“POLISI TANGA WAWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UHALIFU”

January 02, 2015

NA MWANDISHI WETU,TANGA.
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limejiwekea mikakati kabamba ya kukabiliana na uhalifu kwa mwaka huu kwa kuishirikisha jamii kwa kutumia viongozi wa serikali za mitaa na vijiji kusimamia mpango wa ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa na kuhuisha vikundi vya ulinzi shirikishi.

Kauli hiyo ilitolewa  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai wakati akizungumza na MTANDAO HUU ambapo alisema jambo jingine ni kuhamasisha matumizi ya daftari la makazi ili kubaini wageni wanaoingia na kuweza kuwafuatilia nyendo zao.

Alisema kuwa kitu kingine ni kuimarisha usalama kwenye maeneo ambayo yameonekana kuwa na tatizo kubwa la kiuhalifu kwa kuimarisha doria na misako ya mara kwa mara kwa kushtukiza ili kuweza kuwabaini wahusika na kuchukuliwa hatua.

Kamanda huyo alisema licha ya hayo watahakikisha wanawapima madereva wanaoendesha magari yanayosafiri kwenda nje ya mkoa wa Tanga ikiwemo kuwapima vilevi kila wanapotoka stendi kuu ya mabasi iliyopo mkoani hapa kwenda mikoa mingine

Aidha alieleza kuwa watatumia pia wakaguzi wa Tarafa na mfumo wa polisi kata kwa ujumla kama vyanzo muhimu vya taarifa zinazoonyesha dalili za awai za kuwepo kwa uhalifu au mgogoro wa makundi fulani ya jamii na kuyashughulikia mapema kwa kushirikiana na wadau wengine.

Hata hiyo alisema kuwa ndani ya mwaka huu watatoa elimu kwa pande zilizo katika migogoro juu ya hatua za kisheria zifaazo kuchukuliwa ili kufikia ufumbuzi wa kudumu wa migogoro husika kwa kupitia askari kata ikiwemo kuendelea kufuatilia hatua za utatuzi wa migogoro hiyo katika vyombo husika  ili kuendelea kushauri kitu gani cha kufanya kama rufaa badala ya kuchukua sheria mkononi.


JALALA NDANI YA KITUO CHA DALADALA, CHAKE CHAKE PEMBA

January 02, 2015


 Wakazi wa Chake Chake Wilaya ya Kusini Pemba akipita katika jalala lililosambaa takataka kilipo kituo kikuu cha daladala yaendayo Wilayani na katikati ya mji huku baadhi ya wenye maduka na wafanyabiashara ya vinywaji na vitafunwa wakilalamika kwa kuongezeka kwa harufu kali eneo hilo.



SHUGULI MBALIMBALI ZA WAZIRI MKUU PINDA NA MKEWE MAMA TUNU WILAYANI MLELE

January 02, 2015

Wanakwaya wa kwaya ya Makuhani ya Kanisala la EAGT Makanyagio, Mpanda wakiimba katika uzinduzi wa Album yao ya Tuiombee Afrika uliofanywa na mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda kwenye ukumbi wa Shule ya Saint Mary's ya Mpanda Desemba 31, 2014.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanakwaya wa kwaya ya Makuhani ya Makanyagio, Mpanda wakati alipozindua Album yao ya Tuiombee Afrika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Saint Mary's Desemba 31, 2014.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akionyesha DVD ya Tuiombee Afrika ya kwaya ya Makuhani ya Kanisa la EAGT la Makanyagio, Mpanda wakati alipozindua Album hiyo kwenye ukumbi wa Saint Mary's mjini Mpanda Desemba 31, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari ya Usevya wakati alipoitembeklea na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo Januari 1, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Usevya wakati alipoitembeklea na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo Januari 1, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

RIDHIWANI KWETE AANZA ZIARA YA KIKAZI KATIKA VIJIJI 40 CHALINZE

January 02, 2015

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG







 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.
Watioto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea mnara
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi  kuboresha barabara na mawasiliano ya simu
Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Kwa Mduma wakati wa ziara yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata ya Kibindu

TAASISI YA FINCA YATOA MILIONI 17 KWA WAJASILIAMALI (3)

January 02, 2015

SAM_0611
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda wa pili kulia akikabidhi hundi  ya shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vijago jijini walizo kopa kwa ajili ya kufanya biashara kabla wa soko lya kunguliwa na soko hilo mapema mwezi uliopita
SAM_0617
Meneja wa  taasisi hiyo Baraka Jekonea akiongea na vyombo vya habari
SAM_0613
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda akiongea katika halfa hiyo
 
……………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Felix Ntibenda ameipongeza taasisi inayotoa huduma za kifedha (FINCA)kwa kuwafutia  zaidi ya milioni 30 wanachama 35  wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vinyago hela walizo kopa kwa ajili ya kufanya biashara kabla ya soko loa kunguliwa  mapema mwezi uliopita.
Ntibenda alisema  hayo jana wakati akikabidhi hundi  ya shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali hao  mbele ya waandishi wa habari iliyofanyika eneeo la soko hilo lililoko wilaya ya arusha mkoa wa arusha.
Kwa upande wa meneja  taasisi hiyo Baraka Jekonea alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuendeleza ujenzi wa  soko hilo I benki hiyo in warudi katika hali yao ya zamahi ya biashara .
“Sisikama Taasisi ya Kifedha Finca tumeamua kuwasaidia ili tuweze kuwanusuru wahanga hawa kwa janga walilolipata tunaimani kwamba watarejea katika hali yao ya zamani kwani tangu wakumbane na changamoto hiyo maisha yao yamekuwa magumu sana”alisema Jekonea
Pia alitoa wito kwa wafanyabiashara ambao hawajajiunga na taasisi hiyo kufanya hivyo kwa kuwa benki hiyo inajali wajasiriamali na kuwataka kujiunga na taasisi ya mikopo ili kuweza kupata mikopo ya nafuu.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa soko hilo Hamis Juma alishukuru taasisi kwani pesa hiyo itawasaidia sana sana katika kujikwamua na kurejesha hali yao ya awali katika biashara yao.
Hata hivyo kabla ya msaada   huo walijichangisha kiasi cha shilingili laki nane kwa kila muhanga nakufanikiwa kukusanya shilingi milioni mia mbili iliyowasaidi kuanza ujenzi wa soko hilo.
Aidha mwenyekiti huyo ameomba taasisi nyingine ili kuweza kuwasaidia kuwapatia mitaji ili kuweza kuanza upya tena biahsra hiyo ya uuzaji wa vinyago.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

HAFLA FUPI YA BIRTHDAY YA SHARIFA MMASI, MWANDISHI WA MICHEZO WA BINGWA ILIVYOFANA (JANUARY 1 2015)

January 02, 2015
Sharifa Mmasi (kulia) akimlisha Keki, mmiliki wa mtandao wa Kijiwe Chetu Blog, Fadhili Athumani (kushoto) "Prof. FAdhili" katika hafla fupi ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika katika ofisi za New Habari, mkoani Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro (inayochapisha magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, Rai na The African)
Fadhili Athumani (kushoto) akimlisha Keki, Sharifa Mmasi
Happy Birth Day!!
Sharifa Mmasi (Bingwa) akimlisha keki Winnie 
Kutoka kushoto Deo Macha (ITV), Winnie Queen (Daily News), Sharifa Mmasi (Bingwa) na Fadhili Athumani (Mtanzania) katika hafla fupi ya kumpongeza Sharifa katika siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Januari 01, mwaka 2015 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro
Mwandishi wa gazeti la Bingwa, Sharifa Mmasi (Kushoto)  akimlisha Keki, Rodrick Mushi anayeandikia gazeti la Mtanzania (magazeti yote yanachapishwa na kampuni ya New Habari (2006) Ltd)