali  hawawezi  kuendelea  kuona  zao  la  chai  linaoza  hivyo  lazima  lithaminishwe  kwa  kuuzwa  katika  viwanda  vingine  kwa kuwa  bado  mgogoro  huo  unaendelea   na  serikali  inaendelea  kutafuta  ufumbuzi  wa kumaliza  mgogoro huo.

“Tutamaliza  mgogoro  huu  kwa  kupata  suluhisho  la  haraka  ili  wakulima  wapate  haki yao  ya  msingi  na  badae  waendelee  kulilinda  zao  la chai  kama  ilivyokuwa  zamani” alisema   Waziri huyo.

Waziiri huyo alisema kuwa Chama cha UTEGA lazima kifanye mkutano mkuu ili kuadili matatizo yanayokikabili na akaahidi kuwa serikali iko tayari kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mkutano huo.

Aidha alisema kuwa Wizara yake na Wizara ya Viwanda na Biashara wa kushiriiana na Wizara ya Mambo ya Ndani watafanya ukaguzi wa Chama hicho ili kujua kama kinaendeshwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za Tanzania.

Wakulima  hao wakizungumza  katika  mkutano huo  wa  kujadili kero mbalimbali ambazo zinawakabili, walisema kuwa wako tayari kukosa fedha kwa kipindi chote  ambacho kiwanda kitakuwa kimefungwa kuliko kuendelea kunyanyaswa na wawekezaji hao.
KONDE STAR NA MAENDELEO MANTA KUPAMBANA IJUMAA LIGI DARAJA LA KWANZA  PEMBA.

KONDE STAR NA MAENDELEO MANTA KUPAMBANA IJUMAA LIGI DARAJA LA KWANZA PEMBA.

September 19, 2013
Na MASANJA MABULA -PEMBA.
Timu mbili zenye upinzani mkubwa kutoka Jimbo la Konde  na ambazo zinashiriki ligi daraja la kwanza Taifa Pemba , Konde Star na Maendeleo Manta zitapambana  katika uwanja wa Kinyasini Ijumaa ya 20 kutafuta nafasi ya kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu ujao .

Timu hizo ambazo zote inaaminika kwamba zinadhaminiwa na Wabunge , Yussuf Salim Hussein Kibiriti  wa Jimbo la Chambani ( Maendeleo Manta ) na Khatib Said Oboma wa Jimbo la Konde (  Konde Star) zinatarajia kutoa burdani na kuufanya mchezo huo kuwa na ushindani wa hali ya juu .

Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Mpira katika Jimbo la Konde na Wilaya ya Micheweni wameanza kutabiri na kusema kuwa itakuwa ni vita kati ya Obama na Kibiriti ambao kwa pamoja wameonesha nia ya kutaka kuinua kiwango cha soka Jimboni humo .

Tayari katika michezo yake ya awali , viongozi hao waliziongoza timu zao kufanya mauwaji , kwa timu ya Maendeleo Manta kuifunga timu ya Opec  ya Pandani bao 1-0 ambapo mbunge huyo aliahidi kutoa kitita cha shilingi milioni moja baada ya timu hiyo kuifunga Opec .

Naye Obama alihudhuria kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ngerengere jeshini , na kushuhudia timu ya Konde Star ikitoa kipigo cha paka mwizi kwa timu ya Coast Ilanders ya  kutoka Wilaya ya Mkoani cha mabao 4-0.

Kwa matokeo hayo , kila upande umetamba kuondoka na ushindi katika mchezo huo ambao pia umeteka nyoyo z awapenda soka Kisiwani Pemba .

Katika msimu uliopita timu zilikutana mara mbili ambapo katika mchezo wa awali Maendeleo Manta walishinda kwa jumla ya mabao 3-2 ambapo katika mchezo wa marudiano Konde Star iliishinda kwa jumla ya mabao 3-1 michezo yote ilichezwa katika uwanja wa Gombani .