MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAELFU KATIKA MAZISHI YA WATU SITA WA FAMILIA MOJA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO

February 10, 2015

 Mama mzazi wa Kapteni David Mpila akiweka udongo katika kaburi la mtoto wake marehemu David Mpila leo wakati wa mazishi ya watu sita waliokufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia Februari 7.
 Waombeleji wakielekea makaburini.
 Baadhi ya watu wakielekea makaburini.
 Wanafamilia wakiwa na huzuni baada ya miili kuwasili nyumbani
 Miili ikiwasili nyumbani.
 Miili ikiombewa nyumbani kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
 Mpumzike kwa amani.
  Makamu wa rais, Dk. Mohamed Ghalib Bilali akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyokuwa na miili ya watu sita wa familia moja waliofariki kwa ajali ya moto.
Mofisa wa Jeshi la wananchi wa tanzania (JWTZ) wakitoa heshima za mwisho.

Majeneza yenye miili ya watu sita wa familia moja waliofariki kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto eneo la Kipunguni ‘A’ jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Februari 7, ambao walizikwa katika makaburi ya Airwing Ukonga, Dar es Salaam leo.

 Tutawakumbuka daima......
 Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba moja ya jeneza la marehemu waliofariki katika ajali ya moto wakati wa mazishi yao.
 Fatuma Issa ambaye ni mama wa watoto wawili waliofariki katika ajali hiyo akiweka udongo katika makaburi la watoto wake.
 Mtoto pekee aliyenusurika katika ajali hiyo, Emmanuel mpila akiweka udongo katika kaburi la baba yake, Kapteni mstaafu wa JWTZ, David Mpila.
 Mama mzazi wa Kapteni David Mpila akiweka shada la maua.
 Fatuma Issa akiweka shada la maua katika makaburi ya watoto wake Celina na Pauline.
 Mama wa watoto wawili waliofariki katika ajali ya moto, Fatuma Issa akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake, Celina.
 Emmanuel Mpila akiweka shada la maua katika kaburi la mototo wake, Pauline, Emmanuel alipoteza wa toto wawili katika ajali hiyo.

 Baba wa watoto wawili waliokufa katika ajali ya moto, Emmanuel Mpila akiweka shada la maua katika kaburi la mmoja wa watoto wake, Pauline
.

 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiweka shada la maua.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiweka shada la maua.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiweka shada la maua.
 Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani akiweka shada la maua.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwenye majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto nyumbani kwao Kipunguni, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga              Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika leo Februari 10,2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.  
MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR YAFANYIKA LEO

MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR YAFANYIKA LEO

February 10, 2015


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Mwaka wa Sheria kama ishara ya uzinduzi wa kitabu hicho samba samba na maadhimishoya siku ya Sheria Zanzibar(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary(wa pili kushoto) ,[Picha na Ikulu.] sh2 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mohamed Othman Chande (mbele) wakiongoza maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] sh3Mahakimu na Wanasheria wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha siku ya Sheria Zanzibar sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] sh4  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar katika kilele cha siku ya Sheria Zanzibar(katikati) Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary,[Picha na Ikulu.] sh5 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Jaji Mkuu wa Mahakama kuu Tanzania Shaaban Ally Lila (kushoto) alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Zanzibar katika kilele cha siku ya Sheria Zanzibar(katikati) Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary,[Picha na Ikulu.]
sh6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abibakar Khamis Bakary wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.] sh7 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu alipokuwa akisema machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ali azungumze na Wananchi, Mahakimu na Wanasheria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.] sh8 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu baada ya kikizindua kitabu cha Mwaka wa Sheria leo katika Sherehe za Siku ya Sheria zilizofanyika  viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.] sh9 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati  wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande (kushoto) na Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary.[Picha na Ikulu.]

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF

February 10, 2015
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliketi jana Jumapili tarehe 08 Februari, 2015 katika kikao chake cha kawaida.  Pamoja na kujadili maandalizi ya Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika Machi 14 na 15 mjini Singida, Kamati ilijadili na kuamua yafuatayo:-

1.   Zoezi la utoaji leseni kwa vilabu litaanza kabla ya msimu wa ligi 2015/16.  Vilabu vitatumiwa fomu za maombi mapema iwezekanavyo ili viweke nyumba zao sawa na kuleta maombi.  Leseni za vilabu (club licence) ni agizo la CAF na FIFA katika kuhakikisha vilabu vinaendeshwa kwa weredi.  Baadhi ya maeneo yanayoagaliwa katika utoaji wa leseni ni pamoja na kuwepo kwa Sekretarieti, miundo mbinu ya mazoezi na mashindano, hadhi za kisheria (legal status) mikataba ya ajira n.k.

2.   Kamati ya Utendaji imeazimia kufanyika kwa mashindano ya Taifa Cup kwa upande wa wanaume.  Sekretarieti ya TFF imetakiwa kufanya juhudi ili mashindao hayo yaweze kufanyika.

3.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetoa pongezi kwa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) kwa juhudi zake za kukuza soka la vijana kupitia mradi wake wa kuanzisha shule ya soka (Academy) kwa ushirikiano na klabu ya Real Madrid ya Hispania.  Aidha Kamati ya Utendaji ya TFF imeipongeza Kampuni ya Symbion na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa juhudi zao za kuchangia maendeleo ya soka la vijana na mpira wa miguu kwa ujumla ikiwa ni kupitia mpango wa kujenga shule ya soka (academy) uwezeshaji wa mashindano ya vijana chini ya miaka 13 (U-13) yatakayofanyika mwezi April, 2015 mjini Mwanza na ujenzi wa miundo mbinu ya soka na michezo kwa ujumla.

Kamati ya Utendaji imewaomba wadau wengine kufuata mifano hiyo na kuchangia maendeleo ya soka kwani kazi hii inategemeana ni kwa faida ya wadau mbali mbali.

4.   Kamati ya Utendaji ilipokea mabadiliko ya uwakilishi wa Chama cha Soka la Wanawake nchini (TWFA) yaliyotokana na kuondoka kwa Bi. Lina Kessy aliyekuwa Mwenyekiti wake.  Bi. Lina ameajiriwa kama Afisa michezo wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia.  Nafasi ya Mwenyekiti inachukuliwa na Bi. Rose Kisiwa ambaye hapo kabla alikuwa Makamu Mwenyekiti wa TWFA ataendelea kuwa Mwenyekiti mpaka hapo utakapokaa Mkutano Mkuu wa kawaida wa TWFA.

5.   Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kuwepo kwa vitendo vya vurugu na utovu wa nidhamu katika mashindano mbalimbali yanayoendelea nchini.  TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu hususani viongozi wa vilabu kutilia mkazo elimu ya kujitambua ili wachezaji wajue kuwa wao ni hazina ya Taifa na kioo (taswira) cha jamii, hivyo waepuke vitendo vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.  Vitendo hivi si tu vinakwamisha maendeleo, bali pia vinawadharirisha wao, mpira wa miguu na jamii kwa ujumla.

Kufuatia matukio ya hivi karibuni na kuzingatia umuhimu wa kushughulikia masuala ya kinidhamu kwa haraka na weredi, Kamati ya Utendaji imeteua ya Kamati ya kuangalia na kusimamia kanuni za uendeshaji Ligi. Kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Bodi ya Ligi, Kurugenzi ya mashindano, Kamati ya mashindano na kamati ya waamuzi.

                                                                                              
TFF YATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA FIF
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Sidy Diallo wa Shirikisho la soka nchini Ivory  Coast (FIF) kwa kutwaa Ubingwa wa Mataifa Afrika.
Katika salam zake Bw. Malinzi amesema mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa wa Afrika yametokana na juhudi za Rais huyo pamoja na Kamati yake ya Utendaji.
Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi Shirikisho la mpira wa Miguu la Ivory Coast kwa kutwaa Ubingwa huo wa Afrika kwa mara pili.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa Rais Mohamed Gamal wa Chama cha mpira wa miguu nchnii Misri (EFA ),kufuatia vifo vya mashabiki vilivyotokea mwishoni wa wiki katika mchezo uliowakutanisha  Zamalek na ENPPI.
Mashabiki wapatao ishirini na moja (22)  wameripotiwa kupoteza maisha katika vurugu hizo zilizowahusisha mashabiki wa Zamalek na ENPPI na kupelekea Shirikisho la Soka nchini Misri kuisimamisha michezo ya Ligi nchini humo.
Katika salam zake, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewaomba wapenzi wa soka nchini Misri kuwa wavumilivu  katika kipindi hiki cha maombelezo ya vifo vya mashabiki hao.

TFF YAIPONGEZA CAF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Bw Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Bw Issa Hayatou kwa kufanikiwa kuandaa salama fainali za Mataifa Afika nchini  Equatorial Guinea bila ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
Katika salamu hizo kwenda kwa Bw Haytou na nakala yake kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Bw Hicham El Amrani, Bw Malinzi amesema kwa pamoja analipongeza Shirikisho hilo na wenyeji wa michuano kwa kufanikiwa kuandaa mashindano hayo na kumalizika salama.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA LINDI KUTOKUBALI KUUZA MAENEO YA UFUKWE WA BAHARI KWA BEI YA CHINIYA

MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA WILAYA YA LINDI KUTOKUBALI KUUZA MAENEO YA UFUKWE WA BAHARI KWA BEI YA CHINIYA

February 10, 2015

index 
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutokubali kuuza maeneo ya ufukwe wa Bahari  ya Hindi kwa kiasi kidogo cha fedha  kwani thamani ya maeneo hayo ni kubwa.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa rai hiyo jana wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya Raha leo na Ufukoni yaliyopo katika kata ya Rahaleo wilayani humo.
Alisema hivi sasa kuna wageni wengi ambao wanaenda kwa wananchi na kununua maeneo ya ufukweni kwa bei ya chini lakini kama wamiliki wa maeneo hayo watakuwa na subira watayauza  kwa bei kubwa  kwa kipindi cha  miaka michache ijayo.
“Baada ya miaka michache ijayo mkoa wetu  utakuwa tofauti kimaendeleo,  Serikali inampango wa kujenga mji wa kisasa katika eneo la  Mitwero.
“Nawasihi hata kama mtu anashida kiasi gani atafute njia nyingine ya kupata fedha lakini siyo kuuza eneo la ufukweni kwa bei ndogo,  kama kuna aliyebakiza eneo lake asiuze  kwani kimfaacho mtu ni chake”, alisisitiza Mama Kikwete .
Kuhusu elimu MNEC huyo aliwasihi viongozi hao kusimamia elimu ya watoto wao na kuwahimiza waende shule  kwani wakiwa na elimu wataweza kufanya kazi za kitaalamu katika sekta mbalimbali ikiwemo ya gesi inayopatikana mkoani humo.
Kwa upande wa wanawake aliwahimiza kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi  mkuu ujao na hivyo  kufika katika ngazi ya maamuzi  pia kwa kufanya hivyo hawatapoteza haki yao ya msingi ya kuchaguliwa.
Akiwasalimia viongozi hao Mkuu wa wilaya ya Lindi Dkt. Nassoro Hamidi alisema shule za Sekondari zimefunguliwa lakini  wanafunzi walioripoti shuleni ni wachache  na kuwaomba kupita nyumba hadi nyumba kuwahamasisha wazazi wawapeleke watoto wao shule kwani bila ya elimu hakuna maendeleo.
“Serikali ilitoa agizo  kama watoto hawana ada au nguo za shule waende hivyo hivyo kuanza masomo mambo mengine yatafuata baadaye lakini hadi sasa bado idadi ya wanafunzi walioripoti shuleni ni ndogo”, alisema Dkt. Hamidi.
Kuhusu wananchi kujitolea katika ujenzi wa maabara aliwasihi viongozi kuwahimiza kushiriki  katika ujenzi na maabara hizo ziweze kukamilika kwa wakati  ili watoto wajifunze masomo ya sayansi kwa vitendo.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 . Hadi sasa ameshatembelea matawi 64 kati ya  82 yaliyopo wilayani humo.
VIONGOZI WA KANISA LA ANGLICAN WATEMBELA SHAMBA LA WAZIRI MKUU ZUZU DODOMA KUJIFUNZA KILIMO BORA CHA ZABIBU NA EMBE

VIONGOZI WA KANISA LA ANGLICAN WATEMBELA SHAMBA LA WAZIRI MKUU ZUZU DODOMA KUJIFUNZA KILIMO BORA CHA ZABIBU NA EMBE

February 10, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea malisho ya ng’ombe  kwenye shamba lake  lililopo  Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ANGLI4 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba lake la zabibu lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (wapili kushoto) na  kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ANGLICAN1

MBUNGE WA MOROGORO MJINI AWASHANGAZA WAKAZI WA MOROGORO

February 10, 2015


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akisalimiana na wakazi wa Mitaa ya  Kata ya Kichangani manipaa ya Morogoro Katika Mfurulizo wa Ziara zake anazofanya katika kata Zote za Jimbi hilo kwa lengo la Kusikiliza Kero za wananchi wa Jimbo hilo .Katika Hali isiyo ya kawaida Mh Abood Amewashangaza wakazi wa Kata ya Kichangani Pale alipokataa Kuitwa  Mheshimiwa ,Mbunge huyo aliwataka wakazi hao Kumwita Mtumishi.Akilezea Zaidi Mh Abood alisema Namnukuu “Jina Mheshimiwa  Ninaitwa tu nikiwa Bungeni Lakini Nikija Kwenu Msiniite Mheshimiwa bali Mniite Mtumishi Wetu Amekuja” Wakazi hao walishangazwa na hali hiyo na kuishia kusema Tangu Uhuru Katika Wabunge wote waliowahi kuliongoza Jimbo Hilo Hakujawahi Kutokea Mbunge Kama Huyu Maana anawajali ,anawasikiliza na Ameshatatua kero Kubwa zilizokuwa zinawakabili kama Maji,Zahanati,Barabara pamoja na kuwasomesha Watoto wengi Yatima na watoto ambao wazazi wao wana maisha Duni.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Amezungukwa na wakazi wa Mitaa ya Area Six A na B Kata ya Kichangani alipofika kuwasikiliza kuhusu Kero Mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata hiyo.Wakazi hao walimweleza Mh Abood  kuwa Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara za Mitaa.Kuhusu Maji Mh. Abood Aliwajibu Anapambana Usiku na Mchana kutatua Kero hiyo kwa Kushirikiana na Idara ya Maji mkoa wa Morogoro. Kwa Juhudi zake Mwenyewe Ameshachimba visima Karibu Kila Kata Vyenye thamani ya Karibu shilingi  Milioni 550.Na Bado anaendelea Kutumia Kila Mbinu kuhakikisha wakazi hao wanapata Maji safi na salama. Alitoa Shilingi Milion 1 kwajili  ya Kununua Mafuta Kuwasha Mitambo ya Kuchonga Barabara za Mitaa
hiyo. 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh. Aziz Abood akiongea na Mtoto Mdogo wakti wa Ziara yake aliyoifanya kata ya Kichanagani
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akishiriki kukaanga Samaki 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiwa Meza Kuu na wenyeviti wa Mitaa ya Koal A na B Kata ya Kichangani waliojitokeza Kwenye ziara hiyo Ambapo walipewa nafasi ya Kuwasalimia wananchi  na kuishia Kumsifia Mbunge huyo kwa Kumwita Ni jembe Lililo Makini na Kuwaasa wakazi wa Jimbo hilo Kuunga Mkono katika Shuguli zake Pia walimuahidi Mh Abood Kushirikiana nae bega kwa bega katika Kuwaletea wakazi wa Morogoro Maendeleo.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA TFF

February 10, 2015
                                                                                              
KAMATI YA NIDHAMU YAWAADHIBU BEKI WA SHOOTING
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia mechi tatu beki George Michael Osei wa Ruvu Shooting kutokana na makosa ya kinidhamu aliyoyafanya akiwa uwanjani.

Osei ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumkaba na kumchezea kibabe mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe ambapo ni kinyume na mchezo wa kiungwana (fair play) ameadhibiwa kwa kuzingatia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.

Mlalamikiwa alifika mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.

Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema Osei alipopewa nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo na kudai magazeti yametengeneza picha hizo. TFF iliwasilisha ushahidi wa magazeti mawili ya Championi na moja la The Guardian kwa kuzingatia  Ibara ya 96(3) ya Kanuni ya Nidhamu ya TFF Toleo la 2012.

Katika uamuzi wake, Kamati imesema kitendo cha Osei ni kinyume na kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair play), na kuongeza kuwa kanuni za TFF kwa makosa kama hayo ni dhaifu, hivyo kuagiza zirekebishwe ili ziweze kuwa kali zaidi.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo, imetupa malalamiko yaliyowasilishwa na TFF dhidi Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona, na Katibu wa Simiyu (SIFA), Emmanuel Sorogo.

Kwa upande wa Sorogo, Kamati imesema baada ya kupitia vielelezo vya pande zote, hasa upande mlalamikiwa imeridhika kuwa hakushiriki katika kumpiga refa kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake kati ya Shinyanga na Simiyu.

Badala yake aliyehusika ni Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye tayari uongozi umeshachukua hatua dhidi yake kwa kumsimamisha kwanza wakati akisubiri kufikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya SIFA.

Pia barua ya kumsimamisha kocha huyo ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa TFF na Mkurugenzi wa Mashindano. Kamati imeyachukulia maneno ya mlalamikiwa kuwa ni sahihi ndiyo maana hayakupingwa na TFF, hivyo malalamiko dhidi ya mlalamikiwa hayana msingi na yametupwa.

Kwa upande wa Galibona ambaye ripoti za Kamishna na refa zilionyesha kuwa alishiriki kuhamasisha marefa kupigwa baada ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Polisi Mara FC na Mwadui FC, Kamati imesema mlalamikiwa aliwasilisha vielelezo vinne kuthibitisha kuwa hakuhusika.

Kamati imesema licha ya ripoti ya Saleh Mang'ola kumtaja Galibona, lakini maelezo ya refa huyo na msaidizi wake Rebecca Mulokozi waliyoandika Kituo cha Polisi baada ya tukio hilo hayakumtaja mlalamikiwa mahali popote.

Pia barua ya FAM kwenda TFF kuhusu matukio ya mechi hiyo yanamtoa hatiani mlalamikiwa, hivyo Kamati imeamuru kuwa malalamiko dhidi ya Galibona hayana msingi na yametupiliwa mbali.

KIONGOZI VILLA SQUAD APIGWA FAINI 600,000/-
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. 600,000 au kifungo cha mwaka mmoja Katibu Mkuu wa Villa Squad, Mbarouk Kassanda kwa kusika na uhamisho wa mchezaji Omari Ramadhan ambao haukufuata kanuni za usajili.

Villa Squad iliingiza majina tofauti ya mchezaji huyo wa African Lyon, ambapo badala ya Omari Ramadhan ikaingiza Omari Issa Ibrahim'. Kamati imeona Villa Squad ilifanya hivyo ili kudanganya, kuwezesha mfumo wa usajili wa kielektroniki ukubali jina la mchezaji.

Malalamiko ya kutaka kupewa pointi tatu na mabao matatu kwenye mechi dhidi ya Villa Squad kwa kumchezesha mchezaji huyo, yametupwa na Kamati kwa sababu alikuwa ni mchezaji halali aliyethibitishwa (eligible) na TFF.

Kamati ilimuita mchezaji huyo na kumhoji kama alishiriki au alifahamu udanganyifu wa kubadili majina ili aweze kuingizwa katika mfumo wa eletroniki wa usajili lilibaki kuwa suala la mashaka. Inawezakana alishiriki au hakushiriki; Kamati haikupata ushahidi thabiti. Hivyo, Kamati iliamua kumpa mchezaji faida ya mashaka (benefit of doubts) na hivyo kutompa adhabu yoyote.

Kassanda ameadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 40(11) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati Omari Ramadhan ni mchezaji wa African Lyon kwa vile ana mkataba na klabu hiyo.

JKT MLALE YATAKIWA KUILIPA LYON
Klabu ya JKT Mlale imeamriwa kuilipa African Lyon jumla ya sh. 600,000 ikiwa ni ada ya uhamisho na fidia kwa kumtumia mchezaji Noel Lucas kinyume cha taratibu kwenye mechi.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji baada ya kusikiliza malalamiko ya African Lyon ambapo ilibaini kuwa klabu hiyo ilikubali kulipwa sh. 300,000 ilikwa ni ada ya uhamisho.

Kamati imekataa maombi ya African Lyon kutaka pointi tatu na mabao matatu katika mechi yao ambapo Noel Lucas alicheza, kwa vile mchezaji huyo usajili huo ulithibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Pia JKT Mlale imetakiwa kuilipa African Lyon sh. 300,000 nyingine za usumbufu wa kufuatilia malipo ya mchezaji huyo. JKT Mlale imetakiwa kulipa fedha hizo kabla ya mechi yake ya mwisho ya ligi.
  

JUDICIAL AND STANDING COMMITTEES.
Kamati ya Utendaji iliyoketi tarehe 19 Disemba 2014, ilifanya mabadiliko katika kamati ndogo ndogo na zile za kisheria. Kamati hizo ni kama ifuatavyo

KAMATI YA NIDHAMU
1.   Tarimba Abbas (Mwenyekiti)
2.   Advocate Jerome Msemwa ( Makamu mwenyekiti)
3.    Kassim Dau
4.   Nassoro Duduma
5.   Kitwana Manara 
KAMATI YA RUFANI YA NIDHAMU
1.   Advocate Mukirya Nyanduga (Mwenyekiti)
2.   Advocate Revocatus Kuuli (Makamu mwenyekiti)
3.   Abdala Mkumbura
4.   Dr. Franics Michael
5.   Advocate Twaha Mtengela
KAMATI YA MAADILI
1.   Advocate Wilson Ogunde (Mwenyekiti)
2.   Advocate Juma Nassoro (Makamu mwenyekiti)
3.   Advocate Ebenezer Mshana
4.   Geroge Rupia
5.   Mh. Said Mtanda
KAMATI YA RUFANI YA MAADILI
1.   Advocate Walter Chipeta (Mwenyekiti)
2.   Magistrate  George Kisagenta (Makamu mwenyekiti)
3.   Lilian Kitomari
4.   Advocate Abdala Gonzi
KAMATI YA UCHAGUZI
1.   Advocate Melchesedeck Lutema
2.   Advocate Adamu Mambi (Makamu mwenyekiti)
3.   Hamidu Mahmoud Omar
4.   Jeremiah John Wambura
5.   John Jembele

KAMATI YA RUFANI TA UCHAGUZI
1.   Advocate Julius Lugaziya (Mwneyekiti)
2.   Advocate Machare Suguta (Makamu Mwenyekiti)
3.   Idrisa Nassor
4.   Paschal Kihanga
5.   Benister Lugora
KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO
1.   Wallace Karia (Mwenyekiti)
2.   Yahya Mohamed (Makamu mwenyekiti)
3.   Goodluck Moshi
4.   Omar Walii
5.   Ellie Mbise
6.    Deo Lubuva
KAMATI YA MASHINDANO
1.   Geofrey Nyange (Mwenyekiti)
2.   Ahmed Mgoyi (Makamu mwenyekiti)
3.   James Mhagama
4.   Stewart Masima
5.   Steven Njowoka
6.   Said Mohamed

KAMATI YA UFUNDI
1.   Kidao Wilfred (Mwenyekiti)
2.   Athumani Kambi (Makamu mwenyekiti)
3.   Vedastus Rufano
4.   Dan Korosso
5.   Pelegriunius Rutahyugwa
KAMATI YA MPIRA WA MIGUU YA VIJANA
1.   Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti)
2.    Khalid Abdallah (Makamu mwenyekiti)
3.    Ali Mayay
4.   Mulamu Ngh’ambi
5.   Said Tully
KAMATI YA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE
1.   Blassy Kiondo (Mwenyekiti)
2.   Rose Kissiwa (Makamu mwenyekiti)
3.   Zena Chande
4.    Amina Karuma
5.   Zafarani Damoder
6.    Beatrice Mgaya
7.    Sofia Tigalyoma
8.   Ingrid Kimario (Katibu wa Kamati)
KAMATI YA WAAMUZI
1.   Saloum Umande Chama (Mwenyekiti)
2.   Nassoro Said (Makamu mwenyekiti)
3.   Charles Ndagala (Katibu)
4.   Kanali Issaro Chacha
5.   Soud Abdi
KAMATI YA HABARI NA MASOKO
1.   Athuman Kambi (Mwenyekiti)
2.   Alms Kasongo (Makamu Mwenyekiti)
3.   Rose Mwakitangwe
4.   Amir Mhando
5.   Haroub Selemani
KAMATI YA UKAGUZI WA FEDHA
1.   Ramdhan Nassib (Mwenyekiti)
2.   Epaphra Swai (Makamu mwenyekiti)
3.   Jackson Songora
4.   Golden Sanga
5.   Francis Ndulane
6.   Cyprian Kwiyava
KAMATI YA TIBA
1.   Dr. Paul Marealle (Mwenyekiti)
2.   Dr. Fred Limbanga (Makamu mwenyekiti)
3.   Dr. Mwanandi Mwankewa
4.   Dr. Eliezer Ndelema
5.   Asha Mecky Sadik
KAMATI YA FUTSAL NA BEACH SOCCER
1.   Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
2.   Hussein Mwamba (Makamu mwenyekiti)
3.   Samson Kaliro
4.   Shaffih Dauda
5.   Boniface Pawassa
6.   Apollo Kayugi

PRESIDENTIAL COMMISSION FOR AFFAIRS
1.   Omar Abdulkadir (Mwenyekiti)
2.   Emmanuel Chaula (Makamu mwenyekiti)
3.   Victor Mwandiki
4.   Riziki Majala
5.   Zahra Mohamed
6.   David Nyandu
PRESIDENTIAL COMMISSION ON BUSINESS AND INVESTMENTS
1.   William Erio (Mwenyekiti)
2.   Mbaraka Igangula
3.   Advocate Iman Madega
4.   Lt. Col Charles Mbuge
5.   Philemon Ntalihaja

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)