WIZARA HAINA MPANGO WA KUONGEZA TENA MUDA WA KUPIGA CHAPA MIFUGO-MPINA

January 19, 2018
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akizungumza na vyombo mbalimbali vya  habari  katika ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Waziri wake Mhe.Abdalah Ulega na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili yakutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo  baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya  Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya  Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo  baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya  Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya  Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo  baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina. Kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji,  Mashimba Ndaki.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina  mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa  mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda  wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.

Pia Waziri Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuwakatalia wafugaji kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio kuwa sio wakazi halali wa maeneo husika jambo ambalo amesema halikubaliki na kusisitiza kuwa zoezi lisihusishwe na migogoro ya muda mrefu ya matumizi ya ardhi na hivyo kuagiza kuwa ng’ombe na punda wote nchini wapigwe chapa isipokuwa ya kutoka nchi jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi upigaji chapa mifugo, Mpina alisema hadi kufikia Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo wameshapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali.

Aidha amesema wafugaji wote nchini wataoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26 huku akizionya halmashauri ambazo zitashindwa kutekeleza kikamilifu hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wake.

Alisema hadi sasa halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 huku  halmashauri 9 zikiwa bado hazijaanza kabisa zoezi hilo.

Waziri Mpina amezitaja Halmashauri hizo ambazo hadi sasa hazijaanza kupiga chapa ni Tandahimba, Nanyumbu, Mafia, Newala, Halmashauri za miji ya Newala, Nanyamba, Masasi na Manispaa za Kigamboni na Ilemela Mwanza ambapo amesema halmashauri 68 ambazo ziko chini ya asilimia 50 na ambazo haijaaanza kabisa tayari  halmashauri hizo ameziwasilisha kwa Waziri Mkuu.

Pia alisema halmashauri 6 zina ng’ombe wengi wa maziwa walio kwenye mpango wa kuvalishwa hereni  pamoja na mikoa mingine ambapo jumla ya ng’ombe wote wa maziwa nchini 782,995 kwa sasa, aidha jumla ya punda 572,353 wanatarajiwa kupigwa chapa, taarifa kutoka mikoani kuhusu utekelezaji wa zoezi hili zinaendelea kukusanywa kila siku.

Alisema kumekuwa na ongezeko la asilimia 20.8 katika muda wa kipindi cha wiki mbili tangu muda wa nyongeza kutolewa ongezeko hili ni kutokana na juhudi za pamoja za uhamasishaji uliofanywa kati ya Wizara na halmashauri pamoja na mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari .

“Hivyo juhudi kubwa za pamoja baina ya Wizara, Halmashauri, vyombo vya habari na wafugaji zinahitajika ili kukamilisha zoezi la upigaji chapa kwa asilimia 100, kwa kuwa hadi sasa bado asilimia 40.7 ya ng’ombe hawajapigwa chapa “alisema

Aidha Waziri Mpina amesema kipimo cha asilimia hakitakuwa kigezo cha mwisho cha uhakiki mifugo iliyopigwa chapa badala yake ni kuhakikisha kila ng’ombe na punda mwenye umri wa kuanzia miezi sita wamepigwa chapa.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji,  Mashimba Ndaki alipongeza juhudi kubwa zilizofanywa na  wizara hiyo katika kusimamia zoezi la upigaji chapa ambalo limeungwa mkono na wafugaji wengi nchini.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JANUARI 19, 2018 KUTOKA TFF

January 19, 2018
Kamati ya Maadili iliyokutana Januari 18, 2018 imepitia shauri lililowasilishwa na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF wakiwatuhumu viongozi wanne kwa makosa ya kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC na Simba uliochezwa Disemba 30,2017.

Shauri la kwanza lililomuhusu Katibu msaidizi wa Ndanda Ndugu Selemani Kachele,Kamati imegundua kuwa mtuhumiwa aliitwa wakati wa kuhesabu mapato kuthibitisha deni dhidi ya Ndanda lenye thamani ya Shilingi Milioni mbili laki mbili na elfu hamsini(2,250,000),deni ambalo TFF waliagiza wakatwe kwenye mapato ya mechi hiyo,Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mtwara alithibitisha kuwa alimuita kuthibitisha uhalali wa deni hilo baada ya Muhasibu wa Ndanda kugoma kulipa deni hilo ambalo linahusu pango la Ndanda kwa Mama mwenye Nyumba.

Hata hivyo Kamati ilimuhoji zaidi na akashindwa kutoa uthibitisho wa kulipwa kwa deni hilo na hakuna kumbukumbu zozote zinazoonyesha kuwa deni hilo limelipwa.

Kamati imempa onyo kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(a) kanuni za maadili ya TFF toleo la 2013 na imeiomba Sekretarieti ya TFF ifuatilie kama deni hilo limeshalipwa ili kuepusha ulipaji wa Zaidi ya mara moja.

Shauri la Pili lilimuhusu Muhasibu msaidizi wa Simba Ndugu Suleiman Kahumbu.

Kamati haikuendelea na tuhuma dhidi yake baada ya Sekretarieti ya TFF kuamua kuondoa shauri dhidi yake kwa kuwa alitoa ushirikiano na kutosheka kuwa hana hatia na badala yake alitumika kama shahidi wa upande wa washtaki.

Shauri la tatu lilimuhusu Katibu mkuu wa Chama cha soka Mtwara Ndugu Kizito Mbano.
Kamati ilimuhoji mtuhumiwa na alikiri kuwepo kwa mawasiliano na msimamizi wa kituo Ndugu Dunstan Mkundi kuhusu nia ya kughushi fomu ya marejesho ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba SC.

Ndugu Kizito Mbano hakutoa taarifa yoyote ile wala kuonyesha ushirikiano kwa Sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi wakati yeye akiwa msimamizi msaidizi wa kituo na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Mtwara,hivyo Kamati imemkuta na hatia na imemuhukumu kutojihusisha na shughuli za Mpira wa Miguu kwa kipindi cha miaka Mitano(5) kwa mujibu wa kifungu cha 73(7) cha kanuni za maadili TFF toleo la 2013.

Shauri la nne lililosikilizwa lilikuwa la Msimamizi wa Kituo cha Mtwara Ndugu Dunstan Mkundi.
Kamati baada ya kusikiliza shauri hilo imemkuta na hatia kwa kosa la kushindwa kuwasilisha fomu ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba ndani ya saa 48 kama kanuni inavyotaka.

Hiyo ni kinyume na Kanuni ya 32(2) Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2015,Vilevile Kamati imemkuta na hatia ya kushindwa kusimamia mauzo ya tiketi za mchezo kati ya Ndanda FC na Simba  kwa kutotoa taarifa ya tiketi zilizotumika na zile zilizobaki.

Kamati ilibaini kuwa Ndugu Dunstan Mkundi akiwa msimamizi wa kituo hakutoa ushirikiano kwa kutompa taarifa za mapato na idadi ya watazamaji Kamisaa wa mchezo Salum Singano kinyume na Kanuni ya 32(4) ya Ligi Kuu toleo la 2017.


Aidha Mkundi ambaye ni msimamizi wa kituo cha Mtwara ameshindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu utata wa fomu mbili zilizowasilishwa zilizoonyesha utofauti wa mapato kwa kiasi cha shilingi Milioni tatu laki saba kumi elfu(3,710,000).

Washtakiwa wote walihojiwa na Kamati na kuthibitisha kuwa mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba yalikuwa ni Shilingi Milioni thelathini na saba laki saba na themanini elfu(37,780,000) na siyo Shilingi milioni thelathini nne sabini elfu(34,070,000) ambazo Ndugu Mkundi anadai kuwa ndiyo yalikuwa mapato ya mchezo huo.

Kulingana na nyaraka zilizowasilishwa kutoka klabu za Ndanda FC na Simba mapato ya Vilabu hivyo yalitokana na asilimia ya vyanzo kutokana na milioni thelathini na saba laki saba themanini elfu(37,780,000) na siyo Shilingi milioni thelathini nne sabini elfu(34,070,000)kama alivyowasilisha msimamizi huyo wa kituo cha Mtwara nyaraka za fedha alizoweka kwenye akaunti za TFF na Bodi ya Ligi.

Kitendo cha kughushi nyaraka na kupunguza mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba siyo tu kimeharibu taswira ya mchezo wa Mpira wa miguu,bali pia kimepunguza mapato ya TFF,Bodi ya Ligi na taasisi nyingine kama Mamlaka ya Mapato (TRA),Baraza la Michezo la Taifa (BMT),Wamiliki wa Uwanja na Wadau wengine.

Kamati imemtia hatiani Ndugu Dunstan Mkundi kwa makosa hayo na inamfungia maisha kutojishughulisha na mchezo wa Mpira wa Miguu.

Kamati imetoa adhabu hiyo kali ili iwe fundisho kwa wale wote wanaotaka kufanya ubadhirifu wa ufisadi katika mchezo wa Mpira wa Miguu.

Kamati inashauri Sekretarieti ya TFF ifuatilie suala hili kwenye vyombo vya dola na mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

Pia Kamati imeiomba Sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi kutafuta njia bora ya kuimarisha udhibiti wa mapato kwa kuongeza uwajibikaji wa uwazi kwa wadau wote,Vilevile Kamati inashauri Sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi kuharakisha mchakato wa kukusanya mapato yake kwa njia za kielektroniki ili kuziba mianya ya upotevu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUTAMBUA UMUHIMU WA KULIPA KODI

January 19, 2018
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza jambo wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa Mkutano wa pamoja na wachimbaji hao kwenye ofisi za Madini Kanda ya kusini, Leo 19 Januari 2018.
Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Kanda ya kusini Ndg Peter Ludovick akieleza kero za wachimbaji mbele ya Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati wa mkutano na wachimbaji wadogo, Leo 19 Januyari 2018.

Na Mathias Canal, Mtwara

Wizara ya Madini imesisitiza wachimbaji wadogo na wakubwa nchini kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa kila wanachozalisha kwani itasaidia kuongeza pato la Taifa kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ikiwemo ukarabati wa miundombinu, Ujenzi na uimarishaji Wa sekta ya afya, elimu, Sekta ya umeme na sekta ya maji.

Akizungumza Mkoani Mtwara wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa jamii bado haina elimu ya kutosha juu ya ulipaji kodi hivyo ofisi za madini nchini zinapaswa kuongeza msukumo Wa utoaji elimu juu ya ulipaji kodi na utunzaji wa kumbukumbuku za shughuli za uvunaji Madini kwa kila mahali kwenye leseni.

Mhe Biteko alisema kuwa wachimbaji wadogo kote nchini wanapaswa kutambua kuwa hawatakiwi kusalia kukwepa kodi badala yake wanapaswa kutoka kwenye uchuuzi na hatimaye kuhamia kwenye ufanyabiashara na kuhifadhi taarifa zote kwa mujibu wa kanuni kwa kipindi cha miaka 5.

Alisema kuwa mtu yeyote anapoitwa mfanyabiashara anatambulika katika jamii na serikali kwa ujumla wake hivyo kigezo kikubwa na muhimu kwa mfanyabiashara ni kulipa kodi kwa mujibu Wa kanuni, sheria na taratibu.

Akizungumza kwa msisitizo Mhe Biteko alisema kuwa watanzania wamempata Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuongoza Taifa akiwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano hivyo wanapaswa kuunga mkono juhudi za utendaji wake kwa kulipa kodi kwa manufaa ya jamii nzima.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Wa Madini ameupongeza uongozi Wa Ofisi ya Madini Kanda ya Mtwara kwa ushirikiano mzuri na wachimbaji jambo ambalo limeimarisha utendaji wao pasina malalamiko dhidi ya serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Chama Cha wachimbaji Mkoa Wa Mtwara Ndg Festo Balegele akizungumza wakati Wa mkutano huo alimsihi Naibu Waziri wa Madini kutilia mkazo uongezaji thamani wa chumvi inayozalishwa nchini kwa kuikausha (Drying) na kuisaga (Grinding) sambamba na kuongeza Madini joto kwani itapelekea serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumiwa na serikali kuagiza chumvi nje ya nchi.

Alisema kuwa kila mwaka jumla ya tani 350 za chumvi huagizwa nje ya nchi ambapo ikiwasili nchini inauzwa kwa shilingi 500 kwa gramu 500 sawa na shilingi 50,000 kwa kilo 50 kiasi ambacho ni kikubwa Mara tano ya gharama za chumvi inayozalishwa nchini kwani inauzwa kwa shilingi 5000 kwa kilo 50.

Alisema kuwa chumvi inayoagizwa nje ya nchi ni kiasi cha Tani 350,000 kila mwaka huku akisisitiza kuwa serikali ingetilia mkazo na kuboresha miundombinu nchini ingerahisisha upatikanaji wa chumvi nyingi nchini ambayo inauzwa kwa kiasi kidogo chenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya watanzania.

WATATU WALAMBA MAMILIONI YA TATU MZUKA JUMAPILI JACKPOT

January 19, 2018
 Meneja Mawasiliano wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) hivi karibuni wakati wa kuwatambulisha na  kuwakabidhi hundi zao washindi watatu wa TatuMzuka (Jumapili Jackpot),mchezo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki.Maganga amewaomba Watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kuendelea kucheza mchezo huo,kwani umekuwa ukiwakwamua wengi waliobahatika na kuwa wafanyabiashara/wajasiliamali wazuri na vipato vyao vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku.
Pichani kati ni Lucas Swebe akitoa ushuhuda wa namna alivyojishindia fedha taslimi Milioni tano katika  mchezo wa TatuMzuka (Jumapili Jackpot),Pichani kulia ni mshindi mwingine aitwaye Mrisho Maganga aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 22 pamoja nae (kutosho) ni Daniel Mwachali ambaye naye alijinyakulia kitita cha shilingi Milioni 22.
 Meneja Mawasiliano wa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi ya Milioni 22,Danie Mwachali aliyojishindia kwenye mchezo wa TatuMzuka (Jumapili Jackpot) uliofanyika mwishoni mwa wiki.
-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

MAJIJI YA YANGZHOU YA CHINA NA JIJI LA TANGA TANZANIA WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO.

January 19, 2018
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga  Daudi Mayeji kushoto wakitiliana saini ya makubaliano ya undugu na ushirikiano wa Majiji ya Yangzhou ya Jijini China na Jiji la Tanga Tanzania na Meya wa Jiangdu wa Jiji la Yangzhou,Zhang Tong yaliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach mjini Tanga juzi wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Martini Shigella

 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga  Daudi Mayeji kushoto wakitiliana saini ya makubaliano ya undugu na ushirikiano wa Majiji ya Yangzhou ya Jijini China na Jiji la Tanga Tanzania na Meya wa Jiangdu wa Jiji la Yangzhou,Zhang Tong yaliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach mjini Tanga juzi wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Martini Shigella
  Mkurugenzi wa Jiji la Tanga  Daudi Mayeji kushoto wakibadilishana makubaliano ya  ndugu na ushirikiano wa Majiji ya Yangzhou ya Jijini China na Jiji la Tanga Tanzania na Meya wa Jiangdu wa Jiji la Yangzhou,Zhang Tong mara baada ya kutiliana saini katika halfa  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach mjini Tanga juzi wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Martini Shigella
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga  Daudi Mayeji kushoto wakibadilishana makubaliano ya  ndugu na ushirikiano wa Majiji ya Yangzhou ya Jijini China na Jiji la Tanga Tanzania na Meya wa Jiangdu wa Jiji la Yangzhou,Zhang Tong mara baada ya kutiliana saini katika halfa  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach mjini Tanga juzi wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Martini Shigella

 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga  Daudi Mayeji akimpongeza Meya wa Jiangdu wa Jiji la Yangzhou,Zhang Tong mara baada ya kusaini makubaliano hayo kwenye Hoteli ya Tanga Beach mjini Tanga katikati anayeshughudia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga  Daudi Mayeji kushoto na Meya wa Jiangdu wa Jiji la Yangzhou,Zhang Tong kulia wakibalishana makubaliano ya ushirikiano mara baada ya kusaini makubaliano hayo kwenye Hoteli ya Tanga Beach mjini Tanga katikati anayeshughudia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella