Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

March 15, 2017
Leo March 15, 2017 Rais Magufuli ametengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Uledi Abbas Mussa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kutenguliwa kwa uteuzi na kusimamishwa kazi kwa Uledi Abbas Mussa kunaanzia leo tarehe 15 Machi, 2017.
Hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi zaidi dhidi ya Uledi Abbas Mussa kufuatia kutozingatiwa kwa taratibu zinazotakiwa katika kushughulikia masuala ya uwekezaji.
Chanzo Millardayo.com
NI WAJIBU WA MAAFISA MAWASILIANO KUHUISHA TOVUTI ZAO-DKT.JABIR

NI WAJIBU WA MAAFISA MAWASILIANO KUHUISHA TOVUTI ZAO-DKT.JABIR

March 15, 2017
02 SAYANSI
   Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu ya Serikali kwa kuweka taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa zinazotolewa na taasisi hizo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma hizo kirahisi.
Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya matumizi na umuhimu wa tovuti za Serikali katika kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea Mkoani humo.
Dkt. Bakari amesema dhana ya Serikali Mtandao ni  kuhuisha matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi hivyo ni muhimu kwa kila taasisi kuwa na tovuti zenye taarifa za uhakika na zinazoendana na wakati ili  kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.
“Wakala kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za Serikali kutengeneza tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote ziwe na tovuti zao zitakazowarahisisha wananchi kufahamu huduma kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU YA CHAMWINO MIJINI DODOMA LEO

March 15, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha  kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Machi 15, 2017 PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha  kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Machi 15, 2017 PICHA NA IKULU


UMEJIPANGAJE NA SIKUKUU ZA PASAKA ZINAZOKUJA?

March 15, 2017


Na Jumia Travel Tanzania

Je, unafahamu kwamba umebaki takribani mwezi mmoja mpaka kufikia sikukuu ya Pasaka? Umejiandaa vya kutosha katika kusherehekea au unasubiria mpaka zibakie siku chache ndio uanze maandalizi?

Kwa watanzania wengi suala la kuweka mipango kwa ajii ya mambo yajayo limekuwa ni changamoto kubwa kutokana na sababu mbalimbali wanazozifahamu wenyewe. Jumia Travel inakushauri kuzingatia yafuatayo ili kuondokana  na presha ya maandalizi ya siku za mwishoni ya sikukuu ya Pasaka ambayo husherehekewa kuanzia siku ya Ijumaa kuu mpaka Jumatatu duniani kote.

QUALITY GROUP KUANZISHA KAMPUNI LUKUKI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

March 15, 2017
 Ofisa Mtendaji Mkuu  wa Kundi la Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Nicholas Ralph akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Ralph akielezea jinsi uongozi ulivopanga mikakati ya kuboresha kampuni zilizopo na kuanzisha nyinginezo nchini na nje ya nchi.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo

Suleiman Msuya
KAMPUNI ya Quality Group Limited (QGL), imesema inaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa QGL, Nicholas Ralph alisema katika kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi wameanzisha mfumo unaotambua na kudhibiti uhalifu huo kwenye taasisi (e-Governance).

Alisema mfumo huo wa utambuzi na udhibiti unapaswa kuwepo katika idara zote za Serikali kwani una utija ni salama zaidi hasa katika kulekea katika Tanzania ya maendeleo endelevu.

Ralph alisema QGL imewekeza katika sekta mbalimbali  kama afya ambapo wanatarajia kujenga vituo 4,000 vya afya nchini kote pamoja na vioski vya kutoa afya ili kuendana na teknolojia ya sasa na kurahisisha kila mwananchi anapata huduma bora ya afya.

Alisema pia wamekubaliana na kampuni kutoka nchini Urusi ili kusambaza vifaa tiba na kampuni nyingine kutoka Marekani itatoa huduma ya ndege katika huduma ya dharura.

“Pia kampuni ya QGL imeingia makubaliano na kampuni kutoka nchini Ireland kujenga na kuwekea uongozi katika utawala ambapo itasaidia kuongeza teknolojia kwa kampuni za ndani,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kampuni ya QGL imekuwa ikisadia wavuvi katika Kanda ya Ziwa kwa kuwapatia vitendea kazi na matibabu, kusaidia elimu na pia ilisaidia mapambano ya ugonjwa wa Ebola.

Alisema kampuni yao imefanikiwa kuongeza ajira, mafunzo, kukuza uchumi ili kuhakikisha inaunga mkono  mpango wa maendeleo wa Serikali wa 2025.

Ralph alisema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa viongozi na waajiriwa vijana kupitia program ya Moreh Derech ambayo imekuwa na mafanikio makubwa.

Aidha, alisema katika kuhakikisha kuwa wanapanua ushirikiano na taasisi za kimataifa wamesaini makubaliano na Kampuni ya  Solanika International Tractors Limited ya India ambao watakuwa wanaingiza matrekta 1,000 kwa mwaka hivyo kuongeza ajira 1,200 ifikapo mwaka 2018.

“Pia tumesaini barua katika miradi ya madini ambapo tunarajia kuuzungumzia vizuri pindi hatua zote zikiwa zimekamilika,” alisema.

Halikadhalika alisema wamewekeza katika viwanda vya sukari na maziwa ambapo wananchi wengi wa Kitanzania ndio watafaidika kwa kuuza bidhaa husika katika viwanda hivyo vyenye teknolojia ya kisasa na uongozi kutoka Israel, Ulaya na Afrika Kusini.

Ralph alisema QGL imekuwepo kwa zaidi ya miaka 30 ambapo inashirikiana na kampuni kubwa duniani kama General Motors (GM), Honda, Isuzu, Bridgestone na Chevrolet.

Alisema kutokana na ushirikiano huo QGL imeajiri zaidi ya watu 667,300 na kupata faida ya dola za Marekani bilioni 348.6 hayo yakichangiwa na uwajibikaji, uwazi, uaminifu na mafanikio.


Alisema mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa ni sehemu sahihi ya kuchochea maendeleo ya nchi na wananchi wa Tanzania. 
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO KAZI CHA SHIRIKA LA MAGEREZA, JIJINI DAR

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO KAZI CHA SHIRIKA LA MAGEREZA, JIJINI DAR

March 15, 2017
MALE
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao kazi cha Shirika la Uzalishaji mali la Magereza ambapo katika Kikao hicho cha siku mbili Wakuu wa miradi watapata fursa ya kuelezea maendeleo ya miradi mbalimbali ya shirika hilo. Kikao hicho kimeanza leo Machi 15, 2017 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
MALE 1
Baadhi ya Wakuu wa miradi mbalimbali ya Shirika la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika Kikao kazi cha Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(hayupo pichani).
MALE 2
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkaribisha Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw. David Mwangosi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi katika ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
MALE 3
Meza Kuu ikiongozwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali(kushoto) ni Mdhibi Mkuu wa Shirika la Magereza, ACP. Joel Bukuku(katikati) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.
MALE 4
Mkuu wa Magereza Mkoa Mara, ACP. Goleha Masunzu akichangia hoja katika Kikao hicho.
MALE 5
Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Bw. David Mwangosi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Shirika la Magereza (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Miradi ya Shirika la Magereza(wa pili toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya (Picha zote na Jeshi la Magereza).
WIZARA YAKEMEA UBAKAJI WA MTOTO MKOANI IRINGA

WIZARA YAKEMEA UBAKAJI WA MTOTO MKOANI IRINGA

March 15, 2017
JUKIII
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakemea vikali tukio la kubakwa kwa binti wa miaka saba  (jina limehifadhiwa) mkazi wa kata ay Kitanzini, mwanafuzi wa darasa la awali shule ya SUN Academy iliyoko kata ya Kwakilosa, manispaa ya Iringa.
Wizara imesikitishwa na taarifa za awali kuwa mtoto alibakwa katika mazingira ya shule mahali ambapo tunategemea pawe salama kwa mtoto kuishi. Wakati wote Serikali imekuwa ikisisitiza walezi wa watoto kuhakikisha wanalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ubakaji kwani vitendo hivi vimekuwa vikitaarifiwa kuwahusisha watu wa karibu wanaomzunguka mtoto katika familia, shuleni na jamii.
Wizara inapongeza vyombo vya habari vyote vinavyoibua matukio ya ukatili, kwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao utekelezaji wake unahusisha wadau wote nchini.
Wizara inamini kuwa Polisi kwa kutumia weledi na umahiri wao watashirikiana na wananchi, walezi, walimu na marafiki wa mtoto, kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafichuliwa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Wizara inawakumbusha wazazi na walezi kuwa vitendo vya ukatili ukiwemo ubakaji dhidi ya watoto wa kike havikubaliki katika nchi yetu kwani vitendo hivyo vinatia doa kubwa taifa letu. Natoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kuwafichua waliohusika na ubakaji wa mtoto aliyeripotiwa kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Erasto T. Ching’oro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MKUTANO WA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI MKOANI DODOMA KWA MATUMIZI

MKUTANO WA MAAFISA MAWASILIANO SERIKALINI MKOANI DODOMA KWA MATUMIZI

March 15, 2017
LUKO
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao (kulia)  akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas.
LUKO 1
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas (kushoto) akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao. 
LUKO 2
Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa mada juu ya hali halisi ya uhuishaji wa Taarifa za Serikali kwenye Tovuti Kuu ya Serikali na Taasisi za Serikali katika Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano  Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
LUKO 3
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (Maelezo) Bi. Zamaradi Kawawa akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
LUKO 4
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TBC Bi. Edna Rajabu akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
LUKO 5
Afisa Habari Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Margareth Chambili akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
LUKO 6
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Bi. Neema Mbuja akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.
LUKO 7
Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia ya kidigitali kutoka  Kampuni ya Push Observer Kanali Mstaafu Dkt Abas Katalla akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).

NAIBU WAZIRI JAFFO AKAGUA MAANDALIZI YA UJENZI WA DARAJA LA KIJICHI-TOANGOMA TEMEKE

March 15, 2017
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo (katikati) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha Kata za Toangoma na Kijichi, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Toangoma, Mohamed Mketo. (PICHA NA DALILA SHARIF)

Na Dalila Sharif
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amekagua ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijichi hadi Toangoma wilayani Temeke.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, alipokuwa akikagua ujenzi wa daraja hilo, Naibu Waziri alisema ameridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa daraja hilo

“Daraja hilo lenye urefu wa mita 600 na inatakiwa matayarisho yaanze mapema kwa kuchonga barabara  ili ujenzi ukamilike mapema tayari kwa wananchi kulitumia,”alisema Jafo.

Mkuu wa Wilaya  hiyo, Felix Lyaniva alisema anampongeza Naibu Waziri kwa kukagua ujenzi wa daraja hilo kwa kuwa ni nia njema katika kuendeleza maendeleo ya wilaya hiyo.

“Wapo katika harakati za mandalizi ya ujenzi wa daraja hilo litakaloweza kusaidia kupunguza kero za wananchi wanaotembea umbali mrefu kwa miguu katika maeneo hayo,”alisema Lyaniva.

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alimuomba waziri  kuwatatulia wananchi wa eneo hilo  kero inayowakabili ya kutolipwa fidia zao.


“Wakazi wa eneo ambao hadi sasa hawajalipwa fidia ya nyumba zao wamekuwa wakikumbwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua hivyo kuathirika kwa kiasi kikubwa,”alisema Mangungu.

 Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu akifafanua jambo kwa wanahabari kuhusu maendeleo ya mradi huo
DAWASCO KUTUMIA WIKI YA MAJI KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO ZA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

DAWASCO KUTUMIA WIKI YA MAJI KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO ZA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

March 15, 2017
                        Na Mwandishi wetu.

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limepanga kutumia maadhimisho ya 29 ya wiki ya maji inayoanza kesho kutoa elimu ,kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika vituo vyote 10 vya DAWASCO vilivyopo katika Jiji la Dar es salaam , Miji  ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Utaratibu huu umelenga kutoa mwanya kwa wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka Dawasco ,kupata Elimu ya Huduma ya Maji  na kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukaribu zaidi kati ya DAWASCO na wananchi.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Everlast Lyaro amesema madawati haya yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa wiki nzima ya maadhimisho haya ya wiki ya Maji.
Amesema zoezi la kupokea kero na malalamiko kwa waanchi litafanyika hadi siku za Jumamosi na Jumapili ambapo Madawati yatakuwa wazi ili kutoa nafasi zaidi kwa wananchi wengi kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa utatuzi.
Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya maji utafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda ambapo pamoja na mambo mengine Dawasco itapokea miradi ya Jumuiya za watumia maji katika maeneo mbalimbali.
Maadhimisho ya wiki ya Maji yameanza rasmi leo Machi 16 hadi Machi 22 mwaka huu yakibeba kauli mbiu ya “MAJISAFI NA MAJITAKA- PUNGUZA UCHAFUZI YATUMIKE KWA UFANISI”
Wakati huo huo shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) linaendelea na zoezi maalum la ubadilishaji wa Mita za Maji  katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam pamoja na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Zoezi hilo lililoanza mapema October 2016, linalenga kuondoa mita zote za Maji ambazo ni chakavu, Mbovu  na zenye muda mrefu katika makazi ya watu, taasisi pamoja na viwanda ambalo linaenda sanjari  na ufungaji wa Mita mpya za Maji kwenye maeneo mbalimbali.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Everlast Lyaro amesema tangu kuanza kwa zoezi hili tayari mita za Maji takribani 25,000 zimekwisha badilishwa na kwamba uondoaji wa mita Chakavu una lengo la kuongeza ufanisi katika usomaji wa Mita kwa usahihi, kupunguza kiasi cha Maji kinachopotea kutokana na uchakavu na kuakisi matumizi halisi ya Maji yanayotumiwa na mteja

DC KOROGWE AONGOZA OPERESHENI YA KUHARIBU MASHAMBA YA BANGI KUUNGA JITIHADA ZA SERIKALI KUPAMBANA NA MATUMZI YA DAWA ZA KULEVYA

March 15, 2017
  Mkuu wa wilaya ya korogwe,Mhandisi Robart Gabriel kushoto akizungumza na askari katika msitu wa kijiji cha Kijungumoto kata ya Mashewa kabla ya kuanza zoezi la uteketezaji wa mashamba ya bangi wilayani Korogwe



 Ofisa Upelelezi Mkoani wa Tanga,Amedeus Tesha akishiriki uvunaji bangi.
 Mkuu wa wilaya ya korogwe,Mhandisi Robart Gabriel akishiriki uvunaji wa bangi.

JIJI LA TANGA LATAKIWA KUBORESHA SOKO LA MACHINJIONI LA SAHARE

March 15, 2017
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imetakiwa kuboresha miundombinu ya soko la Machinjioni la Sahare lililopo Kata ya Mnyanjani ili liwezekuendana na hadhi ya Jiji kutokana baadhi ya maeneo kuharabika ikiwemo eneo la kushushia ngombe kwa ajili ya kuchinjwa.

Hali hiyo inasababisha wakati mwengine ng’ombe wanaopelekwa kwenye machinjio hayo kukimbia wakati wakishushwa na hivyo kusababisha hatari kwa wakazi wa maeneo jirani hivyo kuomba wajengewe fensi kwenye eneo hilo ili kudhibiti.

Hayo yalibainishwa juzi na Katibu wa chama cha Wachinjaji wa Ngombe Jijini Tanga, Hassani Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea machinjio hayo ili kuweza kutambua changamoto zinazowakabili ambapo alisema tatizo kubwa ni machinjio hayo kukosa uzio.

Alisema licha ya kuwepo kwa suala hilo lakini hata eneo ambalo
limekuwa likishushiwa ng’ombe limekuwa bovu kwa muda mrefu bila kutengenezwa jambo ambalo linapelekea eneo hili kuwa na kikwazo wakati wa ushushaji wa mifugo hiyo.

“Kitendo cha kukosekan uzio kwenye machinjio hii ya Sahare Jijini Tanga kinasababisha athari nyingi ikiwemo wakati mwengine ng’ombe wanaofikishwa kwa ajili ya kuchinjwa kukumbia na kusababisha usumbufu mkubwa kwa jamii ya wakazi wa maeneo ya karibu”Alisema

Licha ya hivyo lakini aliitaka kuona namna ya kuboresha mazingira kwenye machinjio hayo ikiwemo katika sehemu za mitaro ya kupitishia maji ambayo itakuwa ikiyapeleka moja kwa moja kwenye bahari ya hindi.

Aidha pia alisema sanjari na hilo lakini halmashauri hiyo iweze
kuangalia namna ya kuimarisha barabara ya kuelekea kwenye machinjio hayo kutoka kwenye barabara inayoelekea eneo la Sahare ili kurahisisha upitikaji wake nyakati zote bila kuwepo na usumbufu.

“Kwani eneo ambalo limekuwa ni barabara ya kuingilia kwenye machinjio haya limekuwa bovu sana hasa nyakati za mvua magari mengine yanashindwa kuingia hivyo tunaiomba Halmashauri iweze kuona namna ya kulikarabati eneo hili “Alisema.

“Sababu kubwa ya kuomba tungewe uzio kwenye machijio haya ni kuepukana na adha ya kuacha kufanya kazi kila siku na kuanza kukimbizana kusaka ng’ombe ambao wanakuwa wamekimbia kwenye eneo letu hasa wale wakali “Alisema.

Hata hivyo alisema kwenye machinjio hayo katika kipindi cha sikukuu wamekuwa wakichinja ng’ombe kati ya 150 mpaka 200 kwa siku huku kwenye kipindi cha kawaida huchinja kuanzia 60 hadi 100.

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI

March 15, 2017
s
ISO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo.
ISOOOO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo,[Picha na Ikulu,] 15/03/2017.
MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA SADC WA KUJADILI MASUALA YA USALAMA

MASAUNI AFUNGUA MKUTANO WA SADC WA KUJADILI MASUALA YA USALAMA

March 15, 2017
SADC
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) (hawapo pichani), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga.
SADC 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto meza kuu) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga, na kulia ni Afisa wa kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Rokhayatou Diarra.
SADC 2
Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
SADC 3
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wapili kulia meza kuu) akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia meza kuu ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye pia alifungua mkutano huo.
SADC 4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisindikizwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez  (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (kulia), mara baada ya Masauni kufungua Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo ambapo Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo walijadili masuala mbalimbali ya usalama. Warsha hiyo  ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam.
SADC 5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wanne kulia), Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na  Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo mara baada ya Masauni kuufungua Warsha hiyo iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo. Warsha hiyo ilifanyika katika  Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA KAHAMA

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA KAHAMA

March 15, 2017
UPOOOO
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo ya Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya kwanza, Sir George Kahama ,nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
UPOO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimfariji mjane wa Marehemu Sir George Kahama Bibi.Janet Bina nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU YA CHAMWINO, DODOMA, LEO

March 15, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa mikutano katika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Machi 15, 2017
PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa mikutano katika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Machi 15, 2017
PICHA NA IKULU

MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA KUFANYIKA KESHO, SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA ATOA POLE KWA WAFIWA

March 15, 2017
 Marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake.
 Spika Mstaafu, Anne Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo cha Sir George Kahama nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
 Spika Mstaafu, Anne Makinda akimfariji mjane wa marehemu Janeth Kahama.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sofia Simba akimpa pole mjane wa marehemu, Janeth Kahama.


Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Regina Lowassa (wa pili kulia), akiwa kwenye msiba huo.
 Sophia Simba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu katika msiba huo.
 Pole zikiendelea kutolewa kwa mjane wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa msibani.

Na Dotto Mwaibale

MAZISHI ya aliyekuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe Sir George Kahama yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwili  wa marehemu utawasili nyumbani kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business leo hii saa 11 jioni na kukesha hadi asubuhi.

Kesho mwili wa marehemu  utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia  saa mbili kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saa tano nanusu 5.30 asubuhi kwa ibada.

Ibada ya mazishi  itafanyika  katika  makaburi  ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu  9.30 alasiri.