RAIS DKT. MAGUFULI NA MWENYEJI WAKE RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI WAWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA KATIKA WILAYA YA KYOTERA MUTUKULA NCHINI UGANDA

RAIS DKT. MAGUFULI NA MWENYEJI WAKE RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI WAWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA KATIKA WILAYA YA KYOTERA MUTUKULA NCHINI UGANDA

November 09, 2017

1.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na kupongezana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka Hoima nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani Tanga. Sherehe za uwekaji wa jiwe hilo zimefanyika katika eneo la Mutukula Wilayani Kyotera nchini Uganda
1 2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maelezo ya namna ya bomba hilo la mafuta ghafi litakavyojengwa na kuanza kufanyakazi.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta wakijadiliana jambo mara baada ya kupewa maelezo ya mradi huo mkubwa wa bomba la mafuta ghafi.
4
hilo la Ufunguzi la Ujenzi wa Bomba hilo la Mafuta ghafi
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiondoka katika eneo la Mutukula mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la bomba la mafuta.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia ngoma za asili za  watoto wa Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo huku Rais wa Uganda Yoweri Musevini akitazama watoto hao.
15
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakizungumza na mamia ya wananchi hawaonekani pichani katika eneo la Kyatera nchini Uganda mara baada ya ufunguzi wa Bomba la Mafuta. PICHA NA IKULU

WATU MILIONI 126 KUAJIRIWA NA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA KUFIKIA 2024

November 09, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Usafiri wa anga ni miongoni mwa sekta inayochangia ukuaji wa uchumi wa dunia kwa kiasi kikubwa. Ilichangia moja kwa moja kiasi cha dola za Kimarekani trilioni 2.2 ya Pato la Taifa (GDP) la dunia (sawa na 10% ya uchumi wa dunia) mwaka 2015 na kutoa ajira kwa zaidi ya watu milioni 108 duniani kote. Kufikia mwaka 2024, Baraza la Dunia la Utalii na Usafiri linatarajia ajira za moja kwa moja kwenye sekta ya utalii kuwa zaidi ya watu milioni 126 duniani kote.

Ukiachana na mchango wa usafiri wa anga kwenye sekta nyingine pia ina umuhimu mkubwa kwenye utalii. Zaidi ya 54% ya watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani husafiri kwa kutumia usafiri wa anga. Jumia Travel inatambua kwamba utalii ni sekta muhimu kwa nchi nyingi za Afrika, ambapo ni nyanja muhimu katika mikakati ya ukuaji wa uchumi.

Barani Afrika, inakadiriwa kwamba takribani watu milioni 5.8 huajiriwa kwenye maeneo ambayo hupokea wageni wengi kutoka nje ya nchi, hususani wanaoingia kwa kutumia usafiri wa anga, na ilichangia dola za Kimarekani bilioni 46 ya Pato la Taifa katika uchumi wa nchi za Kiafrika kwa mwaka 2014.
Utalii kama sekta nyinginezo za huduma inaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuunga mkono ukuaji wa uchumi endelevu. Ikikuzwa kwenye namna ya uwajibikaji na mikakati mizuri, utalii unaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira huku ikitunza na kuenzi rasilimali zetu bila ya kuziharibu.

Ingawa, kuna umuhimu mkubwa kwa sekta binafsi na serikali kukaa kwa pamoja na kujadiliana. Lengo ni kuhakikisha mipango ya maendeleo ya sekta hii inafanywa kwa kuzingatia utunzwaji wa mazingira, ustawi wa jamii pamoja na faida za kiuchumi inazoweza kuzileta.

Katika serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania ikiwa chini ya uongozi wa Mh. John Pombe Magufuli tumeshuhudia jitihada kubwa katika ukuzaji wa sekta ya usafiri wa anga. Jitihada hizo ni pamoja na manunuzi ya ndege za abiria, upanuzi wa viwanja vya ndege na maboresho kadhaa kwenye wizara husika kwa ujumla.
Hivi karibuni Rais Magufuli akiwa katika ziara yake ya kikazi Kagera alizindua uwanja wa ndege ambao si tu utaongeza fursa za kiuchumi mkoani humo bali pia utaufungua mkoa huo kiutalii. Majengo ya uwanja huo ni ya tatu kwa uzuri baada ya Dar es Salaam na Kilimanjaro.

DC NZEGA ASEMA SAYANSI NA TEKNOLOJIA HAIKWEPEKI KATIKA KILIMO

November 09, 2017
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Shila Wilayani Nzega mkoani Tabora wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kwenye shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo leo. Shule hiyo ni shule pekee wilayani humo kupata bahati ya kuanzisha shamba hilo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mihogo Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngapula kwa ajili ya kupandwa katika mashamba darasa katika uzinduzi wa mashamba hayo ya mbegu wilayani humo leo. 
 Wanafunzi wa Shule ya Shila wakiwa shambani wakati wa uzinduzi wa shamaba darasa hilo.
 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo uliofanyika katika Wilaya hiyo Shule ya Msingi, Shila.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielezea ubora wa mbegu ya mihogo iliyofanyiwa utafiti kabla ya uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya Msingi ya Shila.
 Kaimu Ofisa Ugani wa Halmshauri ya Wilaya ya Nzega, Hassan Mtomekela akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akielekeza jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo hiyo kiutaalamu.
 Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibura, akimuonesha mbegu hiyo mkuu wa wilaya hiyo.

DKT MWANJELWA: SERIKALI KUFANIKISHA UWEPO WA SOKO LA BIDHAA (COMMUNITY EXCHANGE)

November 09, 2017
Na Mathias Canal, Dodoma
Serikali inaendelea na mchakato wa kufanikisha uwepo wa Mfumo wa soko la bidhaa (Commodity Exchange) ambapo miongoni mwa kazi za Mfumo huo utalenga kupunguza gharama za uendeshaji wa masoko ya mazao yote ya chakula na biashara ili kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri na yenye tija.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa Bungeni Mjini Dodoma Wakati akijibu swali la Mbunge wa Lulindi Mkoani  Mtwara Mhe JEROME DISMAS BWANAUSI aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanzisha mfumo wa “Commodity Exchange” ili kuwasaidia wananchi wanaolima Korosho kupata bei nzuri katika misimu husika.
Mhe Naibu Waziri alisema kuwa Maandalizi ya Soko la Bidhaa (Commodity Exchange) yalianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kufanya biashara ya mazao kuwa ya wazi na yenye ushindani kulingana na nguvu ya soko.
Mhe Mwanjelwa alizitaja hatua ambazo zimechukuliwa na serikali mpaka hivi sasa kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa Waraka wa Soko hilo, Kuundwa kwa Bodi ya Soko, kutungwa kwa Sheria ya mwaka 2015 ya Soko la Bidhaa pamoja na kanuni zake, Kufanya uzinduzi wa kuanzisha Soko hilo, Kutoa mafunzo kwa Madalali watakaoendesha soko hilo na Kutoa mafunzo kwa baadhi ya viongozi wa Serikali na Sekta Binafsi ili kujenga uelewa wa pamoja.
Alisema, Ofisi na Jukwaa la soko hilo vimefunguliwa katika jengo la LAPF lililoko Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo kazi za uwekaji wa vifaa katika Ofisi na Jukwaa hilo zinaendelea. 
Mhe Mwanjelwa alisema, Elimu ya Soko la Bidhaa inaendelea kutolewa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za Mkoa na Wilaya na Maafisa Kilimo, Ushirika, Biashara na Maendeleo ya Jamii katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Dodoma na Singida.
Aidha, elimu hiyo imekwisha kutolewa kwa Viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Viongozi wa Vyama vya Msingi na Vyama visivyokuwa vya Kiserikali ili kujenga uelewa wa soko hilo. Pia, elimu itaendelea kutolewa kwa wakulima na wananchi kwa ujumla ili wadau waufahamu mfumo huo wa soko.

DC SHINYANGA AFANYA ZIARA KUSIKILIZA KERO SHINYANGA VIJIJINI,WANANCHI WACHARUKA WATAKA AONDOKE NA VIONGOZI WA KIJIJI

November 09, 2017
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefanya ziara ya kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi katika kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo na Solwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Shinyanga vijijini).

LUSINDE AUWASHA MOTO KOROGWE UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI AWATAKA WANANCHI KUMPA KURA ZA KISHINDO MGOMBEA WA CCM

November 09, 2017
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde  akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM kwani ndiye ambaye anaweza kuwapa maendeleo kwa haraka zaidi
 Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde  akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde kushoto akimnadi mgombea udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduizi (CCM) Mustapha Shengwatu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba sokoni wilayani humo
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji

Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini,Nassoro Hemedi Malingumu akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini Emanuel Charles akizungumza katika mkutano huo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hizo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi wa Kata ya Majengo kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kushirikiana naye kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi zaidi
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuhakikisha hawafanyi makosa kwa kumpa kura nyingi za kutosha mgombea udiwani wa CCM kwani dhamira yake ni kuhakikisha anawapatia maendeleo kwa kiwango kikubwa
Katibu wa CCM Korogwe Mjini Ally Issa Ally akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo katika Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustapha Shengwatu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni 

 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi katikati akifuatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda na kushoto ni Mgombea Udiwani wa CCM Mustapha Shengwatu
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi huo katikati anayeshughudia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda

Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji akisalimiana na makada wa CCM mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni  wakati wa uzinduzi huo kampeni za mgombea Udiwani kupitia chama hicho kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji katikati akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Tanga kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kulia ni Katibu wa CCM Korogwe Mjini,Ally Issa Ally na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakiingia uwanja wa Sabasaba sokoni tayari kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa CCM Kata ya Majengo
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu kushoto akifuatilia kwa umakini hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde alimaarufu Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mjini huku akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM
 Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia kampeni hizo

BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA BILIONI 340 KUENDELEZA UTALII UKANDA WA KUSINI

November 09, 2017
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird, wakielekea kusaini Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Katibu Mkuu Wizara ya maliaasili na Utalii( wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya Ujumbe wa Benki ya Dunia walioshiriki tukio la Tanzania na Benki hiyo kutiliana saini mkataba wa mkopo  nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, akitoa neon la shukurani wakati wa kusainiwa kwa Mkataba wa Mkopo Nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola  za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi. Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, huku Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kulia waliosimama-tai nyekundu) akishuhudia, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kulia waliosimama akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi, Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakionesha Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, baada ya kusainiwa katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)​

Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 150, sawa na takriban Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.

Mkataba wa mkopo huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi, Bi. Bella Bird.

Bw. James alisema kuwa mkopo huo umelenga kuimarisha miundombinu ya utalii katika ukanda huo wa kusini ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, madaraja pamoja na kuibua fursa nyingi za utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi.

Alisema pia kwamba mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wananchi wanaozunguka maeneo ya utalii kwa kuanzisha miradi itakayo chochea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuendeleza uhifadhi katika maeneo yao.