KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI JESHI LA POLISI NCHINI

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI JESHI LA POLISI NCHINI

February 21, 2016

mej1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipokelewa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala, SACP Lucas Mkondya, alipofika kufunga kikao  kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
mej2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza wakati wa kufunga kikao  kazi cha Maafisa Maandamizi wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
mej3
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakati wa kufungwa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa hao uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
mej4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wanne kushoto waliokaa), Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu (kushoto kwa Katibu Mkuu) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, mara baada ya kufungwa Mkutano wao wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MIKAELA PROFESSIONAL TAILORS WAPANIA KUWAINUA WABUNIFU WA MAVAZI JIJINI MWANZA.

February 21, 2016
Idda Adam ambae ni Mkurugenzi wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza, akionyesha mavazi mbalimbali yanayopatikana ofisini kwake, Mtaa wa Ghana GreenView, Nyamanoro Jijini Mwanza.

"Sisi tunahusika na suala la urembo pamoja na ushonaji wa mavazi ya kila aina ikiwemo mavazi ya Kitchen Party pamoja na Harusi (Wanaume kwa wWanawake). Tumelenga kukata kiu ya ushonaji wa mavazi kwa wakazi wa Jiji la Mwanza ambao awali walikuwa wakishona nguo zao nje ya Mwanza;

Pia tunawatumia wabunifu wa mavazi kutoka Jijini Mwanza na kutumia ujuzi wetu wa ushonaji na hivyo kuzalisha mavazi ambayo wateja wetu wamekuwa wakiyafurahia". Anasema Idda na kuwahimiza kutembelea ofisini kwake au kuwasiliana nae kwa nambari 0767 68 28 88.
Idda Adam anasema Mikalea Professional Tailors wabunifu na washonaji wa mavazi ya kila aina.
Mavazi mbalimbali kutoka Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza
Mavazi mbalimbali kutoka Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza
Mkurugenzi akiteta jambo na fundi wake 
Mafunzi Ushonaji wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza wakiendelea na shughuli za ushonaji.
George Binagi-Binagi Pazzo (Kushoto) akizungumza na Idda Adam (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHANDISI NGONYANI ATEMBELEA BANDARI YA TANGA.

February 21, 2016


PRO wa Mamlaka ya Bandari TPA Tanga,Moni Jafuru akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi kulia ili amkaribishe  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto aliyefanya ziara ya kutembelea Bandari hiyo.

Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja baina yao na
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kushoto  ambaye alitembelea bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi zake
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kushoto akizungumza na viongozi wa mamlaka ya Bandrai Mkoani Tanga wakati alipfanya ziara yake kulia kwake ni
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya



PRO wa Mamlaka ya Bandari TPA Tanga,Moni Jafuru akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi kulia ili amkaribishe  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto aliyefanya ziara ya kutembelea Bandari hiyo
 







Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya kushoto akimuonyesha baadhi ya maeneo yanayotumika kupakulia mizigo nangani  Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wa kwanza kulia alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari hiyo.


Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani akisisitiza jambo wakati alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari ya Tanga kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya TangaKaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya

Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya katikati akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani wakitembelea Bandari ya Tanga .

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani kwenye shuti akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya kushoto akimuelezea namna wanavyofanya kazi kulia ni Moni Jafuri ambaye ni PRO wa Bandari ya Tanga wakati alipofanya ziara ya kuitembelea
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kwenye shuti katikati akitembelea bandari ya Tanga kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitazama matishari yaliyonununuliwa na Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga yanayotumika kwa ajili ya ukuaji wa mizigo.
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI FAMILIA YA MOSHA

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI FAMILIA YA MOSHA

February 21, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo Fred Mosha kilichotokea jana alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Katika salamu hizo, TFF imewapa pole familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki kufuatia kifo hicho, na kusema wapo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Fred Mosha mpaka umauti unamfika, alikuwa mkuu wa kitengo cha habari cha Tv/Redio Tumaini iliyopo jiini Dar es salaam na msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Mbagala Saku kwa Mkongo.
Mazishi yanatarajiwa kufayika kesho Jumatatu saa 9 mchana katika makaburi ya Kinondoni.