RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA, AENDESHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

December 04, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akizungumza na  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird leo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akimsindikiza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017.
w4, w5 na w6:  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawari  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 4, 2017.

PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA 8 LA MWAKA LA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

December 04, 2017
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango tayari kwa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya Wahudhuriaji wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya awali ya Heaven  Moshono Arusha pamoja na walimu wao ambao walikuwa uwanja wa ndege wa Arusha wakati Makamu wa Rais anaondoka Arusha mara baada ya kufungua wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Mhandisi Binilith Mahenge mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Arusha ambapo alifungua Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

SERIKALI KUBORESHA KIVUTIO CHA UTALII CHA ENEO LA BARABARA YA LAMI INAYOPITA JUU ZAIDI KUTOKA USAWA WA BAHARI

December 04, 2017
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akiongozwa na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo kukagua moja ya eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.
Bofya kitufe cha PLAY kuangalia VIDEO

Na Hamza Temba, Mbeya
........................................................
Serikali imesema itaboresha mazingira ya kivutio cha utalii cha barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi kutoka usawa wa bahari kuliko barabara zote nchini ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii na kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kutembelea shamba la miti la Kawetire wilayani Mbeya na kujionea sehemu ya barabara ya lami inayopita katikati ya shamba hilo katika mlima Kawetire kwenye safu za milima ya Mbeya.

Eneo hilo la barabara hiyo ambayo hupitisha magari kutoka Jijini Mbeya kwenda katika Wilaya ya Chunya na Mikoa ya Singida na Tabora lina urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari katika Latitude 08’ 35 S na Longitude 33’ 25 E.

“Hatutaki ule utalii wa kutegemea wanyamapori pekee, hii sasa ni sehemu ya aina nyingine ya utalii ambayo ni lazima tuiboreshe tuweke kibao kizuri tuweke mazingira mazuri pamoja na kukitangaza ili watanzania na watalii kutoka nje waweze kutembelea hapa,” alisema Hasunga.

Alisema ili kufikia lengo liliwekwa na Serikali la kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni mbili mwaka 2020 na milioni 8 mwaka 2025 vivutio vyote vya utalii vilivyopo nchini vitatambuliwa, kuimarishwa na kuviwekea miundombinu itakayowavutia watalii kuvitembelea.

Aidha aliuagiza uongozi wa shamba hilo kushirikiana na wakala wa huduma za barabara –Tanroads katika kuboresha mazingira yanayozunguka eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka bango la kisasa la kutambulisha eneo hilo, kujenga bustani na maeneo rafiki ya kupumzikia kwa ajili ya kuwavutia watalii kutembelea eneo hilo na kupiga picha.

Mbali na kivutio hicho aliuagiza uongozi wa shamba hilo kutobomoa majengo ya kale yaliyotumiwa na wakoloni katika shamba hilo na badala yake yatumike kwenye utalii wa mambo ya kale sambamba na utalii wa misitu ya kupandwa inayopatikana pia katika shamba hilo.

Hata hivyo alisema kupitia mradi wa REGROW wa kuendeleza utalii kanda ya kusini Serikali imepokea mkopo wa masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 150 sawa za zaidi ya bilioni 340 za kitanzania kutoka benki ya dunia kwa ajili ya kusaidia kuboresha miundombinu ya vivutio vya ukanda huo.

Kwa upande wake Meneja wa shamba hilo, Arnorld Shoo alisema eneo hilo la barabara limekuwa ni kivutio cha kipekee cha utalii katika shamba hilo ambapo pia hupata mapato kupitia watu na vikundi mbalimbali ikiwemo wanakwaya na wanafunzi ambao hufika eneo hilo kwa ajili ya kupiga picha za kumbukumbu.  
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) na Meneja wa shamba la Miti Kawetire, Arnorld Shoo wakiangalia bango linaloonesha eneo katika shamba hilo ilipopita barabara ya lami ambayo ipo juu zaidi ya nyingine nchini ikiwa na urefu (Altitude) wa mita 2961 kutoka usawa wa bahari wakati wa zaira yake ya kikazi jana mkoani Mbeya. Alisema Serikali itaboresha mazingira ya eneo hilo ili yatumike kama kivutio cha utalii nchini.

ILI KUPUNGUZA AJALI BARABARANI:MADEREVA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU HURIA SINGIDA.

December 04, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wakazi wa Singida waliojitokeza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akizungumza na wakazi wa Singida waliojitokeza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.
 Kikundi cha burudani wakionyesha ukakamavu katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akiimba na kikundi cha burudani huku Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akicheza katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya Singida Mjini. 
Madereva wa vyomo vya moto hasa bajaji na bodaboda wamewahimizwa kujiunga na chuo kikuu huria ili waweze kujiendeleza kielimu na kuboresha huduma zao, ambapo kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi cha Mjini Singida.
Amesema masomo ya chuo kikuu huria humwezesha mtu kujiendelea kwa kupata elimu bora bila kuathiri shughuli zake za kila siku hasa za kujipatia kipato.
“Dereva wa bodaboda, bajaji au mkazi yeyote mkoani kwetu, tusiridhike na elimu tuliyonayo, kumbukeni elimu haina mwisho. Hivyo tutumie chuo chetu hiki cha huria kujiendeleza kielimu. Tukiwa na wasomi wengi mkoa wetu kwa vyovyote   lengo la kuwa na uchumi wa kati na chini ya viwanda utalifikia kwa haraka”, amesema.
Dkt Nchimbi amwataka madereva wa vyombo vya moto kutii na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na sio tu kuendeshwa na kamera za barabarani.
“Baadhi  ya madereva wa vyombo vya moto, hawaheshimu kabisa sheria za usalama barabarani, wanaendeshwa na  kamera. Siku moja yupo dereva mmoja wa bodaboda alikuwa mbele yangu, huku akiandika ujumbe kwenye simu yake. Utamaduni huu haufai kwa sababu ni chanzo cha ajali”,amesema Dkt.Nchimbi.
Aidha amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba kusimamia zoezi la madereva wa bajaji na bodaboda kujiunga na Chuo kikuu Huria.
“Hebu angalia uwezekano wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya madereva hawa kujiendeleza kielimu. Tunataka ifike siku tuwe na madereva hawa wana diploma au digrii, kwa hili nina imani na wewe utaweza kuwasaidia vizuri”, amesema.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema atagharamia safari ya viongozi wa madhehebu ya dini kwa kutoa kiasi cha shilingi laki tano, kwenda kufanya sala maalum kwenye maeneo yaliyokidhiri  kwa vitendo vya ajali.
“Karibu kila wilaya ina eneo ambalo ajali haziishi kutokea mara kwa mara. Nina imani Mungu hajanipa mkoa wenye maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajali. Nimekubaliana na viongozi  wangu wa madhehebu ya dini wataenda katika maeneo hayo, na kuomba Mungu atuondolee balaa la ajali za barabarani kwenye maeneo hayo” amesema.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amewaagiza viongozi wa madereva wa bodaboda na bajaji, kusimamia vema madereva hao ili wapunguze ajali za barabarani.
Mmoja kati ya wakazi wa Manispaa ya Singida, Njolo Kidimanda, amesema kuwa kuna haja  serikali kuongeza kiwango cha faini kwa madai kiwango kilichopo, hakiwaogopeshi kabisa  baadhi ya madereva.
Aidha, Kidimanda ameshauri madereva kuwa mstari wa mbele katika kuchangia damu salama, ili kusaidia majeruhi wa ajali barabarani wenye hitaji la damu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, jumla ya watu 68 wamefariki kutokana na ajali za barabarani kati ya Januari hadi Oktoba mwaka huu. Idadi hiyo imeonyesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na ajali za  barabarani kwa kuwa katika kipindi hicho hicho mwaka jana, watu 152 walifariki.

KILIMAANJARO STARS WAKIFANYA MAZOEZI LEO UWANJA WA MACHAKOS KENYA

December 04, 2017
 Picha mbalimbali za mazoezi ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara wakati wa mazoezi kujiandaa na mechi mbalimbali za kuwania Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa mazoezi wa Machakos, Kenya. Mazoezi hayo yalifanyika leo Jumatatu Desemba 4, 2017 asubuhi. (Picha na Cliford Ndimbo wa TFF).
NINJE AISIFU KILIMANJARO STARS, MBARAK KUIKOSA ZANZIBAR HEROES

NINJE AISIFU KILIMANJARO STARS, MBARAK KUIKOSA ZANZIBAR HEROES

December 04, 2017
Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Kocha Mkuu wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Conrad Ninje amepanga kesho Jumanne Desemba 5, 2017 kuanza kufanyia kazi upungufu ulioonekana kwenye mchezo dhidi ya Libya  uliofanyika Jumapili Desemba 3, mwaka huu.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kenyatta ulioko Machakos hapa nchini Kenya, Tanzania Bara ilipata sare katika safari ya kuwania Kombe la Cecafa – michuano inayofanyika hapa Kenya.
Ninje amesema katika mchezo huo wa kwanza waliecheza katika kiwango cha kuridhisha na kikubwa anataka kuangalia namna ya kufanyia kazi upungufu ikiwa ni pamoja na pale timu inapopoteza mpira.
Anasema kwenye mchezo dhidi ya Libya timu ilicheza kuanzia nyuma kupitia sehemu ya kiungo na kuunganisha sehemu ya ushambuliaji – jambo ambalo limemfurahisha kwa namna timu ilivyotengeneza nafasi.
Akizungumzia mchezo unaofuata dhidi ya Zanzibar Heroes, Ninje amesema ni mchezo mgumu kama ambavyo historia inaonesha wakati timu hizo mbili zinapokutana.
“Lakini kuanzia mazoezi ya kesho nitaiandaa timu kupata ushindi na nimepanga kwenda kuitazama Zanzibar itakapocheza mchezo wake wa kesho dhidi ya Rwanda,” amesema.
Amesema ataiangalia Zanzibar Heroes kiufundi ili kubaini upungufu wao ili naye ajue namna atakavyoweza kutumia nafasi hizo kwenye mchezo unaofuata.
“Ni fahari kwa timu zetu hizi mbili kila mmoja kupambana kupata pointi bahati nzuri wao wanacheza kesho kwa hiyo mchezo wao nitautumia kutazama mapungufu (upungufu wao) yao yatakayoweza kutusaidia,’’ alisema Ninje.
Leo Desemba 4, mwaka huu asubuhi kikosi cha Kilimanjaro Stars kimefanya mazoezi ya kuondoa uchovu baada ya mechi ya jana kabla ya hapo kesho kuanza rasmi kujiandaa kwa mchezo huo unaofuata.
Mbarak Yusuph ndiye mchezaji pekee ambaye hakufanya mazoezi hayo baada ya kuumia misuli kwenye mchezo wa jana dhidi ya Libya.
Mbarak atapumzishwa kwenye mchezo unaofuata ili kuwa tayari kuikabili Rwanda.
Leo jioni Kocha Ninje atakutana na wachezaji kuutathmini mchezo wa Libya ambao ulimalizika kwa sare ya bila kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Kilimanjaro Stars ipo kundi A pamoja na timu za Zanzibar, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.
Kenya wana pointi tatu baada ya kuifunga Rwanda mabao 2-0 wakati Kilimanjaro Stars na Libya wana pointi 1 kila mmoja baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo wao wa kwanza wakati Zanzibar na Rwanda wenyewe hawana pointi huku Zanzibar ikiwa haijashuka dimbani katika kundi hilo.

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPONGEZWA KWA USAMBAZAJI WA DAWA NCHINI

December 04, 2017
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI) katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja katika ziara iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

TIGO YAFUNGUA DUKA JIPYA LA KISASA MJINI SENGEREMA

December 04, 2017


Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema(shati jeupe) Alan Augustine na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo, Beatrice Kinabo wakikata utepe kuzindua duka la Sengerema mkoani Mwanza jana, Meneja Mauzo mkoa wa Geita Lugutu Lugutu akishuhudia.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema(kushoto) Alan Augustine akibadilishana mawazo na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo Beatrice Kinabo, baada ya kuzindua duka la Tigo mjini Sengerema.



Wananchi wa Sengerema wakishuhudia uzinduzi wa duka.
Meneja Huduma kwa wateja kanda ya Ziwa wa kampuni ya Tigo, Beatrice Kinabo, akizungumza na wakazi wa Sengerma wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo jana.

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA

December 04, 2017

 


Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika  bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.