MKAZI WA DAR ES SALAAM AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MBEYA AKIWA NA MENO YA TEMBO KILO 8.5

December 01, 2015
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi


Na Emanuel Madafa,Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya  linamshikilia Lukas Wambura (38)  Mkazi wa Banana – Dar es salaam  mwenye shahada ya dharura ya kusafiria ab-10044029  akiwa na  vipande vinne vya meno yadhaniwayo kuwa ya tembo vyenye uzito wa kilo 8.4 yenye thamani ya dola za kimarekani 30,000, sawa na tshs 64,140,000/=.



Tukio hilo limetokea Novemba  30 -2015 majira ya saa12 jioni  katika eneo la custom – mpakani tunduma, , wilaya ya momba Mbeya ..



Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema  mtuhumiwa huyo  alikuwa anavuka mpaka akitokea nchi jirani ya Zambia kuingia nchini na mzigo huo alikuwa ameuficha ndani ya begi lake la nguo.



Wakati huo jeshi hilo  la polisi linawashikilia watu wanne kwa kukutwa na silaha mbili pamoja na nyara za serikali.



Kamanda Msangi amewataja watuhumiwa hao kuwani  M ohamed Ndilava [55], Mkazi wa Mkwajuni , Nassora Omary [65]  Mkazi wa Tabora na  Mwanza Mtokambali [39] Mkazi wa Njelenje pamoja na  Frank  Jonas  [32], Mkazi wa Bitimanyanga.



Msangi amesema watuhumiwa hao sita walikamatwa Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .



Amesema  watuhumiwa walikutwa na silaha moja aina ya riffle 416 yenye nambari c.6539833 na gobole moja lisilokuwa na namba, pia walikutwa na nyara za serikali  kichwa kimoja cha paa, nyama ya paa na nyama ya sungura vyote vikiwa na thamani ya tshs 1,176,000/=.



Kufuatia matukio hayo  Kamanda Msangi  anatoa  wito  kwa yeyote mwenye taarifa juu ya wahalifu wakiwemo  majangili kuzitoa katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe mara moja.



Mwisho.
(JAMIIMOJABLOGMBEYA )

MBIO ZA KILIMANJARO HEALTH RUN 2015 ZAFANYIKA MKOANI KILIMANJARO.

December 01, 2015
Washiriki wa Mbio za Kilimanjaro Health Run KM 10 wakianza mbio hizo katika eneo la nje ya uwanja wa Majengo mjini Moshi. 
Washiriki wa Mbio za Km  5 zilizowashirikisha zaidi watoto wanao lelewa katka ituo mbalimbali mjin Moshi.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania na Zara Charity,Zainab Ansel akishiriki mbio hizo pamoja na mdogo wake Rahma wakikimbia mbio za Km 5.
Mshindi wa mbio za KM 10 kwa wanaume ,Lameck Msiwa akimaliza mbio katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo kutoka nje ya nchi wakimalizia mbio katika uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Usalama kwa wakimbiaji uliimalishwa zaidi.
Mwanariadha Banuelia Bryton akihitimisha mbio akiwa nafasi ya kwanza katika mbio za KM 10 kwa upande wa wanawake. 
Mkurugenzi wa Zara Tanzania,Zainab Ansel akimalizia mbio za KM 5.
Askari Polisi wa Kikosi cha usalama barabarani ,Salatory Mtanange akiwasindikiza washiriki wa mbio hizo waliokuwa mwishoni kabisa huku akikimbia nao kwa karibu.
Baadhi ya washiriki wa mbio za KM 3 katika mbio za Kilimanjaro Health Run 2015.
Kampuni ya Vinywaji baraidi ya Bonite ya mjini Moshi ilidhamini zawadi kwa washindi wa mbio hizo.
Zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa mbio hizo z
likianza rasmi.
Baadhi ya wakurugenzi wa mashirika mbalimbali waliofika kwa ajili ya mbio za Kilimanjaro Health Run ambazo hufanyika kila mwaka.
Katibu wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro  ( KAA ),Amini Kimaro akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Mkurugenzi wa Zara Tanzania ,Zainab Ansel akizungumza katika sherehe za kilele cha mbio hizo.
Viongozi wa mashirika mbalimbali wakiwa tayari kukabidhi zawadi kwa washindi.
Mshind wa kwanza wa Mbio za Km 10 ,Lameck Msiwa akikabidhiwa zawadi zake mara baada ya kuibuka mshindi katika mbio hizo.
Mshindi wa kwanza kwa wanawake katika mbio za KM ,10 Banuelia Bryton akikabidhiwa zawadi zake.
Mshindi wa pili kwa wanawake Mbio za KM 10 Adelina Aclati akikabidhiwa zawadi.
Mshind kwa upande wa walemavu pia alijipatia zawadi zake.
Diwani wa kata ya Longuo ,Ray Mboya akizungumza katika sherehe mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.