Waziri wa Ajira, Vijana ATEMBELEA BANDA LA LAPF katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa

Waziri wa Ajira, Vijana ATEMBELEA BANDA LA LAPF katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa

July 05, 2016

L1 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo ya ujumla kuhusu Mfuko wa Pensheni wa LAPF katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa. Anayetoa maelezo ni Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko Bi. Rehema Mkamba.
L2 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mifumo ya Kompyta wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili kuhusu upatikanaji wa taarifa za michango ya wanachama kupitia tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz na simu za viganjani kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
L3 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akionyeshwa taarifa yake ya michango ya Hiari LAPF kwenye maonyesho ya biashara ya 40 ya kimataifa jijini DSM. Anayemhudumia ni Afisa Mafao ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi. Irene Michael.
L4 
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo kuhusu shughuli za uwekezaji za Mfuko wa Pensheni wa LAPF pamoja na mipango ya Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, anayetoa maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko Bw. James Mlowe.
L5Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kutoka Jeshi la Polisi wakipata maelezo mbalimbali ya Mfuko kutoka kwa Afisa wa Mfuko Bw. Yohana Nyabili kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini DSM.
L6Wanachama na wadau mbalimbali wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakipata maelezo mbalimbali kuhusu manufaa na huduma za Mfuko ikiwemo utaratibu wa kujiunga na kuweka akiba kwa hiari kwenye Mfuko. Anayetoa maelezo ni Afisa mafao wa Mfuko Bi. Judith Lupondo
TTCL YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA SEKTA YA MAWASILIANO NA TEHAMA SABASABA.

TTCL YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA SEKTA YA MAWASILIANO NA TEHAMA SABASABA.

July 05, 2016


Rais wa Rwanda, Paul Kagame (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mshindi wa Tatu Sekta ya Mawasiliano na Tehama (ICT) Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Prof. Tolly Mbwette (kushoto) kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto) Rais wa Rwanda, Paul Kagame (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mshindi wa Kwanza Sekta ya Mawasiliano na Tehama (ICT) Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Prof. Tolly Mbwette (kushoto) kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto)Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaoshiriki kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaoshiriki kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.Kulia ni baadhi ya wateja na wageni anuai wanaotembelea banda la kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.  Kulia ni baadhi ya wateja na wageni anuai wanaotembelea banda la kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.Kulia ni baadhi ya wateja na wageni anuai wanaotembelea banda la kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.  Kulia ni baadhi ya wateja na wageni anuai wanaotembelea banda la kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaoshiriki kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaoshiriki kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam. Pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette (kulia) Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam. Pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette (kulia).Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wakipiga picha na kufurahia tuzo mbili walizozitwaa katika kwenye maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Mwalimu Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI ZA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VIWANDA

July 05, 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Makame Mbarawa amezitaka Taasisi za Sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kukuza uchumi wa viwanda.

Amezitaka sekta hizo kutumia fursa za uwekezaji zinazotolewa na Serikali kama vile ujenzi wa reli ya kati, njia ya magari ya haraka (Dar- Chalinze express way) na upanuzi wa viwanja vya ndege mbalimbali nchini.

Ametoa pendekezo hilo jijini Dar es salaam wakati akifungua semina ya wataalamu wa Tanzania na China katika kujadili namna bora ya kuboresha miundombinu ya viwanda.

“Naamini kwamba serikali pamoja na Taasisi hizi zikishirikaiana kwa pamoja zitaweza kuboresha viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020”, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, amewataka wadau kutumia fursa hiyo katika kujifunza na kuiga mbinu mbalimbali zinazotumiwa na nchi ya China ambayo imeendelea katika sekta ya viwanda mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo.

Amefafanua kuwa kupitia uboreshwaji wa viwanda nchini, Serikali inatarajia kuongeza pato kutokana na ushindani wa kibiashara ambao utafanywa na wawekezaji kutoka nchi hizo mbili hususani katika masuala ya miundombinu.

“Tunakaribisha wawekezaji wengi kutoka China ambao wataleta mapinduzi ya viwanda nchini kwetu na hivyo kukuza uchumi na pato kwa ujumla”, amesisitiza Mbarawa.

Amesema kuwa suala la kuboresha viwanda linaenda sambamba na utunzaji wa mazingira kwani viwanda vingi vimekuwa vikileta athari katika afya ya mwanadamu.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Dkt. Suzan Kolimba, ameipongeza Serikali ya China kuichagua Tanzania kuwa ni nchi ya kwanza kuifanyia utafiti wa kujadili uboreshaji wa viwanda Afrika na kuahidi kutoa ushirikiano ili kutekeleza maendeleo chanya.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Lu Youqing, amesema kuwa kutokana na ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Serikali ya China na Tanzania anaamini kuwa wadau wa nchi hizo mbili watashirikiana kikamilifu katika kuwekeza na kuboresha viwanda nchini ili kuongeza uzalishaji.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana), wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing wakati wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika.
Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing kulia akiongea na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kushoto akiongea na mjumbe wa mkutano huo mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo .
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kushoto akifurahia jambo na Prof. Ibrahimu Lipumba mjumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.katikati ni Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika. Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

KAMPUNI YA EMOTEC YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA ZA TEHAMA

July 05, 2016
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella, akielezea moja kati ya gunduzi za kampuni yake kwa wageni (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka minne ya Chinese Alumni Association.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella (kulia) akielezea moja kati ya gunduzi ya kampuni yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Profesa Elisante Ole Gabriel (Wapili Kulia) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka mine ya Chinese Alumni Association nchini hivi .

Dar es Salaam, Julai 4, 2016. Kampuni mpya ya masuala ya TEHAMA nchini Tanzania, Emotec Limited yaeleza kuwa imejizatiti katika kutoa huduma bora na zenye ubunifu wa hali ya juu kwa wateja wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec, Bw. Mosses Hella imesema kuwa kampuni yake ina mpango wa kuwa inayoongoza katika utoaji wa huduma na bidhaa bora katika soko la TEHAMA nchini.
“Tumedhamiria kutoa bidhaa za gharama nafuu, huduma bora, za kibunifu na suluhisho kwa wateja wetu. Lengo letu kuu ni kuwa kampuni yenye ubunifu zaidi iliyojizatiti katika utoaji wa huduma bora na za gharama nafuu katika mausuala ya TEHAMA nchini.” Alisema Bw. Hella
Bw. Hella amesisitiza kuwa kampuni yake pia inayo dhamira ya kubuni, kutengeneza, kusambaza na kufanyia marekebisho vifaa mbalimbali vya umeme hususani simu za mkononi, tablet, kompyuta, router na modemu za intaneti pamoja na luninga ambapo wamejikita zaidi katika ubora.
Mbali na hayo aliongezea kuwa Emotec ni kampuni ya masuala ya TEHAMA inayotazamia pia kutoa huduma za vitabu kwa njia ya mtandao (e-content) katika kusaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini.
“Pia tunawekeza katika kubuni na kuchapisha vitabu kwa njia ya mtandao (e-content) kwa ngazi za elimu ya shule ya msingi, sekondari na ya juu ili kusaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini.” Alibainisha
Aliongezea pia shughuli nyingine ambazo kampuni yake inajihusisha nazo ni pamoja na kubuni, kufunga na kusaidia Maabara ya Usimamizi wa Mifumo wa Taarifa, Mifumo ya Usimamizi wa Mapato, Mifumo ya Usimamizi wa Taarifa za Shule, Mifumo ya Usimamizi ya Hoteli na mifumo ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.
Kwa kuongezea zaidi kampuni pia imewekeza katika kubuni, kufunga na kusaidia mifumo midogo ya fedha na program tanzu ya kibenki lakini pia ina mfumo mzuri wa kimtandao kwa bandari, viwanja vya ndege na vituo vya makontena.

“Hivyo basi ningependa kuchukua fursa hii kuwaalika watanzania kutembelea banda letu katika maonyesho ya 40 ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo tunaonyesha bidhaa zentu zenye ubinifu na tekinolojia ya kisasa kabisa kwani hapo ndipo mahali wanapoweza kujua mengi zaidi kuhusu kampuni yetu.” Alihitimisha Bw. Hella

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJITOKEZA WAWEZESHWE KUWEKEZA KWA AJILI YA MAENDELEO

July 05, 2016
Mkurugenzi wa kitengo cha Africa wa JICA, Hideki Watanabe akielezea Jinsi JICA wanavyofanya shughuli za Maendeleo Afrika
Mdau kutoka Namaingo Bi. Mariam akichangia jambo
Mkurugenzi wa Namaingo Bi.Ubwa Ibrahim akimwelezea jambo mwakilishi wa benki ya rasilimali (TIB) walipokutana katika semina ya uwezeshaji mitaji kwa ajili shughuli za maendeleo.
Watoa mada kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za kifedha wakijibu maswali kutoka kwa wadau waliohudhuria semina hiyo.

Washiriki wakifuatilia semina

  

Wajasiriamali wakubwa kwa wadogo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa zilizopo ili waweze kuwezeshwa mitaji ili wawekeze katika shughuli za maendeleo ili kupunguza tatizo la ajira hapa nchini na kusaidia juhudi za serikali na wadau kuleta maendeleo hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Balozi wa Japan hapa nchini Bwana Masaharu Yoshida alipokua akifungua semina ya wadau wa maendeleo iliyojadili uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali kwa ajili ya shughuli za maendeleo iliyofanyika jana (5/6/2016) jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo iliyoandaliwa na shirika la ushirikiano na maendeleo la Japan (JICA) pamoja na taasisi ya sekta binafsi hapa nchini (TPSF) ilihudhuriwa na mashirika na taasisi za kifedha pamoja na wajasiriamali kutoka sekta binafsi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watoa mada walionesha kuwa kuna fursa kubwa kwa watanzania wote walioamua kuwa wajasiriamali kwa kufungua viwanda vidogo kwa vikubwa, wakulima na wafanyabiashara kutumia mashirika na taasisi za fedha kujipatia mikopo nafuu ili kuwezesha kukuza biashara na viwanda vyao na wanaweza kulipa kwa muda mrefu kwa riba nafuu.

Semina hiyo ilibainisha kuwa changamoto kubwa ni kutokua na taarifa kwa watanzania wengi na hivyo kuogopa kuwekeza kwa kutumia taasisi za fedha jambo lililoungwa mkono na washiriki wengi kwani imebainika kuwa ni asilimia 16 tu ya watanzania wanatumia huduma za kibenki hivyo wameaswa kubadilika waweze kunufaika na mitaji ambayo ipo lakini hakuna wanaokidhi vigezo ambapo wanaofuatilia na kunufaika ni watu wachache.

Mwavuli wa wajasiriamali wa Namaingo (Namaingo Business Agency) ni moja ya taasisi zilizohudhuria na ziliahidiwa kupewa ushirikiano na wadau wote wa kuwasaidia kufikia malengo yao kwani mitaji ipo na Namaingo inakidhi vigezo vyote vya kukopesheka kwani mpango kazi wake uko kitaalamu na ushiriki wa serikali na taasisi zake unaifanya iwe mkombozi kwa watanzania wengi maskini.

Akizungumza baada ya semina hiyo Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bi. Ubwa Ibrahim aliwataka watanzania wote wajitokeze kujiunga na taasisi yake wawekwe katika mpango wa kuwarasimisha na kuwawezesha kuingia katika mipango ya kuwainua kiuchumi kwani kuna mradi wa kijiji biashara ambacho wanachama wanatarajia kukopeshwa ardhi, kujengewa nyumba za makazi, kukopeshwa mradi uliokamilika (kilimo na ufugaji) pamoja na utaalamu na usimamizi wa mradi husika.

“Kwa sasa tuko katika hatua ya utekelezaji ambapo tarehe 28 mwezi huu tunasaini mikataba na serikali na wadau wengine Diamond Jubilee. Naomba watanzania waje washuhudie na kusikia juu ya mradi ili waamini maanake kuna watu wanaongea bila kutenda, mimi nawakaribisha  waje waone utendaji na tuwape ushuhuda wa hatua tulizokia kwenye mradi wetu wa kijiji biashara ambapo serikali imetoa ekari 44,000 kwa ajili ya mradi huu. Maendeleo hayakusubiri hivyo kila mtu achangamke aje atuone tumweke kwenye mpango rasmi” alisema Bi.Ubwa.

Mwanasheria wa taasisi hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Bwana Payas alisema kila siku kuna mafunzo katika vituo vya Namaingo vilivyopo Ubungo, Ukonga na Temeke ambapo alisema wajasiriamali hupewa mafunzo kabla ya kuingizwa rasmi katika mpango wa kampuni.  “Namaingo tunawezesha wajasiriamali kusajiliwa TRA, BRELA, TFDA, Bima ya afya, mifuko ya jamii na kuwaunganisha wao kwa wao. Kila Jumamosi tunakaribisha wanachama wapya wanaopewa maelekezo na kuelezwa juu ya mradi wetu mkubwa wa kijiji biashara kilichopo Mbawa, Rufiji ambapo Namaingo inaratibu mradi huo pamoja na wadau wa maendeleo tukisimamiwa na baraza la uwezeshaji chini ya ofisi ya waziri mkuu” aliongeza.


Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com 1458109219454_logo_blog_za_mikoi.png
Dk. Kigwangalla akutana na balozi wa Korea kujadili kuhusu Hospitali ya Mlonganzira

Dk. Kigwangalla akutana na balozi wa Korea kujadili kuhusu Hospitali ya Mlonganzira

July 05, 2016

Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na urafiki na Korea na katika kulidumisha hilo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-young amemtembelea Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Korea na Tanzania zaidi katika sekta ya afya na jinsi Korea ambavyo imekuwa ikisaidia uboreshwaji wa huduma za kiafya nchini.

Akizungumza na Mo Blog kuhusu ugeni huo, Dk. Kigwangalla alisema kuwa balozi Geum-young alitaka kujua kama naibu waziri anafahamu kuhusu ujenzi wa chuo na hospitali ya Mlonganzira ambapo alitaka kufahamu kama serikali itakuwa tayari kutoa watumishi wa afya 900 ambao watahudumia hospitali hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea na jinsi ambavyo nchi hiyo imepanga kuendelea kuisaida Tanzania katika kuboresha huduma za kiafya nchini. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

Katika hilo Dk. Kigwangalla alimuhakikishia balozi kuwa serikali ipo tayari kutoa wataalam wa afya ambao watakuwa wakitoa huduma katika hospitali ya Mlonganzira ambayo itakuwa na vifaa vya kisasa kutoka Korea na itakuwa na vitanda 600 ambavyo vitakuwa vinatumiwa na wagonjwa wanaofika kupata huduma.

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akifanya mazungumzo na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, alipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumza mambo yanayohusu mahusiano ya Tanzania na Korea.

Jambo lingine ambalo walizungumza ni kuhusu msaada wa magari ya kutolea huduma za kiafya ambayo yanatembea 'mobile clinic' ambayo yatatolewa kwa kanda zote nchini na zaidi katika maeneo ambayo yanaonekana kuwa na ugumu kufikika na kuwa na vituo vya afya vichache.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin na wapili kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kulwa.

"Amesema watatuletea convoy zaidi ya sita (kila moja ina magari 10) ambayo yatagawiwa kwa kila kanda nchini, magari haya kila gari linakuwa na mengine 10 ambayo yanakuwa na huduma mbalimbali za kiafya kama chumba cha upasuaji, store ya madawa, maji na mengine ambayo yanahitajika kutoa huduma kwa mgonjwa," alisema Dk. Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo.

Aidha aliongeza kuwa magari hayo ya kutolea huduma za afya ambayo yanatembea 'mobile clinic' yanataraji kuletwa nchini mwakani mwezi Januari na kwasasa wizara imetakiwa kuandika andiko la mradi ili kuonyesha kuwa imekubali kuingia katika mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa maeneo ambayo yana vituo vichache vya afya.

Na Rabi Hume, MO Blog
Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin akibadilishana mawasiliano na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katikati ni balozi wa Korea nchini, Song Geum-young.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young baada ya kumaliza kufanya mazungumzo.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAKUMBUKA WENYE UHITAJI.

July 05, 2016
Siku chache kabla ya kusherehekea Siku Kuu ya Idd, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (pichani), amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula kwa watoto ajili ya yatima pamoja na wazee mkoani Mwanza.
Na BMG
Jana Mhe. Mongella alikabidhi mbuzi 20, mafuta ya kula ndoo 20, kila moja lita 20, mchele mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 50 pampja na sukari mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 25.

Vituo saba vya watoto yatima mkoani Mwanza vilinufaika na msaada huo ni Nabawi Mbugani, Markaz Riyabwa-Nyakurunduma, Markaz Sharif Said-Nyegezi, Markaz Sainaa, Islamic Yatima, Jawhary Butimba, Muuminu Kabuhoro pamoj na Masjid Noor-Nyakato huku kituo cha Wazee Bukumbi nacho kikinufaika na msaada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (wa tatu kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula kwa wahitaji mkoani Mwanza, ili kusherehekea katika sikukuu ya Idd inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu.
Baadhi ya ichimburi a.k.a mbuzi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwa ajili ya kitoweo kwa watu wenye uhitaji wakiwemo yatima na wazee mkoani Mwanza ili waweze kusherehekea vyema siku kuu ya Idd.

MFALME WA AFRO POP TWENTY PERCENT ARUDI KWENYE GEMU KWA KISHINDO NA SAUTI YAKE YA GHARAMA

July 05, 2016
Na Sultani Kipingo
Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki,  huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.
Twenty Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo  za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.
"Nimerudi kuwachinja tena" anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam. "Nimerudi kurudisha sauti ya gharama  kwa jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, " anaogeza.
Tayari Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer Mann Water.
Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses.
"Namkubali sana Twenye Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo", anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na  wasanii nyota kibao wakiwemo  Lady Jay Dee,  Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.
 Twenty Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa "Manemane" uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni "Tamaa Mbaya"  na "Ya nini Malumbano" na "Maisha ya Bongo"   
Mbali na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo. "Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili kuwachinja tena" alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa  na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent)   akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi zake huku  akishuhudiwa na Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto), Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.