MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI JIMBO LA CHALINZE ... CCM YAIBUKA KIDEDEA KWA ASILIMIA 87

April 06, 2014

 CCM 20812 = %86.5 CDM 2628 = %10.9 CUF 473 = % 1.9 AFP 78 = % 0.3 NRA 59 = % 0.2

 
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Chalinze yametangazwa Chama cha Mapinduzi CCM kimepata jumla ya kura 20812,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kimepata idadi ya jumla kura 2828 na chama cha Wananchi CUF kimepata kura 474.
Hivyo chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze

CCM  20812    CDM 2638     CUF 473   AFP 78   NRA 59
April 06, 2014

*RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU MEJA JENERALI KEVIN MSEMWA LEO

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa  aliyekuwa Kamishna wa Utafiti na maendeleo ya Jeshi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu Meja Jenerali Kevin Gerald Msemwa wakati wa hafla ya kuaga mwili wake iliyofanyika katika uwanja wa makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Upanga jijini Dar es salaam leo April 6, 2014. Meja Jenerali Msemwa alifariki April 3, 2014 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salam. 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kamishna wa Utafiti na maendeleo ya Jeshi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu Kevin Gerald Msemwa wakati wa hafla ya kuaga mwili wake iliyofanyika katika uwanja wa makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Upanga jijini Dar es salaam leo April 6, 2014. Meja Jenerali Msemwa alifariki April 3, 2014 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es salam.
April 06, 2014

*MATUKIO YA ZOEZI LA UPIGAJI KURA JIMBO LA CHALINZE LEO, RAIS JAKAYA NA MAMA SALMA WAPIGA KURA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya mrisho Kikwete akisoma karatasi ya kupigia kura kabla ya kupia kura kumchagua Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwenye kituo cha kupigia kura cha Zahanati Msoga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye chumba cha kupigia kura wakati wa kupiga kura za kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura yake ya kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
April 06, 2014

YANGA YAIBANJUA JKT RUVU MABAO 5-1 UWANJA WA TAIFA

 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akiruka kukwepa kwanja la beki wa JKT Ruvu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1. Mabao matatu yalifungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya 7, Dakika ya 15 na Dakika ya 48. 

KMKM BINGWA MPYA LIGI KUU ZANZIBAR

April 06, 2014
Na Abdi Suleiman, Pemba
KMKM imeweza kutetea taji la ubingwa wa soka Zanzibar, baada ya leo jioni kuikong’ota Chipukizi mabao 3-2 katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar 2013/2014 uliopigwa uwanja wa Gombani Pemba.
 
Mabaharia hao wanapaswa kuishukuru pia timu ya Jamhuri ambayo iliilaza Polisi bao 1-0 katika uwanjawa Amani, na kuwasafishia njia washika magendo hao kulipeleka tena kombe la ubingwa makao makuu yao mtaa wa Kibweni.
 
Kwa ujumla mchezo kati ya KMKM na Chipukizi ulikuwa mzuri na uliojaa msisimko, na haikuwa rahisi kutabiri mshindi hadi dakika 15 za mwisho.