World Vision Waacha Wosia Ulinzi Kwa Watoto.

November 14, 2014

 
Shirika lisilo la Kiserikali la World vision Tanzania cluster ya Korogwe limeiomba jamii kuendeleza juhudi za shirika hilo walizozifanya kwa miaka kumi na tano katika tarafa ya Magoma wilayani Korogwe za kumlinda mtoto kwa kuhakikisha anapata huduma na haki zake zote za msingi.
Ombi hilo limetolewa jana na  mratibu wa mradi uliokuwa ukishughulikia maendeleo ya Magoma( Magoma ADP)  George Banyenza katika hafla ya kutia saini hati za makabidhiano iliyohudhuriwa na Watendaji wa World vision, watendaji wa halmashauri ya wilaya Korogwe,Diwani wa kata ya Magoma,Maafisa tarafa na Mtendaji wa kata hiyo, wenyeviti wa vijiji vya kata hiyo na wanufaika wa mradi huo iliyolenga  kukabidhi  rasmi majengo ya ofisi yaliyokuwa yakitumiwa na mradi huo kwa Serikali .
Banyenza alieleza kuwa kwa muda wa miaka kumi na tano World Vision kwa ufadhili wa watu wa ujerumani imekuwa ikiisaidia jamii ya tarafa ya Magoma kupitia watoto kupata huduma za elimu,afya na maji sambamba na kupinga ukatili dhidi ya watoto na kuhakikisha wanapata huduma zote za msingi.
“ADP Magoma imefikia tamati sasa lakini kwa kipindi chote tumekuwa tukiisaidia jamii  kupitia watoto hivyo tunaomba jengo na rasilimali zake tunazoacha ziwe chachu kwa jamii  kuendeleza ulinzi na usalama wa mtoto wa Magoma.” Alieleza Banyenza.
Katika hatua nyingine Meneja miradi Mwandamizi wa World vision  kanda ndogo ya Korogwe Sylvester Masanja, alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kuwa mlezi wa asasi ya jamii ya UKIMAMA iliyokuwa ikilelewa na mradi huo sambamba na kuwapatia chumba kimoja katika jengo hilo kwa ajili ya shughuli za asasi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Lucas Mweri aliyepokea hati za makabidhiano ya jengo na rasilimali zake aliahidi kutunza rasilimali hizo na kuhakikisha zinatumika kwa matumizi yenye tija kwa jamii.
 Magoma ADP imeikabidhi Serikali jengo lenye thamani ya Tsh 68,480,000/- walilolijenga mwaka 2010 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kusaidia watoto na jamii tarafa ya Magoma ambayo imefikia mwisho wa utekelezwaji wake. Stori & picha na Fatna Mfalingundi-Afisa habari Halmashauri ya Wilaya Korogwe

UVUVI HABARAMU WAWAPOTEZEA VIUNGO NA KUJERUHIWA VIBAYA

November 14, 2014


WAVUVI haramu waliokuwa wakijaribu kuvua katika kisiwa cha Karange, kata ya Tangasisi, tarafa ya Pongwe wilaya Tanga kwa kutumia baruti wamejeruhiwa na kukatika viungo vya miili yao,Picha zote kwa hisani ya Blog ya Mwanamke makini


Tukio hilo limetokea Novemba 12, mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana.

Waliolipuliwa na kujeruhiwa na baruti hiyo ni Hamisi Omari Kassimu (38) mkazi wa Mwambani ambae amekatika mkono wa kulia na jicho la kulia, na Adamu Seleman Kapera (32) mkazi wa Mwambani ambae amekatika mikono yote miwili, ameumia macho yote, vidole vinne vya mguu wa kushoto na kuungua kifua.


Chombo kilichokuwa kinatumiwa kwenye uvuvi huo haramu ni Ngalawa TTA 315. Hali ya majeruhi wote ambao wamelazwa kwenye hospitali ya rufaa Bombo ni mbaya.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna mwandamizi msaidizi wa Polisi SACP Frasser Kashai alisema upelelezo unaendelea kuwabaini washirika wao na mtandao mzima wa wavuvi haramu kwa hatua za kisheria.


“Tunatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama mara wanapowaona wavuvi wanaovua kinyume cha sheria kwa kutumia baruti kitendo ambacho kinaleta madhara kwenye rasilimali majini,” alisema Kashai na kuongeza

“Lakini pia samai hao wanaovuliwa kwa baruti wanakwa na madhara makubwa  sana kwa afya za walaji, madhara ya baruti pia ni kama mnavyoona kwa watu hao wanaotumia baruti hivyo basi taarifa zitolewe ili wahalifu washughulikiwe.

KONGAMANO LA TISA LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI LAENDELEO LEO MKOANI DODOMA

November 14, 2014

 Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya,lakini pia alieleza kuwa Wilaya yake ya Igunga ina vijiji 98,vijiji 78 vimejengwa zahati,lakini mpaka sasa zahanati 31 hazijasajiliwa,hivyo ameiomba Serikali kupitia wizara ya Afya kuhalakisha suala la usajili wa zahanati hizo katika kuwasaidia wananchi.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akifafanua jambo katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel,ikiwa ni siku ya pili ya hitimisho la Kongamano hilo,Kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza akifafanua jambo  katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.   
  Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
 Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda pamoja na  Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani kwa pamoja wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
 Pichani shoto ni Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza na Mdau wakifuatilia mada mbalimbali ndani ya kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.   
 Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu pamoja na Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda  wakijadiliana jambo.
Washiriki katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel ikiwa ni siku ya pili ya kilele chake huku likiwa limebeba kauli mbiu ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.


 Baadhi ya Wanahabari na Wahariri waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.  
 Mmoja wa Wanahabari Wakongwe,kotoka gazeti la Habari Leo Beda Msimbe akiuliza swali kwenye Kongamano hilo.
  Baadhi ya Wanahabari na Wahariri waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.  
 Baadhi ya Maofisa kutoka NHIF wakijadiliana jambo wakati wa Kongamano .
 Mkurugenzi Mtendaji wa shirikisho la Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC),Bwa.Abubakar Karsan akichangia jambo katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.  
UGUNGAJI WA SEMINA YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA BARA NA VISIWANI

UGUNGAJI WA SEMINA YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA BARA NA VISIWANI

November 14, 2014
1Wakuu wa Mikoa Bara na Visiwani wakiwa katika ugungaji wa semina yao ya siku taku iliyozungumzia Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania bara iliyofungwa jana na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katika Ukumbi wa Sea Cliff  Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum)2Baadhi ya Wakuu wa Mikoa Bara na Visiwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kuhusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania bara ufungaji huo ilifanyika  jana Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum)3Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara  iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji  katika  Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum)
4Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara  iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji  katika  Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja jana,(Na Mpiga Picha Maalum)6Picha ya pamoja iliyowahusisha washiriki wa Semina ya siku tatu ya kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Barabaada ya kufungwa na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katikat, (Na Mpiga Picha Maalum)8Picha ya pamoja iliyowahusisha washiriki wa Semina ya siku tatu ya kwa Maafisa Tawala Mikoa na Wilaya za Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara  baada ya kufungwa na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katikati, (Na Mpiga Picha Maalum)
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA

November 14, 2014

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr. Seif Rashid akifungua Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wahariri pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali linalofanyika kwenye hoteli ya New Dodoma  mkoani Dodoma jana, Kongamano hilo la siku mbili linaendelea leo na linajadili mafanikio mbalimbali na changamoto zinazokabili mfuko huo katika mikoa mbalimbali na Halmashauri ambazo unatoa huduma zake. Kongamano hilo linamalizika leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA) 2 
Naibu Katibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dr. Deo Mtasiwa  akizungumza katika kongamano hilo wakati akimkaribisha waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid ili kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo. 3 
Kamimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Khamis Mdee  akitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali kwa mwaka mzima. 4 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto, Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Athman Rehani wakiwa katika mkutano huo. 5 
Hance John Mwankenja Afisa Mwandamizi , Matekelezo NHIF pamoja na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa katika kongamano hilo. 006 
Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh. Elibariki Kingu akitoa mada katika kongamano hilo. 6Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Bw. Athman Rehani akitoa mada katika Kongamano hilo. 7 
Mkuu wa Wilaya ya Igunga na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Said Ally wakiwa katika kongamano hilo. 9 
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika kongamano hilo. 10 
Grace Kingalame wa TBC wa pili na wadau wengine wakiwa katika kongamano hilo. 11 
Hosea Cheyo wa TBC Mbeya kushoto na Tom Chilala wa Star TV wakifuatilia mada. 12Wanahabari mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo. 13 14 15 
Baadhi ya maofisa wa NHIF wakiandika mambo muhimu katika kongamano hilo.