RAIS KIKWETE AKAGUA VIFAA NA ENEO MAALUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

RAIS KIKWETE AKAGUA VIFAA NA ENEO MAALUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

September 09, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.PICHA NA IKULU eb3Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madaktari na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jueb4: lius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. eb6 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. eb7
Baadhi ya wahudumu waliovalia mavazi maalumu wa  wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. eb8 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Seif  Rashid jinsi Tanzania ilivyojipanga kupambana na ugonjwa hatari wa ebola baada ya kukagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. eb9 eb10 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. eb11 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.eb2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo ya namna ya kuhudumia abiria wakati wa ukaguzi wa wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma. eb4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa  abiria  atayekutwa na ugonjwa wa ebola  mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
eb5 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke  jijini Dar es salaam leo Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.

COASTAL UNION MAMBO RAHA TU, CHEKI WALIVYOILAZA NJAA POLISI MORO MKWAKWANI

September 09, 2014


 Wanandinga wa Coastal Union (Jezi nyekundu) wakisalimiana na wachezaji wa timu mpya ya ligi kuu soka Tanzania bara, Polisi Morogoro katika mechi ya kirafiki iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika tamasha la 'Coastal Union Day'  septemba 7 mwaka huu uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ambao Wagosi wa Kaya walishinda 2-0. 
 Wachezaji wa Coastal Union wakiongozwa na mlinda mlango maarufu, Shaban Hassan Kado (Jezi namba 30)  kuomba dua kabla ya mechi
 Kikosi cha kazi cha Coastal Union
 Mashabiki wa soka Jijini Tanga walifurika kwa wingi kuitazama timu yao iliyoweka kambi ya mwezi mmoja kisiwani Pemba kujiwinda na michuano mipya ya ligi kuu soka Tanzania bara na itaanza kampeni zake kwa kuchuana na Simba uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, septemba 21
Hapa vijana wa Coastal Union chini ya kocha Mkenya, Yusuf Chipo walikuwa wanapasha moto misuli kabla ya kuanza mechi

*MKUTANO WA MAAFISA MIPANGO KUFANYIKA OKTOBA MWAKA HUU

September 09, 2014

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma.
***********************************************
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ipo katika maandalizi ya mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unatarajiwa kufanyika Oktoba 2014 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na usimamizi wa uchumi na mipango hapa nchini.
Mkutano huu ambao ni wa kitaalamu unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango ambao hukutana kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.
Mkutano huu unatoa fursa kubwa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Pia hutoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. Mkutano huo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, mkutano wa mwaka huu utajikita katika kujadili masuala yafuatayo;
i) Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi, maafisa mipango na watakwimu);
Mkutano utajadili fursa, na changamoto zilizopo katika kuleta maendeleo katika nchi.  Huko nyuma kada hizi zilikuwa zinaratibiwa na iliyokuwa Wizara ya Mipango Uchumi na Uwezeshaji. Kwa sasa watakuwa chini ya uratibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Hatua hii itarahisisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya nchi.
ii) Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021);
Utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16) unaendelea na tayari Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango imeanza kufanya mapitio ya utekelezaji wake ili kujua mafanikio na changamoto. Hivyo, katika mkutano huo wapanga mipango wanaandaliwa waweze kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Mpango wa Pili wa Maendeleo (2015/16 – 2020/21).
iii) Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma;
Serikali imeandaa mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika sekta ya Umma, lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo.
iv) Jinsi ya Kujiandaa na Uchumi wa Gesi
Mkutano utajadili ni kwa jinsi gani Tanzania inajipanga kufaidika na rasilimali ya gesi asilia. Kwa kifupi masuala ya yanayohusu uwekezaji katika gesi asilia, usimamizi na jinsi ya kutumia rasilimali na menejimenti ya mapato yatokanayo na gesi, pamoja na ushiriki wa wananchi katika fursa mbalimbali zinazotokana na ujio wa gesi hiyo. Utayarishaji wa wataalam katika eneo hilo la gesi husani vyuo vya ufundi, vyuo vikuu na kadhalika.
Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Mkutano wa mwisho wa mwaka wa maafisa mipango ulifanyika mkoani Morogoro tarehe 12 Machi 2010 ambapo uliandaliwa na Wizara ya Fedha.  Mada nne zilizowasilishwa na kujadiliwa zilikuwa ni;
        i.            Wajibu wa wataalamu wa mipango katika Maendeleo ya Uchumi: Mipango ya Kiuchumi, Utekelezaji na Uandaaji wa Taarifa;
      ii.            Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki;
    iii.            Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Wafanyabiashara Wadogo na Wakati; na 
    iv.            Ufanisi wa Uwekezaji kutoka nje katika Uchumi wa Tanzania

Imetolewa na:

Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

KITU CHA MOTO: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UAMUZI WA KIHISTORIA WA KAMATI YA SHERIA NA HADHI YA WACHEZAJI YA TFF KATIKA SHAURI LA YANGA NA EMMANUEL OKWI

September 09, 2014


Mshambulaiji wa Simba, Emmanuel Okwi (kulia) katika mechi dhidi ya Gor Mahia

UTANGULIZI
Kwa niaba ya mteja wetu, Emmanuel Arnold Okwi, napenda kutoa maelezo kuhusu Uamuzi wa kihistoria katika soka la Tanzania ambao umefanywa na Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF. Uamuzi huo ni wa kihistoria kwa misingi ifuatayo:
MOSI: Ni mara ya Kwanza katika historia ya soka la Tanzania ambapo Kamati inakaa kujadili haki ya mchezaji dhidi ya klabu kubwa na hatimaye kuamua kwa manufaa ya mchezaji, tena pasipo kupiga kura kwa misingi ya upenzi na unazi. Kamati ya Mwanasheria Mashuhuri na mwenye Msimamo Bw. Richard Sinamtwa iliamua kustafsiri kanuni kwa kufuata ushahidi uliopo na kwa haki kabisa pasipo kujiingiza katika mtego wa kupiga kura kama ambavyo tumekua tukiiona huko nyuma.
PILI: Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti ilitumia busara ya hali ya juu kwa kukataa ombi la Yanga la kutengua uteuzi wa Bw. Hans Pope katika Kamati hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga ilileta hoja ya kumkataa Bw. Hans Pope kwa misingi ya mgongano wa kimaslahi na kumtaka mwenyekiti atoe uamuzi juu ya suala hilo. Endapo mwenyekiti angetoa maamuzi ya kumuondoa Hans Pope, basi angejiingiza katika uvunjaji wa Katiba ya TFF kwasababu yeye sio mamlaka ya uteuzi wa Hans Pope katika Kamati hiyo. Mwenye mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo Yanga walipaswa kuelewa hilo na si kuishinikiza kamati, hususan Mwenyekiti, amuondoe Hans Pope kwenye Kikao.
TATU: Maamuzi ya Kamati yamefungua njia kwa wachezaji wengi ambao mikataba yao inachezewa na vilabu kwa muda mrefu pasipo kuwa na nafuu yoyote ya kisheria kwa wachezaji hao ambao ndio nguzo ya muhimu katika mpira wa Tanzania. Hata hivi sasa kuna wachezaji ambao bado hawajalipwa stahili za mikataba yao ndani ya Yanga. Tunawaomba wajitokeze ili tuwasaidie wapate haki zao za kisheria kama ambavyo imetokea kwa Okwi.
NNE: Pamoja na madai ya Yanga ya kukata rufaa FIFA / CAS, naomba wajue kuwa haki yao ya kukata rufaa inatokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF imetekeleza wajibu wake. Uamuzi huo wa Kamati umejenga msingi muhimu sana katika suala zima la kuheshimu na kutekeleza mikakaba kwa mujibu wa kanuni za FIFA. Endapo Yanga watakata rufaa kama wanavyodai, itakuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha nguzo ya kuheshimu mikataba ya wachezaji inapewa msisitizo unaostahili.
MGOGORO KATI YA YANGA NA OKWI
Mkataba wa Yanga na Okwi, ambao ulisainiwa tarehe 12 Disemba 2014 umekuwa na mapungufu yafuatayo:
1.                  Mkataba huo umempa majukumu mchezaji kufuatilia ITC na suala zima la yeye kupata vibali vya kucheza. Hii ni kinyume na Kanuni za FIFA ambao zinatamka bayana kuwa jukumu la kufuatilia ITC ni la wanachama wa FA, lakini Yanga walimtwisha Okwi zigo hilo. Okwi alitekeleza jukumu hilo.
Kamati ililiona hilo na kusema wazi kuwa hilo sio sahihi. Ni vema wachezaji wajue kuwa hilo sio jukumu lao.
2.                  Pili Yanga, kwa mujibu wa mkataba, walikuwa na haki ya kumkata mchezaji theluthi moja ya mshahara wake wa mwezi endapo atakosa mechi tatu au zaidi. Yanga walimkata Okwi Mishahara ya miezi mitano, kinyume na matakwa ya mkataba na pasipo maelelzo yoyote.
3.                  Yanga na Okwi walikubaliana kuwa mchezaji atalipwa ada ya kusaini mkataba (signing on – fee) ya US$ 100,000, kwa Awamu mbili. Awamu ya kwanza wakati wa kusaini mkataba na awamu ya pili tarehe 27 Januari 2014. Mpaka hivi sasa, Yanga wamelipa US$ 50,000 tu na bado kuna deni la US$ 50,000. Huu ni uvunjaji wa mkataba wa wazi kabisa.
4.                  Kipindi chote mchezaji akiwa na klabu ya Yanga, hajapewa nyumba kama ambayo walikubaliana. Huu ni ukiukwaji mwingine wa mkataba.
Baada ya Okwi kuanza kudai haki zake tajwa hapo juu, Yanga waliamua kutomlipa mteja wetu mishahara ya miezi mitano kinyume na matakwa ya mkataba kati yao.
MPANGO WA SIRI WA YANGA
Yanga walikuwa na mpango wa siri wa kuvunja mkataba na Emmanuel Okwi ili wamkomoe mteja wetu, ashindwe kucheza mpira, kiwango chake kiporomoke na itumike kama onyo kwa wachezaji wengine ambao wanadai haki zao. Mpango huu ulitekelezw kama ifuatavyo:
a.       Tarehe 27 Juni 2014, Yanga waliandika barua kwenda TFF, ikiitaka TFF, pamoja mambo mengine, itambue kuwa mkataba kati yao na Okwi umefutwa. Barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
b.      Tarehe 25 Julai 2014, Yanga waliandika barua ya pili kukumbushia barua yao ya tarehe 27 Juni 2014. Barua hiyo ya pili haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
c.       Tarehe 20 Agosti 2014 Yanga waliandika barua nyingine tena wakikumbushia hoja zao tajwa hapo juu. Kwa mara ya tatu, barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
d.      Yanga waliandika barua nyingine ya nne tarehe 25 Agosti 2014 ikiwa na hoja zile zile za kusitisha mkataba na mteja wetu. Kwa mara ya nne barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
Baada ya TFF kupanga tarehe ya kikao cha Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji na kutoa barua ya wito tarehe 27 Agosti 2014 ndipo kwa mara ya kwanza mchezaji Emmanuel Okwi akafahamu kuwa Yanga wameomba kuvunja mkataba wake.
Tarehe 27 Agosti 2014, Emmanuel Okwi aliiandikia Yanga KUKUBALI ombi lao la kuvunja mkataba.

Mambo muhimu ya kujiuliza ni:
Mosi, Kama Mkataba ulikuwa ni kati ya Yanga na Okwi, ni kitu gani kiliifanya Yanga ishindwe kumpa angalau nakala ya barua nne ambazo ilizipeleka TFF?
Pili, Wakati Yanga wanaomba kuvunja mkataba, walikuwa wameshamlipa Okwi stahili zake kwa mujibu wa Mkataba huo?
Tatu, Je visingizio vya kuvunjwa kwa mkataba wa Okwi vina uhusiano na idadi ya majina ya wachezaji wa kigeni wa Yanga?
Ni bayana kuwa Yanga walitafuta kila aina ya kisingizio ili mteja wetu aonekane kuwa ndio amevunja mkataba wakati ni wazi kuwa Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja mkataba huo tarehe 27 Januari 2014 kwa kushindwa kumlipa mteja wetu US$ 50,000 za ada ya kusaini mkataba.
HOJA MBELE YA KAMATI
Mbele ya Kamati Yanga walileta hoja kuwa: Hans Pope ana mgongano wa maslahi kwa kuwa amemsajili Okwi Simba na yeye ni mjumbe wa Kamati hii; Okwi amekataa kuongeza au kupunguza mkataba kama ilivyopendekezwa na Yanga; Okwi ameleta madai yasiyo na msingi ya kutaka apewe nyumba ya kuishi; hajacheza mechi 6 hivyo kuikosesha Yanga ubingwa. Okwi amefanya makubaliano na Klabu ya Wadi Geldi ya Misri wakati ana mkataba na Yanga. Hivyo basi Yanga waliitaka Kamati itamke kuwa mkataba kati yao na Okwi umesitishwa, imfungie Okwi kucheza mpira Tanzania Maisha na ailipe Yanga dola za kimarekani laki mbili.
Tukimwakilisha Okwi, tulitoa hoja kuwa: Mteja wetu amekubali ombi la Yanga la kuvunja mkataba ambalo limo katika barua zake nne; Yanga ndio wamevunja mkataba kwa kushindwa kulipa signing fee US$ 50,000; Mishahara ya miezi mitano US$ 15,000 na kodi ya nyumba US$ 2,800. Madai hayo ni kwa mujibu wa mkataba.
Baada ya Maswali toka kwa Kamati kwa pande zote mbili, Yanga waliomba kufuta barua zao, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na kamati.
Kamati, hatimaye ilifanya maamuzi ya kihistoria katika kulinda haki za kimkataba za wachezaji kama ambayo imeelezwa hapo juu.Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, anapaswa kuipongeza kwa dhati kamati kwa maamuzi ambayo wanajenga mpira wa nchi hii. Vilabu vinapaswa kufahamu kuwa haki za mchezaji lazima ziheshimiwe.
Hoja za Yanga kuwa hakukuwa na madai ya fedha sio sahihi kwasababu Majibu toka kwa Okwi na mabishano ya maneno mbele ya kamati hiyo ilijadili kwa kina madai ya fedha ya Okwi na hata Yanga walikiri kutolipa madai hayo. Hivyo basi si sahihi kusema kuwa eti suala la madai ya fedha halikujadiliwa. (ona kiambatisho MNA1)
Msingi wa malalamiko ya Yanga ni barua ya tarehe 27 Juni 2014, ambayo hakuna sehemu ambayo inatamka suala la Simba. Kama kuna kesi dhidi ya Simba, wasubiri wakati wa kupitia pingamizi za usajili lakini suala ambalo Yanga walilalamikia ni kusitisha mkataba na Okwi na madai ya fidia.
Kamati ya Sheria na Mwenyekiti wake hawana mamlaka ya kujadili uteuzi au uwepo wa Hans Pope kwenye kikao hicho. Mamlaka ya Uteuzi ndio, kwa mujibu wa katiba ya TFF, yenye uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo.
Kwakuwa rufaa ni haki ya kila mtu, Uamuzi wa kukata rufaa Fifa / CAS ni haki ya kisheria lakini tuwakumbushe Yanga kuwa “UKITAKA HAKI, TENDA HAKI KWANZA”.

DK. DAMAS DANIEL NDUMBARO (PhD)
Maleta & Ndumbaro Advocates

Muwakili wa Mchezaji

KIINGILIO MECHI YA YANGA v AZAM FC NGAO YA JAMII BUKU 5 TU

September 09, 2014


Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.

Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.

IVO MAPUNDA ATAMBA KUTWAA 'NDOO' YA LIGI KUU CHINI YA PATRICK PHIRI

September 09, 2014


 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MLINDA mlango namba moja wa Simba sc, Ivo Philip Mapunda amepania kufanya makubwa katika msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi Septemba 20 mwaka huu.
Simba chini ya kocha mkuu, Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ itaanza kampeni ya kusaka ubingwa dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union, Septemba 21 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na MPENJA BLOG mchana huu, Ivo amesema kocha Patrick Phiri ameleta mabadiliko makubwa katika kikosi cha Simba na wanatarajia kushirikiana naye ili kufikia malengo yao.
Ivo aliongeza kuwa wakati wa utawala wa Mcroatia, Zdravko Logarusic, wachezaji walikuwa na mipaka ya kucheza mpira na hawakutumia vipaji vyao kwa uhuru, lakini kwa kocha Phiri mambo ni tofauti kwasababu wachezaji wanafanya kile wanachoweza na kuonesha vipaji kwa uhuru.
Kipa huyo mkongwe aliyewahi kucheza Yanga na Gor Mahia ya Kenya alisema kwamba mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo ambao unatakiwa kucheza vile ambavyo unajua, halafu baadaye  unaongeza vitu vingine kutoka kwa mwalimu.
“Tunachotarajia ni kufanya vizuri kwasababu mwalimu aliyekuja nadhani kwa namna moja ama nyingine ameleta mabadiliko. Simba ambayo iliyokuwepo msimu uliopita na ya sahizi ni tofauti, ukiangalia mechi tulizofanya majaribo tumefanya vizuri”. Alisema Ivo.
“Timu inafanya vizuri kutokana na kwamba mwalimu anajaribu kuwapa wachezaji uhuru wa kufanya kile kinachowezekana uwanjani. Unajua Uwanjani unapompa uhuru mchezaji, nadhani anacheza vizuri bila wasiwasi,”.
Mlinda mlango Ivo Mapunda enzi za utawala wa kocha Zdravko Logarusic

 ”Alipokuwepo Mwalimu Logarusic nadhani kulikuwa na mipaka fulani ambayo lazima mchezaji ufuate na usipofuata anakuwa mkali na wachezaji walikuwa wanapoteza kujiamini”.
“Kwahiyo nategemea kwamba tutafanya vizuri na lengo letu ni kuleta mabadiliko ambayo lazima tushike nafasi ya kwanza katika msimu wa ligi ambao utaanza hivi karibuni,”.
Kuhusu kusajiliwa kwa kipa bora wa msimu uliopita, Hussein Shariff ‘Casillas’ kutoka Mtibwa Sugar, Ivo alisema ni changamoto nzuri kwake kwasababu anaamini kuna vitu vipya atavichukua kwa kipa huyo kijana hali kdhalika naye atajifunza kutoka kwake kutokana na uzoefu alionao.
 “Changamoto katika nafasi ya golini zipo. Unajua changamoto zinakuja pale unapofanya vibaya na hiyo nafasi mwingine anaitolea macho. Kinachofanyika zaidi ni mazoezi ya ziada na utulivu unapokuwa kwenye mchezo ili kupunguza makosa ambayo mwingine hawezi kuyafanya”.
“Kitu kikubwa kinachoweza kunifanya pengine nionekane kama nacheza  vizuri ni jinsi ya kuongea na wachezaji kadri mchezo unavyoendelea,”
“Kutokana na uzoefu wangu najua nini cha kufanya pindi mchezo unapoendelea. Nakuwa nausoma mchezo na kujua nifanye nini ili tuweze kukwepa madhara ambayo yakitokea watu wataangalia golikipa alikuwa ni nani.”
“Uwepo wa golikipa mwingine Casillas nadhani itanisaidia mimi. Unapokuwa na mtu mwingine tofauti toka timu nyingine, unajifunza kitu kingine. Kama kipa huwezi kujua kila kitu, kwahiyo unaweza kujifunza kutoka kwa kipa anayechipukia hata kama ni kipa mzoefu”.
“Hivyo Casillas ananisaidia mimi tunapokuwa mazoezini au atakapokuwa anacheza mechi nitajifunza kwake na yeye anajifunza vitu kutoka kwangu”.
Simba chini ya uongozi mpya unaoongozwa na Rais Evans Elieza Aveva wamepania kufuta machungu ya kufanya vibaya kwa miaka mitatu mfululizo.
Ili kuhakikishwa wanafanya vizuri, kamati ya usajili chini ya ‘Big Boss’. Keptein wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe, imefanya usajili makini.

Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Simba ni Emmanuel Okwi, Pierre Kwizera, Pual Kiongera, Shaaban Kisiga, Abdi Banda, Joram Mgeveke na wengineo