Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ambaye pia ni mmiliki wa magazeti ya
Jambo Leo na Staa Spoti, Juma Pinto wakati wa hafla ya maadhimisho ya
miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ikulu, Dar es Salaam
juzi..PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
TBL YAPATA TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA NCHINI
Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia) akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL), Lillian Makau cheti cha shukurani cha kutambua
ushiriki wa kampuni hiyo katika mapambano dhidi ya Malaria nchini,
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Katikati ni Balozi wa Malaria Tanzania, Leodegar
Tenga.
Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake
ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na
wananchi.
Katibu wa Afya wa TBL (katikati), akitoa maelezo jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti kutoa elimu na tiba ya malaria kwa wafanyakazi pamoja na wananchi.
Wananchi wakiwa katikasherehe za maadhimisho ya hayo kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam.
Makau akielezea mikakati ya TBL ya kuisaidia jamii na wafanyakazi katika mapambano dhidi ya Malaria. |
Wageni waalikwa wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani
Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Seif Rashid , akimkabidhi Meneja Vipaji wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Lillian Makau (kulia) jinsi kampuni hiyo inavyoshiriki
katika mapambano dhidi ya malaria kwa kuisaidia jamii na wafanyakazi
wake, alipotembelea banda la TBL wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Malaria Duniani, Dar es Salaam jana. Katikati ni Katibu wa Afya wa TBL,
James Lyimo. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi.
Katibu wa Afya wa TBL, James (kushoto0 akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi wakati wa maadhimisho hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Seif Rashid akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi
mbalimbali zinazoshirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya
Malaria nchini.Mstari wa mbele kutoka kulia ni Athuman Mfutakamba,
Waziri Dk. Rashid Balozi wa Malaria nchini, Leodgar Tenga.PICHA ZOTE NA
KAMANDA WA MATUKIO BLOG
*MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI,KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali
alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo April
28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama
na Afya Duniani.
Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika
mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa
vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa
Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014,
Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya
mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea
Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku
ya Usalama na Afya Duniani.
Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth
Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika
katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho
kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya
Duniani yaliyoadhimishwa leo.
Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa
kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani
yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
salaam.
Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa
kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani
yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
salaam.
Watumishi wa taasisi mbalimbali wakiwa
kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani
yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea maandamano kwenye
maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Wanamuziki wa bendi ya 'OUT Jaz Band' wakitumbuiza
kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi
Nicolas Mgaya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali
pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo
April 28-2014 katika viwanja vya mnazi
mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi K. Lwakatare mkuu
wa usalama na mazingira Vodacom kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya
yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabizi zawadi maalum Naibu Waziri
wa Kazi na Ajira Mhe. Makongoro Mahanga wakati wa maaadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali
pa kazi Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
salaam.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja...
Picha ya pamoja....
BLACK BURN MABINGWA WAPYA WA NSSF CUP PANGANI
NAHODHA WA TIMU YA BLACK BURN AMBAO NI MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA NSSF CUP PANGANI AKIPOKEA KOMBE TOKA KWA MKURUGENZI UENDESHAJI NSSF,C,Cresentias Magori . |
NA OSCAR ASSENGA,PANGANI
Timu ya Soka Black Burn FC ya mjini hapa,imetwaa ubingwa wa
kombe la NSSF mwaka 2014 baada ya kuichapa Ushongo FC bao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa kijiji cha Mwera.
BAADA YA KUKABIDHIWA KOMBE WAKAPIGA PICHA YA PAMOJA. |
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo mbili kuwa na upinzani wa jadi ulishuhudiwa na mamia ya mashabiki walioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa NSSF,Cresentias Magori .
Black Burn ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuliona lango la wapinzani wao Ushongo FC baada ya Farid Nassoro kufunga bao dakika ya 49
lililotokana na shuti lililopita katikati ya walinzi na kumchanganya
mlinda mlango wa Ushongo,Sebastian Charles .
Dakika ya 60 uwanja huo ulilipuka kwa kushangiliwa baada ya
mshambuliaji,Amour Janja kuipatia timu yake ya Usongo FC ambayo ilikuwa ikichezea katika uwanja wake wa nyumbani kupachika wavuni bao la kusawazisha.
MENEJA WA NSSF MKOA WA TANGA,FRANK MADUGA kulia akipiga picha na mwamuzi bora mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya mpira jana |
Hata hivyo bao hilo halikudumu muda mrefu kwani dakika ya 77 Black Burn iliongeza bao la ushindi kupitia kwa Jumaa Soud ambapo hadi dakika 90 zinamalizika timu hiyo ikatoka kifua mbele kwa bao 2-1.
Kwa ushindi huo,Black burn ilikabidhiwa na Magori kombe,seti ya sare na pesa taslimu sh 200,000 na Usongo ikatwaa seti ya sare n ash 100,000 huku msindi wa tatu Mwera City ikitwaa seti moja ya sare.
Ligi hiyo ya NSSF ilianza Machi 15 mwaka huu kwa kushirikisha timu 14 ambazo zilizoingia nusu fainali ni Ushongo iliyocheza na Urafiki na kuifunga baoa 2-1 huku Blackburn FC nayo ikiifunga Mwera City bao 2-1.
SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII NCHINI (NSSF) WAFUNGUA TAWI JIPYA KATA YA MWERA WILAYANI PANGANI.
BAADA YA KUKATA UTEPE WA OFISI HIYO HAPA DC MTASIWA AKISAINI KITABU CHA WAGENI KUSHOTO NI MKURUGENZI WA UENDESHAJI NSSF CRESCENTIUS MAGORI |
KABLA YA UFUNGUZI WA OFISI HIYO ALIWEZA KUSALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SHIRIKA HILO |
KUSHOTO NI MENEJA WA NSSF MKOA WA TANGA,FRANK MADUGA AKIMUONGOZA MKUU WA WILAYA YA PANGANI,HAFSA MTASIWA MARA BAADA YA KUMPOKEA KWA AJILI YA UFUNGUZI WA TAWI HILO |
MENEJA WA NSSF MKOA WA TANGA,FRANK MADUGA AKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO KABLA YA KUMKARIBISHA MKURUGENZI UENDESHAJI WA NSSF CRESCENTIUS MAGOTI |
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza jambo kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Pangani,Hafsa Mtasiwa |
MKUU WA WILAYA YA PANGANI,HAFSA MTASIWA AKIZUNGUMZA KWENYE HAFLA HIYO YA UFUNGUZI WA OFISI YA NSSF TAWI MWERA WILAYANI HUMIO |
MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA TANGA,SUZANI UHINGA AKIZUNGUMZA JAMBO KWENYE HAFLA HIYO |
MKUU WA WILAYA YA PANGANI,HAFSA MTASIWA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA TANGA MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA UFUNGUZI WA OFISI HIYO. |
Balozi Seif Akutana na Balozi Ndogo wa China Mjini Dodoma.
Balozi
Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bwana Xie Yunliang
akiwasilisha agizo la Serikali yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi la kuridhia na kukubali kusaidia Ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Mau Tse Tung uliopo Mtaa wa Mpirani - Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Balozi
Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang akibadilishana mawazo na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake
ndani ya Jengo la Pius Msekwa Bungeni Mjini Dodoma.Pembeni yao upande wa kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiishukuru Serikali
ya Jamuhuri ya Watu wa China kupitia Balozi Wake Mdogo aliyepo Zanziobar
Bw. Xie Yunliang kwa kukubali wazo la SMZ la kuiomba China kusaidia
ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung Jina linalotokana na Muasisi
wa Taifa hilo la China.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR)
Na Othman Khamis OMPR.
Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China
imeridhia na kukubali kugharamia ujenzi wa Kiwanja cha michezo
kilichopewa jina na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la Mau Tse Tung
kilichopo miperani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa na Balozi Mdogo wa
Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bw. Xie Yunliang wakati
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
hapo katika Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Msekwa Bungeni Mjini
Dodoma.
Balozi Xie Junliang alimueleza Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Timu ya wataalamu wa China inatarajiwa
kukifanyia utafiti na uchunguzi kiwanja hicho baadaye mwaka huu sambamba
na utiwaji saini Makubaliano ya ujenzi wa kiwanja hicho unaotarajiwa
kufanyika mapema mwaka ujao.
Alisema ujenzi wa uwanja huo uliopewa
heshima ya Jina la Kiongozi muasisi wa Taifa la China Marehemu Mao Tse
Tung utajumuisha kiwanja cha mchezo wa soka pamoja na michezo mengine ya
ndani mfano mchezo wa Table Tennis.
“ Tunatarajia ujeni wa kiwanja cha Mao
utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wanamichezo wa michezo
tofauti ukiwemo ule unaopendwa zaidi wa soka “. Alisema Bwana Xie
Junliang.
Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar
alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uhusiano wa kidugu
uliopo kati ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla pamoja na China
unastahiki kuenziwa zaidi.
Alimuhakikishia Balozi Seif kwamba
Jamuhuri ya Watu wa China itaendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania
kwa ujumla katika harakati zake za kujikwamua kiuchumi.
Alisema matengenezo makubwa ya ujenzi wa
Hospitali ya Abdulla Mzee iliyopo Mkoani Kisiwani Pemba, ujenzi wa
maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar pamoja
na matayarisho wa matengenezo ya chumba cha wagonjwa mahututi { ICU }
mwezi Juni mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni miongoni mwa
uthibitisho wa uhusiano wa pande hizo mbili.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Jamuhuri ya Watu wa
China kwa moyo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa
ujumla katika miradi ya Kiuchumi na Maendeleo.
Balozi Seif alisema mchango wa Serikali
ya China kwa Zanzibar umesaidia kuiwawezesha asilimia kubwa ya Jamii
Zanzibar kustawika Kijamii na hata kiuchumi kupitia miundo mbinu
iliyowekwa na Serikali kwa msaada wa Nchi hiyo rafiki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alitolea mfano msaada mkubwa uliotolewa na China katika ujenzi wa skuli
za Wilaya za Sekondari katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Alisema mradi huo mkubwa wa sekta ya
Elimu umekuja kufuatia ongezeko kubwa la idadi wa wanafunzi
wanaofanikiwa kujiunga na masomo ya Sekondari katika maeneo tofauti ya
Zanzibar.
“ Kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi
hasa eneo la Wilaya ya Magharibi katika Kisiwa cha Unguja
tumelishuhudia hivi karibuni katika skuli ya Kijitoupele na Serikali
kupitia Wizara ya Elimu tunaliangalia tatizo hilo kwa mtazamo wa kujenga
skuli mpya katika Mtaa wa Pangawe “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliipongeza China kupitia Balozi wake huyo kwa mchango wake mkubwa
katika Nyanja ya Elimu mchango ambao tayari watoto wa Zanzibar
wanaendelea kufaidika nao.
MASHAMBA YA BALAL KUGAWANYWA KWA WANANCHI WILAYA YA KILOMBERO.
Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali.
KILOMBERO.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imeamua kufuta miliki ya mashamba yote makubwa yasiyoendelezwa na taratibu mpya zinafanyika ili kuyamilikisha kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imeamua kufuta miliki ya mashamba yote makubwa yasiyoendelezwa na taratibu mpya zinafanyika ili kuyamilikisha kwa wananchi.
Kati ya mashamba hayo, matatu ni ya aliyekuwa
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali na
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Simba, Marehemu Priva Mtema yaliyoko
katika vijiji vya Lungungole na Merera ambayo wananchi wameshayavamia na
kuendeleza shughuli za kilimo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Kilombero juzi, Mwenyekiti wake, David Ligazio alisema
taratibu za kuomba hatimiliki za mashamba hayo zifutwe zinaendelea.
Ligazio alisema wamiliki wa mashamba hayo
wameshapewa notisi na orodha yao imeshawasilishwa kwa Kamishna wa Ardhi
ili aridhie kufutwa kwa hati za mashamba hayo.
Alisema uamuzi wa kuyataifisha umekuja baada ya
halmashauri kubaini kuwa yamekuwa hayaendelezwi na hivyo kusababisha
maeneo hayo kuwa misitu wakati wananchi wanahitaji maeneo ya kulima.
Alisema ukaguzi wa kumbukumbu umeonyesha kuwa
idadi kubwa ya wamiliki hao hawapo wilayani Kilombero na maeneo hayo
yanamilikiwa kwa hati za muda mrefu bila kufuata taratibu.
Alisema utaratibu unaofanyika sasa ni kuwaagiza
watendaji na wenyeviti wa vijiji, kuanisha ukubwa halisi wa mashamba
hayo ili kurahisisha kazi ya kuyagawa kwa wananchi katika siku zijazo.
Akizungumzia hatua hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema taarifa hiyo
haijafika ofisini kwake, lakini akabainisha kuwa kuna watu wengi
wanaomiliki ardhi kubwa mkoani Morogoro bila kuwa na hatimiliki wala
kufuata taratibu huku wakiwa wanawatisha wananchi.
Aliwataka wananchi hao kujisimamia, waondoe
unyonge na kuzingatia taratibu za ardhi, kwamba inatakiwa kugawiwa
kupitia mkutano mkuu wa kijiji, vinginevyo wana haki ya kujitwalia
maeneo hayo na kufanya maendeleo mengine.
“Kuna matukio unakuta mtu anakaa na mwenyekiti wa
kijiji na kujifungia, wanajadili wenyewe na kugawiana maeneo ya kijiji
bila kuwashirikisha wananchi, hawa wananchi wanatakiwa kukataa hali
hiyo,” alisema.
Maeneo yanayogawiwa
Mwenyekiti wa halmashauri aliyataja maeneo
mashamba yanayotakiwa kugawanywa kwa wananchi na ukubwa wake katika
mabano kuwa ni Lungongole (ekari 375) na Merea (ekari 373).
Pia kuna shamba lenye ukubwa wa hekta 887 linalomilikiwa na Balali, ekari 491 zinazomilikiwa na George Teni katika Kijiji cha Kisegese na ekari 500 zinazomilikiwa na Aloyce Lyenga katika Kijiji cha Idete.MWANANCHI
Pia kuna shamba lenye ukubwa wa hekta 887 linalomilikiwa na Balali, ekari 491 zinazomilikiwa na George Teni katika Kijiji cha Kisegese na ekari 500 zinazomilikiwa na Aloyce Lyenga katika Kijiji cha Idete.MWANANCHI
JK AWAVISHA NISHANI ZA MUUNGANO MIAKA 50 IKULU DAR
Dk. Mwele Malecela, akisubili kukabishiwa nishani ya baba yake Samuel Malecela, ambaye yeye hakuwepo
Waalikwa wakiwa katika dhifa hiyo
Mkuu wa Pili wa Majeshi Nchini Jenerali Mstaafu David Musuguri, akiwasalimia makamanda baada ya kuwasili katika dhifa hiyo.
Mzee david Msuya, akisubili kukabidhiwa
M\zee Joseph Sinde Warioba au mze wa Serikali tatu, akisubili naye kukabidhi nishani
Mzee Jenerali david Musuguri akiwa amekaa sambamba na Mkuu wa kwanza wa majeshi Jenerali Mirisho Sarakikya
Tajiri namba tatu nchini Reginald Mengi, akisubili naye kukabidhiwa nishani kwa Utu wake wa kuwajari watanzania wenzake
mama Fatma Karume, akisalimiana na Mwele na kulia ni mama maria Nyerere
Mama Salma Kikwete (katikati), akiwa katika dhifa hiyo
Wapambe wa viongozi wakiwa katika dhifa hiyo
Rais Mstaafu wa zanzibar Dk, Salimin Amour, akiwasili katika dhifa hiyo
Viongozi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya dhifa kuanza
Rais Jakaya Kikwete naye akiimba wimbo wa taifa
Viongozi wakifuatilia majina ya watunukiwa
mama maria Nyerere, akitunukiwa
Mama Fatma karume, akitunukuwa
Mtoto wa Rais Mstaaf Ali Hassan Mwinyi akitunukiwa kwa niaba ya baba yake
Mzee William Makapa, akitunukiwa
Mwele akikabidhiwa
Mzee David Msuya, akitunukiwa
Mzee Warioba, akienda kutunukiwa
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid karume, akitunukiwa
Mtoto wa Marehemu Edward Moringe Sokoine, akitunukiwa kwa niaba ya baba yake
Mzee Salim Ahemed Salim, akitunukiwa
Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzizibar, akitunukiwa
Shamsi Vuai nahodha, akitunukiwa
Rais akipumzika kidogo
Mtoto wa marehemu paul Bomani, akikabidhiwa tuzo kwa niaba ya baba yake
Geroge Kahama, akikabidhiwa
Mzee Job Lusinde, akikabidhiwa
Subscribe to:
Posts (Atom)