DKT KALEMANI AWAPA MAAGIZO WAKANDARASI WA REA NCHINI

March 26, 2018

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii ch a Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Y ona Mark na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuluni Selemani Omari

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akiteta jambo mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumban i Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark


Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisalimiana na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji ni awamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na waataalamu mbalimbali wanaotekeleza mradi wa rea awamu ya tatu mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi huo

Ssehemu ya wakandarasi wakifuatilia uzinduzi huo


WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wa wakala wa nishati vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki ili kuweza kutoa fursa ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo muhimu.

Dkt Kalemani aliyasema hayo leo wakati akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III) katika kijiji cha Magumbani kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uwashwaji wa huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili kuwawezesha kupata huduma hiyo ilikuwa haipo awali katika eneo hilo

Alisema kwani hayo ndio malengo waliowapa ikiwa ni mpango mkakati wa kuha kikisha wanafikia malengo ya kuwapelekea umeme watanzania wote ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze kunufaika kupitia huduma hiyo

“Leo tutaangalia mlipowasha lakini niwaagize wakandarasi tunataka kuona kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kwani wananchi wanauhitaji mkubwa wa kufikiwa na huduma hiyo hivyo hakikisheni hilo mnalitilia mkazo mkubwa “Alisema.

Hata hivyo alisema bado kuna changamoto ya wananchi kutapeliwa na mafundi ambao wamekuwa wakiwabambikia bei kuwaambia walipe kidogo kabla ya kulipia 27000 ambazo wanapaswa kulipa jambo ambalo ametaka likomeshwe haraka.

“Mameneja, Wakandarasi tuna changamoto wananchi kutapeliwa kuna tabia imezuka mafundi wanawabambikia bei wanaawaambia walipe kidogo kabla ya kulipa elfu 27000 labda niwaambie tu kwamba mtu wa namna hiyo atakayepatikana watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria”Alisema Waziri huyo.

Alisema mradi huo utakwenda kila kijiji, kitongoji na nyumba kwa nyumba huku akieleza hata kama nyumba unayokaa utaona hakuna sehemu ya kutundukia waya weka hata kwenye mti ili mradi uweze kufikiwa na huduma hiyo.

Aidha alisema kusudio lingine ambalo alilojia ni kuweka msukumo kwa wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana ili kuweza kumaliza mradi huo kwa wakati ili walengwa waweze kunufaika nao.

Waziri huyo pia aliwataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu ya umeme ikiwemo Transfoma kwa kuhakikisha kutokuiba mafuta kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ukuaji wa maendeleo.

“Ndugu zangu tukishirikiana kuilinda miudombinu ya umeme kwani serikali inatumia gharama kubwa kuifikisha kwenye maeneo yenu lakini pia Diwani wa Kata hii anzeni kutenga fedha kwa ajili ya kuunganisha kwenye taasisi za umma kwenye maeneo yenu”Alisema.

MBUNGE ROSE TWEVE KUWAWEZESHA WANAWAKE WA UWT MKOA WA IRINGA

March 26, 2018


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose tweve akiwa na naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele pamoja na katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizerwakiangalia shughuli zinazofanywa na vikundi vya wanawake wa UWT tafasa ya mazombe

KAMPUNI YA IVORI IRINGA IMEMPONGEZA RAIS DR MAGUFULI KWA UFUMBUZI WA TATIZO LA SUKARI YA VIWANDANI

March 26, 2018






Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuinua sekta viwanda hapa nchini.


Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiwa na waandishi wa habari wa mkaoni Iringa wakitembelea maeneo ya kiwanda cha Ivori Iringa

Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari katika jengo jimpya ambalo litafunguliwa kiwanda kipya hivi karibuni
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa pamoja na mdau wa chama cha mapinduzi (CCM) Hamza Ginga.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

KAMPUNI ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa imempongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna alivyolipatia ufumbuzi suala la sukari ya viwandani ikisema litanusuru viwanda vilivyotaka kufungwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

Katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Machi 19, pamoja na mambo mengine yanayohusu sukari, Rais Magufuli alisema hakuna sababu kwa taifa kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza sukari toka nje ya nchi wakati uwezo wa wafanyabishara kuzalisha sukari hiyo nchini upo.

Dk Magufuli alisema mahitaji ya sukari nchini ni tani 590,000 kwa mwaka, ambapo tani 455,000 ni kwa ajili ya matumizi ya majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya viwandani.

Alisema kwasasa kuna upungufu wa tani 125,000 za sukari ya kutumia majumbani na tani 135,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.

Akizungumza na wanahabari wakati akielezea mafanikio na changamoto uzalishaji katika viwanda hivyo, mkurugenzi wa kampuni hizo, Suhail Esmail Thakore alisema wamepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa serikali wa kushughulikia upungufu huo.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuchukua hatua ya haraka sana kushughulikia tatizo la sukari. Taarifa tuliyopata mara baada ya kikao kile ni kwamba taratibu za kupata vibali vya kuagiza sukari ya viwandani kwa kuzingatia mahitaji ya viwanda vyetu zinaendelea. Hiiimetupa uhakika wa kuendelea na uzalishaji,”alisema

Alisema viwanda vyake viliingiwa na hofu ya kusimamisha uzalishaji baada ya serikali kuzuia uagizaji wa sukari hiyo toka Novemba mwaka jana.

“Viwanda vyetu vivyoatumia malighafi zinazozalishwa na wakulima wa ndani ya nchi, zinazalisha bidhaa mbalimbali zinazojulikana kwa jina la Ivori zikiwemo tomato na chill sauce, pipi, chocolate na unga wa cocoa,” alisema.

Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Thakore alisema kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya bidhaa hizo ndani ya nchi, na zinahitajika sana katika nchi jirani za Kenya, Kongo, Rwanda na Burundi hali inayowasukuma kuongeza uwekezaji ili kuunga mkono azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda

Thakore alisema kwasasa viwanda vyao vinazalisha asilimia 30 tu ya mahitaji yao yote ya soko na katika kukabiliana na changamoto hiyo wameanza na ujenzi wa kiwanda kipya cha pipi kitakachowawezesha kufikia hadi asilimia 50 ya soko.

“Tunatarajia kufungua kiwanda hicho kipya kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu. Na mwaka 2019/2020 tutaanza ujenzi wa kiwanda kingine kikubwa cha kuzalisha bidhaa hizo hatua itakayotuwezesha kukaribia mahitaji ya soko letu,” alise

Akitoa mfano wa mahitaji ya soko la nje ya nchi, mfanyabishara huyo alisema walitakiwa na wafanyabiashara wa Burundi kusambaza tani 30 za bidhaa hizo kila mwezi lakini wanashidwa kufikia kiwango hicho kwasababu uzalishaji wa sasa hauwawezeshi kufanya hivyo.

Akizungumzia mahitaji ya sukari kwa ajili ya viwanda vyao alisema, wanahitaji zaidi ya tani 1,600 kwa ajili ya kiwanda cha Ivori Ltd na tani zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kiwanda cha Iringa Food and Bevarage.

“Hata hivyo mahitaji hayo yataongezeka mara mbili zaidi kutokana na upanuzi wa kiwanda tunaofanya. Kwahiyo tutaiomba serikali itusaidie kupata sukari hiyo ili kukidhi mahitaji ya viwanda vyote na upanuzi wake,” alisema

Thakore alitoa wito kwa watanzania kujiwekea kipaumbele cha kutumia bidhaa za ndani ili kuinua maendeleo ya viwanda, na kuongeza ajira na mapato ya wadau na Taifa.

WAGOMBEA URAIS WA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV WAONGEA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZII

March 26, 2018
Mahojiano na DJ Luke Kabla ya Kutangaziwa Mshindi
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwana Lucas Mukami (DJ Luke), akifanyanya mahojiano mafupi na Swahilivilla, kabla ya matokeo ya uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV siku ya Jumamosi March 24, 2018

UTARATIBU ULIOTUMIKA KUONGEZA MAMBO 11 YA MUUNGANO

March 26, 2018


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwasilisha taarifa ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka fedha 2017/2018 na mapendekezo ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19. Taarifa iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, hii leo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola alifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria mara baada ya kuwasilisha taarifa yao kwa Kamati hiyo hii leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia majadiliano ya wajumbe wa kamati mara baada ya kuwasilisha taarifa yao. Kutoka kushoto ni Bw. Richard Muyungi Mkurugenzi wa Mazingira, Bi. Oigenia Mpanduji Mkurugenzi wa Sera na Mipango na Bi. Butamo Phillip Naibu Katibu.


Pichani, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Saed Ahmed Kubenea (kulia) na Mhe. Joseph Kizito Mhagama wakifuatilia majadiliano katika Kamati yao hii leo Mjini Dodoma.

TPDC YAIMARISHA SEKTA YA AFYA KIDUNDAI, LUSHOTO

March 26, 2018
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai, Ndg. Waziri Mdoe (Kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni nne kutoka kwa mwakilishi wa TPDC, Ndg. Asiad Mrutu (Kulia). Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya jengo la zahanati inayoendelea kujengwa katika Kijiji hicho. Na Mwandishi Wetu. Katika jitihada endelevu za utekelezaji wa dhana ya uwajibikaji kwa jamii, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo ni Shirika la Mafuta la Taifa kwa mujibu wa Sheria ya Petroli (2015) limeendelea kuitekeleza dhana hiyo kwa vitendo kwa kutoa vifaa vya ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kidunda Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. Katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, TPDC imeweza kukabidhi hundi ya Shilingi milioni nne ambazo Kijiji kiliomba kusaidiwa ili kuwezesha ujenzi wa zahanati hiyo ambapo kwa mujibu wa serikali ya Kijiji, fedha hizo zitawezesha manunuzi ya mizunguko ya nondo 40 yenye futi 40 kila moja, mifuko ya saruji, matofali na gharama za kumlipa fundi ambapo mpaka kufikia hapo zahanati itakuwa imefanikiwa kuezekwa. Akizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kumaliza makabidhiano, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai kilichopo Kata ya Vuga, Waziri Mdoe alisema “kwa niaba ya halmashauri ya kijiji, tunayo furaha isiyo kifani kwa ndugu zetu kutoka TPDC kwa moyo wa kutoa walioonyesha kwa kusaidia ujenzi wa zahanati yetu ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho ili kuondokana na adh ya kutembea umbali wa kilomita nane ili kupata huduma ya afya”. Mdoe aliongezea kuwa, ni matumaini ya kijiji kwamba TPDC litaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Kijiji cha Kidundai kwani mahitaji yao ni mengi yakiwemo maji, barabara na shule Akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa Kijiji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Asiad Mrutu ambaye ni Mjiolojia alisema “kipekee nimshukuru Mwenyekiti na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji kwa ushirikiano waliouonyesha toka tulipofika siku ya kwanza katika Kijiji hiki tukiwa na lengo la kutafuta eneo la uwekezaji, niseme tu kuwa huu ni mwanzo na tutaendelea kushirikiana bega kwa bega kusukuma gurudumu la maendeleo ya Kidundai mbele.” Pamoja na kukabidhi hundi hiyo, Mrutu aliusisitiza uongozi wa Kijiji kuchanganua gharama za miradi ya maendeleo iliyopo katika mipango ili kurahisisha pale ambapo mdau wa maendeleo anaetaka kuchangia kufahamu ni kiasi gani kitatosha badala ya kueleza mahitaji kwa ujumla, hii itasaidia kupata msaada kirahisi na pia kupata msaada unaokidhi mahitaji ya mradi husika. Mchango wa ujenzi wa zahanati hiyo umekuja baada ya TPDC kufanikisha zoezi la kupata ardhi kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya utafiti wa mafuta na gesi hapa nchini kwa lengo la kuongeza kiasi cha gesi asilia nchini ambacho kwa sasa ni futi za ujazo trilioni (TCF 57.538) na upatikanaji wa mafuta ili kuweza kulihakikishia taifa nishati ya kutosha kwa ajili uzalishaji wa umeme, vyombo vya usafiri, matumizi ya nyumba na kuhakikishia nishati ya kutosha kwa maendeleo ya viwanda nchini. -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''