SIKUKUU YA UHURU KUSHEREHEKEWA KWA KUFANYA KAZI

SIKUKUU YA UHURU KUSHEREHEKEWA KWA KUFANYA KAZI

November 23, 2015

magufuli1 
K wa mujibu wa  Sheria ya Sikukuu za Kitaifa  (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike  kwa kufanya kazi.  Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu  (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu.  Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo. Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi,  fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.
Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo,   sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.
Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU 23 Novemba, 2015
KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI

KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI

November 23, 2015

SEF1
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
SEF2
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
SEF3
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
SEF4
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
SEF5
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………
Katibu  Mkuu  Kiongozi  Balozi Ombeni  Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema  amekagua mashine za MRI na CT-SCAN  na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
Pia,  amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama  na kuwa na maduka yao ya ndani.
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando  na  watendaji wa MNH  ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

NSSF YADHAMINI TAMASHA LA KUSOMA VITABU WANAFUZNI WA SHULE ZA MSINGI

November 23, 2015

 Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama akiwaonyesha fomu ya kujiunga na uanchama wa hiari na fao la matibabu baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF wakati wa tamasha la wa kusoma vitabu wanafunzi wa shule za msingi, lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF. 
Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama (kushoto) akifafanua jambo kwa wanachama wapya waliojiunga uanchama wa hiari na fao la matibabu wakati wa tamasha la kusoma vitabu wanafunzi wa Shule za Msingi lililofanyika jijini Dar es Salaam kudhaminiwa na NSSF.
 Watoto Brianna Michalis Kelly Godfrey wakisoma vitabu wakati wa tamasha la  kusoma vitabu wanafunzi wa Shule za Msingi lililofanyika jijini Dar es Salaam kudhaminiwa na NSSF.
Mtoto Baraka Ngonyani (kushoto) akisoma kitabu wakati wa tamasha la kusoma vitabu lililoandariwa na toKay&Sons na kudhaminiwa na NSSF. Katikati ni mtoto Fidelis Kennedy.
 Ofisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Mshangama akifafanua jambo kwa uanachama wa hiari na fao la matibabu kwa wanachama wapya waliojiunga na NSSF wakati wa tamasha la wa kusoma vitabu wanafunzi wa shule za msingi, lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
 Ofisa Mawasiliano wa tKay&Sons, Angelina Pesha akiwafundisha watoto.

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

November 23, 2015

Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano Dkt. Carina Wangwe kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akielezea umuhimu wa kujiunga katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda akielezea umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga na kutathmini programu mbalimbali za maendeleo nchini wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Baadhi ya wadau mbalimbali wa takwimu wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ofisi hiyo pamoja na viongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika baada ya kumaliza maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora". (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Na Emmanuel Ghula

Wizara, Idara, Wakala, Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyokuwa ya Serikali na Wadau wa Maendeleo  wametakiwa kutumia takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa matumizi ya takwimu bora ndio msingi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Leo tunasherehekea Siku ya Takwimu Afrika, siku ambayo inatukumbusha umuhimu wa Takwimu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa letu. Ukiwa na takwimu bora utaweza kutoa huduma zilizo bora,” amesema Prof. Mkenda.

Prof. Mkenda amesema uwepo wa takwimu bora zinazoonesha mahitaji halisi ya wananchi ndio dira katika utaoji wa huduma muhimu za kila siku pamoja na upangaji na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ya kitaifa.

“Maadhimisho haya leo yanazitaka Serikali zetu kuimarisha mifumo ya kitakwimu kwa kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa Takwimu. Serikali kwa upande wake itahakikisha inaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwekeza katika teknolojia ya kisasa zaidi ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya ukusanyaji wa Takwimu bora na kwa wakati,” amesisitiza Prof. Mkenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu imelenga katika kuufahamisha umma kuhusu umuhimu wa Takwimu bora kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

“Siku hii ya Takwimu Afrika ni muhimu sana kwetu sisi hasa watakwimu kwani tunaitumia kuelimisha umma juu ya umuhimu wa Takwimu katika mustakabali wa maendeleo ya Taifa,” amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema kupitia maadhimisho haya yanayoongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora", itawasaidia wananchi kutambua kuwa uwepo wa takwimu bora ndio njia ya upatikanaji wa maendeleo stahiki.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Dkt. Carina Wangwe amesema wakiwa kama watumiaji wakubwa wa Takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika utekelezaji wa majukumu yao ndio wanathamini mchango wa takwimu rasmi katika kupanga mipango ya maendeleo.

“Sisi ni wadau wakubwa na watumiaji wa takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, leo hii tupo hapa ili kushirikiana na ofisi hii ili kuhakikisha teknolojia ya kisasa inatumika katika uboreshaji wa Takwimu na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii,’ amesema Dkt. Wangwe.

Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa tarehe 18 Novemba, kila mwaka, Kwa hapa Tanzania maadhimisho haya yamefanyika Novemba 23, 2015 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
BENKI YA STANDARD CHARTERED YATEUA MKURUGENZI WA KWANZA MTANZANIA

BENKI YA STANDARD CHARTERED YATEUA MKURUGENZI WA KWANZA MTANZANIA

November 23, 2015
Sanjay - 3
Sanjay Rughani (pichani) anakuwa Mtanzania wa kwanza kuiongoza benki ya Standard Chartered Tanzania akipokea uongozi wa benki hiyo kutoka kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Liz Lloyd, ambaye amerudi katika makao makuu ya benki hiyo, London, kuchukua nafasi ya Mshauri wa Kisheria wa benki hiyo.
Sanjay alijiunga na benki ya Standard Chartered Tanzania mwaka wa 1999 akiwa kama Meneja msaidizi wa kitengo cha Fedha. Baada ya miaka miwili Sanjay alipata cheo cha Meneja wa kitengo cha Fedha kwa Bara la Afrika, kazi ambayo aliifanya akiwa katika makao makuu ya benki hiyo, London. Alirudi nyumbani Tanzania mwaka wa 2002 na kupata cheo cha Mkuu wa Kitengo cha Fedha nchini Tanzania, kazi ambayo aliifanya hadi mwaka wa 2006.
Mwaka wa 2007, Sanjay alipata tena cheo kingine, wakati huu akihamishiwa Ghana, ambapo aliongoza Kitengo cha Fedha nchini humo huku pia akisimamia Afrika Magharibi, yaani Gambia, Cote d' Ivoire na Sierra Leone, kazi ambayo aliifanya hadi Mei, 2013.
Juni, 2013 Sanjay alipandishwa tena cheo na kuwa Mkuu wa Operesheni za Kifedha na Mratibu wa Huduma za Kifedha kwa Bara la Afrika akiongoza kitengo hicho ambacho ni sehemu ya Kitengo Kikuu cha Fedha katika nchi kumi na tano za Afrika, akilenga kuboresha huduma za kifedha za benki hiyo zilingane na huduma zake za kimataifa katika nchi zilizoendelea. Sanjay alifanya kazi hii hadi alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Benki hiyo hapa Tanzania hapo mwanzoni wa mwezi huu wa kumi na moja.
Lamin Manjang, Mkurugenzi wa benki ya Standard Chartered Kenya na Afrika Mashariki, amesema, “Nafurahi kumkaribisha tena Sanjay nyumbani Tanzania na kwenye timu yangu ya Afrika Mashariki kufutatia umahiri wake katika kazi mbalimbali ambazo amezifanya katika benki yetu. Pia nafurahi kuwa sasa benki yetu nchini Tanzania ina Mkurugenzi wake wa kwanza wa Kitanzania. Hii inaonyesha ubora wa wafanyakazi wetu nchini Tanzania. Tunaendelea kuweka kipaumbele kwa kuwapa wafanyakazi wetu bora nyadhifa mbalimbali za uongozi barani Afrika ili kuweza kuboresha maendeleo katika nchi mbalimbali ambapo tunafanya shughuli zetu za kibenki.”
Tanzania inaendelea kupewa kipaumbele katika mipango ya benki hiyo katika bara la Afrika na Afrika Mashariki haswa kutokana na ukuaji wake wa kiuchumi na kuweko katika ‘Klabu ya 7%’, ambayo ni listi ya nchi ambazo uchumi wake unakadiriwa kuendelea kukua kwa kasi zaidi katika miaka kumi ijayo.
Kufuatia kuteuliwa kwake Mkurugenzi huyo mpya wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani alisema, “Tanzania ina fursa nyingi sana za kibiashara na ninafurahi kurudi nyumbani kuiongoza benki ya Standard Chartered kwenda kwenye hatua nyingine ya kimaendeleo. Nchi yetu inaendelea kuchangia mafanikio ya Umoja wa Afrika Mashariki kwa njia mbalimbali ikiwemo ukuaji mzuri wa uchumi. Pia ugunduzi wa hifadhi za gesi nchini Tanzania unatarajiwa kuleta maendeleo zaidi ya kiuchuni hapa nchini kwetu.”
Sanjay ana shahada ya udhamili ya Kifedha na Rasilimali watu, na shahada ya Uchumi. Pia ni mwanachama wa Chama cha Wahasibu, ACCA. Sanjay pia ni Mjumbe wa Bodi wa benki ya Standard Chartered Uganda. Ameoa na ana watoto wawili.
Mgogoro wa Zanzibar watua ikulu ya Marekani

Mgogoro wa Zanzibar watua ikulu ya Marekani

November 23, 2015
Na Mwandishi wetu Washington 
Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).
Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti nchini Marekani wakionyesha mabango yao 
Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.
Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.
"Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.
Pichani ni Bango la waandamanaji wa Zadia
Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"
Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa Mataifa.

HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA KESHO NA MAHAKAMA.

November 23, 2015
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitoa taarifa kwa wananchi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Katika kesi hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James Millya, John Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo.

Mahamaka hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa washtaki na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa ambae ni Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali kupelekewa nyaraka za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao hapo kesho.

Mapema kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema kitendo hicho kinaondoa dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa wananchi wote wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.

Licha ya Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda Mahakamani hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya Mahakama hiyo hadi pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe alipowasihi kurejea majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa tena.


Ni zaidi ya siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili Mkoani Geita na watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni chuki za kisiasa ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Mmoja wa Mawakili wa Chadema John Mallya akitoa taarifa kesi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema
Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo.
MAJALIWA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE NA KUJITAMBULISHA

MAJALIWA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE NA KUJITAMBULISHA

November 23, 2015

JA1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA2
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia  ofisini kwake , Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA3
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA4
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA5
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha kwa watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA6
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA7
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  na  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA8
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Dkt Florence Turuka  baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JA9
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  na  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha  alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue  jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.
Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.

TANZANIA YACHAGULIWA NA UNESCO KUWA MJUMBE WA KAMATI YA URITHI WA DUNIA

November 23, 2015


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na Waandishi wa Habari (hawako pichani) leo tarehe 23/11/2015 katika Ofisi za Wizara hiyo ambapo amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia kwa kipindi cha miaka minne. Uchaguzi huo umefuatia uamuzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaohusu Urithi wa Dunia uliofanyika mjini Paris, Ufaransa tarehe 18-20 Novemba 2015. (Habari Kamili SOMA TAARIFA KWA UMMA HAPO CHINI)
 
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Tanzania kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Urithi wa Dunia. Alieleza kuwa katika Kamati hiyo Tanzania itawakilishwa na Bw. Donatius Makamba ambaye ni Mkurugugenzi Idara ya Mambo ya Kale Wizara ya Maliasili na Utalii akisaidiwa na Dkt. James Wakibara, Mwikolojia Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Dkt. Mohammed Juma, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji kutoka Zanzibar.
 Bi. Eliwasa Maro Mkurugenzi Msaidizi Utafiti Mafunzo na Takwimu Wizara ya Maliasili na Utalii akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika Mkutano huo na Waandishi wa Habari.
 Sehemu ya washiriki wa Mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakinukuu baadhi ya mambo muhimu.
 (Na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili na Utalii)
TANAPA receive anti-poaching aircraft from Germany

TANAPA receive anti-poaching aircraft from Germany

November 23, 2015

ta1
1. Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier (right) handing over a symbolic key of a light Husky aircraft for anti-poaching operations to Director General of TANAPA Allan Kijazi. Others in the picture from left are Director of Wildlife Herman Keraryo and Acting Director General of Tanzania Wildlife Authority Martin Loibooki.
ta2
 Director General of TANAPA Allan Kijazi making a brief presentation about TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier during the handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.
ta3
 Director General of TANAPA Allan Kijazi presenting some of the souvenirs of TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier.
ta4
5. Germany Ambassador to Tanzania Hon. Egon Kochanke (right) and the Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation Ambassador Liberata Mulamula during the event.
ta5
Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier (second right) posed in a group picture with some of the Germany Members of Parliament who accompanied him during the handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.
ta6
 Director General of TANAPA Allan Kijazi speaking with media during the event.
TA7
Some of the invitees during the handing over event. From left to right are Arusha Regional Administrative Secretary Mr. Mapunda, African Wildlife Foundation Country Director John Saleh and TANAPA’s Director of Tourism and Marketing Ibrahim Mussa.
…………………………………………………………………………………….
Germany Foreign Minister Frank-Walter Steinmeier yesterday handed over symbolic key of two Husky aircrafts to Tanzania National Parks and Tanzania Wildlife Authority respectively. The aircrafts will be used for anti-poaching operations in the protected areas.
Director General of TANAPA Allan Kijazi said that the aircrafts would take the joint approach by the Germany Government through Frankfurt Zoological Society, TANAPA and TAWA to tackle poaching in the protected areas.
The Husky A-1C is an ideal plane for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights and slow speeds-similar to that of a helicopter and has proven long-term success rate for its use in finding poacher camps and recording GPS positions for follow-up actions by teams on the grounds.
The Huskies will be used to monitor two of Tanzania’s elephant hotspots, Selous Game Reserve and Serengeti National Park.
Tanzania is home to some of the most elephant and rhino populations on the planet but of recent days it has experienced a severe threat from a massive upsurge in poaching. Issued by Corporate Communications Department Tanzania National Parks 23rd November, 2015 T: 027 250 1933 E: dg@tanzaniaparks.com W: www.tanzaniaprks.com