RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGEA NA WAHARIRI, WATANGAZAJI NA WAANDISHI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA 4,2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGEA NA WAHARIRI, WATANGAZAJI NA WAANDISHI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA 4,2016

November 05, 2016

1jhdfdh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4,2016
2 baadhi ya wapigapicha wakichukua matukio katika mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipoongea na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4,2016
e2

3Mkurugenzi wa Azam Media Tido Muhando akiuliza swali  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokua akiongea na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4,2016
e4

e9Mwandishi wa habati wa  Shirika la utangazaji BBC Sammy Awami akiuliza swali  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokua akiongea na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4,2016
e10Mhariri mtendaji wa magazeti ya Serikali (TSN) Dr. Jim Yonazi akiuliza swali  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokua akiongea na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4,2016
4

6

7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na msanii wa Mrisho Mpoto mara baada ya kuongea  na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 4,2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI WAKUNGA

November 05, 2016

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani ,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) na Mkurugenzi Shirika la AMREF Health Africa Dkt. Florence Temu (kulia). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye   Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Umati uliohudhuria na kushiriki Matembezi ya Hisani ya Kusomesha Wauguzi  Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground.
                                     ..................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.3 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.

Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.
Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.
Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
MSUVA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI OKOTOBA

MSUVA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI OKOTOBA

November 05, 2016
msuva-leo
 Winga Simon Msuva wa Young Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Msuva alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang’anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.
Katika mwezi Oktoba ambao ulikuwa na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).
Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
RAIS DKT SHEIN AFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO PEMBA

RAIS DKT SHEIN AFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO PEMBA

November 05, 2016
z1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika Ndege ya Shirika la Ndege la AIR Tanzania mada baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo,Rais akiwa kisiwani humo atafungua miradi mbali mbali ya Maendeleo,
z2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa wakati alipotembelea sehemu mbali mbali baada ya kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,(kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu.
z4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,
z5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,
z6
Baadhi ya wananchi kutoka shehia mbali mbali katika Wilaya ya Chake chake Pemba wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo.
z7
Viongozi wa Idara ya Mahakama wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo Chakechake Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo.
z8
Majaji wa Mahkama Kuu na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Idara hiyo wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo Chakechake Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo
z9
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(kushoto) wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake zilizofanyika leo Viwanja vya Mchezo wa Tenis Chakechake Pemba,
z10 z11
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake zilizofanyika leo Viwanja vya Mchezo wa Tenis Chakechake Pemba, [Picha na Ikulu.] 05 Nov 2016.

PINDA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA

November 05, 2016
 Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
 Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara,
Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya MakaoMakuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana.
(Picha zote na Bashir
Nkoromo).
BUNGE LAPITISHA RASMI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WA 2016.

BUNGE LAPITISHA RASMI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WA 2016.

November 05, 2016


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akitoa hoja kabla Kamati ya Bunge zima kujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ambao umepitishwa leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge akitoa maelekezo wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ili mjadala uwe na tija kwa maendeleo ya tasnia ya habari, wanahabari na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Aannastasia Wambura akichangia hoja juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Possi Abdallah akichangia hoja juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Mhe. Saada Mkuya Salum akichangia hoja juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Wabunge wakiwa kwenye mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) wakifuatilia mjadala wa Wabunge wakati wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) wakifuatilia mjadala wa Wabunge wakati wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni wakifuatilia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo mara baada ya kupitishwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma. Wa nne kulia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
EU YAWEKEZA EURO MILIONI 1.7 KITUO CHA UTAMADUNI MAKUMIRA

EU YAWEKEZA EURO MILIONI 1.7 KITUO CHA UTAMADUNI MAKUMIRA

November 05, 2016
Umoja wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya burudani itakayogharimu kiasi hicho.

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer amefanya ziara chuoni hapo ambapo amejionea shughuli za ujenzi zinazoendelea katika chuo hicho na kusema kuwa kupitia chuo hicho cha utamaduni wa Tanzania na makabila yake utaendelezwa ili kuleta manufaa kwa vijana na jamii nzima.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za kutunza utamaduni kwani vijana wataweza kutengeneza fursa za ajira kupitia sanaa za utamaduni.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akizungumza katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha,mara baada ya kutembelea kituo hicho.(Picha na Ferdinand Shayo).

Meneja mradi huo Randall Stubbs amesema kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo ya ngoma za utamaduni wa makabila ya wamasai, wameru na wachaga ikiwa ni pamoja na kufanya maonyesho ya utamaduni katika maeneo mbalimbali.

“Ujenzi utakapokamilika kutakua na ukumbi wa kisasa, jengo maalumu la mafunzo kwa utamaduni wa bara la Afrika, Asia na Ulaya ili utamaduni uweze kuwa endelevu na kurithishwa vizazi na vizazi” alisema Randall.
Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelekezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer alipotembelea kituoni hapo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha, mara baada ya kutembelea kituo hicho.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha utamaduni cha Makumira jijini Arusha.
Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kulia).

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO MHANDISI FELCHESMI MRAMBA, ATEMBELEA VITUO VIPYA VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VYA JIJINI DAR ES SALAAM

November 05, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam .


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea vituo vitatu vipya vya kupooza na kusambaza umeme vilivyo kwenye mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.

Vituo alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha Ilala Mchikichini.

Kwa takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali ya juu.

“Nimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya kubadilisha miundombinu yetu ya umeme, wakazi wa jiji la Dar es Salaam, sasa watapata umeme wa uhakika na ulio na ubora wa hali ya juu, jambo la kufurahisha sana ni kwamba mabadiliko haya yamekwenda sambamba na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda, bila shaka umeme huu utawezesha kufikia azma hiyo ya serikali.” Alisema Mhandisi Mramba, baada ya kukagua kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha katikati ya jiji.
Mhandisi Mramba alisema, nia ya TANESCO ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya kukatika umeme mara kwa mara au kupata umeme hafifu usio na nguvu. “Mmeona mitambo hii nimipya kabisa nay a kisasa inayotumia teknolojia ya kisasa.” Alitoa hakikisho.

Maboresgho hayoyalihusisha ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) , kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupoozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema,

Alisema, ujenzi wa mfumo huo wa njia ya umeme wa ardhini (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 ni kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City.Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika ulio kwenye viwango stahiki,

Naye Meneja Mwandamizi wa Miradi yausafirishaji na usambazaji umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Geirge Chegere, alimueleza Mhandisi Mramba kuwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.

Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuriya Muunganowa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, baadaye mwezi huu wa Novemba.


Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.akielezea hatuailiyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, akielezea teknolojia ya kisasa ya mashine ndogo yenye kufanya kazi kubwa
Kituo cha City Centre
Mhandisi Mramba, akitembelea mitamboya kituo cha City Centre
Fundi mitambo ya umeme akiwa kazini kituo cha Ilala Mchikichini
Mhandisi Mramba, (kushoto), akizungumza wakati alipotembelea kituo cha Kupooza na kusambaza umeme cha Kurasini kujionea maendeleo yaujenzi wa kituo hicho
Mitambo ya kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Kurasini
Mhandisi Chegere (wapili kulia), akipatiwa maelezo ya mitambo ya kituo cha City Centre
Jengojipya la kituo cha Ilala Mchikichini
moja ya mashine mpya kituo cha Ilala Mchikichini
Chumba cha mitambo mipya ya umeme kituo cha Ilala Mchikichini
Mhandisi Mramba, akiwa na wahandisiwenzake, Chegere (kulia) na Mgaya, kwenye kituo cha City Centre
Mitambomipya kituo cha Kurasini