MHARIRI WA MICHEZO WA GAZETI LA MTANZANIA, MWANI NYANGASSA, AONGOZA TEAM MAUZO YA NEW HABARI (2006) LTD KUSAMBAZA GAZETI HILO LILILOFUNGULIWA DESEMBA 27.

December 28, 2013
KUFUATIA kufunguliwa kwa Gazeti Bingwa la Habari Tanzania, MTANZANIA, linalochapishwa na Kampuni ya NewHabari (2006) LTD, Waandishi, Wahariri pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni hiyo leo walinaswa na Kamera yetu wakisambazas gazeti hilo katika Mitaa ya Dar es salaam.

Mpiga picha katika pita pita zake alikutana na Mhariri wa Michezo wa Gazeti hilo, lililotoka kifungoni leo, Mwani Nyangassa akiwa na nakala zake mkononi, katika juhudi za kulitangazia umma ujio mpya wa gazeti hilo.

Tizama katika picha matukio katika kilichojiri leo katika mitaa ya Sinza, Morroco, Kariakoo, Ubungo na maeneo mengine ya Jiji la Dar es salaam.
Mwani Nyangassa akifanya mauzo katika mitaa ya Jiji la Dar es salaam
Mhariri wa Michezo wa gazeti la Mtanzania, lililotoka kifungoni leo, Desemba 27, akionesha nakala la gazeti hilo, alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Limerudi tena!!!!

Soma Waraka wa Absalom Kibanda kwa Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa ujumla

December 28, 2013

Saturday, December 28, 2013

Na Absalom Kibanda, pichani na haya ndio maoni yake.
MHESHIMIWA Rais wangu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Nakusalimu kwa salamu ya utii inayotambua na kuheshimu kwa dhati mamlaka makubwa na ya juu uliyonayo kama mkuu wa taifa letu ambalo mazingira yake ya leo yanapaswa yawe wenye mwelekeo wa kushangilia kama si kujivunia uhuru ambao tuliupata mwaka 1961 na 1964 kwa kutegemea upande tulipo katika muungano wetu.

Mheshimiwa Rais, najisikia faraja iliyojaa majonzi moyoni kupata fursa hii adhimu kukuandikia waraka ambao msukumo wake unasukwasukwa na dhamira njema kabisa ambayo aghalabu kiini chake si kingine bali mapenzi mema kwa nchi na viongozi wetu wote.

Ni faraja kwa kuwa nimepata fursa ghali na adimu ya kuteta na kiongozi wetu mkuu kwa upendo, uhuru na kwa kujiamini, huku nikiwa na uchungu pia kwa sababu ujumbe ambao unabebwa na waraka huu ni wa kuumiza sana nafsi, roho, akili na mwili.

*GAZETI LA MTANZANIA KAMA MANDELA, LAANZA RASMI KUSOMWA JANA

December 28, 2013

 Mhariri wa michezo wa Gazeti la Mtanzania Mwani Nyangasa (katikati) na mtayarishaji wa kurasa, Zuhura Sufiani (kushoto) wakipozi na magazeti ya Mtanzania wakati wakifanya Promosheni ya gazeti hilo lililoanza kuingia rasmi mtaani jana Desemba 27, baada ya kufungiwa kwa miezi mitatu.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006 Ltd, Absalom Kibanda (katikati) akijumuika na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa kulinadi gazeti lao lililotoka kifungoni na kuanza kuingia mtaani rasmi jana Desemba 27.chanzo sufianimafotoblog