WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA FIFA

WAZIRI MKUU AKUTANA NA RAIS WA FIFA

February 22, 2018

PMO_8628
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Bandera ya FIFA kutoka kwa Rais wa Shirikisho  la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari  uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu. leo February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania
PMO_8673
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Jezi namba Tisa kutoka kwa Rais wa Shirikisho  la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari  uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu. leo February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania
PMO_8613
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Kinyango Rais wa Shirikisho  la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari  uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu. leo February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU 

MHE BITEKO: "MULUGO WEWE NI NOMA...!"

February 22, 2018
 
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kijiji na kata ya Saza, Wilaya na Mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Songwe

Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu juhudi za mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.

Mhe Biteko ametoa pongezi hizo kwa mbunge huyo wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Songwe.

Naibu waziri huyo alisema kuwa mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi wake hususani katika kuchochea shughuli za maendeleo ili kuongeza ufanisi wa maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Pongezi hizo zinajili wakati ambapo mbunge Mulugo amefanikiwa kutatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya kikundi cha TUJIKOMBE na Kampuni ya Bafex kwenye eneo la uchimbaji dhahabu la mlima Elizabeth.

Katika kumaliza mgogoro huo kampuni ya Bafex imekubali kugharamia mradi utakaochaguliwa na kikundi hicho kama fidia ya gharama walizozitumia wachimbaji hao kuendeleza eneo hilo.

"Mheshimiwa Mulugo wewe ni hazina ya Songwe, namuomba Mungu aendelee kukutunza kwaajili ya watu hawa. Mimi nipo Bungeni muda wote wewe ajenda yako ni watu wako na unafanya hivyo bila kuchoka. Kwakweli wewe ni NOMA" Alisema Mhe. Biteko huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Sambamba na hayo pia amempongeza Mbunge huyo kwa ushirikiano mzuri baina yake na serikali ya Wilaya pamoja na Chama Cha Mapinduzi jambo ambapo linaakisi uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema kuwa kilio hicho cha wananchi kimedumu kwa muda mrefu hivyo jukumu la serikali ni kutatua kero za wananchi sio kuchochea migogoro.


DALALI ATAKA TAWI LA SIMBA CREAM TANGA KUANZISHA TIMU YA VIJANA U-17

February 22, 2018
 ALIYEKUWA Mwenyekiti  wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa  tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati alipolitembelea
 ALIYEKUWA Mwenyekiti  wa Simba, Hassani Dalali akizungumza na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa  tawi la Simba Cream la Jijini Tanga wakati alipolitembelea kushoto ni Mwenyekiti wa Tawi hilo John Bukuku kulia ni Katibu akifuatiwa na katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi hilo Edgar Mdime
 Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akisoma risala fupi katika ziara ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali
 Katibu Mkuu wa Tawi hilo akizungumza machache
 Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
 Mmoja wa wanachama wa Simba kutoka Tawi la Simba Cream Chongowe akiuliza swali
  Katibu Msaidizi na Mwekahazina wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime akiteta jambo na mwanachama wa tawi hilo
 Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
Sehemu ya wapenzi,wakereketwa na wanachama wa klabu ya Simba wakimsikiliza Dalali
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wapenzi,wanachama na wakereketwa wa Simba Jijini Tanga
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali akiwa kwenye picha na Katibu Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina wa Tawi hilo
ALIYEKUWA Mwenyekiti  wa Simba, Hassani Dalali amelitaka tawi la Simba Cream la Jijini Tanga kuanzisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ili iweze kuwa hazina kubwa ya wachezaji kwa siku za mbeleni.
Licha ya hivyo lakini pia inasaidia kuweza kuinua vipaji vya wachezaji wachanga ambao wanaweza kuonekana thamani yao siku zinazokuja kwani mkoa wa Tanga una vipaji vya soka vingi.
Dalali aliyesema hayo juzi akizungumza na wanachama wa Simba katika tawi la Simba Cream la Tanga mjini ambalo lilianzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na aliyekuwa Rais wa Simba Evans Aveva.

Alisema uanzishwaji wa timu hiyo utakuwa na faida kubwa kwa kusaidia timu hiyo kuwa na hazina ya wachezaji ambao wanaweza kuwatumia kwa miaka ijayo ili kuendelea kuwika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma hapa nchini.

“Kwani timu hiyo inapoanzishwa na kuweza kuwa imara itatuwezesha tunapotaka wachezaji tunakuja kuchukua mkoani Tanga kwa sababu tutakuwa tumewekeza mtaji mkubwa wa vijana”Alisema.

Hata hivyo alisema tawi la Simba la Kinondoni kwa miaka ya nyuma ndio ambalo liliwasaidia kuwapelekea mchezaji Uhuru Selemani na baadae yeye kumpeleka kwenye klabu ya Coastal Unon .

MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA WAJADILIANA NA WAHARIRI DAR

February 22, 2018
 Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania (WFT), Mary Rusimbi akizungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.

 Mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
 Mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
 Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakifuatilia mijadala anuai katika mkutano huo.
MTANDAO wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi leo umekutana na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi nchini.

Akiwasilisha mada kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano huo, mtoa mada na mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga aliwataka wanahabari kuangalia mfumo mzima wa siasa za vyama vingi na nini kinachoitenganisha siasa ya Tanzania na nchi nyingine bila kujali tofauti za itikadi za vyama kwenye masuala yanayohusu utu wa mwanamke, ushiriki wa mwanamke kuchangia fikra za siasa na uongozi.

Aliwataka kuchambua na kuangalia mambo yapi yatakayounganisha wanasiasa wote katika kutetea masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na utu na haki za mwanamke na pia mfumo wa uongozi utakaowezesha vyama vya siasa kuimarisha demokrasia shirikishi yenye mrengo wa jinsia ndani ya vyama.

Pia kuchambua mfumo wa uongozi unaowezesha vyama kutatua migogoro ndani ya vyama vyao bila kutumia vitisho, na hususani vinavyoashiria kumsababisha mwanamke wa Tanzania asipende kushiriki katika shughuili za siasa au anaposhiriki ajisikie yuko salama.

Kwa upande wake Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza katika majadiliano hayo, alisema malengo ni kujadili kwa pamoja umuhimu wa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia katika masuala ya siasa na  uongozi nchini nchini.

Kujenga makubaliano ya pamoja jinsi waandishi wa habari watakavyochechemua umuhimu wa kuzingatia misingi ya jinsia kwenye masuala ya siasa na uongozi katika majukumu yao, na kujengeana uwezo wa masuala ya usawa wa jinsia na uongozi kwa ujumla.

--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.


Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470


          http://joemushi.blogspot.com

"NI BORA TUKAWIE LAKINI TUFIKE" MHE BITEKO

February 22, 2018

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua kinu cha kuchakata dhahabu mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya mitambo ya uchenjuaji madini katika mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua njia ya kwenda kwenye mgodi wa chini mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza Wilayani SongweLeo 22 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Songwe

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu utendaji unaofanywa na kampuni ya uchimbaji madini ya dhababu wa Shanta Gold Mine kwa kukubali kuendana na matakwa ya serikali kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi katika sekta hiyo.

Alisema kuwa Wizara hiyo imedhamiria kuboresha sekta ya Madini ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali hiyo ambayo imechezewa na wajanja wachache katika kipindi cha muda mrefu.

Mhe Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo Leo 22 Februari 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza Wilayani Songwe.

Kampuni ya SGM haipo kwenye kundi la wawekezaji walalamikaji kuwa serikali kupitia sheria ya madini inawakimbiza wawekezaji jambo ambapo sio kweli badala yake serikali imeweka utaratibu yakinifu wa uchumi fungamanishi utakaoboresha sekta ya Madini na kuwanufaisha watanzania.

"Twendeni kwa watanzania tukawaulize wamenufaika  kwa kiasi gani na uwepo wa migodi mbalimbali ya uchimbaji nchini, jibu ni jepesi tu kuna watu wachache wamenufaika na rasilimali hiyo jambo ambapo hatutalifumbia macho tena" Alisema Mhe Biteko na kuongeza kuwa

"Serikali inahitaji wawekezaji ambao wanafuata sheria Na taratibu za nchi hata kama ni wachache wanapaswa kufahamu kuwa wanapaswa kufuata sheria kwani kufanya hivyo sio ombi bali ni lazima"

Aliongeza kuwa Wizara ya Madini itaendeleza ushirikiano kwa kiasi kikubwa na mgodi huo ili kuinua zaidi uwekezaji wao na hatimaye kuwa na uzalishaji wenye tija ambao utapelekea serikali kukusanya kodi kwa kiasi kikubwa kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla wake. 

Alisema kuwa watumishi wote katika Wizara ya Madini na wawekezaji katika sekta ya madini wanapaswa kusimamia haki katika utendaji wao huku wakiunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha nidhamu ya uwajibikaji hususani kujitenga na utoaji ama upokeaji wa rushwa.

Alisema dhamira ya serikali ya awamu ya tano ni kuwarahisishia huduma wachimbaji wadogo kupitia malezi bora ya Wizara ya madini ili kufikia hatua ya kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kufikia uwekezaji mkubwa katika uchimbaji wa rasilimali hiyo.

Katika hatua nyingine wawekezaji hao wametakiwa kuwaamini wataalamu wa Madini wa hapa nchini pasina kuwa na Mashaka nao kwani serikali inawafahamu na wengi wao wakiwa wanafanya kazi nje ya nchi.


WILAYA YA GAIRO YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI KUTOA CHAKULA CHA MCHANA MASHULENI

February 22, 2018
 Mhe. Mchembe akishiriki ugawaji chakula kwa wanafunzi Shule ya Msingi Kibedya mara baada ya kutembelea baadhi ya shule Kata ya Kibedya na Chakwale. Wanafunzi wakipata chakula cha mchana.
  Mkuu wa Wilaya ya Gairo akishiriki uchimbaji wa mtaro wa kutandaza mabomba. Waliopo nyuma yake ni Mhe. Maneno Diwani wa Chakwale na Mtendaji Kata ya Chakwale
Mhe. Mchembe akiongea na wananchi kuhamasisha umaliziaji wa madarasa 5 shule shikizi ya Iringa.
 Diwani wa Kata ya Mangapi Mhe. Maneno akiongea na wananchi. Waalimu wa mazoezi wote wa shule shikizi wanaishi nyumbani kwa Diwani kama familia.

BIL.1.7 KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU

February 22, 2018
Uwekezaji katika sekta ya elimu Nchini kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu (EQUIP-Tanzania) ambao umelenga kuboresha mchakato wa kufundisha na matokeo ya kujifunza kwa watoto nchini umeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa Mkoani Simiyu.

Uwekezaji huo ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) umeleta ufanisi wa elimu na kufanya viwango cha ufaulu kuwa juu kutoka asilimia 36 mwaka 2013 mpaka asilimia 68 2017.

Na katika kutimiza hayo Jumla ya kiasi cha shilingi Bil 1.7 kutoka DFID kupitia mradi wa kuinua ubora wa Elimu Nchini (Equip) zimetolewa kwa Serikali ya Mkoani Simiyu kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu Mkoani humo .

Akizungumzia nia ya serikali ya Uingereza wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan , Mkuu wa DFID-Tanzania Elizabeth Arthy alisema wametoa kiasi hicho cha fedha kwa serikali ya Mkoa wa Simiyu ili kuhakikisha wanatatua changamoto ya miundombinu iliyopo.

Arthy alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho kinatarajiwa kutumika katika kuboresha miundombinu hiyo na kujenga vyumba vya madarasa, ofisi za walimu pamoja matundu ya vyoo kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ufanisi wa utoaji elimu kwa walimu na wanafunzi.

Mkuu huyo alieleza kuwa tangu shirika lake lianze kusaidia katika Elimu ,Mkoa wa Simiyu umeweza kupata mafanikio makubwa na ya haraka ambayo yamesaidia kuuweka Mkoa katika nafasi nzuri Kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu elimu ya Msingi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka aliuelezea mpango wa kuinua ubora wa elimu Tanzania kwa Mkoa wake kuwa ni mpango ambao umeweza kuleta mabadiliko makubwa ya kukuza viwango vya ufaulu wa wanafunzi.

Mtaka anaeleza wanalishukuru shirika la maendeleo ya uingereza (DFID) kupitia mpango wa kuinua ubora wa elimu kwa kuona kuwa Tanzania na Mkoa wake unahitaji msaada huo wa kuinua kiwango cha ufaulu pamoja na uboreshaji wa mazingira ya elimu.

Amesema kupitia msaada huo wa fedha kiasi cha shilingi Bil 1.7 zilizotolewa kwao na shirika la DFID kwa mwaka huu za kuboresha mazingira ya elimu ,zitawasaidia kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambavyo vyote hivyo ni changamoto kubwa Mkoani kwake.

Anaongeza kuwa kupitia fedha hizo anaanimi tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo utapungua kwa kiasi kikubwa na kwamba atasimamia vema fedha hizo ili ziweze kutumika ipasavyo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Raisi utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akizungumza mbele ya makamu wa Rais juu ya mchango wa serikali ya Uingereza katika kuboresha elimu.
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza nchini Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya msingi Gamondo A iliyoo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Bibi Elizabeth Arthy alipotembelea shule ya msingi Gamondo A mkoani Simyu, kuona utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania.

WAZIRI JAFO APANIA KUBORESHA SEKTA YA AFYA KWA WAKINA MAMA WAJAWAZITO KWA KUJENGA VITUO VYA AFYA

February 22, 2018
Na Victor   Masangu, Chole  Kisarawe   
WAKINAMAMA  wajawazito katika kijiji  cha Kihare kata ya Maluwi Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani  waliokuwa wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya afya kutokana na  ukosefu wa kutokuwa na  wodi maalumu  ya kujifungulia kwa  kwa kipindi cha  muda mrefu na kuwalazimu kutembea umbari wa kilometa 15 kufuata huduma hatimaye kilio chao kimepata mkombozi baada kukamilika kwa jengo la wazazi.

Aisha Ramadhani na Fatma Iddy ni baadhi ya wakinamama ambao walisema kwa miaka mingi wamekuwa wanateseka pindi inapofika wakati wa kujifungua kutokana na zahanati ya Kihare ambayo  walikuwa wanaitumia katika kupata huduma ya matibabu ilikuwa haina jengo la wodi ya wazazi hivyo ilikuwa inawalazimu kufunga safari ya umbari wa kilometa 15 kwa kutumia usafiri wa baiskeli,pikipiki au wakati mwingine kutembea kwa  miguu.

Walisema  kwamba hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua kutokana  na kutokuwepo kwa wodi ya kujifungulia hivyo walikuwa wanachanganywa na wagonjwa wengine wa kawaida kitu hali ambayo ji hatari kwa afya zao na mtoto, hivyo wameipongeza serikali ya awamu ya tano na juhudi za Mbunge wa jimbo lao  kwa kuamua kujenga jengo hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa katika utoaji wa huduma.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jonathan Budenu  amekiri kuwepo kwa changamoto ya wakinamama wa kijiji cha Kihare  kutembea umbari mrefu wa kilometa 15 kwa ajili ya kwenda kufuata huduma ya kujifungua katika kituo cha afya chole,ambapo kwa sasa wameanza harakati za ujenzi wa  wodi kwa kutumia  za halmashauri pamoja na michango ya wananchi.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi  Selemani Jafo amebaini kuwepo kwa hali hiyo wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati ya Kihare ambapo  amesema kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya afya.

Jafo alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha inaborsha sekta ya afya hivyo ujenzi wa vituo hivyo vya afya vitaweza   kupunguza adha ya wagonjwa hususan kwa  wakinamama wajawazito kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.

“Kwa kweli katika hili la wakinamama wajawazito wamekuwa wakipata shida kubwa sana, kwani wakti mwingine wanasumbuka ya kufuata huduma ya afya kwa kutembea umbali mrefu, hivyo tumetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 500, kwa kila ujenzi wa  kituo cha afya kimoja nah ii kwa kweli itapunguza sana adha ya wakinamama waliyokuwa wakiipata pamoja na wananchi wote kwa ujumla,”alisema Jafo.

Waziri Jafo akiwa  katika ziara yake ya kikazi  Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ambapo ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu, afya maji, pamoja na kuweza kukutana na viongozi, watendaji , pamoja na kungumza na wananchi wa vijiji,vitongoiji, kata kwa lengo la kuweza kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo kwa lengo la kuweza kuzitatua.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo akizungumza na baadi ya viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya afya, maji, barabara, pamoja na elimu pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais  Tamisemi,  Seleman Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wauguzi na madaktari wa  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbai ya maendeleo pamoja na kuzungumz na wananchi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) UNAOFANYIKA KAMPALA NCHINI UGANDA

February 22, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika Mkutano huo Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC unaojadili masuala mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Sekta ya Miundombinu na  Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wa nne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati Wimbo wa Jumuiya ya  Afrika Mashariki ulipokuwa ukipigwa katika ukumbi wa mkutano uliopo katika  eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wanne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano huo Maalumu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unao endelea jijini Kampala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni akifungua Mkutano huo maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki Kampala nchini Uganda.
Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya a Afrika Mashariki wakifatilia hotuba mbalimbali katika Mkutano huo maalum.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pamoja na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir mara baada ya Mkutano  Maalum wa 19 wa Jumuiya hiyo uliofanyika  Kampala nchini Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Kampala Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU