January 28, 2014

BALOZI MDOGO WA INDIA NA MWAKILISHI WA (WHO) WAMUAGA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) anefanyia kazi Zanzibar Dk.Pierre Kahozi,leo alifika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga  Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mdogo wa India anefanyika kazi Zanzibar Pawan Kumar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi kumuaga  Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mdogo wa India anefanyika kazi Zanzibar Pawan Kumar,baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi kumuaga  Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi. Picha na Ramadhan Othman IKulu.

RAIS KIKWETE AKAGUA MAENEO YA MAFURIKO MKOANI MOROGORO.

RAIS KIKWETE AKAGUA MAENEO YA MAFURIKO MKOANI MOROGORO.

January 28, 2014
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mahema yaliyowahifadhi wahanga wa Mafuriko katika kijiji cha Magole,mkoani Morogoro wakati alipotembelea maeneo yaliathiriwa na mafuriko na kuwapa pole wananchi jana. D92A5298 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua nyumba zilizoharibiwa na mafuriko katika kijiji cha Mateteni, Dakawa Mkoani Morogoro jana. D92A5306 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasaidia watoto kuteka maji katika kisima kilichipo katika kijiji cha Mbigiri kata ya Mateteni, Mkoani Morogoro wakati alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko jana. D92A5340 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasaidia watoto kuteka maji katika kisima kilichipo katika kijiji cha Mbigiri kata ya Mateteni, Mkoani Morogoro wakati alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko jana. D92A5357 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua nyumba zilizoharibiwa na mafuriko katika kijiji cha Mateteni, Dakawa Mkoani Morogoro jana. D92A5369 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto Amos Msisiri(5) katika kijiji cha Mbigiri kata ya Mateteni Dakawa Mkoani Morogoro wakati Rais alipokagua maeneo yaliyoathiriwa na Mafuriko yaliyotokea hivi karibuni na kuleta uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu(picha na Freddy Maro).
January 28, 2014
January 28, 2014

MAKAMU RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA NA MANAIBU WAKE IKULU DAR,AKUTANA PIA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA STATOIL TANZANIA.

02Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na manaibu wake, Mwigulu Nchemba na Adam Malima, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 28, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Statoil Tanzania Oystein Michelsen (wa pili kushoto) Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Oivind Holm (wa pili kulia) Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Genevieve Kisanga (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi, Grace Usara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
January 28, 2014

MWANDISHI WA HABARI LEO KILIMANJARO, ARONLD SWAI, MWENYEKITI MPYA UVCCM WILAYA YA HAI

Arnold Swai (wa kwanza kushoto)wakati wa upigaji kura, zoezi lilofanyika juzi, wilayani Hai kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti
Mjumbe wa Halmshauri kuu CCM wilaya ya Hai, Fuya Kimbita, akizungumza katika zoezi la kupiga kura lililoshuhudia Mwandishi wa Habari Leo, Arnold Swai akiibuka kidedea.

MKWAKWANI KUKARABATIWA TENA BAADA YA KUMALIZIKA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU

January 28, 2014

Na Oscar Assenga, Tanga.
UONGOZI wa Uwanja wa Mkwakwani umesema awamu ya pili ya ukarabati wa uwanja huo unatarajiwa kufanyika mara baada ya kumalizika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara mwaka huu lengo lao likiwa ufikie kwenye viwango vya kitaifa na kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga,
  Gustav Mubba wakati akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo ambapo alisema suala la ukarabati wa uwanja huo ni mkakati wao waliojiwekea kila mwaka.

YANGA YALITIKISA JIJI LA TANGA,COASTAL KUWAFUNGA MIDOMO YANGA KESHO.

January 28, 2014


  Kocha wa Yanga,Hans Van Der Pluijm kulia akitoka kwenye uwanja wa Mkwakwani leo asubuhi mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo kushoto ni Ofisa Habari wa timu hiyo,Baraka Kizuguto.
TIMU ya Dar es Saalam Yanga Africa imetua jijini Tanga juzi na kulakiwa na wapenzi pamoja na wanachama wao wakiwa na matumaini makubwa kuweza kuibuka na ushindi kwenye mechi yao dhidi ya Coastal Union ya Tanga kesho 

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani unatarajiwa kuwa mkali na upinzani wa hali ya juu kutokana na timu zote kufanya maandalizi nje ya nchi kwa Yanga kwenda Uturuki na Coastal Union wao wakitokea Omani.

Yanga wao waliwasili mkoani Tanga juzi wakitokea jijini Dar es Salaam wakiwa wachezaji wao 20 ambao watatumika kwenye mechi hiyo na kufanya mazoezi kwenye viwanja vya Gymkana na CCM Mkwakwani wakiwa na idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza kuwaona wachezaji mahiri wa timu hiyo.

Mazoezi ya timu hiyo yalikuwa yakiongozwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi Hans Van Der Pluijm akisaidiana na Charles Boniface Mkwasa na Juma Pondamali “Mensa”ambayo yalikuwa wakianza saa moja asubuhi mpaka saa tatu asubuhi.

Akizungumzia mechi yao na Coastal Union ya Tanga, Hans Van Der Pluijm alisema alichofuata mkoani hapa ni kuhakikisha anachukua pointi tatu na sio kitu kingine kwani wachezaji wake wana kiwango kizuri ambacho kinafanikisha malengo yake hayo.

Kocha huyo alisema msimu huu matarajio yake makubwa ni kutaka kuendelea kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara akisema hilo linawezekana kutokana na uongozi imara na mshikamano uliopo kwenye klabu hiyo.

Hata hivyo Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kutumia akili wanapokuwa mchezoni pamoja na kucheza pasi ndefu kwani hiyo ndio silaha ya ushindi kwenye mechi zao kwenye mzunguko huo wa pili wa ligi kuu hapa nchini.

January 28, 2014

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUANZA KURINDIMA FEBRUARI 13 MJINI NGOME KONGWE,ZANZIBAR.


Picha wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara la 11 katika kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16 katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.

Jumla ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico.

Kutoka Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu Mandingo,Segere Original na Kazimoto.

Pichani ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.

Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.
January 28, 2014
*MTEMVU AZINDUA BONANZA LA MAVETERANI YOMBO MAKANGARAWE,TEMEKE

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Matemvu akikagua timu ya Veterani ya Yombo Kilakala wakati wa uzinduzi wa michuano ya maveterani ya Ujirani Mwema, katika Kata ya Yombo Kilakala, Temeke, Dar es Salaam juzi. Timu 12 kutoka sehemu mbalimbali za jiji zilishiriki kwenye michuano hiyo. Timu hiyo ilicheza na Kigamboni Veterani.
 Mtemvu akikagua timu ya Kigamboni Veterani. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Makangarawe, Victor Mwakasendile.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mtemvu akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, ambapo aliahidi kuyadhamini kwa timu zote kuzinunulia jezi za TMK. Kushoto ni Mwakasendile na Mungia Mbwana mratibu wa michuano hiyo.
 Timu za New Kivule Veterani (waliovaa Bluu) na Kitunda (waliovaa bluu nyeusi) wakipepetana

DC MWANGA AWAPA KAZI MGAMBO.

January 28, 2014
Na Oscar Assenga,Lushoto.

MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaj Majid Mwanga amewataka vijana
walihitimu mafunzo ya mgambo kata ya Lukozi Tarafa ya Mlalo wilayani humo kufuatilia na komesha vitendo vinavyofanywa na vijana vya kuwapa mimba wanafunzi kike  pamoja na kuwakamata wazazi wanaowaozesha watoto wao wakiwa bado mashuleni.

Mwanga alitoa agizo hilo jana wakati akifunga mafunzo ya mgambo ya
  miezi sita kata ya Lukozi Tarafa ya Mlalo kwa wahitimu wapatao 99 ambapo kati yao wa kike watano na wakiune tisini na nne.

Alisema wahitimu hao wana jukumu kubwa la kuhakikisha pia

wanalidhibiti suala la utoro kwa wanafunzi pamoja na kutoa elimu juu ya athari za ukimwi na rushwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema suala lengine ambalo wanapaswa kulitia
mkazo mkubwa ni kuwaeleza vijana wengine mafanikio yaliyoyapata wakati wa mafunzo  hayo ikiwemo kulinda vyanzo vya maji na misitu.

Aidha aliwataka vijana hao kushiriki katika shughuli mbalimbali za

maendeleo kama ujenzi wa maabara pamoja na kuwa mstari wa mbele kuzuia vitendo viovu kwenye jamii zao ikiwemo wizi,uporaji.

Hata hivyo DC Mwanga aliwataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri
  kwenye familia zao kupitia kauli mbiu ya Jeshi la Polisi Tanzania ya kuwa “Katika familia yangu hakuna uhalifu na  Utii wa sheria bila shuruti n wa kila mwananchi na kila kiongozi.

MATUKIO YA PICHA KWENYE MECHI YA COASTAL UNION NA OLJORO JKT YA ARUSHA.

January 28, 2014