Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh.
milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo
ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya
Kagera Sugar. Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa
Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Adhabu hiyo
imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu
kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.Nayo Polisi
Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa
kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto
Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza kuvurugika.
Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans
imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa
kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)