Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
“IKIWA hujawahi kupata tatizo huwezi jua kama wapo binadamu
wenzetu wanaotabika kusaka dawa au vitu vinavyoweza kuwaondoshea maswahibu yao
yanayoendelea kuwapa wakati mgumu katika maisha yao bila kuangalia wanaishi kwa
mtindo gani,”. Ndivyo alivyoanza kusema Sheikhe Hussein Msopa maarufu kama
Sharifu Majini.
Chifu Hussein Msoma maarufu kama Sheikhe Sharifu Majini akiwa katika majukumu yake ya kawaida kama anavyoonekana pichani.
Ndio, sheikhe huyo mwenye maskani yake Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, unaweza kushangazwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea katika ofisi ya sheikhe hiyo, huku kila mmoja wake akiwa na shida yake inayohitaji utatuzi. Kwa wale ambao hawajui lolote kuhusu sheikhe Sharifu majini, pindi wanapopita katika mtaa huo, wanaweza kudhani labda kuna harusi, msiba ayu shughuli yoyote ya kijamii kutokana na ingia tokay a watu katika nyumba ya sheikhe huyo inayotoa huduma mbalimbali za kuombea watu, kuwapatia dawa zikiwamo zinazohusiana na mambo ya majini.

Sheikhe Sharifu Majini pichani.
Watu wanaweza kushangaa au kujiuliza. Je, ni kweli mtu mwenye
tatizo anaweza kupata ufumbuzi wa shida yake atakapomuona sheikhe huyo? Katika
mazungumzo na mtandao huu yaliyofanyika wiki iliyopita, sheikhe Sharifu anasema
kwamba amedhamiria kuwakomboa wale wenye mahitaji na matatizo yanayohusu
majini, ukosefu wa uzazi kwa njia za ushirikiana, kusumbuliwa na majini pamoja
na kuzitafsiri ndoto mbalimbali zinazohusiana na mifumo ya maisha ya mwanadamu. Sheikhe huyo anasema kwamba uamuzi wake wa kuamua
kujihusisha na masuala hayo umetokana na kufahamu adha kubwa inayowakumba
binadamu, jambo linalowafanya waishi kwa mashaka katika kipindi chote cha
maisha yao.
“Mtu anaweza kwenda hospitali kufanya uchunguzi wa afya ya
matatizo ya uzazi na kukuta hana tatizo lolote. Lakini kila anavyojitahidi ili
ashike mimba kwa ajili ya kufurahisha nafsi au ndoa yake anajikuta anashindwa
kufanikiwa.