CHADEMA YAPATA PIGO TANGA,MWENYEKITI WA KATA WAO ARUDI CCM.

January 15, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kata ya Mwanzange jijini Tanga,Said Bakari amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuchoshwa na sera zisizotekelezeka ndani ya chama chake ambazo hazina mashiko.

Uamuzi huo aliutangaza katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata hiyo ulikuwa ukihutubiwa na Mwenyekiti wa cha Mapinduzi wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni ambao aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kati kwenye mkutano huo,Bakari alisema awali alijiunga na chadema akitokea chama cha mapinduzi akidhani  chama hicho kina mashiko na wananchi badala yake mambo aliyoyakuta hayakuwa kama alivyotarajia.

RAIS KIKWETE ASHAURIWA JUU YA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

January 15, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameshauri kuwachagua mawaziri waledi na wazalendo ambao watahakikisha wanafanya kazi zao ipasavyo lengo likiwa ni kuharakisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kipindi kifupi kilichobakia.

Ushauri huo ulitolewa leo na Mtaalamu wa Uendelezaji Biashara
nchini(Business Development Expert) ,Mtaturu Mkonongo wakati
akizungumza na TANGA RAHA BLOG ambapo alisema kabla ya kuelekea uchaguzi mkuu mabadiliko kwenye nafasi za mawaziri unapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa ikiwemo uwajibika kwa watakaoteueliwa.
January 15, 2014

Wednesday, January 15, 2014

BREAKING NEWS.....MAGARI MAWILI YAWAKA MOTO IRINGA WAKATI WANAFUNZI WAKIJIFUNZA KUUNGA NGAO


Wananchi Iringa  mjini  wakilitazama daladala  lililowaka  moto wakati likiwa kwa mafundi kuunga likichomelewa leo eneo la uwanja wa  samora
Daladala  likiwaka  moto  huku kikosi cha zimamoto na uokoaji  wakizima moto huo
Gari la Zimamoto na uokoaji mjini Iringa likizima moto  uliokuwa ukiteketeza daladala eneo la Samora  leo
January 15, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL NA MKEWE MAMA ZAKIA BILA WAWAJULIA HALI MAWAZIRI WALIOLAZWA MUHIMBILI, CLEOPA MSUYA NA HARUNA ALI SULEIMAN.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo, Jan 15, 2014. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo. Kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman, aliyelazwa katika jengo la Moyo Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipofika kumjulia hali leo. Katikati ni mke wa Makamu, Mama Zakia Bilal (kushoto) ni Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga. Picha na OMR Meneja wa Jengo hilo la Moyo, Sr. Salome Kassanga.