MKUU WA WILAYA YA NGORONGORO HASHIMU SHAIBU AKILA KIAPO MBELE YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA DAUDI FILEX NTIBENDA

March 03, 2015

 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Hashimu Shaibu akila kiapo cha utumishi mbele ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda  jana katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo
chanzo libeneke la kaskazini blog
 MBEYA INAWEZA KUPAA KIUCHUMI – WAZIRI MKUU

MBEYA INAWEZA KUPAA KIUCHUMI – WAZIRI MKUU

March 03, 2015


index  
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema mkoa wa Mbeya unaweza kupaa kiuchumi kama utazingatia fursa za kibiashara ilizonazo na kuwekeza zaidi kwenye viwanda vya usindikaji mazao ya kilimo na mifugo.
Ametoa kauli hiyo  jana (Jumatatu, Machi 2, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mkapa, jijini Mbeya.
“Nguvu kubwa mnayo katika biashara hasa kama mtajitahidi kutumia vema fursa kubwa ya uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mifugo mliyonayo,” alisema.
Waziri Mkuu alisema mkoa wa Mbeya katika msimu wa 2013/2014 umeweza kuzalisha tani 4,159,907 za nafaka na kuuwezesha kuwa na ziada ya chakula ya tani 3,347,680.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema mkoa wa Mbeya bado una fursa nzuri ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na unaweza kuiwezesha kama nchi kuuza chakula katika masoko ya Afrika na Afrika ya Mashariki kama watajipanga vizuri.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi hao kwa kuuwezesha mkoa wa Mbeya kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa. “Katika taarifa ya mkoa, nimeelezwa kuwa mwaka 2013, mkoa huu ulichangia shilingi trilioni 3.951 na hivyo kushika nafasi ya tatu kati ya mikoa yote nchini ikitanguliwa na mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.”
Alisema kutokana na ukuaji wa kasi wa idadi ya watu ambao ni asilimia 2.7, mtu akichukua pato hilo la mkoa na kuligawanya kwa idadi ya watu wa mkoa wa Mbeya anapata wastani wa pato la kila mwananchi kuwa ni sh. 1,420,427. “Kipato hicho, ni sawa na shilingi 118,369 kwa mwezi au shilingi 3,946 kwa siku sawa na Dola za Kimarekani (US $) 2.3,” alifafanua.
Waziri Mkuu alibainisha kwamba mtu akichukua wastani wa pato la kila mwananchi kwa mwaka 2013 na kupanga kwa mikoa yote, mkoa wa Mbeya unashuka na kushika nafasi ya sita kitaifa. Aliitaja mikoa inayowatangulia kuwa ni Dar es Salaam sh. 1,990,043/- ambao ni wa kwa kwanza; wa pili ni Iringa (sh. 1,660,532/-); wa tatu ni Arusha (sh. 1,448,782/-); wa nne ni Kilimanjaro (sh. 1,444,882/-); wa tano ni Ruvuma (sh. 1,438,392/-) na wa sita ni Mbeya (sh. 1,420,427/-).
“Nawashauri muongeze juhudi za kuipita mikoa hiyo kwa kuwa mna fursa nyingi za kuongeza uzalishaji hasa katika mazao ya kilimo cha kahawa, kakao, mpunga, mahindi, viazi, pamoja na mazao ya maliasili kama vile mazao ya misitu, na uvuvi na uchimbaji madini,”.
Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku saba mkoani Mbeya leo kwa kufanya majumuisho ya ziara yake na amerejea jijini Dar es Salaam jana jioni (Jumatatu, Machi 2, 2015)
UAMUZI KAMATI YA MASHINDANO KUHUSU TIMU ZA UJENZI RUKWA NA VOLCANO FC YA MOROGORO

UAMUZI KAMATI YA MASHINDANO KUHUSU TIMU ZA UJENZI RUKWA NA VOLCANO FC YA MOROGORO

March 03, 2015

images
Timu za Ujenzi Rukwa na Volcano FC ya Morogoro zimeshushwa madaraja mawili hadi ligi za wilaya baada ya kushindwa kufika uwanjani kwenye mechi zao za Ligi Daraja la Pili (SDL).
Uamuzi huo umefanya na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za matukio mbalimbali ya ligi hiyo.
Ujenzi Rukwa ilishindwa kwenda Kigoma kuikabili Mvuvumwa FC ya huko wakati Volcano FC haikutokea kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo ilitakiwa kucheza na Wenda FC.
Uamuzi wa Kamati ya Mashindano umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 27 ya SDL ambapo mbali ya kushushwa madaraja mawili, lakini pia timu hizo zimepigwa faini ya sh. milioni moja kila moja. Vilevile matokeo yote ya mechi zao kwenye Ligi hiyo yamefutwa.
Nayo Singida United imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Ujenzi Rukwa kubainika kumchezesha mchezaji asiyestahili (non qualified) kwenye mechi iliofanyika Februari 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Mchezaji Emmanuel Elias Mseja wa Mbao FC amepigwa faini ya sh. 100,000 na kufungiwa mechi tatu baada ya kukojoa uwanjani kwenye mechi dhidi ya AFC iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Pia viongozi wa Mbao FC, Abdallah Chuma (Daktari) na Meneja Yasin Abdul wamefungiwa miezi sita na faini ya sh. 100,000 kila mmoja kwa kumtukana na kumtishia maisha Kamishna wa mechi hiyo.
Nayo klabu ya AFC imepigwa faini ya sh. 300,000 kutokana na washabiki wake kuifanyia vurugu timu ya Bulyanhulu FC kwenye mechi yao iliyofanyika Februari 7 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu ya Magereza Iringa imepigwa faini ya jumla ya sh. 200,000 kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting), na uwanjani kwenye mchezo wao na Njombe Mji uliochezwa Februari 21 mwaka huu. Naye mchezaji wa timu Amasha Mlowasa amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 100,000 kwa kumtukana mchezaji mwenzake kwenye mechi hiyo.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI RUVUMA KUSHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU KAPTENI KOMBA

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MKOANI RUVUMA KUSHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU KAPTENI KOMBA

March 03, 2015

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na  akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma Helena Shumbusho mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea mkoani humo tayari kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Kada wa CCM na Mbunge wa jimbo la Mbiga Magharibi Marehemu Kapteni John Damiano Komba aliyefariki hivi karibuni katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam, mwili wa Kapteni John Komba unazikwa leo huko kijijini kwao Lituhi mkoani Ruvuma. kn2 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Mwigulu Nchemba  na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na wananchi wa Songea  baada ya kuwasili mkoani humo tayari kwa mazishi ya Marehemu Kapteni Komba. kn4 
Msanii wa TOT Khadija Omary Kopa akiwasili uwanjani hapo.
MCT YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA BLOGGERS TANZANIA(TBN)

MCT YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA BLOGGERS TANZANIA(TBN)

March 03, 2015
Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers wakipiga picha ya ukumbusho na mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga (wa tano kulia) katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo. Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo.Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN.Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limekubali kuanza ushirikiano na uhusiano mzuri na Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) mara kitakapo maliza mchakato wa usajili wake na kutambulika rasmi kisheria. MCT imesema kwa hatua ya kwanza itafanya mazungumzo na viongozi wa TBN na kujadiliana namna gani ya kuisaidia TBN. Kauli hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mkajanga alipokuwa akizindiwa hafla ya kwanza ya mwaka 2015 ya wamiliki na waendeshaji wa blogu na mitandao mingine ya kijamii iliyofanyika katika Hoteli ya Serena. Katibu huyo Mtendaji wa MCT alisema kwa maendeleo ya sasa ya teknolijia ya habari na mawasiliano ni vigumu kuzitenga blogu kama vyombo vya habari, hivyo kuahidi kushirikiana na TBN kuhakikisha inafikia malengo yake ya kuwaunganisha bloggers na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili. Alisema MCT inasubiri TBN ipate usajili kisheria toka mamlaka husika serikalini na baada ya zoezi hilo itaanza kushirikiana maramoja na chombo hicho kilichoanzishwa kuwaunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini na wale wanaofanya shughuli za nje ya nchi. "...MCT ipo tayari wakati wowote kuanza kushirikiana nanyi kikazi, tunachosubiri ni TBN kusajiliwa rasmi...mtakapo maliza usajili tu njooni ofisi, tutazungumza na viongozi wenu ili kujua nini cha kuwasaidia. Naombeni msichelewe tuanze hili mara moja," alisema Kajubi Mkajanga akizungumza na wana-TBN kabla ya kuzinduwa sherehe hiyo. Awali akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi alisema kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikitekemewa na kundi kubwa la jamii katika kusambaza taarifa kwa haraka licha ya uwepo wa changamoto kadhaa ndani ya tasnia hiyo. Alisema pamoja na mambo mengine, TBN imeanzishwa kwa lengo la kuwaunganisha waendeshaji na wamiliki wa blogu pamoja na mitandao mingine ya kijamii, na pia kuhakikisha wana-TBN wanapata fursa ya kujifunza zaidi maadili ya tasnia ya habari na mawasiliano ili kufanya kazi zao kiufanisi zaidi. Aidha aliishukuru Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kwa kusaidia kufanikisha tukio la kukutana 'bloggers', pamoja na Benki ya NMB na makampuni mengine ya Coca Cola, AIM Group na kampuni ya huduma za intanenti ya Raha kufanikisha tukio hilo la kuwaleta pamoja bloggers wa Tanzania. Akisoma risala ya wana-TBN kwa mgeni rasmi, Mjumbe wa TBN, Henry Mdimu alisema licha ya blogu kuwa chanzo kikubwa cha habari na mstari wa mbele kuwafikishia wananchi habari kwa haraka zaidi lakini bado zimekuwa hazitambuliwi na mamlaka zinazosimamia na kutetea tasnia nzima ya habari. "...Pamoja na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na 'bloggers' na waendeshaji wa mitandao ya kijamii, bado hawatambuliki rasmi na mamlaka husika pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa tasnia hii likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Idara ya Habari (Maelezo), MISA-Tan na hata Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo vya Habari nchini (TMF). "..Tunasema hivi maana tunaona kwa namna moja ama ingine wadau hawa muhimu hawajumuishwi katika harakati au michakato yoyote ile mnayoifanya kwenye tasnia hii. Mfano kupata semina za MCT, kupewa vitambulisho (Press card), kushiriki katika mafunzo na hata mashindano ya kila mwaka ya wanahabari yanayoandaliwa na MCT," alisema Mdimu akisoma risala ya TBN mbele ya mgeni rasmi Bw. Mkajanga. Kwa upande wa waalikwa rasmi kutoka ubalozi wa Marekani wakizungumza katika hafla hiyo kupitia kwa mwakilishi wao ameahidi kuisaidia TBN katika programu mbalimbali ili kuchochea uhuru wa habari nchini Tanzania. *Imeandaliwa na www.thehabari.com -- Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com