VIJANA WASOMI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KULILETEA TAIFA MAENDELEO

November 26, 2017
 Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Amina Sanga akitoa mada kwenye kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark jijini Dar es Salaam jana lenye lengo wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.
 Vijana wasomi wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
 Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Muonekano wa ukumbi katika kongamano hilo.
 Meza kuu katika kongamano hilo. Kutoka kulia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Philip Sanga, Mgeni rasmi wa Kongamano hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila , Mchungaji John Kanafunzi na Mratibu wa kongamano hilo, Ephraim Mwambapa.  
 Wanakwaya wa Haleluya Celebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu.
 Burudani ikiendelea.
Maombi yakifanyika.
Waratibu wa kongamano hilo wakijitambulisha. Kutoka kushoto ni Sarafina Kabwe, Irene Sadock, Michael Mhagama na Yona Kilindu.
Katibu Mkuu  wa Kongamano hilo, Lendian Bigoli, akitoa mada.
Mratibu wa Kongamano hilo, Ephraim Mwambapa akitoa mada katika kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk.Philip Sanga akihutubia kwenye kongamano hilo.
Mgeni rasmi wa kongamano hilo,Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na waratibu wa kongamano hilo.
Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Abundant Bressing Centre (ABC), Flaston Ndabila amewataka Vijana wasomi na wanataalumu nchini kumsaidia Rais Dk.John Magufuli kuliletea Taifa maendeleo.

Ndabila ametoa mwito huo jijini Dar es Salaam jana wakati akiwahutubia wasomi wanataaluma katika kongamano la siku moja la vijana wasomi kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo lilifanyika Hoteli ya Landmark lenye lengo kwa wasomi hao kutumia taaluma walizonazo katika kuitumikia jamii na taifa kwa ujumla.

"Ninyi wasomi mmesomeshwa kwa ajili ya kuwatumia wananchi na taifa msaidieni Rais wetu John Magufuli kuliletea taifa la Tanzania na kanisa maendeleo kwani hakuna mtu mwingine tunaye mtegemea zaidi yenu" alisema Askofu Ndabila.

WAZIRI MHAGAMA AITAKA HALMASHAURI YA BAHI KUKAMILISHA UJENZI WA SOKO LA KIGWE

November 26, 2017


Na. MWANDISHI WETU – DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.

“Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko hili”.

Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.

“Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel

Kwa upande wake mkazi wa Kigwe Bi.Anastazia Mkatato alieleza kuwa kujengwa kwa soko hilo litatatua changamoto iliyopo ya kukosa soko la kudumu kwani yaliyopo ni madogo yanayomilikiwa na watu binafsi.

“Ninaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini iliyoamua kutujengea soko hapa Kigwe na hii itatupa nafasi ya kuuza mazao na bidhaa kwa wingi kupelekea kukuza uchumi wetu.”Alieleza Anastazia.

Naye Mratibu wa Mradi Taifa Bw.Walter Swai alieleza kuwa soko hili ni muhimu kwa wana Kigwe na maeneo jirani , hivyo tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha vifaa vinawekwa ikiwemo Meza za kuuzia mbidhaa sokoni.

“Tayari Ofisi yangu itachukua changamoto hii ya kukosekana kwa meza za kuuzia na kuitatua ndani ya mwezi mmoja hivyo niwaahidi kutekeleza haya.”Alisisitiza Bw.Swai

Ujenzi wa soko la Kigwe umegharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 68 ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ilitoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 50 pamoja na Mfuko wa jimbo kuchangia jumla ya shilingi Milioni 15. Dhumuni la mradi ni kuwa na eneo rasmi la kufanyia biashara na kuwezesha wajasiliamali wa Kigwe na kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleao yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kigwe alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe Lililopo Bahi Dodoma.

DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017

November 26, 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakiwaonyesha waandishi wa habari, tuzo ambayo PSPF ilinyakua katika mashindano ya kimataifa wakati wa mkutano wa taasisi ya hifadhi ya jamii Duniani, International social security association, taasisi tanzu ya ILO, tuzo ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017 mjini Adis Ababa Ethiopia mwezi uliopita. Tukio hili limefanyika pembezoni mwa mkutano wa kampeni ya uzalendo na utaifa iliyoongozwa na waziri Mwakyembe kwenye ukumbi wa mikutano wa PSPF jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umenyakua tuzo ya kimataifa yaISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017, baada ya kuwa Mfuko unaotoa huduma bora kupitia ubunifu wa mafao ya muda mfupi, yaani service quality in short-term products.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuonyesha tuzo hiyo iliyokwenda sambamba na kampeni ya uzalendo na utaifa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu alisema, Mfuko huo unajivunia kwa kuwa Mfuko wa kwanza miongoni mwa Mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii nchini, kuanzisha bidhaa na huduma za muda mfupi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na hivyo kuvutia mifuko mingine ambayo kwa sasa nayo imeanza kutoa huduma hizo.

“Mwaka huu katika mkutano wake wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani yaani International Social Security Association, taasisi tanzu ya Shirika la Kazi Duniani,(ILO) imeipatia PSPF tuzo baada ya kuwa Mfuko bora barani Afrika katika utoaji huduma bora kupitia ubunifu wa Mafao ya muda mfupi yaani service quality kwenye short-term products.” Alifafanua Bw. Mayingu.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliipongeza PSPF kwa kujinyakulia tuzo hiyo na kuliletea taifa heshima kubwa kimataifa.

“Kupambanishwa katika bara la Afrika na kushinda vigezo kadhaa ndipo unaambiwa bwana wewe unapata hii tuzo na tuzo hii imetolewa na taasisi yenye ushirikiano wa karibu sana na ILO hongereni sana.” Alipongeza Dkt. Mwakyembe.

Alisema ushirikiano wa karibu miongoni mwa wafanyakazi wa PSPF ndio umepelekea mafanikio hayo.

“Niwapongeze viongozi wote wa PSPF, Wafanyakazi wote wa PSPF, kwa kazi nzuri mnayoifanya mpaka mnatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.” Alisema.


Aidha kabla ya tukio hilo, Waziri aliwahamasisha watanzania kujenga moyo wa uzalendo na kujivunia utaifa wao kwani mambo hayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa.


“Sisi tuliokuwepo kabla ya uhuru, niwaombe sana, tuwasaidie vijana wetu wa sasa kutambua tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi, kwa kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yetu kama ambavyo ilikuwa hapo awali.” Alisema.

Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muunganmo wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao mjini Dodoma, na Waziri aliwahamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia fedha ili kufanikisha swala hilo muhimu kwa taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyemba, akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kiujenga uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Leah Kilimbi, akizungumzia maudhui ya hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. ASdam Mayingu, akizunhgumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakayti wa hafla hiyo.
Josephine Kulwa, akimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw.Sami Khalfan, wakifuatilia hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa DAWASA, Bi. Nelly Msuya akizungumza kwenye hafla hiyo.