CHOPA YA CCM YATUA MANYARA,MWIGULU NCHEMBA AENDELEA KUKUSANYA KURA ZA CCM

CHOPA YA CCM YATUA MANYARA,MWIGULU NCHEMBA AENDELEA KUKUSANYA KURA ZA CCM

September 28, 2015



Mwigulu Nchemba mmoja ya wajumbe 32 wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akisalimiana na Wananchi wa Karatu Mjini jioni ya leo alipofika kwaajili ya Kuomba kura kwaajili ya Rais,Mbunge na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi.

Sehemu ya Wananchi wa Karatu Mjini waliofika Uwanjawa Mazingira Bora kusikiliza Mkutano wa hadhara wa Mwigulu Nchemba.

Mwigulu Nchemba akitoa darasa kwa Wananchi wa karatu kuhusu biashara ya Kumuacha Dr.slaa na kumpatia Edward Lowassa aliyehamia kutoka CCM.Dr.slaa aliyetumia Jasho na Damu kuuimarisha Upinzani wenye meno,Hii leo ameondolewa kwakuwa DILI imewekwa mezani ili Mtu mwenye kashafa mbalimbali chafu aweze kuwania Urais.Kwaaina ya Mgombea waliosimamisha UKAWA,Mwigulu amesema itakuwa rahisi sana kwa Magufuli kushinda kwa asilimia kubwa sana ya Kura.

Wananchi wa Mbulu Vijijini wakisikiliza Mkutano wa Mwigulu Nchemba wakati akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa BashinetMbulu Vijijini wakati alipokwenda kumuombea Kura Rais Mtarajiwa J.Pombe Magufuli na kuwanadi Madiwani na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Manyara.
Mkutano wa kampeni za CCM Uwanja wa Garagara Jimbo la Mtopepo

Mkutano wa kampeni za CCM Uwanja wa Garagara Jimbo la Mtopepo

September 28, 2015

8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi na wanachama wa CCM Jimbo la Mtopepo katika mkutano wa kampeni zinazoendelea katika uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Unguja Septemba 28, 2015
Picha zote na Ikulu.
2
Mke wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Kwanza Mama Fatma Karume akiwaombea kura wagombea wa nafasi za Uongozi kupitia chama cha Mapinduzi alipokuwa akizungumza na Wananchi na wanaCCM katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za CCM katika Uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
3
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban alipokuwa akiwaombea kura Wagombea nafasi za Uongozi katika Chama cha Mapinduzi CCM  wakati wa Uchaguzi Mkuu ukifika,jimbo la Mtopepo leo katika mkutano wa kampeni zinazoendelea,uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Unguja.
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja CCM Yussuf Mohamed Yussuf wakati wa Mkutano wa hadhara kampeni za CCM jimbo la Mtopepo   katika uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Unguja.
4
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakisikiliza sera zilizokuwa zikitolewa na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  jimbo la Mtopepo leo katika mkutano wa kampeni zinazoendelea,uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Unguja.
5 6
WanaCCM na Wapenzi wa Chama hicho wakinyoosha  mikono juu kumuuunga kama ishara ya kuwachagua wagombea wa CCM wakati  Mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein   jimbo la Mtopepo leo katika mkutano wa kampeni zinazoendelea,uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Unguja.
7
WanaCCM na Wapenzi wa Chama hicho wakisikiliza sera zilizokuwa zikitolewa na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa kipindi cha pili cha Uongozi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  Jimbo la Mtopepo leo katika mkutano wa kampeni zinazoendelea,uwanja wa Garagara Wilaya ya Magharibi A Unguja

LOWASA ALITETEMESHA JIJI LA TANGA

September 28, 2015



Tangakumekuchablog
 MKUTANO wa mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa, leo  umelazimu kusitisha shughuli zote za biashara na usafirishaji na badala yake watu wengi kwenda katika mkutano wake uliofanyika uwanja wa Tangamano.
Shamrashara za jiji kuzizima zilianza toka asubuhi baada ya vijana wenye pikipiki, magari na kila aina ya vipando vikiwemo magari ya punda na bodaboda za baskeli kupitia mitaani mkuanzia barabara ya kwanza hadi ya 21.
Huduma ya usafiri wa daladala ulikuwa wa kusuasua kuanzia saa 5 asubuhi  baada ya watu wengi kufika katika uwanja wa Tangamano mapema ili kuwahi nafasi na kujionea shamrshamra za mkutano.
Baadhi ya abiria ambao walikuwa wakienda Raskazone na majanimapana wakalazima kushushwa Tangamano badala ya mwisho wa gari kutokana na abiria wote kushuka uwanjani hapo.
Kwa upande wa huduma za maduka wamiliki na wauzaji wakalazima kufunga biashara zao baada ya kukosa wateja kufuatia watu wote kukimbilia Tangamano kusikiliza sera za mgombea Urais wa Ukawa, Edward Lowassa.
Baadhi ya wakazi wa Ngamiani walisema haijawahi kutokea mitaa kuwa meupe na kudhani kuwa hakuna watu na mitaa kukimbiwa ilhali wengi wamenda katika mkutano wa kampeni za mgombea wa Ukawa.
Nao abiria wa bodaboda na baskeli wamevihama vituo vyao kushiriki katika mkutano huo na kuviwacha vitupu na abiria wao kutembea kwa miguu jambo ambalo wengi wamedai imekuwa kero.
“Mimi nimetoka Mikanjuni kwa mguu hadi kufika hapa sijakutana na daladala ya aina yoyote na kila umuonae anelekea uwanja wa mkutano wa mgombea urais wa Ukawa” alisem Mwarami Sharif
Alisema mkutano huo umeleta usumbufu kwa watu wa kipato cha chini ambao hawana usafiri binafsi kwani wengi wao wamelazika kutembea kwa miguu kwenda hospitali kuwaona wagonjwa na wanaorejea majumbani.
Hata hivyo mkutano huo uliahirishwa kutokana na maelfu ya watu kufurika na kuhatarisha usalama wa watu kutokana na kukosa hewa na kukanyagana na hivyo mgombea huyo wa Urais kusema bora usalama wa wapiga kura wake na hivyo kuwataka siku ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi na kumuingiza Ikulu.
Taarifa zilizoifikia tangakumekuchablog ni kuwa watu zaidi ya 80 walizimia uwanjani hapo na kupatiwa matibabu katika vituo vya afya iliyosababishwa na kukosa hewa kutokana na wingi wa watu waliojitokeza uwanjani hapo.

 Maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga wakimiminika katika uwanja wa Tangamano kwa kutumia kila aina ya usafiri ukiwemo Punda, Pikipiki Baiskeli na vipando tofauti tofauti ilimradi kufika na kusikiliza sera za Mgombea Urais, Edward Lowassa





 Kutokana na maelfu ya watu kufurika Uwanja wa Tangamano na maelfu wengine walikimbilia katika majengo ya gorofa ili tu kusikiliza na kumuona mgombea Urais , Edward Lowassa ambapo hata hivyo maofisa usalama waliwamuru kushuka ili kuepusha magarofa kuanguka kutokana na wingi wa watu katika majengo hayo




WASANII WA BONGO MOVIE WAIBUKIA MJINI IRINGA,WATANGAZA KUTEMBEA NCHI NZIMA KWA BAJAJ KUMUUNGA MKONO DKT MAGUFULI

September 28, 2015
Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-IRINGA
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda  nafasi ya Urais.
  Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
 Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
 Magufulika staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.
  Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
 Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema leo mchana
wazee wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.
  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
 Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
 Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

September 28, 2015
FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU(JAMIIMOJABLOG)
~watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
AINA ZA BAWASIRI
~Kuna Aina mbili za bawasiri
(A) BAWASIRI YA NDANI
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika
(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia
(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe
(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
CHANZO CHA TATIZO
~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO
👉MATATIZO YA UMRI
👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
👉UZITO KUPITA KIASI
👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
DALILI ZA BAWASIRI
👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZSZOKOBOLEWA
👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
👉EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
👉kupata upungufu wa damu (anemia)
👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
👉kuathirika kisaikolojia
👉kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali
WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612.

WAFANYAKAZI KISSA PHARMACY LTD WATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI TANGA(AMBONI CAVES)

September 28, 2015





Wafanyakazi wa Kissa Pharmacy Ltd  Pharmaceuticals Whole Sale And Retali Mbeya Tz wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika eneo la mapango ya Amboni (AMBANI CAVES ) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria ndani ya Mapango hayo sanjali na kuhamasisha utalii wa ndani.Picha na Emanuel Madafa Baba JJ


Wafanyakazi Kissa Pharmacy wakisikiliza kwa makini maelezo ya mmoja wa watoa huduma katika mapango hayo Ndugu Allan Yohana kabla ya kuanza rasmi shughuli ya kutembelea mapango hayo.(JAMIIMOJABLOG)






muonekano kwa baadhi ya maeneo ndani ya mapango hayo ya Amboni Caves .













Mkurugenzi Kissa Pharmacy Mbeya Ndugu Gasper Kilango Singo akiwa ndani ya mapango hayo .





The Amboni Caves are the most extensive limestone caves in East Africa. They are located 8 km north of Tanga City in Tanzania off the Tanga-Mombasa road. The caves were formed about 150 million years ago during the Jurassic age. It covers an area of 234 km². According to researchers the area was under water some 20 million years ago. There are altogether ten caves but only one is used for guided tours.