MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAZINDULIWA MKOA WA SHINYANGA

November 13, 2017
Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Novemba 13,2017 umezindua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yenye kauli mbiu "Zuia ajali,Tii sheria,Okoa Maisha". 

DC SHINYANGA AZINDUA MRADI WA MTOTO MWEREVU

November 13, 2017
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amezindua mradi wa Mtoto Mwerevu unaolenga kuwapatia lishe watoto wenye umri wa siku 1000 katika kata tano za manispaa ya Shinyanga ambazo ni Kizumbi,Ibadakuli, Chamaguha,Mwawaza na Mwamalili.
Mradi huo utakaodumu kwa muda wa miaka minne unatekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) linalotoa huduma za kijamii kwa upande wa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumatatu Novemba 13,2017 katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga,Matiro alilitaka shirika la TVMC kuwafikia walengwa ili kupunguza idadi ya watoto wenye udumavu katika jamii.
“Nawapongeza kwa kuanzisha mradi huu,mnachotakiwa kuzingatia ni kushirikisha walengwa wote wanaotakiwa ili mradi huu uwe na mafanikio mazuri,shirikisheni viongozi wa mitaa na kata kwani wao ndiyo wapo karibu zaidi na jamii”,alisema Matiro.
Akielezea kuhusu mradi huo, Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema lengo la mradi wa Mtoto Mwerevu ni kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri wa siku 1000 katika kata tano za manispaa ya Shinyanga.
“Baada ya kufanya utafiti,tulibaini kuwa kati ya kata 17 za manispaa ya Shinyanga,tulibaini kuwa kata tano za Kizumbi,Ibadakuli, Chamaguha,Mwawaza na Mwamalili kuna idadi kubwa ya watoto waliodumaa kutokana na kukosa lishe bora”,alisema Ngangala.
“Tumepanga kutekeleza mradi huu kwa kipindi cha miaka minne lakini tutaanza kwa majaribio ya mwaka mmoja na kama kutakuwa na mafanikio basi tutaendelea kutekeleza mradi huu ambao walengwa wakuu ni akina mama wajawazito na akina mama wanaonyonyesha”,alieleza Ngangala.
Alisema mojawapo ya mbinu watakazotumia kufanikisha mradi huo kuwa ni kuhamasisha akina mama wajawazito na wanaonyonyesha kutumia lishe bora kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula.
Ngangala aliyataja makundi matano muhimu ya chakula katika kupambana na udumavu kwa watoto kuwa ni nafaka,mizizi na ndizi, vyakula jamii ya nyama na mikunde,mboga mboga,matunda na sukari,asali na mafuta.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha mradi huo watafanya kazi zaidi na vikundi mbalimbali katika jamii ambavyo vitakuwa mstari wa mbele kuhamasisha namna ya kunyonyesha,jinsi ya kuandaa chakula cha mtoto,faida za kunawa,kilimo cha bustani ya mboga mboga pamoja na ufugaji kwa ajili ya lishe bora.
Uzinduzi wa mradi wa mtoto mwerevu umehudhuriwa na maafisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga, ,mwakilishi wa mkurugenzi wa manipaa,maafisa kilimo kata na maafisa watendaji wa kata na mitaa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga wakati wa kuzindua mradi wa Mtoto Mwerevu unaotekelezwa na shirika la TVMC-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa watekelezaji wa mradi wa mtoto mwerevu kushirikisha walengwa katika jamii

DK. KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WAWILI (UJERUMANI NA CHINA) OFISI KWAKE MJINI DODOMA LEO KUHUSU MAENDELEO YA UHIFADHI NA UTALII NCHINI

November 13, 2017
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter (kushoto) ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini. 
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Wächter (katikati) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika kuendeleza Uhifadhi na Utalii nchini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo amemuomba kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipokea zawadi ya taswira la Ua la Taifa la China kutoka kwa Balozi wa nchi hiyo nchini, Bi. Wang Ke ofisini kwake mjini Dodoma leo. Amemuomba balozi huyo kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo amemuomba kushirikiana na Wizara yake kuweka mkakati wa pamoja wa kuongeza idadi watalii na wawekezaji katika sekta hiyo kutoka nchini China.  (Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii).
Shirika la Amref lazindua Mradi wa Uchechemuzi katika Sekta ya Afya mkoani Shinyanga

Shirika la Amref lazindua Mradi wa Uchechemuzi katika Sekta ya Afya mkoani Shinyanga

November 13, 2017
Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo huku viongozi mbalimbali wakishuhudia.                        
Shirika la Amref Health Africa hii leo limezindua mradi wa uchechemuzi katika sekta ya afya (Health System Advocacy HSA) mkoani Shinyanga, wenye lengo la kuongeza ushawishi katika sekta ya afya ili kuboresha zaidi sekta hiyo mkoani humo. Meneja mradi huo, Josiah Otege amesema lengo ni kufanya uchechemuzi (ushawishi) katika maeneo manne ya sekta ya afya ambayo ni kuimarisha uzazi wa upango, bajeti ya afya, kuongeza idadi ya watumishi wa afya, kuboresha afya ya uzazi pamoja na utawala bora katika sekta hiyo. Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mgeni rasmi Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume ambaye alimwakilisha Katibu Tawala mkoani humo Albert Msovela, alilipongeza shirika la Amref kwa kuanzisha mradi huo ambao alisema utasimamiwa vyema ili kuhakikisha unaleta mabadiliko chanya katika jamii. Mradi huo ambao ni wa miaka minne kuanzia mwaka huu, unatarajiwa kutekelezwa katika halmashauri tatu za mkoa wa shinyanga ambazo ni Msalala, Shinyanga Vijijini pamoja na Kishapu. Meneja mradi huo wa HSA, Josiah Otege akizungumzia mradi huo. 
Na Binagi Media Group

SHIRIKA LA FOUNDATION FOR CIVILI SOCIETY WAPANGA KUSAIDIA WATOTO WANAOTIBIWA MOI

November 13, 2017
Katika kuhakikisha kuwa wanaisaidia Jamii inayowazunguka shirika lisilo la kiserikali la The Foundation Foundation for civil Society limejipanga kuwasaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatikana katika Taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa shirika hilo kuadhimisha siku yao maarufu ya “GIVING TUESDAY” ambayo hutumia siku hiyo kuisaidia jamii.

Akieleza mikakati ya kuadhimisha siku hiyo kwa mwaka huu mwakilishi kutoka shirika hilo Ndugu Karin Rupia amesema kuwa baada ya kuona changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wanaohudumiwa katika taasisi hiyo wameamua kuitumia siku hiyo kuwasaidia watoto hao huku akiwataka watanzania kuwaunga mkono katika kutekeleza Jukumu hilo.

Mwakilishi huyo amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika kwa siku mbili ambapo siku ya kwanza itakuwa tarehe 25 Novemba ambapo wataitumia kuchangia damu kwa ajili ya watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ,zoezi ambalo litafanyika ndani ya taasisi hiyo ya Mifupa MOI kuanzia saa tatu asubuhi hadi majira ya mchana

Katika zoezi la pili litafanyika tarehe 28 Novemba ambayo ndiyo siku maalum ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday” ambapo katika siku hiyo shirika limejipanga kusaidia watoto katika kuwapatia mahitaji mbalimbali ambapo shughuli kubwa itakuwa ni kuwasaidia watoto kupata upasuaji ambapo amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasaidia watoto mia moja kupata huduma hiyo ya upasuaji.pamoja na kuwadaia vifaa mbalimbali vitakavyosaidia katika kwa watoto hao ambapo watanzania wametakiwa kujitolea kuchangia kwa kasi ili kusaidia shirika hilo kufikia malengo hayo.

Ili kushiriki katika zoezi hilo la kuchangia damu kwa ajili ya ,kuwa unaweza kupiga simu namba 0762767237.
Video ikifafanua kuhusu siku hiyo ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday”

  Mchango wa Asasi za Kiraia kwenye Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi

Mchango wa Asasi za Kiraia kwenye Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi

November 13, 2017
                    Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Vijijini ADLG iliyopo Jijini Mwanza, Jimmy Luhende akichangia mada kwenye Mkutano wa Sekta ya Uziduaji 2017 uliofanyika Mjini Dodoma.
Novemba 02-03, 2017 ulifanyika Mkutano wa Sekta ya Uziduaji (Madini, Mafuta na Gesi) Mjini Dodoma ambapo miongoni mwa maazimio kwenye mkutano huo ni Asasi za Kiraia kushiriki ipasavyo katika kuhakikisha Taifa linanufaika na Rasilimali zake.
Ungana na BMG kujua yaliyojiri kwenye mkutano huo ulioandaliwa na muungano wa Asasi za Kiraia zinazoangazia masuala ya Utawala Bora kwenye sekta ya Uziduaji nchini HakiRasilimali.
 USAJILI TIMU ZA WANAWAKE WATANGAZWA

USAJILI TIMU ZA WANAWAKE WATANGAZWA

November 13, 2017

USAJILI TIMU ZA WANAWAKE WATANGAZWA

Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Wakati Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikitarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, tayari usajili wa msimu kwa timu zote 12, umekamilika.
Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano, usajili ulipangwa ufanyike kati ya Oktoba 25 na Novemba 12, mwaka huu na kwamba kuanzia leo Novemba 13 hadi 17, mwaka huu ni kipindi cha pingamizi.
Novemba 18, mwaka huu kutakuwa na kikao cha  Kamati ya Sheria kabla ya Novemba 20, mwaka huu kutoa leseni za wachezaji.
Novemba 24, mwaka huu kutakuwa na Semina ya Viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna jijini Dar es Salaam.
Ligi hatua ya makundi ikianza Novemba 26, mwaka huu ukomo utakuwa Desemba 9, mwaka huu Ligi Kuu na kupata jumla ya timu nane ambazo zitacheza ligi hatua ya Nane Bora ‘Super 8’ itaanza Desemba 20, mwaka huu. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.
Timu zilizosajili kutoka Kundi A ambazo ziko Dar es Salaam ni Simba Queens ya jijini Dar es Salaam iliyopanda daraja msimu huu. Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen zote za Dar es Salaam pamoja na timu za Fair Play ya Tanga na mabingwa watetezi – Mlandizi Queens.
Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka kituo cha Dodoma. Timu nyingine ni Marsh Academy pia ya Mwanza; Panama ya Iringa; Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens ya Singida.
MAHAKAMA YAMHUKUMU ‘MSANII LULU’ MIAKA 2 JELA KWA KIFO CHA KANUMBA

MAHAKAMA YAMHUKUMU ‘MSANII LULU’ MIAKA 2 JELA KWA KIFO CHA KANUMBA

November 13, 2017
_98725855_9c3337b4-dc8f-4663-868e-b031f8808aac
Leo Novemba 13, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael “Lulu” kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake marehemu Steven KanumbaHukumu hiyo imesomwa na Jaji Sam Rumanyika ambaye amesema, ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na wazee wa baraza waliotoa maoni yao kuwa kweli mshtakiwa Lulu aliuwa bila ya kukusudia.Lulu ametiwa hatiani chini ya kifungu cha sheria Namba 195 cha cha mwenendo wa mashtaka ya jinai.

IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MAAFA

November 13, 2017
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. William Ngeleja akitoa maelezo ya awali kuhusu utendaji kazi wa kamati hiyo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 bungeni Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa .
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.
 Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu  (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Idara yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe hao iliyoandaliwa na Ofisi hiyo mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe.  Aida Kenani akichangia hoja wakati wa wakati  wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa bungeni mjini Dodoma.
 Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa mhe. Abdallah Mtolea (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati na Watendaji wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi hiyo kwa lengo la kutoa uelewa wa masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Mmoja wa wawezeshaji kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili kutoa uelewa wa masuala  ya Menejimenti ya maafa nchini Novemba 12, 2017. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)

IDARA YA UTALII YAMTAKIA MAISHA MAPYA ALIYEKUWA MKURUGENZI MSAIDIZI WA IDARA YA UTALII, BI.UZEELI KIANGI BAADA YA KUSTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA

November 13, 2017
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati) katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu (kushoto) akimkabidhi moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma.
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akiwa na Afisa Utalii, Nina Kisando (katikati) wakiwa wanatabasamu huku wakionesha moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.
Baadhi ya Watumishi wa Idara ya Utalii wakimsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi akizungumza katika hafla ya kustaafu kwake kwa Mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma.

Mikoa ya Dar, Pwani na Morogoro yashauriwa kufuata sheria za uhifadhi wa maliasili

November 13, 2017
Na Tulizo Kilaga

WANANCHI katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam inayopatikana kanda ya mashariki wametakiwa kuzingatia umuhimu wa hifadhi za misitu nchini kwa kuhakikisha kila mwananchi anazingatia maagizo ya Serikali pamoja na kufuata sheria za nchi zinazohusiana na uhifadhi wa maliasili.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo, mkoani Morogoro wakati akifungua mkutano wa siku moja wa kanda ya mashariki kuhusu utekelezaji wa randama ya makubaliano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) ulioandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kufanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), tarehe 9 Novemba, 2017.

Mkuu wa Mkoa huyo wa Pwani ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo alisema randama hiyo iliyosainiwa na pande hizo mbili imelenga kuimarisha usimamizi wa misitu nchini na utawala bora, kufanya Uperembaji wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania na Kuboresha ukusanyaji, ugawaji, utumiaji na kufuatilia matumizi ya asilimia tano ya tozo ya upandaji miti.

Injinia Ndikilo alisema, inasikitisha kuona dhamana ya kudhibiti uharibifu mkubwa wa misitu unaofikia kiasi cha hekta 372,000 kwa mwaka ambacho ni sawa na asilimia 1.1 ya eneo lote lenye misitu inayokadiriwa kuwa hekta milioni 48 na sawa na kufyeka zaidi ya hekta 1,000 kwa siku wanaachiwa TFS.

Alisema tafiti zinaonyesha kuwa utegemezi mkubwa wa misitu kwa ajili ya nishati (mkaa na kuni), hususani katika mkoa wa Dar es salaam unachangia nusu ya uharibifu wa misitu nchini.

Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza kuwa zaidi ya asilimia sabini ya mkaa unaozalishwa mikoani huingia Dar es Salaam kwa njia zisizo halali kama vile magari yaliyofunikwa, baiskeli na pikipiki, na endapo hatua madhubuti za kudhibiti uharibifu huo hazitachuliwa kwa haraka nchi itakuwa jangwa siku za karibuni.

Injinia Ndikilo alisema juhudi za pamoja zinatakiwa katika kuilinda na kuhifadhi misitu yetu, na kuwataka viongozi waliofika katika mkutano huo kuondoka wakiwa wamepikwa hasa kwa kuwa wamejadili mambo mbalimbali kuhusu usimamizi wa misitu na majukumu ya kila mdau katika kuhifadhi na kuilinda.

MBIO ZA TIGO DODOMA HALF MARATHON ZAFANA I

November 13, 2017
Wafanyakazi wa Tigo walioshiriki katika mbio ndefu za  Tigo Dodoma Half Marathon wakiwa na bango linalosema 'Tumekusoma' kabla ya kuanza kwa mbio hizo ndefu jijini Dodoma leo. Tumekusoma ni  kampeni mpya ya Tigo inayolenga kuwapa wateja wake urahisi wa kutumia huduma za simu pamoja na faida zaidi za bonasi kila watakapotumia namba mpya ya *147*00# kununua muda wa maongezi, bando, data na kufanya miamala ya fedha. 
Mshindi wa mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Marwa  akimaliza mbio hizo zilizofanyika mjini Dodoma hapo jana. 
Baadhi ya waheshimiwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na medali na vyeti walivyotunukiwa kwa kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana.
Naongoza kwa mfano na vitendo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dr Hamisi Kigwangala akimalizamio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana. Mhe Dr. Kigwangala alishiriki katika mbio za kilometa 21.

KAMPUNI YA TATU MZUKA IKISHIRIKIANA NA NAIBU WAZIRI MAVUNDE WAKABIDHI MATOFALI 3000 NA MIFUKO YA SARUJI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA MSINGI MPYA ZA MBANDE NA MUUNGANO MKOANI DODOMA

November 13, 2017
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde  mwishoni mwa wiki amekabidhi matofali 3000 na mifuko ya saruji 100 katika Kata ya Makutupora kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Shule za Msingi Mpya za Mbande na Muungano Wilaya ya Dodoma mjini mkoani Dodoma.

Msaada huo alioukabidhi umetoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka  ambayo ilikabidhi zawadi kwa washindi katika droo ya michezo hiyo,Mavunde aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi ili kusaidia kuboresha Elimu nchini.
 
Waziri Mavunde alisema kuwa ujenzi wa shule hizo utasaidia kupunguza adha inayowapata wanafunzi kutembea umbali mrefu  wa zaidi ya kilomita 7 kufuata shule katika eneo la Veyula.
 "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakikabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa mmoja wa viongozi katika kata ya Makutupora  kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande. Kwa ajili  ya ujenzi wa madarasa mawili  kila moja.
  "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakiwashukuru baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa kata ya Makutopora mara baada ya kukabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoka kijiji cha Makutopora na Mbande kushuhudia tukio la makabidhiano ya matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande,iliyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ikishirikiana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde.