WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AHIMIZA MAHAKAMA KUTENDA HAKI

January 31, 2018
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ameitaka Mahakama kutenda Haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi yanayoweza kukwamisha Haki kutendeka.

Pia ameitaka kutoa fidia ipasayo, kukuza usuluhishi ipasavyo, kukuza usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro  na watoe haki bila kujali sababu za hali ya mtu kijamii ama kiuchumi

Waziri Kabudi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya Mahakama vya Chimala jijini. Kauli mbiu katika siku ya sheria mwaka huu inasema, Matumizi ya Tehama katika utoaji haki kwa wakati na kuzingatia maadili.

Waziri Kabudi pia ameitaka Mahakama ipunguze kuchelewesha kesi bila sababu za msingi na iongeze kasi ya usikilizwaji wa Mashauri kwa 

Ameongeza Wizara inathamini maonesho ya siku ya sheria na maendeleo yanayofanywa na Mahakama katika kuendeleza kuboresha mfumo wa sheria na kwamba Mahakama imekuwa ya kwanza kubadilika katika sekta ya sheria. Hivyo Wizara itahakikisha maboresho ya mahakama yanafanikiwa.

Kabla ya ufungaji wa maonesho hayo, Waziri Kabudi pia amezindua  Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni.

Akizindua jengo hilo la Mahakama lililogarimu zaidi ya Sh.milioni 500  Prof.Kabudi amesema, mkakati wa Mahakama hadi kufikia mwaka jana walikuwa wanahitaji  Mahakama Kuu 19, Mahakama za Hakimu  Mkazi 14, Mahakama za Wilaya 109, Mahakama za Mwanzo 3003 huku wakiwa na uhitaji mkubwa wa ukarabati wa mahakama nyingi nchini. 

Aliipongeza Mahakama kwa ubunifu, umakini na ufanisi waliouonesha kwa kufanya utafiti wa kutumia Moladi na ujenzi bora, imara na wenye gharama nafuu. Prof. Kabudi pia ameipongeza mahakama kwa kujenga majengo hayo katika wilaya mpya, hasa Kigamboni na amewataka kutafuta viwanja zaidi ili jitihada za kuongeza mahakama Kigamboni zifanyike kwa kuwa ipo moja tu.

Pia ameshauri wananchi wa Kigamboni kuhakikisha wanajaribu kutafuta usuluhishi  nje ya Mahakama kwa matatizo yanayowezekana na ikishindikana ndiyo wapeleke mahakamani. 

"Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya Mahakama kila mwaka ili kuboresha huduma...nitoe rai kwa watumishi na watumiaji mtunze miundombinu, serikali imetumia fedha gharama nyingi muilinde na kuitunza,"amesema. 

Amebainisha mfumo wa Mahakama wa Tehama utapunguza gharama kwa kuwa utasaidia kesi kuendeshwa wakati shahidi akiwa eneo lingine na hata mtu kutumia simu ya kiganjani kupata taarifa za mahakama, kufungua kesi ama kulipa.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omary Othmani Makungu amefurahi nakuahidi kutumia elimu aliyoipata ili kujenga jengo kama hilo kwa gharama nafuu kwani wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika ujenzi wa mahakama Zanzibar.

Katika Wiki hii ya Sheria Mahakama amezindua majengo mapya katika mahakama za Bagamoyo, Kawe, Mkuranga, Kigamboni na Kituo cha Mafunzo Kisutu.
Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Pamalagamba Kabudi akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa Mahakama wakati wa uzinduzi mahakama ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, kulia kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Ferdnandi Wambari na kulia kwake ni Jaji Mkuu  Kuu Zanzibar Omary, Othaman Makungu.
 Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akipanda mti katika jengo jipya la mahakam ya mwanzo na Wilaya ya Kigamboni, baada ya kumaliza kuzindua mahakama hiyo mpya.
Waziri wa katiba na Sheria Profesa Pamalagamba Kabudi akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa mahakama nchini Tanzania na Zanzibar

Balozi wa Ujerumani Tanzania ashiriki maadhimisho ya wahanga utawala wa Hitler

January 31, 2018
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter akizungumza na wanafunzi walioshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani. Kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter.

Wanafunzi hao wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Wanafunzi hao wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter pamoja na Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) pamoja na wanafunzi (nyuma) wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

BALOZI wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter ameshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, yalioshirikisha wanafunzi mbalimbali wa Shule za Sekondari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo aliwataka vijana kujitambua, kupenda kujifunza historia na pia kutokubali kutumika kuchochea vurugu katika maeneo yao.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa mfumo wa 'Nazism' uliolenga kuwateketeza Wayahudi kwa kuamini si binadamu bora yalipoteza uhai wa watu takribani milioni sita wakiwemo watoto. Mfumo ambao pia ulitokomeza watu wenye ulemavu na wafupi kwa kuangamizwa kwa kutumia gesi za sumu na pamoja na moto. 

Aidha alisema baadhi ya maeneo vijana wanaweza kujikuta wanatumika katika matukio yanayochangia vurugu hivyo kuna kila sababu ya wao kupewa elimu ya kujua historia kwa undani ili wasiweze kutumika kwa namna yoyote. 

"Upo umuhimu wa vijana kutokubali kushiriki katika masuala ya ukatili, vurugu za aina yoyote ile...alisema vijana wanapaswa kujitambua na kufahamu historia na jukumu lao la kulinda amani kwa faida ya mataifa yao," 

Vijana hao kutoka shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam walipata elimu pia kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter juu ya historia ya mauaji hayo, ambapo walipata fursa za kujadili na kuuliza maswali tofauti kutoka kwa balozi huyo raia wa Ujerumani.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: DK. KIGWANGALLA AELEZA HATMA YA WAVAMIZI KATIKA HIFADHI YA BONDE LA MTO KILOMBERO

January 31, 2018