DKT. SAMIA AMWAGA MABILIONI KUINUA FURSA ZA UCHUMI WA BULUU.

February 15, 2023


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (wa nne kushoto) akiwa kwenye boti ya uvuvi iliyopewa jina la Mv. Blue Economy na kubainisha mambo kadhaa juu ya uwekezaji wa serikali kwenye Uchumi wa Buluu, mara baada ya kutembelea kikundi cha ushirika cha Mchukuuni kilichopo jijini Tanga ambacho kinajishughulisha na kilimo cha mwani na ufugaji tango bahari ama jina lingine la zamani jongoo bahari.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye kikundi cha ushirika cha unenepeshaji kaa kiitwacho Jifute kilichopo Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga kujionea namna wanavyojishughulisha na unenepeshaji wa kaa hao pamoja na vizimba vilivyojengwa mahsusi kwa ajili ya kufuga kaa 600 kwa wakati mmoja

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (aliyesimama) akiwa kwenye mazungumzo mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba (aliyekaa), kabla ya Naibu Waziri Ulega kuanza ziara ya kikazi mkoani humo.



Na. Edward Kondela

Serikali imeendelea kutekeleza bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 katika uwekezaji wa uchumi wa buluu kupitia maji ya Bahari ya Hindi, maziwa na mito ikiwemo kuhamasisha ufugaji wa viumbe maji.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo (15.02.2023) wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Tanga ambapo katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, kwenye Sekta ya Uvuvi ametembelea vikundi vya ushirika vya ukuzaji viumbe maji vya Jifute kinachonenepesha kaa pamoja na Mondura na Mchukuuni vinavyojishughulisha na ufugaji wa tango bahari ama kwa jina lingine la zamani jongoo bahari pamoja na ukulima wa mwani.

Ili kukuza uchumi wa buluu, Naibu Waziri Ulega amesema serikali imeweka Shilingi Bilioni 2.5 kwa ajili ya kuendeleza zao la mwani ambapo tayari Shilingi Milioni 447 zimeshatolewa kwa vikundi mbalimbali, Shilingi Bilioni 11.5 zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza boti za kisasa za uvuvi na Shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba vya kufugia samaki aina ya sato kwenye Ziwa Victoria.

Mhe. Ulega amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti kuinua uchumi wa buluu kwa kutenga fedha nyingi huku wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakikaribishwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia kuweka mazingira mazuri ya ukuzaji viumbe maji.

Aidha, amewataka wadau wa Sekta ya Uvuvi hususan vikundi vya ushirika vya wavuvi kuchangamkia fursa ambayo serikali imetoa fedha ili kuongeza mahitaji ya ukuzaji viumbe maji kutokana na masoko yaliyopo ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainabu Abdallah amesema anafurahishwa na namna Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyoweka juhudi za kuwasaidia vijana katika uwekezaji kwenye viumbe maji kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutaka uwekezaji wa kisasa kwa kuongeza mnyoyoro wa thamani, huku akibainisha kuwa wilaya yake iko tayari kutenga maeneo mengi zaidi kwa ajili ya shughuli za ukuzaji viumbe maji.

Akisoma risala ya kikundi cha ushirika cha kilimo cha mwani na ufugaji tango bahari cha Mchukuuni kilichopo jijini Tanga, Bw. Abdallah Mtondo amelalamikia kitendo cha baadhi ya watu ambao siyo waaminifu kuiba matango bahari katika mashamba yao hususan nyakati ambapo maji yamefunika mashamba hayo.

Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu hao ambao wamekuwa wakiwarudisha nyuma katika shughuli za ufugaji ili kujiongezea tija jambo ambalo Naibu Waziri Ulega amelitolea kauli kali na kutaka mamlaka husika kuingilia kati jambo hilo huku akisisitiza wanunuzi wa mwani na tango bahari kununua mazao hayo kwenye vikundi vinavyotambulika na kusajiliwa.

Awali kabla ya kuanza ziara ya kikazi Mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba na kufanya naye mazungumzo juu ya namna serikali kupitia wizara hiyo inavyofanya jitihda mbalimbali za kufungua fursa kwa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kwa kufuga na kuuza mazao yanayotoka katika sekta hizo.

RAIS DKT SAMIA AANDIKA HISTORIA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA BOMBO,AFANYA UWEKEZAJI MKUBWA WA ZAIDI YA BILIONI 2 KITENGO CHA MIONZI .

February 15, 2023



Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Mionzi na Picha katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo akizungumza kuhusu uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa ajili ya ujenzi wa jengo na ununuzi wa Mashine ya CT scan ambao umesaidia kwa asilimia kubwa kuwapunguzia mzigo wananchi waliokuwa wakifuata huduma hiyo mikoa mengine, kulia ni Mteknolojia Mionzi katika Hospitali hiyo, Bw. Athumani Rajabu

Mashine ya CT Scan inayotumika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga- Bombo

Mteknolojia Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo  Bw. Athumani Rajabu akizungumza wakati akionyesha mashine kubwa waliyoipata yenye uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi kwa wagonjwa zaidi ya 100 kwa siku na Serikali imefanya kama zawadi kwa wananchi wa  mkoa wa Tanga.
Mteknolojia Mionzi katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Bw.  Athumani Rajabu, akifanya matayarisho ya awali kabla ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kipimo cha CT Scan


Na Oscar Assenga,Bombo- Tanga.

SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu umeweka historia kubwa katika Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Tanga Bombo baada ya kufanya uwekezaji wa kiasi cha zaidi ya Bilioni 2 zilizotokana na miradi ya Uviko 19 kwa ajili ya ujenzi wa jengo na ununuzi wa Mashine ya CT Scan ambao umesaidia kwa asilimia kubwa kuwapunguzia mzigo wananchi waliokuwa wakifuata huduma hiyo mikoa mengine.

Akizungumza leo Mkuu wa Idara ya Kitendo cha Mionzi na Picha katika Hospitali hiyo Dkt Goodluck Mbwilo alisema kwamba wanaishukuru Serikali kwa uwekezaji huo mkubwa ambao umeandika historia kwa mkoa huo  ambapo awali hawakuwahi kuwa na mashine kama hiyo kutokana na kwamba mashine hizo zilikuwa zikipatikana kwenye hospitali za Rufaa za Kanda na  Taifa.

Alisema kwenye hospitali hizo ndio zilikuwa zikipatikana lakini kwa sasa kila hospitali ya mkoa kupitia Rais Dkt Samia ameweza kufanikisha hilo na hiyo itasaidia kutoa huduma bora kwa watanzania wakiwemo wagonjwa wa ajali na wenye matatizo ambao wanahitaji huduma ya CT Scan kwa ajili ya uchunguzi.

Aidha alisema kwamba awali wagonjwa walikuwa wakipata rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili au Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambako huko napo gharama zilikuwa ni kubwa sana hivyo kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwenye hospitali ya Bombo hivyo wananchi wachangamkie fursa hiyo kwa kuweza kupata matibabu na kuokoa gharama kubwa ambazo awali walikuwa wakizitumia.

“Kwa kweli tunaishukuru Serikali ya awamu yaa Sita kwa uwekezaji huu mkubwa ambao awali haukuwepo haya ni mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya kwa mkoa wetu hivyo niwaombe wananchi watumie fursa hiyo kujitokeza kuweza kuja kupata vipimo”Alisema

Hata hivyo alisema kwa sababu gharama za vipimo zipo chini ukilinganisha na hospitali binafasi huku akiwashauri watanzania hususani wakazi wa Mkoa wa Tanga na mikoa mengine kuchangamkia mpango wa fursa ya kuwa na bima ya afya ili kuwarahisishia kupata huduma za matibabu pindi wanapokuwa wakiugua.

Awali akizungumza Mteknolojia Mionzi katika Hospitali hiyo, Athumani Rajabu alisema mashine kubwa waliyoipata ina uwezo mkubwa inaweza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa zaidi ya 100 kwa siku na Serikali imefanya kama zawadi kwa wananchi wa  mkoa wa Tanga.

Alisema mara nyingi wagonjwa ambao wanapata ajali hususani za barabarani na magonjwa  ambayo hayaambukizi kama Saratani ,Kiharusi wanapopata wagonjwa wa nama hiyo kipindi cha nyuma walikuwa wanashindwaa kujua yupi ana madhara zaidi au atapata unafuu zaidi hivyo wote walikuwa wanapatiwa Rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali inapokuwa ikijitokeza wanapofika Muhimbili na kufanyiwa vipimo vya CT Scan wengine wanagundulika wana matatizo kidogo ambao wangeweza kupona kwenye hospitali walizotoka.

Athumani alisema kwamba hiyo mashine imeweza kupunguza gharama kwa wananchi  zisizo za lazima  ambao wamekuwa na uhitaji wa huduma za matibabu za upasuaji wa kichwa hivyo  uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na Serikali umetoa kama msaada kwa sababu ya ghamara zinazotolewa zipo chini

mfano ukienda sehemu za pembezoni,kandokando  huduma ya Ct Scan imekuwa ikichangiwa na wagonjwa hadi laki nne hadi tatu na nusu.

Hata hivyo alisema kwamba mradi huo uliofanywa na Serikali wananchi watatibiwa kwa gharama  nafuu za laki na nusu kwa waagonjwa ambao hawatawekewa dawa na laki mbili na arobaini ambao watawewekewa dawa ukiangalia gharama hizo na zile zinazotozwa kwenye hospitali zengine ni kama utaona ni msaada ambao serikali imeamua kutoa kwa wananchi,

Athumani alisema awali hospitali hiyo haijawahi kuwa na na daktari bingwa wa mionzi lakini kwa sasa wamepata madaktari ambao wapo kwenye hospitali hiyo na wanashauku ya kuweza kuwahudumia wananchi wa mkoa wa Tanga huku akieleza kwamba kuna huduma nyengine za Ct Scan zimeongezeka na huduma za utrsa sound kuangalia mishipa ya damu kwa watu wanaovimba miguuu ikiwemo kuangalia ubongo wa watoto wadogo

Mwisho.