February 01, 2014
Release No. 016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 2, 2014

TARIMBA KUONGOZA KAMATI YA NIDHAMU
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa wajumbe kuunda kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili za rufani za vyombo hivyo.

Rais wa zamani wa Yanga, Tarimba Abbas ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza Kamati ya Nidhamu. Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.

Kamati ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.

Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.

Kamati ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.

TFF, CRDB KUTATHIMINI TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeagiza kifanyike kikao cha dharura kati ya Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za elektroniki.

Lengo la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.

Viwanja vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.
   
MECHI YA STAND, KANEMBWA MEZANI TENA
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.

Maagizo hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini Shinyanga.

Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.

Pia Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
February 01, 2014

*MWENYEKITI WA CCM DR. JAKAYA KIKWETE AWASILI MKOANI MBEYA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano akipunga mkono wakati akishuka kutoka kwenye ndege jana jioni ya leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya tayari kwa sherehe za kuzaliwa kwa CCM zitakazofanyika tarehe 2 Februari ambapo asubuhi kutakuwa na matembezi ya mshikamano kisha kuhitimishwa kwenye uwanja wa wa Sokoine.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe tayari kwa maadhimisho ya sherehe za miaka 37ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Ndugu Abdallaha Bulembo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya tayari kwa sherehe za kutimiza miaka 37 tangia kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya Mjini Ndugu Ephraim Mwaitenda kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya.
 Boda Boda zikiongoza msafara wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete aliyewasili mkoani Mbeya kwa ajili ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

 Bodaboda zikiongoza msafara wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwenye uwanja wa kimataifa wa Songwe.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete(katikati) akiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa wa Mbeya tayari kuongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa wa Mbeya.
February 01, 2014

JAJI MARK BOMANI ATETEA SERIKALI TATU

Dar es Salaam. Jaji mstaafu, Mark Bomani, ametetea kuwepo kwa muundo wa Serikali tatu na kuwabeza wanaodai kuwa ni wa gharama kubwa.
Amesema dhana hiyo si sahihi na kwamba anayedai kuwa itakuwa hivyo. Ni vyema akawa na ushahidi wa kina badala ya maneno matupu.
Kulingana na mapendekeo ya Jaji huyo kuhusu mabadiliko ya Katiba, ambayo Mwananchi ina nakala yake, suala la gharama kubwa za uendeshaji wa Serikali tatu halina msingi wowote.
“Naungana na Jaji Warioba hoja kwamba Serikali tatu ni gharama kubwa haina ushahidi wowote. Serikali tatu si lazima ziwe na gharama kubwa kuliko Serikali mbili na suala hilo linategemea mambo mengi,” alisema.
Alisema mathalan Bunge la sasa la Serikali mbili lina gharama kubwa kwa sababu lina wabunge 380 wakati Bunge la Muungano litakuwa na wabunge 75 na hata kama zikiongezeka gharama za Bunge jipya la Tanganyika bado kutakuwa na idadi ndogo ya wabunge.
“Hiyo inaashiria kuwa gharama za za kuendesha Bunge la Muungano na lile la Tanganyika zitapungua” alisema. Bomani alisema mfumo wa Serikali mbili una matatizo kwani hata Uingereza ambako kuna Serikali za idadi hiyo ikiwemo ya Ireland ya Kaskazini, kuna matatizo mengi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA YANGA.

February 01, 2014
Hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu yetu ya mpira, uongozi na baadhi ya wanachama.
 
Ni haki na ni kwa nia njema tu ya wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi, Ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo mema na mabaya. 
Ushindi au mwenendo mzuri wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, Wachezaji, Walimu, Viongozi, Wanachama na wapenzi kwa ujumla.
 
Uongozi ulikutana na wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na kuchukua hatua ya kubadilisha technical bench yote na kutoa adhabu na onyo kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi kilichopita.
February 01, 2014

ANGALIA PICHA AJALI YA BASI BARABARA YA NYERERE

Kikosi cha jiji cha uokoaji na zimamoto wakishirikiana na polisi trafiki kuzima moto uliokuwa ukiteketeza basi la abiria katika eneo la Vingunguti Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo .

February 01, 2014

BREAKIN NEWZZZ:- IRINGA UVCCM KIMENUKA ONA KILICHOTOKEA LIVE!!

                              Tumaini Msowoya  akiwa na meme  wake Frank  Kibiki  wakati wa harusi yao

                     Aliyekuwa mwenyekiti UVCCM mkoa  wa Iringa Tumain Msowoya  .....................................................................................................................
MWENYEKITI wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa mwanahabari Tumain Msowoya ametishia kujiuzulu nafasi yake hiyo baada ya wajumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa kupinga uamuzi wake wa kuchomoka ajenda ya kumteua mume wake kuziba nafasi tano ambazo anapaswa kuteua kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM. 
 
 Msowoya alifikia uamuzi huo wa kutangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo jana katika baraza kuu ya UVCCM mkoa lililofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa . 
 
 Kamujibu wa kanuni ya UVCCM ilipaswa ateue wajumbe watano wa baraza la UVCCM mkoa ambapo wajumbe wanne alikwisha teua katika baraza la vijana lililofanyika Desemba 8 mwaka 2012 hivyo kubaki nafasi moja ambapo jana
alipaswa kuiziba nafasi hiyo na kumteua mume wake Frank Kibiki aliyekuwa katibu wa UVCCM Iringa vijijini ambae kwa sasa yupo rikizi. 
KIJANA AANIKA SIRI 7 ZA KUVUNJA NDOA NA MBUNGE MZEE!

KIJANA AANIKA SIRI 7 ZA KUVUNJA NDOA NA MBUNGE MZEE!

February 01, 2014
Stori: Imelda Mtema na Ojuku Abraham
YULE ‘hendsam’boi’ Michael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) na miezi michache mbele ndoa ikavunjika, ameibuka na kuanika siri 7 zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar, juzi, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.
Michael Christian‘hendsam’boi’ aliyevunja ndoa
na ndoa hiyo na mheshimiwa huyo ndani ya Ofisi za Global.
SIRI YA KWANZA
Kijana Michael aliianika siri ya kwanza kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima.

SIRI YA PILI
Akizungumza kwa hisia kali, Michael aliye na taaluma ya uuguzi, aliiweka wazi siri ya pili ya kuamua kuivunja ndoa yake na mheshimiwa huyo kuwa ni kitendo cha kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka.
Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.
SIRI YA TATU
Kijana huyo aliendelea kwa kuifunua siri ya tatu kuwa ni kitendo cha kufungishwa ndoa bila kuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui.
February 01, 2014

*AJALI MBAYA YA GARI YAUA ASKARI POLISI 5 PAPOHAPO MKOANI DODOMA

 Gari hilo lililopata ajali na kuua askari hao.
**************************
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Askari polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1.          D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2.          F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3.          H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4.          WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5.          WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. 
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. 

Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.
Aidha Kamanda MISIME ametoawito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Baadhi ya wananchi wakiangalia gari hilo, lililopata ajali na kuua askari hao.
 Gari hilo lililopata ajali na kuua askari hao.
**************************
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Askari polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1.          D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2.          F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3.          H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4.          WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5.          WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. 
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.
Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. 

Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.
Aidha Kamanda MISIME ametoawito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Baadhi ya wananchi wakiangalia gari hilo, lililopata ajali na kuua askari hao.
Chanzo.Sufianimafoto.com
February 01, 2014

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AWASILI INDIA KUANZA ZIARA YAKE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mashada ya mauwa wakati wa mapokezi nyake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo mkewe Mama Mwanamwema Shein katika ziara rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ulinzi wakati wa mapokezi yake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo mkewe Mama Mwanamwema Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi wakati wa mapokezi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,pamoja na ujumbe waliofuatana katika ziara rasmi nchini India.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Uhusiano wa Mambo ya Nje Mam Raj Behamni, mara baada ya mapokezi na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakilipowasili katika Uwanja wa dege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,pamoja na ujumbe katika ziara rasmi nchini India. 
Picha na Ramadhan Othman.
February 01, 2014
February 01, 2014

*MAANDALIZI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM MKOANI MBEYA KESHO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la Mage Kolimwa (wapili kulia), katika Kijiji cha Mlimanyoka, Kata ya Nsalanga, wilala ya Mbeya mjini. Kinana alifika kumsaidia mkulima huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, inayofanyika Kitaifa Jumapili hii mjini Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisaidiana na vijana kuandaa jukwaa litakalotumika wakati wa mapokezi ya matembezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Sokine mjini Mbeya. Matembezi hayo yanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
Vijana wakiwa kwenye mazoezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika Jumapili hii mjini Mbeya.

WAMILIKI WA UWANJA WA MKWAKWANI KULA SAHANI MOJA NA TFF.

February 01, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
WAMILIKI wa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga wamesema kuwa endapo mapato yatakayotangazwa na bodi ya
ligi kuu kati ya Coastal Union na Yanga yatakuwa chini ya milioni 70 hawataridhika nao badala yake watazungumza na shirikisho la soka nchini TFF kuwaambia wauondoe mfumo kielectroniki kwenye uwanja huo kwa sababu utakuwa hauna manufaa kwao.

Kauli hiyo ilitolewa na TANGA RAHA BLOG Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(CCM)Gustav Mubba aliyema hayo jana wakati akizungumzia madhara yaliyotokana na mfumo huo ambao ulianza kutumika kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara akisema madhara mengine ni ununuzi wa tiketi kwenye vituo kuleta usumbufu kwa mashabiki wa soka kutokana na kununu lakini wakati wa utumiaji mfumo unakuwa taratibu wakati mwengine kugoma.

Mubba alisema utaratibu huu unawanyima  mapato wamiliki wa viwanja kwa sababu mpaka muda huu hawajui zimepatikana kiasia gani pamoja na kutokuwa na mwakilishi kwenye mchakato wa kusehabu mapato yaliyopatikana.