WAZAZI WALALAMIKA KUFUNGWA KWA MATAWI YA CHUO KIKUU CHA ST, JOSEPH

March 01, 2016

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

BAADHI   ya wazazi wa wanafaunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika  matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.

February 26 mwaka huu ,tume ya vyuo vikuu ilitangaza kufuta kibali cha chuo kikuu cha St Joseph (SJUIT) tawi la Arusha ikiwa ni wiki moja imepita tangu kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo kwa Chuo kikuu cha St Joseph tawi la Songea,vyuo vilivyoko chini ya shirika la kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI).

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na hatua hiyo huku wakidai kuwaathili kisaikolijia watoto wao ambao wengine walikuwa katika maandalizi ya mitihani.

“Nadhani ingekuwa ni jambo la busara  kwa TCU kukaa meza ya mazungumzo na uongozi wa chuo badala ya kuchukua hatua ya kukifutia vibali….Chuo hiki kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kuzalisha wataalumu mbali mbali.”alisema Mrisho Sume.

Nchi yetu ina wataalamu wachache  katika sekta ya Sayansi na Teknalojia ,chuo hiki kilikuwa ni kimojawapo kinachotoa wataalamu hao hivyo mchango wake unapaswa kuheshimika na kusaidiwa pale inapobidi,” aliongeza Sume ambaye mwanaye alikuwa akisoma katika chuo cha Sayansi ya kilimo katika chuo hicho tawi la Songea.

Mzazi mwingine alijitambulisha kama Mariam Ali alisema taarifa alizokuwa nazo ni kuwa uamuzi wa kufunga baadhi ya matawi hayo ulifikiwa bila ya kukipa taarifa chuo hicho juu ya mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kukipa muda wa kuyafanyia kazi.

“Binti yangu alikuwa akisoma tawi la Arusha na nimepata taarifa kuwa  timu ya ukaguzi kutoka tume ilifika chuoni hapo   kwa ajili ya ukaguzi lakini cha kushangaza ni kuwa chuo hakikupewa taarifa ya mapungufu yaliyoonekana ili yafanyiwe kazi na badala yake kililetewa barua za kufutiwa vibali.”alisema Mariam.

Uamuzi ulifanywa ni wazi haukuzingatia haki na unatuumiza sisi wazazi pamoja na watoto wetu, tulitegemea TCU kukipatia chuo  ripoti ya mapungufu waliyoyagundua na kupewa muda wa kuyafanyia kazi  na endapo kingeshindwa kuyafanyia kazi katika muda ambao kimepewa tume ingekuwa na haki ya kutoa adhabu,” aliongeza Mariam.

Naye John Budigle alisema tangazo lilitolewa na TCU kuhusu kufunga vyuo hivyo lilisema moja ya matatizo yaliyopelekea kufungwa ni migomo ya wanafunzi huku akiongeza kuwa migomo yote  ilitokana na kucheleweshewa mikopo na siyo matatizo ya chuo .

“Mimi kwa mtizamo wangu naona kama TCU imetumia nguvu kubwa kwenye suala hili, kama chuo kilifanya makosa kilipaswa kupewa maelekezo ya kushughulukia kasoro au mapungufu kwani hakuna chuo kisichokuwa na mapungufu hata hivyo vya umma. “alisema Budigle.

“Hatua hii inawavunja moyo wawekezaji katika sekta ya elimu. Hawa ni wadau katika elimu na ni vizuri TCU wakatuchukuliwa hivyo. Wao ni wasimamizi ambao wanatakiwa kuwaongoza na kuwarekebisha pale wanapokosea. Kitendo cha kukifutia vibali bila kufuata haki kinawavunja moyo wadau wa elimu pamoja na wanafunzi pia,” aliongeza Budigle.

Akitangaza hatua hiyo hivi karibuni  Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alizitaja sababu za kufikia uamuzi huo kuwa ni matukio ya migogoro ya muda mrefu baina ya uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na ukiukwaji wa sheria za uendeshaji wake kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu.

Mwisho.

NEW HIT SONG: INNO BIZ ft.P-SILA-NI MZURI.

March 01, 2016
Msanii wa Kizazi Kipya "Inno Biz" kutoka Jijini Mwanza, ameachia Wimbo Mpya. Wimbo huo Umepokelewa vizuri Jijini Mwanza na tayari umeanza kutambulishwa katika Radio mbalimbali za Jijini Mwanza.

Wimbo huo unaitwa "NI MZURI" na umepikwa na Producer ni P-Sila, Studio ikiwa ni Acute Music ya Jijini Mwanza.

"Audio ya ngoma hii imepokelewa vizuri Jijini Mwanza na Mikakati niliyonayo ni kui-push zaidi kote nchini, kabla ya kuanza kutengeneza Video yake ili kuwapa burudani mashabiki zangu wote kwa maana ya wale wa Audio na Video". Anasema Inno Biz.
Pakua na Sikiliza Wimbo huo hapa chini.

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOPELEKEA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NAMABENGO ILIYOPO MKOANI RUVUMA KUANDAMANA.

March 01, 2016
Wanafuzi 106 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Namabengo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kumwona mkuu wa mkoa Said Mwambungu kumpelekea malalamiko dhidi ya vitendo vya udharirishaji wanavyofanyiwa na makamu mkuu wa shule hiyo Shaibu Champunga. Ebu wasikilize kupitia RUVUMA TV on Line.

EWURA YATANGAZA KUSHUKA KWA BEI YA MAFUTA NCHINI

March 01, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu bei kikomo za mafuta aina ya petroli kuanzia leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Umeme, Mhandisi Anastas Mbawala.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (katikati), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Umeme, Mhandisi Anastas Mbawala na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Petroli, Gerald Maganga.


 Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini kuanzia kesho Machi 2, 2016.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, Mkurugenzi Mkuu wa  (EWURA), Felix Ngamlagosi alisema bei ya Petroli imeshuka sh. 31 kwa lita sawa na asilimia 1.70, Dizeli sh. 114 kwa lita sawa na asilimia 7.10 na mafuta ya taa kwa sh. 234 kwa lita sawa na asilimia 13.75 ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Alisema hapa nchini kwa sasa Petroli itauzwa Sh. 1,811, Dizeli sh. 1,486 na mafuta ya taa sh. 1,465.

Alisema kupungua kwa bei hizo kwa soko la ndani  kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.

Hata hivyo alisema hakutakuwa na mabadiliko yeyote ya bei ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga kwa mwezi huu na kwamba hiyo imetokana na kutopokea mafuta mapya kupitia Bandari ya mkoa huo katika kipindi cha Februari mwaka huu.

"Mamlaka inapenda kuujulisha umma kuwa bei hizi kikomo za mafuta kwa eneo husika zinapatikana vilevile kupitia upigaji wa simu ya mkononi kwa mitandao yote kwenda  namba  *152*00# na kisha kufuata maelekezo.


Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta zitaendelea kupangwa na soko hivyo Ewura itaendelea kutoa taarifa za bei kikomi lengo likiwa ni kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa hiyo.

Aidha amevitaka vituo vyote vya mafuta nchini na kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Alisema wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

Alibainisha kuwa wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta kwa lita na kwamba stakabadhi ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo, au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.



RAIS DKT. MAGUFULI AMLAKI RAIS MUSEVENI WA UGANDA JIJINI ARUSHA LEO

RAIS DKT. MAGUFULI AMLAKI RAIS MUSEVENI WA UGANDA JIJINI ARUSHA LEO

March 01, 2016


JAK
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati alipowasili jijini Arusha leo tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga.(PICHA NA IKULU)
MHA1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiongea na wanahabari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
MHA3 MHA5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika  mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
PICHA NA IKULU

MKUTANO MKUU WA LAPF KUFANYIKA MACHI 10-11, 2016 UKUMBI WA AICC JIJINI ARUSHA

March 01, 2016
 Viongozi meza kuu.

 Meneja Masoko na Mawasiliano Mfuko wa Pensheni wa LAPF  James Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika machi 10 na 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti.
 Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja  na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.

Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.

Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.

" LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia" alisema Mlowe.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika  kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.

Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .

Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)


GAPCO YAWAPA NEEMA WALEMAVU KATIKA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON 2016

March 01, 2016

Walemavu wakishangilia kwa pamoja na viongozi wa kampuni ya GAPCO ambao walikuwa ndiyo wadhamini mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizofanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walemavu wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Viongozi wa kampuni ya GAPCO wakiwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili toka kushoto) akiwaangalia walemavu wakitimua mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kila mmoja akionyesha ustadi wa kuendesha baskeli.
Mwanadada Linda Macha (32) ambaye aliweza kuwashinda wenzake katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Mshindi wa mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30) akishangilia mara baada ya kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10 zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshindi wa kwanza kwa mbio za walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea cheki ya Shilingi Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO, wanaomkabidhi ni Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu (anayepiga makofi toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair. Picha zote na Cathbert wa Kajunason Blog.
 WAZIRI AWAPA MOTISHA TWIGA STARS

WAZIRI AWAPA MOTISHA TWIGA STARS

March 01, 2016
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unaotarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa Machi 04, 2016 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura alipotembelea kambi ya timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.
Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji atapata gawio la shilingi laki tatu (300,000) kama motisha na kuongeza kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidia timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mchezo wa Machi 04, 2016 dhidi ya Zimbabwe utakayochezwa katika uwanja wa Chamazi.
Aliongeza kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga Special Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi.
Mwesigwa pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.
Msaada huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmoja aliyechangia shilingi milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS shilingi milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) shilingi milioni 10.

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU KWA HIYARI KUOKOA MAISHA

March 01, 2016
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
 Mfanyakazi wa Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kushoto) akimfanyia vipimo mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa hiyari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
  Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakifanyiwa vipimo katika zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akipimwa presha kabla ya kushiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki. 
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akishiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kitengo cha dharura wametoa rai kwa watanzania kujitolea kwa hiyari kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopokelewa hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwa siku mbili mwishoni mwa wiki katika eneo la Karume jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru amebainisha kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwani litasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji huo wanaopokelewa hospitalini hapo kama vile waliopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto.

“Hospitali ya Taifa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100 lakini tunafanikiwa kupata wastani wa chupa 40 hivyo kuwepo na upungufu wa chupa 60 kila siku. Hali hii inapelekea kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa dharura tu huku wengine wakisubiri.” Alisema Profesa Maseru

“Wataalamu wananiambia kuwa kwa kawaida, damu inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa takribani mwezi mzima kabla ya muda wake wa kutumika kwisha, na kutokana na uhifadhi wa damu kwa muda mfupi ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa watu kuchangia mara kwa mara.  Kitaalamu mwanamume anaweza kuchangia mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka.” Aliongezea Profesa Maseru

“Katika wakati wa kutoa huduma ya tiba ya dharura, haswa kwa wagonjwa wa ajali, watoto na wamama wajawazito, upatikanaji wa huduma ya  Ambulance na damu kwa wakati huongeza nafasi ya kuishi kwa wahitaji kwa kiasi kikubwa mno na huduma hizi huokoa maisha ya mamilioni ya wagonjwa kila mwaka duniani kote,” alisema na kumalizia, 

“Natoa rai kwa wakazi wa Dar es slaaam na Watanzania wote kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba ya damu ya kutosha, kwani asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji damu wa kujirudia Mpango wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi mahitaji ya damu nchini.”

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif, kampuni inayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa ving’amuzi kwa ajili ya matangazo ya dijitali ambao walidhamini zoezi hilo amesema kuwa hii ni mara ya pili wao kudhamini zoezi hilo kutokana na umuhimu wake katika kuokoa maisha ya watanzania wote kwa ujumla.

“Hakuna asiyefahamu katika maisha yetu yanayotuzunguka ajali zimekuwa nyingi zinazopelekea watu kupoteza maisha maelefu kubaki mejeruhi wenye uhitaji mkubwa wa damu ili kupata matibabu. Kama tunafuatilia vyombo vya habari basi tutakuwa tunasikia ni mara ngapi kwa wiki ajali zinatokea barabarani na kuacha majeruhi wengi. Kwa upande wa akina mama wajawazito wanahitaji damu kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kujifungua. 

Hatuwezi kukaa pembeni na kuwatizama wakikosa msaada wakati uwezo huo tunao.” Aliongezea Bi. Hanif


“Tumejisikia faraja sana kuwa wamojawapo wa wadau walioshiriki kufanikisha zeozi hili na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Muhimbili katika kuwahamasisha watanzania wajitokeze zaidi. 

Kwa mujibu wa wataalamu tunaweza kujitolea damu mpaka mara nne ndani ya mwaka, nina uhakika kila mtanzania akifanya hivyo basi benki yetu ya damu itajaa na tutaweza hata kusaidia wengine wan chi za jirani wenye uhitaji.” Alimalizia Makamu wa Rais kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania.

GAPCO ILIVYOWABEBA WALEMAVU KILIMANJARO MARATHONI 2016.

March 01, 2016
Washiriki wa mbio za Km 10 upande wa walemavu wakijiandaa kushiriki mbio hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya GAPCO.
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume katika mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni kwa kutumia kiti chenye magurudumu ya kusukuma kwa mikonoo kwa upande wa walemavu,Vosta Peter akihitimisha mbio hizo zilizodhaminiwa na kkampuni ya GAPCO katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake katika mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni kwa kutumia kiti chenye magurudumu ya kusukuma kwa mikono kwa upande wa walemavu,Linda Macha akihitimisha mbio hizo zilizodhaminiwa na kampuni ya GAPCO katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Washiriki wengine wa mbio hizo wakihitimisha katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akimkabidhi Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake katika mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni kwa kutumia kiti chenye magurudumu ya kusukuma kwa mikonoo kwa upande wa walemavu,Linda Macha mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi Miioni moja kutoka kwa wadhamini wa mbio hizo kampuni ya GAPCO.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akimkabidhi Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume katika mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni kwa kutumia kiti chenye magurudumu ya kusukuma kwa mikonoo kwa upande wa walemavu,Vosta Peter mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi Miioni moja kutoka kwa wadhamini wa mbio hizo kampuni ya GAPCO.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

"TIGO HALF MARATHONI" YAVUNJA REKODI YA IDADI YA WASHIRIKI .

March 01, 2016
Washiriki zaidi ya 4000 wakiwa wamejitikeza kushiriki mbio za "Tigo Half Marathoni " km 21 ikiwa ni rekodi mpya tangu kuanza kwa mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Raia wa Kigeni wakipiga serfie kabla ya kuanza mbio za Tigo Half Marathoni kwa wakimbiaji wa mbio za Km 21.
Wanariadha waloifanya vizuri katika mbio za Igombe Marathoni za mkoani Tabora waliodhaminiwa na kampuni ya Tigo wakiwa katika mavazi maalum toka kwa mdhamini wao.
Washiriki wa Mbio za Km 21 za Tigo Half Marathon wakianza mbio nje ya geti la chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Mrembo wa Tanzania mwaka 2004 Faraja Kota pia laikuwa ni miongoni mwa wakimbiaji walioshiriki mbio za Km 21.
Wakimbiaji wa timu ya Taifa ya riadha ya Tanzania walioshiriki mbio za Km 21 wakifarijiana,wanariadha hao walitumia mbio hizo kama sehemu ya mazoezi
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania RT Anthony Mtaka akizungumza jambo na msatahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Raymond Mboya,katikati ni mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga.
Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 21 ,Grace Kimanzi raia wa Kenya akimaliza mbio katika uwanja wa c huo kikuu cha Ushirika.
Mshindi wa kwanza wa  mbio za Km 21 upande wa wanawake Grace Kimanzi  akitoka katika eneo la kukimbilia mara baada ya kumaliza mbio hizo,
Mshindi wa tatu  katika mbio za Kilimanjaro Marathoni ,Km 21 upande wa wanawake Failuna Abdi akipewa msaada na mkurugenzi wa mbio hizo John Bayo na baadae kuwekwa katika kiti cha kubebea watu wenye matatizo muda mfupi baada ya kualiza mbio hizo .
Washiriki wa mbio za Km 21 upande wa wanaake ,nafasi ya kwanza hadi ya 10 wakiwa katika jukwaa kungojea kupokea zawadi toka kwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi katika mbio hizo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipeana mkono na mmoja wa washiriki wa Mbio hizo .
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Severine Kahitwa akipeana mkono na mwanariadha wa Tanzania ,Fabian wakati wa zoezi la utoaji zawadi kwa washindi.
 Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akikabidhi mfano wa hundi kwa washindi wa mbio hizo.
Washiriki wa mbio hizo wa nafasi ya kwanza hadi ya kumi wakiwa katika picha yi a pamoja na mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye.
Waziri Nape Nnauye akitoa mfano wa hundi kwa washindi wa mbio hizo upande wa wanawake.
Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo George Lugata akibadilishana mawazo na mmoja wa maofisa wa kampuni hiyo walipokutana uwanjani hapo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wa zamani,Mohamed Babu (kushoto) akizungumza jambo na mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Uhuru Expedition ,Joseph Kitani kabla ya kuanza kwa mbio hizo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kasakazini.